1 Makampuni ya kuchapisha vitabu hayakusita kuchapisha kitabu baada
2 ya ithibati ya kamati kupatikana, kwa sababu hiyo ilikuwa thibitisho
3 kwamba kitabu hicho kitatumiwa katika shule za serikali na zile zenye
4 kupata ruzuku ya serikali. Ithibati ilionyesha kwamba kitabu kitapata
5 wanunuzi, jambo ambalo lilisaidia kupunguza gharama ya kuchapisha
6 vitabu vya Kiswahili ambavyo havikuwa, na hadi sasa havina, wasomaji
7 wengi nje ya shule. Waandishi walipata moyo wa kuandika walipojua
8 kwamba vitabu vyao vitatumiwa kote katika Afrika Mashariki. Vitabu
9 viliuzwa kwa wingi. Kwa mfano, vitabu vinne vya Ronald Snoxall
10 viliuzwa takriban nakala 1,000,000. l6*
12 Nguvu za ithibati hazikuishia Afrika Mashariki tu. Uwezo wa ithibati
13 wa Kamati ulikuwa ukiheshimiwa kote ulimwenguni, kama asemavyo
16 "Wachapishaji wa Ulaya, Marekani na sehemu zingine za ulimwengu
17 wamekuwa wakitegemea ithibati iliyotolewa na kamati ya Kiswahili
18 ya Afrika Mashariki kwa miswada waliopelekewa na waandishi
19 binafsi, Waafrika na Wazungu ili kuwasomea na kuwasahihishia."
20 (Ratcliffe, ILC Bulletin Na 21, 1951: 3).
22 Ili kuwatia moyo Waafrika waweze kuandika kusudi watosheleze
23 mahitaji ya vitabu vya fasihi, Kamati ilianzisha mashindano ya kuandika
24 insha mnamo 1935. Ili kuwapa motisha ya kuendeleza vipawa vilivyo-
25 gunduliwa katika mashindano ya insha, mashindano ya uandishi yalianzi-
26 shwa katika mwaka wa 1939. Kutokana na mashindano hayo miswada
27 mingi ilipelekewa Kamati. Mashindano hayo yalianza kuwashirikisha
28 washindani Wazungu katika mwaka 1942 ili kukuza uandishi wa Kiswahili
29 miongoni mwa watawala wa siku za baadaye. (Ratcliffe 1942: 9). Kwa
30 hivyo, kamati ilikuwa ikitekeleza malengo iliyokusudiwa.
32 Ilikuwa ikichapisha vitabu vya Kiswahili sanifu ili iwashawishi waandishi
33 wapya, na ilihakikisha kwamba vitabu vilikuwa vikitafsiriwa kwa
34 Kiswahili. Kamusi ya Kiswahili-Kiswahili ilichapishwa mnamo 1935 hali
35 kamusi ya Kiswahili-Kiingereza na ya Kiingereza-Kiswahili zilichapishwa
38 16* Mahojiano ya mwandishi na R. A. Snoxall Februari 10, 1984. Vitabu hivyo ni: Elimu ya
39 Kiswahili Kitabu cha Kwanza. Kitabu cha Pili na Kitabu cha Tatu vilivyoandikwa na E. G.
40 Morris na R. A. Snoxall; na Kitabu cha Nne kilichoandikwa na R. A. Snoxall na E. A. Ibreck
41 vilivyochapishwa na Longman (hadi 1959.)
45 mwaka 1939. Kamati iliendelea kujibu maswali ya umma kuhusu maneno
46 mapya, asili ya maneno, maneno yaliyoazimwa n.k., na maneno yaliyo-
47 kubaliwa yalichapishwa katika jarida la l.L.C. Bulletin. Hapo awali
48 nakala za l.L.C. Bulletin zilikuwa zikitolewa bure kwa wale waliokuwa
49 wakipenda. Baadhi ya vitabu vya sayansi vilikuwa vimetafsiriwa kwa
50 Kiswahili. 17* Vitabu hivyo vilikuwa msingi bora ambao ungetumiwa
51 kuanzisha utafiti wa masomo ya Kiswahili na uchapishaji.
55 Katika utangulizi wa kitabu kinachoitwa A Handbook of the Swahili
56 Language, Askofu Steere alijadali suala la tahajia au hati za maandishi ya
57 Kiswahili, kwa undani. Karibu maandishi yote ya Kiswahili kabla ya
58 wakati wake yalikuwa yameandikwa kwa hati za Kiarabu. Mengi kati ya
59 maandishi hayo yalikuwa ni tenzi na mashairi ya kidini na mambo ya
60 kawaida yaliyoandikwa kwa lahaja ya kishairi ya Kaskazini ambayo
61 Steere alishuku iwapo ilieleweka na watu wengi. Ingawa Kiswahili cha
62 wakati wake kilikuwa kikitumiwa katika kuandikiana barua, Steere
63 anasema kwamba barua kama hizo zilianzia na salamu kwa Kiarabu na
64 pia maneno na vifungu vya maneno ya Kiarabu vilikuwa vikichanganywa
67 Steere alitambua kwamba hati za Kiarabu hazifai kuandikia Kiswahili
68 kwa sababu lugha ya Kiswahili inazo irabu tano ikilinganishwa na irabu
69 tatu za Kiarabu. Kuhusu konsonati, hati za Kiarabu zinao upungufu wa
70 konsonanti cha, g, p, na v. Steere aliandika hivi:
72 "Kwa hivyo, Waswahili wanalazimika kuandika ba, f, au p waki-
73 kusudia kuandika mb au b; wanaandika ghain badala ya g, ng, ng'; fa
74 badala ya v, mv na f; ya badala ya ny na y; shin badala ya ch na sh; pia
75 wanaiwacha n inapozitangulia d, j, y na z." (Steere 1870: 5)
77 Kwa hivyo, ni wazi kwamba hati za Kiarabu hazifai na hazitoshelezi
78 maandishi ya Kiswahili kwa sababu ya kutatanisha. Ili kuonyesha
79 matatizo ya hati hizi, Steere anaandika hivi:
81 "Nilipokuwa Zanzibar, kulikuwa na barua iliyotoka Kilwa kuhusu
82 vita. Barua ilitaja kwamba mtu mmoja kati ya wale waliopigana
85 17* Baadhi ya vitabu hivyo ni Mafunzo Katika Hygiene ya Kuwafunza Watu wa Afrika ya
86 Mashariki, London 1924; Stronomia - Elimu ya Dunia na Jua na Mwezi na Nyota, UMCA
87 Zanzibar 1901; Jiolojia, UMCA Zanzibar 1901; Lojiki - Mlango wa Filosofia 1, UMCA
88 Zanzibar 1901 na Mlango wa Filosofia 2, UMCA Zanzibar 1901.
92 alikuwa amekufa au amevuka na hakuna aliyeweza kusema kile
93 kilichokuwa kimetendeka. Konsonanti mbili za mwisho zilikuwa fa
94 na gaf zikiwa na vitone vitatu juu yake. Ikiwa vitone viwili vilikuwa
95 vya herufi ya kwanza, mtu huyo alikuwa amekufa. Ikiwa vitone
96 viwili vilikuwa vya herufi ya pili alikuwa hai, lakini vitone hivyo
97 vilikuwa katikati hivi kwamba hakuna aliyeweza kuvigawanya.
98 Iwapo Kiarabu kingekuwa na herufi v ingekuwa wazi." (Steere
101 Zikilinganishwa na hati za Kiarabu, hati za Kirumi hazileti matatizo
102 yoyote katika kuandika Kiswahili. Sababu yake ni kwamba wasomi wengi
103 wa Kiswahili waliokuja baada ya Krapf na Steere waliamua kutumia hati
104 za Kirumi walizokuwa wamezizoea badala ya hati za Kiarabu zilizokuwa
105 zikitumika kuandika Kiswahili. Maneno na mizani katika Kiarabu mara
106 nyingi huishia kwa konsonati. Hili pia ni jambo lingine linalozifanya hati
107 za Kiarabu zisifae kukiandika Kiswahili.
109 Dhehebu la UMCA lilichapisha vitabu kufuatia mtindo uliotumiwa
110 katika kuchapisha vitabu vya Steere. Misheni wa Kizungu walifanana na
111 waanzilishi wa uchunguzi wa Kiswahili kwa kuwa ilikuwa rahisi kwao
112 kutumia hati za Kirumi badala ya zile za Kiarabu. Mkutano wa Dar es
113 Salaam wa 1925 uliamua kutozitumia hati za Kiarabu pamoja na
114 konsonanti za Kiarabu kama vile kh. 18* Uamuzi huu wa l925 uliwakasirisha
115 wengi wakiwa ni pamoja na gazeti la Mombasa, Al-Islah, kama ilivyo-
116 jadiliwa kwa kireru katika sehemu ifuatayo.
118 Profesa Carl Meinhof alipohudhuria mkutano wa Mombasa wa 1928,
119 waliohudhuria walikuwa na nafasi ya kushauriana naye kuhusu othografia
120 ya Kiswahili. Meinhof alikubaliana na nyingi kati ya tahajia iliyopendeke-
121 zwa kwa kuwa ilikuwa rahisi bila kutatanisha, isipokuwa katika herufi ch
122 na ng'. Meinhof alipendekeza c itumiwe badala ya ch. Badala ya kutumia
123 alama tatu za maandishi (ng') kusimamia sauti moja, alipendekeza
124 kutumiwa kwa n yenye mkia itumiwe kama ilivyo katika maandishi ya
127 Lakini mashauri haya ya Meinhof hayakukubaliwa. Wasomi wa
128 Kiswahili wakati huo walijiona kuwa sahihi, na kwamba mapendekezo ya
129 Meinhof yalifaa tu katika maandishi ya kifonetiki katika isimu lakini
130 hayakufaa othografia ya kawaida ya Kiswahili. Katika majadiliano yao
133 18* Baadaye matumizi ya kh yalikubaliwa. Katika makala ya mhariri ya kitabu cha Hemedi
134 Abdalla - Utenzi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima (uk. 7) Allen anaandika: "Kwa
135 hivyo ninatumia othograria sanifu ikiwa ni pamoja na kutumiwa kwa herufi kh iliyoidhini-
136 shwa kutumiwa kwa hiari mnamo 1958".
140 walitaja kwamba ingekuwa vigumu kupiga taipu n hiyo yenye mkia.
141 Tatizo hili lingetatuliwa hapo mwanzoni kwa kupiga taipu herufi j juu ya n
142 wakingojea kurekebishwa kwa mashine. Suluhisho hili halikukubaliwa,
143 na kwa hivyo tatizo la kuandika sauti ya kwanza ya neno ng'ombe kwa
144 sauti mbili na alama (ng') lingali laendelea.
146 Upungufu mwingine wa othografia ya Kiswahili unaoweza kutajwa
147 hapa ni kule kukosa kutofautisha konsonanti za kipua (nazali) ambazo
148 ni mizani kamili na zile ambazo huambatana na irabu ili ziunde
149 mizani kamili. (Taz. Mkude 1982). Mifano ya konsonanti za kipua
150 (nazali) ambazo ni mizani kamili ni m na n za kwanza katika maneno
151 mmea na nne. Sauti n ya neno nguruwe ni sawa na sauti ya n yenye mkia.
152 Kwa hivyo, kama tungefuata othografia sanifu kikamilifu badala ya
153 nguruwe tungeandika ng'guruwe.
155 Othografia ya Kiswahili sanifu haikukosa malalamiko. Kulikuwa na
156 upinzani na kutoelewana hata kati ya misheni. Kasisi Roehl katika makala
157 yake "Hali ya lugha katika Afrika Mashariki" (Africa Vol.3, Na.2, 1930),
158 anaeleza masikitiko yake kwamba Idara ya Elimu huko Dar-es-Salaam
159 ilikuwa imeanzisha othografia kinyume cha mapendekezo ya wataalamu
160 wa isimu wa misheni. Roehl analalamika kwamba, kati ya makosa
161 mengine, othografia inazipa nafasi za kipekee sauti za Kiarabu na
162 kulazimisha zitumike babala ya kuwapa wazungumzaji wa Kiswahili
163 uhuru wa kuzitamka kutegemea vile wanavyotamka sauti za lugha yao na
164 kuziandika sauti hizo vile wanavyozitamka. Roehl 19* anaeleza kwamba
165 othografia ya Kiswahili yatakikana iwe ya Kiswahili wala si ya Kiarabu au
168 Kasisi Roehl anaeleza zaidi kwamba katika kuunda othografia ambayo
169 inafaa Kiswahili zaidi, isiwe ni Tanganyika pekee ambayo inatoa uamuzi.
170 Anapendekeza Kenya, Uganda na Congo (Zaire) zihusike ili kuunda
171 othografia sanifu kwa watu wote wanaotumia Kiswahili. Kama tunavyojua
172 sasa upungufu mkubwa uliofanywa na nchi za Afrika Mashariki katika
173 kusanifisha Kiswahili ulikuwa ni kushindwa kushirikisha Zaire katika
174 shughuli za Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki kama alivyo-
175 pendekeza Kasisi Roehl. Upungufu huo, licha ya jitihada za Ronald
176 Snoxall, unaeleza kuwepo kwa tofauti kadha kati ya Kiswahili cha Zaire
179 Kama inavyofahamika na kuelezwa wazi na wasomi kama vile John
180 Williamson katika uchambuzi wake wa Kingwana cha maandishi (I.L.C.
183 19* Roehl hakutaja sauti za Kiarabu alizokuwa akimaanisha. Yawezekana alimaanisha sauti
184 kama vile dh katika fedheha dhulumu na adhibu au gh katika ghadhabu gharika na lugha
185 ambazo hazipatikani kwingine ila katika maneno yaliyoazimwa kutoka Kiarabu.
189 Bulletin Na. 21, 1951: 15-16), lahaja ya Kingwana haifuati upatano
190 maalum kwa sababu ya kukosa kusanifishwa. Williamson alipata kwamba,
191 katika makala moja herufi y na j zilitumiwa moja badala ya nyingine. Kwa
192 hivyo maneno kama vile miji, jina, pamoja na kijana yalitumiwa katika
193 sehemu moja ya makala, na kwingine katika makala hiyo hiyo maneno
194 hayo yangeandikwa kama muyi, yina, pamoya na kiyana. Herufi r na l pia
195 zilitumiwa moja badala ya nyingine. Habari, mara na hubiri yaliweza
196 kupatikana katika makala moja na habali, mala na hubili. Herufi k na g
197 zilichanganywa hivi kwamba maneno miziko na mizigo, ukonjwa na
198 ugonjwa pia yalipatikana katika makala moja.
200 Kupatikana kwa maneno kama vile muyi, habali, miziko, ukonjwa
201 katika makala moja na mji, habari, mizigo na ugonjwa katika othografia ya
202 Kingwana yaonyesha kwamba ni rahisi kusanifisha. Iligunduliwa kwamba
203 ilikuwa rahisi kusoma na kuelewa maandishi ya Kiswahili sanifu cha
204 Afrika Mashariki kwa kutujia ujuzi wa Kingwana:
206 Snoxall 20* anaeleza kwamba alijaribu mara mbili kukifanya Kingwana
207 kifuate taratibu za Kiswahili sanifu cha Afrika Mashariki. Kwanza
208 alimtuma C. G. Richards aliyekuwa mkurugenzi wa East African Literature
209 Bureau kwenda Belgian Congo (Zaire) kuwahimiza wasanifishe Kingwana.
210 Richards alienda huko lakini hakufanikiwa. Snoxall alitamani kusambaza
211 Kiswahili sanifu cha Afrika Mashariki ambacho chatumiwa na watu
212 wengi zaidi. Maoni yake ni kwamba, Kingwana chatumiwa katika sehemu
213 moja ya nchi moja, na kwa kuwa wanaokizungumza wanafahamu
214 Kiswahili sanifu, ingekuwa rahisi kuwaleta pamoja na wale wanaotumia
215 Kiswahili sanifu cha Afrika Mashariki: "Ingekuwa kazi rahisi ikifanywa
216 kwa bidii". (Snoxall ibid.)
218 Jaribio la pili alilofanya Snoxall lilikuwa ni kuwaalika Wabelgiji wawili
219 kutoka Kongo (Zaire) kuhudhuria mkutano wa Kamati ya Kiswahili ya
220 Afrika Mashariki mjini Nairobi. Wabelgiji hao waliitikia mwaliko lakini
221 walishangaa kuona kwamba kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
222 ilikuwa na wajumbe Waafrika. Wabelgiji hawakufikiria kwamba wajumbe
223 wa Kiafrika kama vile Shaaban Robert wangeweza kuwa wataalam wa
224 lugha yao. Kwa hivyo Wabelgiji hawakutaka kujiunga na Kamati ya
225 Kiswahili ya Afrika Mashariki. Hawakuona kama ingekuwa vizuri
228 Ingawaje, Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, iliweza kuwajulisha
229 watawala wa Kongo ya Ubelgiji kwamba tofauti kati ya Kingwana na
230 Kiswahili sanifu ilikuwa ni matamshi yasiyofuata kanuni za safuri. Maoni
233 20* Mahojiano na mwandishi February 10 1984. Hali imebadilika sasa kwa kuwa Kiswahili cha
234 Zaire kimesanifishwa.
238 hayo ya Kamati yalipelekewa watawala wa Kongo na Bwana Sandrart wa
239 kutoka Rwanda aliyetumwa na Kongo ya Ubelgiji kuhudhuria mkutano
240 wa kumi na tatu (13) wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mnamo
241 1950. Bwana Sandrart aliweza kuifahamisha Kamati mambo kadha
242 kuhusu Kingwana. Tofauti za kimatamshi hazikutatiza kueleweka kwa
243 Kiswahili katika kukisanifisha ndiko kulikopendekezwa na Roehl katika
244 Zaire, Rwanda na Burundi.
246 Iwapo Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ingefaulu kuwashawishi
247 watawala wa Kibelgiji kutumia Kiswahili sanifu, hali hiyo ingewezesha
248 kutumiwa kwa vitabu vya Kiswahili sanifu katika eneo kubwa zaidi.
249 Kiswahili kingepata matumizi mapya ya kuwaunganisha Wazungu wenye
250 asili za Uingereza na Ubelgiji mbali na kuwaunganisha Waafrika wa
251 makabila na mataifa mbalimbali, kwa kuwa kungekuwa na lugha moja ya
252 mawasiliano katika Afrika Mashariki na Kati. Pia Wakongo wangekuwa
253 na Kiswahili sanifu. Kushirikishwa kwa Kongo na nchi zingine zinazotumia
254 Kiswahili katika kukisanifisha ndiko kulikopendekezwa na Roehl katika
257 Canon G. W. Broomfield alijibu makala ya Kasisi Roehl kwa haraka
258 alipoiandika makala yake "Kukifanya Kiswahili kiwe cha Kibantu"
259 (Africa Vol.4 Na. 1,1931). Broomfield anaanza kwa kumfahamisha Roehl
260 kwamba othografia ambayo Roehl anaizungumzia ilifanywa na kamati
261 mjini Dar es Salaam mwezi Oktoba 1925. Kwa hivyo, anaeleza kwamba
262 othografia hiyo haikubuniwa na Idara ya Elimu kama alivyodai Roehl.
263 Anasema kwamba Tanganyika pamoja na Zanzibar zilihudhuria na
264 kwamba Kenya haikuhudhuria kutokana na kutoelewana hata ingawa
267 Anaendelea kueleza kwamba othografia iliyoidhinishwa ni ile ambayo
268 ilikuwa ikitumiwa kwa miaka mingi na UMCA isipokuwa kutokutumiwa
269 kwa kh. Maneno ambayo hapo awali yalikuwa yakiandikwa kwa kutumia
270 konsonanti mbili zikifuatana kama vile hatta, milla na marra ingebidi
271 yatumie konsonanti moja: hata, mila na mara. Kutumiwa kwa kh katika
272 maneno kama vile khabari, khatia na khalisi, ilibidi yatumie h pekee:
273 habari, hatia na halisi.
275 Katika makala hiyo Broomfield anataja pia kwamba mmishonari
276 mmoja alipinga othografia hiyo katika mkutano wa Dar es Salaamu wa
277 1925, lakini wanachama watano waliiunga mkono. Maelezo haya yana-
278 onyesha kwamba ni watu wachache sana waliohusika katika kuamua
279 suala la othografia. Yawezekana kwamba kanisa la Roehl, misheni ya
280 Lutheran, haikualikwa kutoa maoni yao au kuhudhuria mkutano huo
283 Kuhusu msamiati wa Kiarabu katika Kiswahili ambao unasababisha
287 kuwepo na konsonanti za Kiarabu katika othografia ya Kiswahili,
288 Broomfield anaeleza kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu ni maneno
289 ya Kiswahili. Anadai kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu ni maneno
290 ya Kiswahili hivi kwamba Kiswahili hakijawahi kuwepo bila ya maneno ya
291 Kiarabu na kwamba hakiwezi kuyaondoa. Kwa hivyo hakubaliani na
292 maoni ya Roehl, ya ukweli kwamba hapo mwanzo Kiswahili kilikuwa
293 lugha safi ya Kibantu na kwamba maneno ya Kiarabu yaliazimwa. Ukweli
294 kwamba Kiswahili kilikuwepo kabla ya kuja kwa Waarabu hauwezi
295 kubishaniwa. Hii ndiyo sababu mhariri wa jarida la Africa alisahihisha
296 maoni ya kupotosha ya Broomfield katika maoni ya mhariri yaliyotangulia
299 Majadiliano ya othografia yaliendelea wakati wa vita vya pili vya dunia.
300 Mjadala huo wa wanakamati ulihusu mageuko ya irabu yaliyosababishwa
301 na mfuatano wa irabu mbili katika neno moja. Mageuko hayo ni kama vile
302 kuenda na tuataka kuwa kwenda na twataka. Kasisi A. R. Pittway kutoka
303 Kenya, aliyefanya uchunguzi wake katika lahaja ya Kimvita, aliuanzisha
304 mjadala katika jarida la Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Bulletin
307 Pittway anaeleza kwamba kwa kuwa usanifishaji unahusu lahaja tofauti
308 kusiwe na lahaja yoyote muhimu itakayopuuzwa. Anasema kwamba
309 maneno ambayo si ya Kiunguja, semi, na miundo ya kisarufi, yastahili
310 kukubaliwa kutumiwa sambamba na Kiswahili sanifu ili kutajirisha lugha.
311 Kwa maoni yake, kukubaliwa kwa matumizi hayo ya kilahaja kutasaidia
312 kufanya Kiswahili kipendwe sana na watu.
314 Pittway anaendelea kupendekeza kwamba mw inayotangulia u igeuzwe
315 kuwa mu. Anaeleza kwamba ni kawaida mu kugeuka kuwa mw inapo-
316 tangulia a,i,e na o, lakini kifonetiki si jambo la kawaida kwa mu kugeuka
317 kuwa mw inapotangulia u. Pittway alitaka mabadiliko hayo kwa sababu
318 dhehebu lake la C.M.S. Iililokuwa limeamua kusanifisha Biblia na Kitabu
319 cha Maombi lilihitaji muongozo. Alisema kwamba mabadiliko hayo
320 yalikuwa muhimu kwa sababu matumizi ya mu na mw katika vitabu
321 vilivyopitishwa na Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki yaelekea
322 hayakufuata kanuni yoyote.
324 Kama ilivyotarajiwa, makala ya Pittway iliyoandikwa mara tu baada ya
325 kuchapishwa kwa kamusi za Kiingereza-Kiswahili na Kiswahili-Kiingereza,
326 ilipingwa mara moja. Katika jarida, Bulletin Na. 14 la 1948, Ronald
327 Snoxall anatahadharisha dhidi ya othografia inayokwenda kinyume cha
328 kamusi sanifu iliyoichukua kamati miaka mingi kutayarisha. Kwa hivyo
329 pendekezo la Pittway halipaswi kukubaliwa kuvuruga othografia iliyo-
330 kubaliwa. Snoxall anapendekeza othografia iliyotumika katika kamusi
331 ikubaliwe vile ilivyo.
335 Maoni mengi kuhusu pendekezo la Pittway yalitolewa na Kasisi Fr.
336 Alfons Loogman wa Bagamoyo aliyetahadharisha dhidi ya kukubali kanuni
337 za lugha zibadilishe othografia iliyokubaliwa. Loogman anaeleza kwamba
338 kusanifishwa kwa Kiswahili kuna maana kwamba lahaja moja ilichaguliwa
339 kuwa msingi wake na kwamba inabidi lahaja zingine ziwe tayari kupoteza
340 baadhi ya miundo na kanuni za sarufi zao licha ya umuhimu wa lahaja
341 hizo. Hata hivyo Loogman anaunga mkono kanuni ya mgeuko wa sauti
342 uliotajwa na kusema kwamba hakuna mtu angependa kusema yaitu, waivi
343 au maino badala ya yetu, wevi na meno.
345 Katika kukomesha mjadala huu, katibu wa kamati Kasisi B. J. Ratcliffe
346 anakiri kwamba hakuna othografia inayoweza kutosheleza mahitaji yote
347 ya lahaja zote. Anatoa msimamo rasmi kueleza hivi:
349 "'M' ya Kiswahili kwa kawaida husimamia 'm', 'u' hutoweka kabla
350 ya konsonanti, na mara nyingi huwa 'w' inapotangulia irabu ila
351 wakati inapotangulia kiini cha neno linaloanzia kwa 'u' au kabla ya
352 'w' au hugeuka kuwa 'w' wakati mwingine iwapo maneno yanahitaji
353 kugeuka huko." (ibid. uk. 6).
355 Ni jambo zuri kwamba Kamati ilipinga mabadiliko ya othografia.
356 Kama watu wangekuwa huru kurekebisha othografia katika siku hizo,
357 hatungejiepusha na makosa. Tungekumbwa na othografia ya kizamani
358 kama ile ya Kiingereza ambapo maneno yanaandikwa kwa njia tofauti
359 sana na vile yanavyotamkwa. Nikitoa mifano miwili tu, neno Leicester
360 hutamkwa Lesta, na Gloucester hutamkwa Glosta.
362 2.3 Maoni kuhusu usanifishaji
364 Kumbukumbu iliyojulikana kwa jina "Kiswahili cha Kisasa", I.L.C.
365 Bulletin Na. 7 1934, iliandikwa na afisa wa Idara ya Elimu nchini Kenya.
366 Kumbukumbu hiyo ilipelekewa katibu wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika
367 Mashariki na Mkurugenzi wa Elimu ili ijadiliwe katika mkutano wa
368 Kamati. Mwandishi ambaye hakutaja jina lake alitahadharisha Kamati
369 kwamba Kiswahili walichokuwa wakishughulikia kilikuwa kikiendelea
370 kuwa lugha ngeni kwa Waswahili wenyewe kwa kutengenezewa kanuni
371 mpya na wageni. Sehemu moja ya kumbukumbu hiyo ilisema hivi:-
373 "Tumesanifisha Kiswahili, na katika shughuli za kufanya hivyo
374 yaonekana Kiswahili kimekuwa lugha mpya. Bila shaka sote tunakiri
375 kwamba kama lugha zingine Kiswahili kitaendelea na kitapanuka
379 katika nyanja za muundo, semi na msamiati kwa kuathiriwa na
380 ustaarabu wa walowezi. Lakini maendeleo hayo yafaa yatokane na
381 mawazo ya Waswahili; haifai kuwalazimisha kuyapokea. Lakini
382 hivyo ndivyo ilivyo; tuko katika harakati za kuwafunza Waswahili
383 Iugha yao kupitia vitabuni, vingi ambavyo si vya Kiswahili kimuundo
384 au kimawazo, na ambavyo lugha yake inafanana kidogo sana na
385 lugha inayozungumzwa. Labda tuna haraka sana kuhepa ukweli
386 kwamba Waswahili wenyewe wana uwezo wa kurekebisha lugha yao
387 kufaa mahitaji ya siku hizi na kwamba tayari wanafanya hivyo kwa
388 haraka ya kustaajabisha. Hivi ndivyo hali ilivyo huko Mombasa na
389 inaweza kudhihirishwa na wachunguzi wengi. Jambo muhimu sana
390 ni kwamba jitihada zetu hizi za kupata mwana haramu huyu,
391 Kiswahili cha Kiingereza, zina matokeo ya kututenganisha na jamii
392 tunaojaribu kuelimisha. Au tukieleza kwa maneno mengi, tunafikiria
393 kwa Kiingereza hadi wao wanafikiria kwa Kiswahili na hatuwezi
394 kuziba pengo hili." (I.L.C. Bulletin Na. 7 1934: 4).
396 Mwandishi anafikiri kwamba sifa nyingi zisizo na kifani zilitolewa
397 kuwasifu wachunguzi wakuu wa Kiswahili kama vile Krapf, Steere,
398 Sacleux, Taylor, Veltten na Beech bila ya kujali kazi zao ambazo
399 zingetumiwa shuleni. Anafikiri kwamba kamati ilikuwa na haraka sana ya
400 kuandika vitabu na kutafsiri vingine na kwamba katika kufanya hivyo
401 wakaguzi wasiokuwa na ujuzi waliajiriwa. Anaendelea kusema kwamba
402 wale wanaoitetea hii lugha mpya wanasema kwamba ndiyo ya pekee
403 inayoweza kueleweka na makabila yasiyokuwa ya Waswahili. Anakanusha
404 wazo hili kwa kusema kwamba ni rahisi kwa Waafrika kujifunza Kiswahili
405 kuliko Kiswahili hiki kilichochanganywa na muundo wa Kiingereza.
407 Ili kuthibitisha kwamba Waswahili walipinga mtindo huu mpya wa
408 Kiswahili na othografia yake, mwandishi wa "Kiswahili cha Kisasa"
409 aliambatisha makala kutoka gazeti la 'Al-lslah' la Mombasa. Makala hiyo
410 ilikuwa ya Juni 20, 1932 ambayo mwandishi aliishambulia othografia
411 mpya ya Kiswhili. Othografia iliyokubaliwa kama tulivyoeleza haikuwa
412 na baadhi ya herufi kama vile kh inayopatikana tu katika maneno
413 yaliyoazimwa kutoka kwa Kiarabu. Othografia iliyokubaliwa ingekuwa
414 na h badala ya kh na hii ni mojawapo ya sababu zilizomfanya mwandishi
415 wa makala ya Al-lslah alalamike. Makala hiyo inasema hivi:
417 "Ni madhara makubwa tupatayo kwa Kiswahili hiki kilichoharibiwa
418 ni Wazungu. Kiswahili ni lugha ya watu wa Pwani, nacho hakiwi safi
419 ella kitanganyikapo na Kiarabu. Tangu kufika Wazungu, wame-
420 kigeuza na kukiharibu kwa wapendavyo wao; wamepunguza baadhi
424 ya harufu ambazo ni lazima ziwemo katika baadhi ya maneno, na
425 pengine hubadilika maana kwa kukosekana harufu hizo. Wameitungia
426 vitabu vya nahau, na pengine hao watungao vitabu hivyo ni
427 Wazungu wageni hawajui sana lugha hii, na ambao wavitowa
428 makosa ni Wazungu wa bara, wasiojuwa Kiswahili. Na wakiambiwa
429 ni mtu wa Pwani kuwa ni makosa, hawakubali ella kile kile chao ..."
430 (I.L.C. Bulletin Na. 7, 1934: 8).
432 Mwandishi wa "Kiswahili cha Kisasa" anaendelea kutilia nguvu mambo
433 aliyoyataja kwa kusema kwamba baadhi ya vitabu vilivyochapishwa hivi
434 karibuni vilikuwa tafsiri ya neno kwa neno ya vitabu vya Kiingereza.
435 Anasema kwamba matumizi ya kanuni za sarufi yalikuwa yakihimishwa
436 sana jambo ambalo lilifanya vitabu vilivyochapishwa kuwa sahihi kisarufi,
437 lakini vilikuwa mbali sana na Kiswahili halisi kwa kuwa sarufi peke yake
438 haiundi lugha. Anataja upungufu mkubwa wa Kiswahili "kipya". Upungu-
439 fu huo ni, tafsiri ya neno kwa neno, kuzingatia matumizi ya kanuni za
440 sarufi bila ya kujali methali na semi pamoja na kutojali tabia ya kishairi ya
441 Kiswahili. Mwishowe anatoa mifano ya sentensi ambazo zina upungufu
442 kutokana na vitabu vilivyoandikwa kwa Kiswahili sanifu vilivyokuwa
443 vikitumika shuleni wakati huo.
445 Katika jarida hilo hilo la Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki,
446 kufuatia makala hiyo ya "Kiswahili cha Kisasa" kuna jibu lake lililo-
447 andikwa na Kasisi Canon Broomfield mwandishi wa kitabu kijulikanacho
448 kama Sarufi ya Kiswahili, ambaye kwa wakati huo alikuwa mhariri
449 kutoka Zanzibar. Canon Broomfield alikuwa ameombwa na katibu wa
450 Kamati kumjibu mwandishi wa "Kiswahili cha Kisasa" kwa manufaa ya
453 Katika jibu lake Canon Broomfield anaonelea kwamba mwandishi wa
454 "Kiswahili cha Kisasa" ametia chumvi suala la kugeuka kwa Kiswahili
455 kuwa lugha mpya. Anasema kwamba marekebisho yaliyokuwa yakitokea
456 yalikuwa hayana budi kuwepo kwa kuwa lahaja moja ndiyo ilichaguliwa
457 kuwa msingi wa kusanifisha Kiswahili. Kwa hiyo marekebisho yalifanywa
458 ili kusaidia kutumiwa kwa lahaja hiyo kama lugha ya mawasiliano kote.
459 Usanifishaji ulihitaji kusomesha Kiswahili hicho ambacho chaonekana
460 kuwa kipwa. Anaeleza zaidi kwamba Kiswahili sanifu chaonekana kuwa
461 lugha mpya zaidi katika lahaja zinazotofautiana sana na Kiunguja,
462 ambacho ndicho msingi wa usanifishaji.
464 Kuhusu athari za Kiingereza katika Kiswahili, Broomfield anaeleza
465 kwamba hilo ni jambo lisiloweza kuepukika kwa sababu lugha mbili
466 zinapotumika katika eneo moja hazina budi kuathiriana na haziwezi
467 kubaki kuwa safi, pia matokeo ya kuazima huenda yakatajirisha lugha
471 inayoazima. Anatoa mifano ya semi za Kiebrania zilizoingia katika
472 Kiingereza kupitia tafsiri ya Biblia. Sasa semi hizo zimekuwa Kiingereza.
473 Anatetea kile kinachoonekana kama tafsiri za neno kwa neno au tafsiri za
474 semi za Kiingereza kwa kusema kwamba Kiingereza kinaathiri Kiswahili
475 cha mazungumzo cha Waafrika wanaozijua lugha zote mbili. Anasema
476 kwamba mabadiliko kama hayo ni ya kawaida kwa kuwa lugha hubadilika
477 kila mara na kwamba Kiswahili cha wakati huo hakikuwa sawa na
478 Kiswahili cha wakati wa Krapf. Haoni kama Kiswahili kinaweza kujiepu-
479 sha na kuazima kwa istilahi za ufundi na teknolojia. Broomfield anaandika
482 "Maendeleo yoyote ya kielimu huhitaji kuwa na mabadiliko na
483 maendeleo ya lugha itakayotumika kueleza elimu hiyo. Tupende
484 tusipende, Kiswahili kitabadilika na kuendelea kwa haraka, kwa
485 sababu hizi. Katika wakati huu kuna maandishi machache sana na
486 tunaanza kusanifisha lugha hii, pia Waafrika wanaojua kusoma na
487 kaundika ni wachache sana. Tena Afrika inawasiliana na ustaarabu
488 wa Uropa; elimu mpya na utaalamu mpya wa kila aina unawafikia
489 Waafrika. Kiswahili cha miaka ishirini tu iliyopita hakifai siku hizi.
490 Ni lazima lugha ibadilike na itabadilika, tupende tusipende..."
491 (Broomfield I.L.C. Bulletin Na 7, 1934: 4).
493 Njia za kukuza lugha zitakuwa ni pamoja na kuazima maneno kutoka
494 lugha za kigeni hasa Kiingereza na kuunda maneno mapya. Broomfield
495 anaonya kwamba lazima watu wajifunze maneno hayo na vile yanavyo-
496 tumika. Anatoa mfano wa maneno kumi na tisa (19) yaliyoundwa
497 kutokana na neno vote aliloliazima kutoka kwa Kiingereza, ambayo
498 anasema, kwamba yanaweza kueleweka vizuri baada ya kujifunza maana
501 Broomfield anasema kwamba mwandishi wa kumbukumbu hakuzi-
502 shughulikia lahaja tofauti za Kiswahili ambazo zatofautiana kimsamiati,
503 kimatamshi, sarufi na semi ambazo zaifanya kazi ya wahariri wa Kamati
504 ya Kiswahili ya Afrika Mashariki kuwa ngumu. Anasema kwamba
505 wahariri hawatarajiwi kuandika upya miswada wanayopelekewa. Anaeleza
506 kwamba, Kiunguja kinapotumiwa kama msingi wa usanifishaji jitihada
507 zinafanywa kuzihusisha lahaja zingine kwa kuwa lahaja zote kubwa
508 zitakichangia Kiswahili katika siku za baadaye.
510 Broomfield anakanusha madai ya mwandishi wa kumbukumbu kwamba
511 kuna chochote katika kazi za Meinhof, Werner, Madan, Torrend,
512 Domet, Stigand na kadhalika ambacho chaweza kufaa shuleni.
514 "Yako wapi maandishi hayo; je, twapata chochote kinachoweza
515 kutumika kama vitabu vya shule vya jiografia, historia, hesabu,
519 afya, elimu ya viumbe, kilimo au uraia? Mbali na uchunguzi wa
520 kiisimu unaokusudiwa kusomwa na Wazungu, maandishi mengine
521 mengi, zaidi ni mkusanyiko wa mila, ngano na hadithi. Nyingi kati
522 ya hizi ni za lugha isiyo na adabu na nyingi hazina umuhimu wowote
523 wa kielimu." (Broomfield, I.L.C. Bulletin Na. 7, 1934: 19).
525 Anakiri kwamba uandishi wa vitabu umefanywa kwa haraka na
526 kwamba baadhi ya vitabu hivyo havikosi upungufu lakini kuchaguliwa
527 kwa Kiswahili na kule kupenda kwa nchi zote za Afrika Mashariki
528 kutumia Kiswahili wastani kumesabibisha hali kuwa hivyo. Wale walio-
529 andika vitabu walifanya hivyo kwa sababu hapo awali hakukuwa na
530 vitabu kama hivyo na ni juu ya wale wanaotoa lawama kuandika vitabu
533 Mwisho kabisa Broomfield anataja kwamba kusanifisha na kuunganisha
534 lugha ni kazi ngumu sana na kwamba wale wanaoishughulikia hawata-
535 pendwa. Makala iliyoandikwa katika gazeti la Al-Islah imeandikwa kwa
536 Kimvita na wale ambao hawatumii lahaja hiyo hawataisifu kamwe. Pia
537 Broomfield anasema kwamba, katibu wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika
538 Mashariki alijibu makala ya Al-Islah lakini gazeti hilo halikuichapisha.
540 Huko kuonekana kwa Kiswahili kuwa ni lugha ngeni kwa sababu ya
541 kutafsiri wakati wa usanifishaji, kwa maoni yangu, hakungeepukika. Hiyo
542 ilikuwa deni ambayo ilibidi Kiswahili kilipe kwa maendeleo yake ya
543 haraka. Kiswahili ambacho hapo awali kilikuwa tu lugha ya biashara,
544 kilianza kutumika kwa haraka kama lugha ya elimu siyo tu Uswahilini bali
545 kote katika Afrika Mashariki. Kwa hivyo Kiswahili hakikuwa tena lugha
546 ya Waswahili tu kama vile mwandishi wa "Kiswahili cha Kisasa"
547 alivyosema bali kilikuwa lugha ya halaiki kubwa ya watu wa Afrika
548 Mashariki nzima. Ili kukiwezesha Kiswahili kiumudu wadhifa huo, ilibidi
549 vitabu vitayarishwe kwa muda mfupi. Siku hizo hakukuwa na Waafrika
550 wa kutosha ambao wangeweza ama kuandika vitabu vilivyohitajika au
551 kutafsiri vya Kiingereza kwa Kiswahili.
553 Maoni kwamba Kiswahili kilikuwa kikichafuliwa kwa kusanifishwa na
554 kwa kutumiwa kwa kuandikia na kutafsiria vitabu vya shule hayakuwa
555 Kenya pekee. Nchini Zanzibar, kilikotoka Kiunguja, kulikuwa na hofu
556 kwamba lahaja ya Kiunguja itachafuliwa na jitihada za usanifishaji.
557 Akitoa ripoti yake kuhusu vitabu vya shule ya mwaka 1927, Mkaguzi wa
558 Shule wa Zanzibar, Bwana G. B. Johnson alieleza masikitiko yake
559 kwamba ni sharti vitabu vinavyotumiwa Zanzibar vikubalike huko
560 Tanganyika. Alisema kwamba ni sharti vitabu hivyo viwe vya "Kiswahili
561 kilichorekebishwa kuambatana na maagizo ya Kamati ya Uchapishaji ya
562 Tanganyika". Ilibidi vitabu vya Zanzibar vikubalike Tanganyika kwa
566 sababu Zanzibar ilikuwa ikihitaji vitabu vichache sana na gharama ya
567 kuchapisha vitabu vya shule za Zanzibar pekee ilikuwa kubwa.
569 Zanzibar ilifurahia uamuzi wa kutumiwa kwa Kiunguja kuwa msingi wa
570 kusanifisha Kiswahili. Lakini kulikuwa na hofu kwamba ingewabidi
571 Wazanzibari kutumia maneno na miundo kutoka Tanganyika. Jambo hili
572 liliwakera sana kama inavyodhihirishwa na maneno ya Johnson.
574 "Yaonekana wazi kwamba hatimaye Zanzibar italazimika kutumia
575 vitabu vya shule vilivyoandikwa kwa lugha yao iliyochafuliwa. Hili
576 ni jambo la kusikitisha hata ingawa yaonekana haliepukiki. Hii ni
577 gharama kubwa ya kulipa dhidi ya usanifishaji wa Kiswahili. Watu
578 wa Zanzibar wanaojiona kwamba wanakitumia Kiswahili safi
579 wanachukizwa na kutumiwa kwa Kiswahili cha bara ambacho kwao
580 wanakiona kwamba ni lugha iliyoharibiwa. Kuhakikisha kwamba
581 shule zetu zinatumia Kiswahili sanifu kutakuwa kazi ngumu isiyo-
582 pendeza na itachukua muda kabla matumizi ya bara hayajakuba-
585 Kutumiwa kwa Kiswahili kama lugha ya vitabu vya shule kulikuwa ni
586 matumizi mapya ya lugha hiyo. Lugha ya vitabu vya shule ni tofauti na
587 lugha ya mazungumzo. Katika Kiswahili, tofauti hiyo ilionekana kuwa
588 kubwa sana kwa sababu ya maendeleo ya haraka yaliyochukua muda
589 mfupi na kwa kuwa Waafrika hawakutumiwa kuyatekeleza maendeleo
590 hayo. Jambo muhimu lililosababisha masikitiko ni kule kutumika shuleni
591 kwa vitabu vilivyotafsiriwa vibaya vikiwa na ithibati ya Kamati ya
592 Kiswahili ya Afrika Mashariki. Matumizi ya semi na miundo ya Kiingereza
593 katika vitabu hivyo vilivyotafsiriwa neno kwa neno hayakukanushwa na
594 Broomfield kama nilivyotaja. Baadhi ya wanakamati pia waliyapigia
595 makelele matumizi hayo.
597 Alipokuwa akiandika kuhusu siku hizo za mwanzo wa usanifishaji wa
598 Kiswahili, Snoxall anatukumbusha kwamba kulikuwa na vitabu vichache
599 sana na kwamba kamati ilitegemea sana tafsiri za Kiingereza zilizokuwa
600 zikitafsiriwa na wanakamati wenyewe. Vitabu vya waandishi kama vile
601 Rivers-Smith, Mkurugenzi wa Elimu Tanganyika, vilifaa sana. Snoxall
602 anasema kwamba baadhi ya tafsiri hizo zilikuwa za neno kwa neno na
603 anashangaa iwapo wanafunzi walizielewa. (Snoxall 1982: 3) 22*.
606 21* Zanzibar Protectorate Administrative Reports for the Year 1927 - Iliyochapishwa 1928.
607 Sehemu iliyonakiliwa inagusia mkutano wa Mombasa wa 1928.
608 22* Mfano mmoja ambao Snoxall anaukumbuka sana kutoka kitabu cha Uraia ambacho
609 kilikuwa tafsiri ya A Manual of Citizenship na Rivers-Smith ni: "Watu wa Taifa hilo
610 wamekwisha panda kipawa kingine katika ngazi ya ustaarabu". Wanafunzi walitaka kujua ni
611 nini "Ngazi ya ustaarabu" na ilikuwa wapi?
617 3.0 Miaka ya mwanzo ya usanifishaji
621 Kipindi cha kuanzia 1930 hadi 1938 kilikuwa muhimu sana kwa historia
622 ya usanifishaji wa Kiswahili.
624 Katika kipindi hicho, msingi imara sana uliwekwa na kukaanzishwa
625 kiwango cha juu cha kufanya kazi. Kamati ya Kiswahili ya Afrika
626 Mashariki ilihitaji msingi imara hivyo ili kuiwezesha kufanya kazi wakati
627 wa vita. Sifa nyingi za mafanikio ya Kamati zatokana na kazi nyingi na ya
628 kuchosha iliyofanywa na Frederick Johnson aliyekuwa katibu wa kwanza
629 wa Kamati hiyo. Mbali na kutafsiri vitabu vingi, Johnson alifanya kazi
630 nyingi ya kutunga kamusi za Kiswahili-Kiswahili, Kiswahili-Kiingereza na
631 Kiingereza-Kiswahili.
633 Nitaanza sehemu hii kwa kujadili hali nzuri ya wakati huo iliyoisadia
634 kamati kufanikiwa. Hasa sera ya lugha ya nchi za Afrika Mashariki wakati
635 huo, iliwataka maafisa waliozifanyia kazi nchi hizo, wapite mitihani ya
636 lazima ya Kiswahili. Kisha tutaijadili kazi yenyewe ambayo Kamati
639 Serikali zote za Afrika Mashariki, Kenya, Uganda, Tanganyika na
640 Zanzibar ziliunga mkono Kamati kwa kuwa zote ziliwakilishwa katika
641 Kamati. Sera ya lugha za nchi zote zilikisaidia Kiswahili kama tutakavyo-
642 endelea kufafanua. Wafanyakazi Wazungu wa nchi hizi zote ilibidi
643 wajifunze Kiswahili na waipite mitihani. Walioshindwa kufauli mitihani
644 hiyo walibaki kuwa wafanyakazi wa muda wala si wa kudumu. Kwa hivyo
645 iliwabidi maafisa wa serikali Wazungu wajifunze Kiswahili. lli kupandi-
646 shwa cheo kazini iliwabidi wapite mitihani ya juu ya Kiswahili. Sera hii
647 ilikipa Kiswahili hadhi. Mitihani hiyo ya Kiswahili ilisababisha mahitaji
648 ya kuchapisha vitabu vitakavyowasaidia maafisa hao kujitayarisha kufanya
649 mitihani hiyo. Pia vitabu hivyo vilinunuliwa kwa wingi kwa kuwa maafisa
650 hao walitamani kupita mitihani ili wazihifadhi kazi zao. Kwa hivyo
651 mitihani hiyo ilisaidia kukuza na kueneza Kiswahili pamoja na kuongeza
652 idadi ya vitabu vilivyochapishwa wakati huo. Sasa tutajadili vile sera ya
653 lugha ilivyokuwa katika kila nchi. 23*
656 23* Maagizo haya yapatikana katika kitabu cha Ratcliffe na Elphinstone kiitwacho Modern
657 Swahili 1932: 295-310.
661 Nchini Kenya, kulingana na barua ya Katibu Mkuu namba 40 ya Juni, 1,
662 1931, mbali na mitihani ya Wazungu waliokuwa wafanyakazi wa Jeshi la
663 King's African Rifles ambayo ilikuwa na maagizo yake tofauti, maafisa
664 wengine wote Wazungu waliokuwa wakifanya kazi katika Koloni iliwabidi
665 wafanye mitihani ifuatayo ambayo ilikuwa ya lazima.
667 Mtihani uliotangulia ulikuwa, mtihani wa kwanza wa mahojiano kwa
668 Kiswahili ambao ilibidi ufanywe kabla ya mwaka mmoja kwisha tangu
669 kuajiriwa kwa kazi isiyokuwa ya kibarua. Iwapo afisa aliyehusika
670 hangepita mtihani huo ilimaanisha kwamba hangepata nyongeza ya
671 mshahara ya kila mwaka na pia ingesababisha kushushwa cheo na kuwa
672 mfanyakazi wa kibarua. Kiwango cha Kiswahili kilichohitajika ni cha
673 kumwezesha afisa huyo kufanya kazi kwa kutumia Kiswahili pasipo
674 mahitaji ya mkalimani.
676 Mtihani wa pili ulikuwa wa Kiswahili sanifu kiwango cha chini. Mtihani
677 huu ulitahiniwa baada ya mwaka mmoja kwisha na kabla ya miaka miwili
678 na nusu kwisha tangu afisa aajiriwe. Wale ambao hawakupita mtihani huo
679 walichukuliwa hatua sawa na wale ambao hawakupita mtihani wa
680 kwanza. Ili mtu aweze kupita mtihani huo ilibidi awe amefikia kiwango
681 cha kuelewa na kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha na ujasiri.
683 Mtihani wa Kiswahili sanifu kiwango cha juu ndio uliokuwa wa tatu na
684 wa juu sana kati ya hiyo mitihani ya lazima. Mtihani huo ulikuwa wa
685 mahojiano pamoja na wa kuandika. Ulikuwa wa Wazungu wenye vyeo
686 vikubwa na ulifanywa baada ya miaka mitatu na kabla miaka kumi
687 haijakwisha tangu waajiriwe. Kukosa kupita mtihani huo kwa muda
688 uliowekwa kuliathiri cheo cha afisa aliyehusika na kumaanisha kwamba
689 hangeendelea kupewa nyongeza za mshahara. Ili mtu aweze kupita
690 mtihani huo ilibidi aijue vizuri sarufi ya Kiswahili na aweze kuzungumza
691 Kiswahili kwa ufasaha.
693 Maagizo yaliyoihusu Uganda yapatikana katika tangazo la barua
694 namba 40 ya Disemba 29, 1928 kutoka afisini mwa Katibu Mkuu.
695 Maagizo hayo ni sawa na ya Kenya isipokuwa kwamba kuna tofauti
696 chache nitakazoeleza. Kuhusu mtihani wa kiwango cha kwanza wa
697 mahojiano, maafisa waliokuwa wakifanya kazi Buganda, waliruhusiwa
698 kufanya mtihani wa Kiluganda kwa kiwango hicho, lakini maafisa
699 waliokuwa wakifanya kazi katika sehemu zingine za Uganda ilibidi
700 wafanye mtihani wa Kiswahili.
702 Maafisa waliokuwa wakifanya kazi katika tawala za mikoa na wa Idara
703 ya Elimu ilibidi wapite mtihani wa Kiswahili sanifu, kiwango cha chini
704 kabla hawajathibitishwa kazini. Maafisa wengine wote wangethibitishwa
705 kabla hawajapita mtihani huo, lakini baada ya kufanya kazi kwa muda wa
706 miaka minne hawangepata tena nyongeza ya mshahara mpaka kwanza
712 Mtihani wa Kiswahili sanifu, kiwango cha juu nchini Uganda ulikuwa
713 ukifanywa na maafisa wa tawala za mikoa, na idara za elimu, kilimo,
714 mifugo, misitu na polisi. Maafisa wote wa idara hizi ilibidi wapite mtihani
715 huo, la sivyo, mshahara wao haungezidi pauni 720. Nchini Uganda,
716 maafisa wa serikali wangefanya mitihani ya kiwango cha chini na cha juu
717 ya lugaha zingine za Uganda badala ya Kiswahili.
719 Nchini Zanzibar, dondoo kutoka maagizo ya serikali ya Zanzibar
720 yanaeleza kwamba ni lazima maafisa wote wa Kizungu wapite mtihani wa
721 Kiswahili sanifu, kiwango cha chini kabla mwaka mmoja haujakwisha
722 tangu waingie nchini. Wale ambao hawangepita mtihani huo ama
723 hawangeendelea kuwa waajiriwa wa kudumu au hawangepata nyongeza
724 ya mshahara ya kila mwaka. Wauguzi ambao hawangepita mtihani huo,
725 ingebidi wasimamishwe kazi.
727 Wale waliokuwa wakifanya mtihani wa Kiswahili sanifu kiwango cha
728 juu walikuwa maafisa Wazungu ambao walikuwa wafanyakazi wa
729 kudumu. Baada ya kupita mtihani huo walipewa kiinua mgongo cha pauni
730 hamsini (50). Mbali ya huu mtihani wa Kiswahili kiwango cha juu
731 maafisa Wazungu wa Zanzibar walikuwa huru kufanya mtihani wa
732 Kiarabu au Kigujerati wa kiwango hicho. Watahiniwa wa mtihani wa
733 kiwango cha juu wa Kiswahili, Kiarabu au Kigujerati ilibidi waweke
734 amana ya rupia arobaini na tano (45), pesa ambazo wangerudishwa
737 Maagizo yaliyoihusu Tanganyika yapatikana katika 'Maagizo kwa
738 watu wote kutoka Afisi ya Katibu Mkuu, Dar es Salaam, Juni 15, 1931'.
739 Kulingana na Maagizo hayo ilibidi maafisa wa Kizungu wapite mtihani wa
740 Kiswahili sanifu, kiwango cha chini kabla mwaka mmoja haujakwisha
741 tangu waajiriwe nchini. Wale ambao hawangepita mtihani huo hawa-
742 ngeendelea kuwa waajiriwa wa kudumu.
744 Mtihani wa Kiswahili sanifu, kiwango cha juu ulikuwa ukitahini ujuzi
745 kamili wa Kiswahili, sarufi na muundo wa lugha kwa jumla. Watahiniwa
746 waliofaulu walitakikana waweze kueleza maagizo, sheria na kanuni za
747 serikali vizuri kwa Kiswahili. Pia walitakikana waweze kutafsiri kwa
748 ufasaha maandishi ya Kiswahili kwa Kiingereza na ya Kiingereza kwa
751 Maagizo haya yote yaonyesha wazi kwamba sera ya lugha katika Afrika
752 Mashariki wakati wa ukoloni ilikiunga Kiswahili mkono hasa wakati huo
753 wa siku za mwanzo za Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Sera hiyo
754 ilikusudiwa kuwawezesha Wazungu kuwaelewa Waafrika wanapofanya
755 kazi zao. Sera hii iliwaridhisha wanakamati ambao walijivunia kazi zao
756 kwa kuona kwamba zilitambuliwa na serikali. Juhudi za Kamati ya
760 Kiswahili ya Afrika Mashariki hazikuzinufaisha shule tu, bali ziliwafaidi
761 maafisa wa Kizungu ambao ilibidi wajitayarishe kufanya mitihani hiyo ya
762 lazima. Ufafanuzi huu unatusaidia kuelewa ni sababu gani iliyowafanya
763 wanakamati wawe na moyo thabiti wa kufanya kazi nyingi ngumu ya
764 kusanifisha Kiswahili kwa kujitolea.
766 Sasa tutaigeukia "warsha" ili tuone machache kati ya mambo muhimu
767 yaliyokuwa yakifanywa na Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
768 kabla ya vita vya pili vya dunia.
770 Kwa kifupi kazi nyingi na ngumu ilifanywa na maafisa wa serikali na
771 misheni kutoka Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar waliojitolea
772 kusanifisha Kiswahili. Hawakuwa na vitabu vya kutosha vya Kiswahili
773 ambavyo wangetegemea kuwasaidia katika kazi zao. Mjadala mfupi
774 unaofuata watokana na Jarida la Kamati - ILC Bulletin Na. 1 ya 1930.
775 Waonyesha baadhi ya matatizo yaliyoikumba Kamati.
777 Kabla ya kufikia uamuzi kuhusu msamiati sanifu, orodha za maneno
778 zilipelekewa wahariri wa Kamati pamoja na kuchapishwa kwenye Jarida
779 la ILC Bulletin ili kuwapa wahariri pamoja na raia nafasi ya kuyajadili.
780 Maoni na mapendekezo tofauti yalijadiliwa na Kamati kabla orodha
781 iliyokubaliwa haijachapishwa kama msamiati sanifu. Maoni na mapende-
782 kezo yaliyotolewa na wahariri kabla uamuzi haujafikiwa yalitofautiana
783 sana kama inavyodhihirishwa hapa chini.
785 Kasisi B. J. Ratcliffe, mhariri wa Kenya, anapendekeza kwamba 'irabu' na
786 'herufi' zitumiwe badala ya kuazima 'vokali' na 'konsonanti' kutoka Kiingere-
787 za. 'Herufi' ilipendekezwa badala ya 'harufu' ambalo lilikuwa likitumiwa
788 kwa wingi na Waswahili wa Mombasa ili kulitofautisha na neno harufu la
791 Naye katibu wa Kamati, Frederick Johnson anashuku iwapo neno irabu
792 latumiwa na watu wengi au latumiwa na Waswahili wachache wanaoandika
793 kwa kutumia hati za Kiarabu. Kwa maoni ya Johnson neno herufi au
794 harufu lilimaanisha hati yoyote ya maandishi iwe vokali au konsonanti.
795 Kisha anafikia uamuzi kwamba neno lenye kumaanisha konsonanti
796 lilikuwa lahitajika. Hivyo ndivyo neno konsonanti lilivyoazimwa.
798 Mengi kati ya maneno tunayoyaona kuwa ya kawaida siku hizi, ilibidi
799 yatolewe uamuzi. Mfano mmoja ni neno shule. Kasisi A. B. Hellier,
800 mhariri wa Tanganyika alipendekeza neno shule lililoazimwa kutoka
801 Kijerumani badala ya neno skuli lililoazimwa kutoka lugha ya Kiingereza.
802 Naye Canon Broomfield alikuwa na maoni kwamba maneno yote mawili
803 yangetumiwa kumaanisha vituo tofauti vya elimu. Broomfield aliyekuwa
804 mhariri wa Zanzibar alipendekeza neno skuli litumiwe kumaanisha vituo
805 na vyuo vya kufunzia walimu nalo neno shule limaanishe shule za vijijini
810 Maoni yalitofautiana sana hivi kwamba inashangaza iliwezekanaje
811 kamati ikaweza kutimiza mambo mengi hivyo. Tukitazama mifano ya
812 maneno lindi na kina, twaona kwamba wahariri wote wanne walikuwa na
815 Bwana Morris, mhariri wa Uganda alipendekeza kwamba neno lindi
816 litumiwe badala ya kina. Kasisi Ratcliffe wa Kenya alisema kwamba neno
817 sahihi ingekuwa kwina wala si kina. Canon Broomfield kutoka Zanzibar
818 alisema kwamba neno kimo lilitumiwa kumaanisha urefu wa kwenda juu
819 na wa kwenda chini, na kwamba neno kina lilikuwa halijulikani Zanzibar.
820 Naye Kasisi Hellier alijaribu kutoa suluhisho kwa kusema kwamba
821 "tukitumia kimo kumaanisha kwenda juu na kina kumaanisha kwenda
822 chini tutakuwa tumepiga hatua mbele" (ILC Bulletin Na. 1 1930: 5).
824 Baada ya kusoma aya za hapo juu mtu anaweza kushawishiwa kushuku
825 ujuzi wa kamati na wahariri wake. Maoni kama hayo yangekuwa ya
826 haraka na yasiyo ya kweli kwa sababu watu hao walikuwa wakishughulikia
827 karibu kila kitu, kuanzia maneno ya kawaida ya kila siku ambayo
828 yalihitajika hadi sarufi ya Kiswahili. Wewe unayesoma kitabu hiki, jihisi u
829 mmoja kati ya wanakamati, naye Kasisi A. B. Hillier anakufahamisha
830 kama alivyoifahamisha Kamati kwamba:
832 "Sarafu za senti hamsini, senti kumi, na senti tano kwa sasa hazina
833 majina. Ni muhimu zipewe majina ya kutumiwa shuleni na ya
834 kutumiwa na umma." (ILC Bulletin Na. 1, 1930: 10).
836 Je, kama mwanakamati ungetoa mapendekezo gani, hasa unapojua
837 kwamba baadhi ya wasemaji wa Kiswahili walikuwa wakitumia maneno
838 mengi kama vile "peni la senti kumi" na "peni la senti tano"? Maneno nusu
839 shilingi kumaanisha senti hamsini, peni kumaanisha senti kumi na nusu
840 peni kumaanisha senti tano yalikuwa ni afadhali kuliko deka na pente
841 kutoka Kigiriki na ashara na hamsa kutoka Kiarabu ambayo yalipendeke-
842 zwa kumaanisha senti kumi na senti tano.
844 Maelezo ya hapo juu yanaonyesha baadhi ya shida zilizowakumba
845 wasanifishaji wa Kiswahili mapema katika shughuli za usanifishaji.
846 Kufanikiwa kwao kulitokana na jitihada za pamoja za misheni wa
847 madhehebu mbalimbali pamoja na msaada na ushirikiano wa serikali za
848 kikoloni za Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar.
850 Mashauriano mengine mengi kama hayo yaliyojadiliwa hapo juu
851 yalifanywa na matokeo yake yalikuwa ni kusanifishwa kwa maneno mengi
852 ya Kiswahili. Kamati ilitoa orodha za maneno ya Kiswahili, ikayajadili,
853 kisha ikachapisha yale yaliyokubaliwa kama Kiswahili sanifu. Katika
854 jarida la ILC Bulletin Na. 9 la Oktoba 1935, Kamati inajadili orodha ya
855 maneno ya Kiswahili yenye asili ya Kibantu na kutoa maelezo ya chanzo
859 chake. Orodha hiyo inayo maneno kama vile kanzu, shamba na kizibao.
860 Katika Jarida hilo Johnson pia anajadili chanzo cha baadhi ya maneno
861 naye Kasisi Hellier anayo orodha ya msamiati anaoupendekeza wa vipimo
864 Katika Jarida la mwaka uliofuata, I.L.C. Bulletin Na. 10 ya 1936
865 kumbukumbu tatu za J. W. T. Allen, Broomfield na F. Johnson
866 zimechapishwa. Kumbukumbu hizo ni maoni ya Kamati kumjibu Clement
867 M. Doke aliyetoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kugawanya maneno
868 katika kitabu cha Bantu Linguistic Terminology. Mapendekezo ya Doke
869 yangesababisha kuwe na maandishi ya maneno kama vile waSwahili,
870 muIngereza, mUngu, waDaudi na kwamtu badala ya Waswahili, Mwi-
871 ngereza, Mungu, wa Daudi na kwa mtu. Kamati ilikataa mapendekezo ya
872 Doke katika makala hayo na mengine yaliyochapishwa katika jarida
875 Masuala ya kisarufi pia yalijadiliwa na kuchapishwa katika jarida la
876 Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Kwa mfano matumizi ya KA
877 na KI yalijadiliwa na A. B. Hellier katika jarida la 1931 naye F. Johnson
878 alijadili kinyume cha kiambishi "kuto-" katika jarida la 1933. Katika
879 makala yake, Johnson anatoa rai kwamba neno kutoenda latokana na
880 maneno kutoa na kwenda. Naye mwanakamati Ronald Snoxall anapinga
881 maelezo ya Johnson na kumsahihisha kwa kueleza kwamba to katika neno
882 kutoenda ndicho kiungo cha kinyume.
884 Masuala mengine kuhusu kusanifishwa kwa Kiswahili yalishughulikiwa
885 na Kamati pia, na matokeo yake yakachapishwa kwenye jarida. Masuala
886 hayo yalikuwa ni pamoja na kutoa sababu za kutumiwa kwa irabu
887 zikifuatana kulikoelezwa na Broomfield mnamo 1931; kuhesabu katika
888 Kiswahili na A. B. Hellier 1932; alfabeti za Kiswahili na A. B. Hellier
889 1934; mjadala kuhusu alama za kuwakifisha; pamoja na kukadiriwa kwa
890 vitabu vya shule vya wakati huo, kulikofanywa na Kamati ya Kiswahili ya
893 Mnamo mwaka 1934 ilibidi Kamati ipime kazi yake. Jambo hili
894 lilisababishwa na kumbukumbu "Kiswahili cha Kisasa" iliyoandikwa na
895 afisa mmoja wa Idara ya Elimu, Kenya. Baada ya kuipokea kumbukumbu
896 hiyo, katibu alimuomba Broomfield aijibu. Kumbukumbu hiyo, majibu
897 yake, pamoja na dondoo la gazeti Al-Islah la Mombasa zilizochapishwa
898 katika Jarida, ILC Bulletin la 1934 tayari zimejadiliwa katika sura ya pili.
900 Baadhi ya makala zilirudiwa katika matoleo ya Jarida ya hapo mwanzo.
901 Kwa mfano, makala ya Snoxall kuhusu kitendo kutoa, ilichapishwa
902 katika Jarida namba 6 la 1933 na kurudiwa tena katika Jarida namba 8
905 Makala iliyojadilia suala la a mbili katika maandishi ya Kiswahili katika
909 Jarida namba 2 la 1931, ilichapishwa tena katika jarida Bulletin namba 6,
910 la 1933. Kuna sababu mbili za kuchapisha upya makala hayo. Sababu ya
911 kwanza ni kuwa ILC Bulletin lilikuwa jarida changa lililokuwa likitoa
912 nakala chache, na lilikuwa na wasomaji wachache na waandishi wa
913 makala za kuchapishwa hawakuwa wengi pia. 24* Inawezekana kwamba
914 watu ambao wangeandika makala ya kuchapishwa kwenye jarida walikuwa
915 na kazi nyingi ya kuandika na kutafsiri vitabu vya Kiswahili ili kutosheleza
916 mahitaji ya vitabu hivyo. Sababu ya pili ni kwamba matolea machache ya
917 kwanza hayakuchapishwa kama vitabu bali yalipigwa taipu na kutolewa
918 nakala. Jarida la kwanza lililochapishwa kama kitabu lilikuwa toleo
919 namba 6 la Oktoba 1933. Kupigwa chapa huko kulipoanza, ndipo baadhi
920 ya makala zilipoanza kuchapishwa upya ili ziweze kuwafikia wasomaji
923 Yale yaliyojadiliwa hapo juu ni baadhi ya mambo muhimu ya kupanga
924 lugha kitaaluma, ambayo hujulikana pia kama "uhandisi wa lugha",
925 uliofanywa na Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Jarida hali-
926 kuchapishwa katika mwaka 1937 kutokana na kifo cha Frederic Johnson
927 aliyekuwa katibu wa kwanza wa Kamati. Johnson alifariki akiwa Aden
928 mnamo mwezi Machi, 1937.
932 Wazungu wengi, baadhi yao wakiwa misheni waliondoka Afrika
933 Mashariki kwenda nchi zao mbalimbali za Ulaya kujiunga najeshi wakati
934 wa vita vya pili vya dunia. Kwa sababu hizo hizo na kwa kuwa ilikuwa
935 hatari kusafiri wakati wa vita, Wazungu wengi waliotarajiwa kujiunga na
936 misheni kadha hawakuwasili. Kulikuwa na ukosefu wa pesa kwa sababu
937 ya kugharamia vita. Wanafunzi wa Afrika Mashariki waliopevuka
938 pamoja na wengi wa walimu wao walijiunga na jeshi lililokuwa likilinda
939 Afrika Mashariki. Kwa sababu hiyo shuguli zote za kielimu zilififia kama
940 inavyodhihirishwa na maelezo yafuatayo ya Mkurugenzi wa Elimu,
943 "Mahitaji ya viongozi wa jeshi, ya Waafrika ambao walijua kusoma na
944 kuandika, yalikuwa mengi kama yalivyokuwa katika miaka ya vita
945 iliyotangulia. Idadi ya vijana walioacha shule za misheni na za
946 serikali kabla hawajamaliza masomo yao ilikuwa kubwa. Mshahara
947 mkubwa unaolipwa na jeshi pia umesababisha walimu wa Kiafrika
948 wengi wa shule za msingi kuacha kazi za kufundisha." 25*
951 24* Hapo mwanzo bila shaka nakala zilikuwa chache sana. Kufikia 1953 nakala zilizokuwa
952 zikichapishwa zilikuwa kati ya 500 na 600.
953 25* Kenya Education Department Annual Report 1942, Government Printer - Nairobi, (pia
954 tazama Lugumba na Ssekamwa 1973: 19).
958 Hali katika nchi zingine za Afrika Mashariki ilikuwa mbaya pia. Nchini
959 Uganda, kwa mfano, vijana wa kiskauti wa shule walitumiwa kusaidia
960 askari polisi katika kulinda mji mkuu Kampala. Baadhi ya shule, kama
961 vile shule ya kilimo ya Gulu ilibidi ifungwe baada ya Mzungu aliyekuwa
962 akiisimamia kuambiwa arudi kwao Ulaya. (Lugumba na Ssekamwa
965 Kuhusu Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Whiteley 1969,
966 anadai kwamba hakukuwa na kazi nyingi iliyofanywa na Kamati. Hata
967 hivyo maoni ya Whiteley yanapingwa vikali na mafanikio ya Kamati ya
970 Jarida la Kamati ILC Bulletin lilichapishwa kila mwaka wakati wa vita,
971 vitabu vingi vilichapishwa, miswada ilipokewa na kushughulikiwa, ku-
972 likuwa na mashindano ya uandishi wa Kiswahili na vitabu kadha
973 vilitafsiriwa. Pia jitihada zilifanywa kukisanifisha Kiswahili cha Zaire ili
974 kiwe sawa na Kiswahili cha Afrika Mashariki. Baadhi ya mikutano ya
975 Kamati haikuweza kuitishwa wakati wa vita na bila shaka kama haku-
976 ngekuwa na vita Kamati ingefanikiwa zaidi kati ya 1939 na 1945. Maelezo
977 yafuatayo yanaonyesha kwamba hatuwezi kudunisha mafanikio ya Kamati
978 katika miaka hiyo ya hatari.
980 Jarida la lLC Bulletin Na. 13 la 1959 linatoa orodha ya maneno na
981 mapendekezo ya matumizi yake ili wasomaji wa jarida watoe maoni yao.
982 Ni muhimu kutaja kwamba kamati inapendekeza majina kama vile kabila,
983 chupa na jumba yatumiwe katika ngeli za 9/10 (Ngeli ya N, kwa mfano:
984 Kabila hii badala ya kabila hili). Kamati ilifikiria kwamba, endapo majina
985 hayo yangetumiwa kama majina ya ngeli za 5/6 JI-MA), yangevuja sifa ya
986 maana kwa kuleta hisia mbaya hivi kwamba neno makabila lingeleta
987 maana ya ushenzi, hali neno majumba lingeonyesha maana ya nyumba
988 kubwa zisizo na umbo zuri lililolingana.
990 Katika maelezo hayo kamati ilitilia maanani sana uwezo wa ngeli za 5/6
991 wa kuleta hisia mbaya ya jina ambalo si muhimu likilinganishwa na maana
992 ya kuonyesha ukubwa wa jina. Maoni haya ya kamati kuhusu sarufi ya
993 Kiswahili yalipingwa. Bwana E. B. Huddon aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
994 Mashariki nchini Uganda, katika I.L.C. Bulletin Na. 14 ya 1940 anata-
995 hadharisha kwamba, Wazungu wanaweza kupendekeza kutumia kwa
996 kabila hii (ngeli ya 9) badala ya kabila hili (ngeli ya 6), Dachi-Madachi
997 badala ya Dachi-Wadachi nk. lakini itachukua muda kujua ni matumizi
998 gani yatakayoshika. Anatoa mfano wa vile mabibi na mabwana yanavyo-
999 tumiwa kama wingi wa bibi na bwana na wala maneno ambayo tungetarajia,
1000 ambayo ni, wabibi na wabwana hayatumiki kamwe. Pia tamko wake zake
1001 ni matumizi sahihi hata ingawa hayafuati kanuni za viambishi vya ngeli.
1003 Majadiliano haya pamoja na ya matumizi ya viambishi m-wa kuonyesha
1007 wingi yanaendelea katika matoleo kadha yajarida la I.L.C. Bulletin. Kasisi
1008 Canon A. B. Hellier katika jarida la 1941 kwa mfano, anasisitiza kwamba
1009 kamati inao wajibu wa kukomesha matumizi yasiyokuwa sanifu katika
1010 shule licha ya matumizi ya watu. "Ikiwa baadhi ya watu wataamua kusema
1011 Mataliana badala ya Waitaliano inasikitisha, lakini hatuwezi kuwazuia;
1012 lakini tunaweza kuzuia matumizi kama hayo yasiingie katika vitabu vya
1013 shule". Vile vile Hellier anasema kwamba, Kamati haitashawishiwa
1014 kuandika Waingereza na Waitaliano kama Wengereza na Wetaliano ati
1015 kwa sababu baadhi ya ai huwa e. 26*
1017 Hellier anasema kwamba maneno kama vile rafiki adui na mke ni
1018 baadhi ya maneno ambayo hayafuati kanuni za viambisho vya ngeli katika
1019 hali ya wingi. Anajadili neno mbona kwa kirefu na kudai kwamba ni sawa
1020 na tamko 'kwa nini?'. Hakubaliani na maelezo ya Bull na Snoxall ya hapo
1021 awali kwamba neno mbona, chanzo chake ni navona. Anasema kwamba
1022 nivona ni chanzo kinachofaa zaidi na kwamba ndilo neno lililotangulia
1025 Katika jarida namba 14 mapendekezo ya maneno ya Kiswahili ya
1026 msamiati uliochapishwa katika jarida namba 13 yanatolewa; kisha
1027 maneno yaliyokubaliwa ambayo yamesanifishwa yamechapishwa katika
1028 jarida I.L.C. Bulletin Na. 14 la 1941. Ningependa kutaja kwamba Kamati
1029 iliona ni muhimu maneno mlangobahari na pembemraba yaandikwe
1030 hivyo badala ya kuyagawa pembe mraba na mlango bahari.
1032 Kamati pia ilipendekeza maneno ya lugha zingine za Kiafrika yatumiwe
1033 walipokosa maneno ya Kiswahili yanayofaa. Kwa mfano, neno lililo-
1034 sanifishwa la ugonjwa wa ngombe 'ndigano' latokana na neno la Kimasai
1035 'oldikana'. Pia neno ugonjwa mwingine wa ngombe 'kimeta' ni la Kihehe
1036 kinachozungumzwa katika Wilaya ya Malangani, Tanzania. Labda neno
1037 la homa mbaya ya matumbo lililosanifishwa 'entereki' ni la Kimasai pia.
1039 Jarida la I.L.C. Bulletin Na. 16 la 1942 lilichapisha matokeo ya
1040 uchunguzi pamoja na mapendekezo ya Kamati kuhusu mambo kadha ya
1041 sarufi, matumizi na msamiati. Jarida namba 17 la 1943 pia lilichapisha
1042 matokeo ya uchunguzi wa sarufi, matumizi, msamiati na othografia. 27*
1043 Jarida namba 18 la 1944 lilimkumbuka Dkt. Ludwig Krapf na kumsifu
1044 kwa kazi zake za uchunguzi wa Kiswahili na uandishi wake aliouanza
1045 miaka mia moja iliyopita. Mwaka 1944 uliadhimisha miaka 100 tangu
1046 Krapf afike Afrika Mashariki. Mbali na orodha za maneno ya Kiswahili na
1047 Kiingereza, maana, na matumizi yake, makala fupi pia zilichapishwa.
1048 Mwisho kabisa Kamati inawashukuru wanafunzi wa Chuo cha Serekali
1051 26* Tazama sehemu ya othografia, sura ya pili.
1052 27* Ili kupata mengi kuhusu othografia soma sura ya pili.
1056 cha Uchapishaji cha Dar es Salaam pamoja na mwalimu wao kwa
1057 kuchapisha Jarida la I.L.C. Bulletin kwa miaka mingi.
1059 Makao makuu ya Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki yalihami-
1060 shwa kutoka Dar es Salaam kuenda Nairobi mnamo mwaka 1942.
1061 Wasomaji wa Jarida walijulishwa anwani mpya ya Kamati katika toleo
1062 namba 16 la mwaka huo. Katika jarida namba 17 la 1943 katibu wa
1063 Kamati anawashukuru wasomaji wa jarida kwa kutoa maoni na mape-
1064 ndekezo yao kwa wingi kuhusu Kiswahili. Alisema kwamba maoni na
1065 mapendekezo hayo yalikuwa mengi sana hivi kwamba hayangechapishwa
1066 yote au kujibiwa moja moja. Yaonekana kwamba labda vita viliwafanya
1067 wananchi wa Afrika Mashariki watambue kwamba walikuwa ni jamii
1068 moja na kwamba Kiswahili ndicho kingewaunganisha na kuwawezesha
1071 Inaripotiwa kwamba katika mwaka uliotangulia (1942), Kamati iliende-
1072 lea kuwasiliana na idara za utangazaji za Kenya na Tanganyika pamoja na
1073 jeshi kuhusu uchapishaji wa vitabu pamoja na mafunzo ya Kiswahili kwa
1074 wanajeshi. Katibu aliendelea kuwasiliana na nchi zingine kwa kuandikiana
1075 barua kwa kuwa vizuizi vya wakati wa vita havikumruhusu kusafiri.
1076 Anarekodi mwamko mpya wa kukipenda Kiswahili uliothibitishwa na
1077 barua nyingi alizozipokea kutoka kote katika Afrika Mashariki. Katibu
1078 Ratcliffe anaandika hivi:
1080 "Usafiri wa wanajeshi na kuongezeka kwa njia za usafiri kumeongeza
1081 sana mahitaji ya othografia sanifu." (I.L.C. Bulletin Na.17 la 1943: 14).
1083 Moja kati ya shughuli kubwa sana za Kamati ya Kiswahili ya Afrika
1084 Mashariki ilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanajeshi wamefunzwa
1085 Kiswahili. Jeshi liliwaendea Kamati, nayo Kamati iliwashauri vilivyo.
1086 Sera ilinuia kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya wanajeshi kote katika
1087 Afrika Mashariki. Baadhi ya maafisa vijana wa Kiingereza ilisemekana
1088 hawakupenda kujifunza Kiswahili kwa kuwa hawakuona umuhimu wa
1089 lugha hiyo baada ya vita (Snoxall: mahojiano na mwandishi). Waafrika
1090 wote waliojiunga na jeshi ilibidi wajifunze Kiswahili, ili waweze kuwasiliana
1091 na wanajeshi wenzao waliokuwa wakitumia lugha tofauti. Kwa hivyo,
1092 Kiswahili kikawa lugha ya wanajeshi. Shule zilizokuwa zikisomesha
1093 watoto wa wanajeshi pia zilitumia Kiswahili. (Kwa maelezo zaidi, tazama
1096 Kimoja kati ya vitabu vilivyotumika sana ni Upcountry Swahili
1097 Exercises kilichoandikwa na Breton. Lakini kitabu kilichotayarishwa na
1098 kuchapishwa na sehemu ya Elimu ya Jeshi la Afrika Mashariki ili
1099 kusomesha wanajeshi Kiswahili kiliitwa A Kiswahili Instruction Book for
1100 the East African Command.
1104 Kiswahili walichofunzwa wanajeshi kilikuwa cha mwanzo tu. Hata
1105 baadhi ya wanajeshi waliokijua Kiswahili vizuri hawakukifikiria kuwa ni
1106 Kiswahili safi. Mmoja wao ni C. A. R. Savage aliyekuwa mwanajeshi huko
1107 Jinja, Uganda. Bwana Savage aliyekijua Kijaluo, Kiacholi na Kiswahili
1108 vizuri alikuwa mwanakamati wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
1109 kutoka Uganda. Siku moja mabwana Savage na Snoxall wakiwa safarini
1110 kwenda Nairobi kwa gari la moshi kuhudhuria mkutano wa Kamati,
1111 Bwana Savage alitunga ubeti ufuatao wa Kiingereza kukieleza Kiswahili
1112 cha bara kama kile walichofunzwa wanajeshi:
1114 "Natives who speak Swahili here
1115 Have never heard of Bishop Steere
1116 Their primitive upcountry speech
1117 No rules of Grammar serves to teach
1118 Sometimes really zealous learner
1119 Some concords may pick up from Werner
1120 But "Safi" stuff is heard alone
1121 When Ratcliffe talks to Elphinstone." 28*
1125 Wenyeji wanaoongea Kiswahili huku
1126 Hawajamsikia Askofu Steere
1127 Lugha yao ya bara isiyostaarabika
1128 Haifuati kanuni za sarufi
1129 Mara nyingine mwanafunzi mwenye bidii
1130 Hujifunza viambisho vitabuni vya Werner
1131 Lakini lugha iliyo safi husikika tu
1132 Ratcliffe azungumzapo na Elphinstone.
1134 Kamati ilianzisha ushirikiano na Belgian Congo (Zaire) katika shughuli
1135 za kuleta pamoja maendeleo ya Kingwana na ya Kiswahili sanifu (tazama
1138 Vitabu vinane vipya vilichapishwa mnamo 1942. Vitabu vingi vilipigwa
1139 chapa na misheni za Afrika Mashariki. Pia miswada ishirini na tano
1140 ilipelekwa Kamati, ikiwa ni ya masomo mbalimbali kama vile kilimo,
1141 mazoezi ya viungo na mbinu za kusomeshea. Baadhi ya miswada ilipelekewa
1142 Kamati ili kamati iikague na ithibitishe kwamba othografia ilikuwa sanifu,
1143 nayo miswada mingine ilipelekewa Kamati ili Kamati iisanifishe na
1144 kuichapisha ikiamua kufanya hivyo. Kwa sababu ya vita, katibu anaeleza
1145 kwamba kulikuwa na upungufu wa karatasi na kwamba ilichukua muda
1148 28* Snoxall, mahojiano na mwandishi, Februari 10, 1984. Sehemu moja ya ubeti huo pia
1149 yapatikana katika Whiteley, 1969: 79).
1153 mrefu kutuma miswada Uingereza ili ichapishwe.
1155 Kama vile nilivyotaja katika mwanzo wa sehemu hii, mashindano ya
1156 uandishi wa Kiswahili yaliiendelea wakati wa vita. Zawadi mbili za
1157 kwanza za uandishi wa insha ya kuelekezwa zilishindwa na Wakenya
1158 wawili kutoka shule za wavulana za Alliance na Mangu. Zawadi ya tatu
1159 ilishindwa na mtu mmoja kutoka Masasi, Tanganyika. Katika shindano la
1160 uandishi wa insha ambapo mwandishi hakuelekezwa, zawadi ya kwanza
1161 na ya tatu zilishindwa na waandishi kutoka Makerere, Uganda, nayo
1162 zawadi ya pili ilishindwa na mwandishi kutoka Dar es Salaam, Tanganyika.
1163 Mashindano mengine yalikuwa ni mashindano ya uandishi na mashindano
1164 ya insha ya wanafunzi wa shule za Wazungu. Akizungumzia ufasaha wa
1165 lugha mhariri wa jarida anasema kwamba Kiswahili kilichotumiwa
1166 chaonyesha kwamba waandishi walikuwa wanaimudu lugha, na walijieleza
1167 vizuri. (I.L.C. Bulletin Na. 17, 1943: 16).
1169 Katika jarida, I.L.C. Bulletin Na. 18 la 1944, ripoti ya mwaka
1170 uliotangulia inaonyesha kwamba mnamo 1943 kulikuwa na mawasiliano
1171 na makundi ya Afrika Mashariki na ya kimataifa ambayo yangesaidia
1172 katika utoaji wa vitabu vya fasihi ya Kiswahili. Katibu alitembelea mikoa
1173 ya Mashariki, Kati na Kaskazini ya Tanganyika kukadiria mahitaji ya
1174 vitabu vya Kiswahili katika shule na vituo vingine vya elimu. Vitabu kumi
1175 vya Kiswahili vilichapishwa na kamati ilipokea miswada ishirini na nane
1176 kuichunguza. Kamati yenyewe iliongezea orodha hii kwa kutafsiri vitabu
1179 Mnamo 1943 Waafrika walioshiriki kwenye mashindano ya uandishi wa
1180 Kiswahili, wakiwa ni pamoja na askari jeshi walikuwa 215, lakini
1181 hakukuwa na yeyote aliyeshiriki kutoka shule za serikali za watoto wa
1182 Kizungu. Kitengo cha Kamati kilichokagua mashindano hayo kiliridhika
1183 kwamba mashindano hayo yalisaidia katika kueneza ujuzi wa kusoma na
1184 kuandika. Miswada iliyopokelewa ilionyesha kukua kwa vipawa vya
1185 uandishi ambao ulihitajika sana kwa kuwa kulikuwa na upungufu wa
1186 fasihi ya Kiswahili iliyoandikwa na Waafrika.
1188 Kati ya wale walioshinda zawadi katika mashindano ya 1943 wali-
1189 kuwemo Maurice Otunga wa Holy Ghost College, Mangu, Kenya na
1190 Josiah Muli wa Alliance High School, Kikuyu, Kenya. Katika mashindano
1191 ya 1944, Robert Matano wa Alliance High School, Kikuyu, na Moses
1192 Kinyanjui wa Holy Ghost College, Mangu, pia walishinda zawadi.
1194 Ripoti ya 1944 ilichapishwa katika I.L.C. Bulletin Na. 19 ya 1945.
1195 Ripoti hiyo inataja kwamba Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
1196 ilikumbwa na matatizo. Hata hivyo jarida halikueleza aina ya matatizo
1197 hayo. Labda kamati ilikuwa na wasiwasi kuhusu pendekezo la Waku-
1198 rugenzi wa Elimu wa Serikali za Afrika Mashariki kwamba Kamati
1202 iunganishwe na halmashauri ya uchapishaji - East African Literature
1203 Bureau - iliyonuiwa kuanzishwa. Miswada iliyoendelea kupokewa na
1204 Kamati iliwapa ofisi ya katibu pamoja na wahariri wa Kamati kazi za
1205 kutosha za kufanya mwaka huo. Wahariri hao walipongezwa kwa
1206 kufanya kazi kwa bidii, licha ya upungufu wa wafanyakazi wakati wa vita.
1207 Vitabu kumi vipya vilichapishwa mnamo 1944 na miswada kumi na tisa
1208 ilipokelewa. Kwa upande wake kamati ilitafsiri vitabu kumi na vinne.
1210 Kazi iliyofanywa na Kamati wakati huu wa vita, kulipokuwa na
1211 upungufu wa pesa na wafanyakazi ilikuwa nyingi na ya kushangaza. Kati
1212 ya 1942 na 1944, kipindi kifupi cha miaka mitatu Kamati iliripoti kwamba
1213 ilichapisha jumla ya vitabu ishirini na vinane (28). Ilikuwa imetafsiri
1214 vitabu kumi na vinane (18), pamoja na kushughulikia miswada sabini na
1217 Vita havikupunguza usomaji wa vitabu, bali vitabu viliuzwa kwa wingi
1218 zaidi. Ratcliffe anaandika kwamba "ingawaje ni wakati wa vita, vitabu vya
1219 Kiswahili havijawahi kununuliwa kwa wingi jinsi hii". (Ratcliffe I.L.C.
1220 Bulletin Na. 18, 1944: 4). Mnamo 1943 pekee, Ratcliffe anaripoti kwamba
1221 zaidi ya vitabu 330,000 vya Kiswahili vilivyochapishwa huko Uingereza
1222 viliuzwa katika Afrika Mashariki, mbali na nakala 70,000 za vitabu
1223 vilivyochapishwa Afrika Mashariki. Kamati inapendekeza Kiswahili kitu-
1224 miwe katika kuelimisha watu kwa wingi badala ya kutumia lugha za
1225 kwanza zilizokuwa zikipendekezwa, ambazo zilitumiwa na idadi ndogo ya
1226 watu wa kabila moja moja.
1228 Jarida la I.L.C. Na. 19 la 1945, lilichapishwa mwezi Novemba wa
1229 mwaka ambao vita vya pili vya dunia vilimalizika. Jarida linashangilia
1230 kukomeshwa kwa uhasama huko Ulaya. Kumalizika kwa vita kulileta
1231 mabadiliko mengi. Yasemakana kwamba Kamati ya Kiswahili ya Afrika
1232 Mashariki ilipewa miradi mipya na kwamba mambo yaliyokuwa yakitiliwa
1233 mkazo kuliko hapo awali yalikuwa ni kusoma na kuandika pamoja na
1234 ukuzaji wa lugha za kwanza. Mhariri wa Jarida anasema hivi - "Mengi
1235 yamesemwa na yangali yanasemwa kuhusu kuhitajika kwa Kiingereza
1236 kama lugha ya kusomesha masomo mengine, lakini itachukua muda
1237 mrefu kabla Kiingereza hakijakuwa tiba ya Waafrika ya kutojua kusoma
1238 na kuandika". (I.L.C. Bulletin Na. 19, 1945: makala ya mhariri).
1240 Kutiliwa mkazo huku kwa Kiingereza na lugha za kwanza mara tu
1241 baada ya vita, kulikuwa ndiyo mwanzo wa kudhoofika kwa shughuli za
1242 Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Usanifishaji wa Kiswahili
1243 ulikuwa umeanza kushuka kutoka upeo wake. Kamati ilitambua hivyo na
1244 ikajaribu kuonyensha kwamba Kiingereza hakingeweza kutumiwa ku-
1245 pigana na hali ya kutojua kusoma na kuandika. Ilibidi lugha za Kiafrika
1246 zitumiwe. Kwa kuwa ingekuwa ghali sana kukuza lugha nyingi za kwanza,
1250 ingekuwa bora Kiswahili kitumiwe. Kiswahili kilikuwa kimejitambulisha
1251 kama lugha sanifu iliyotumika kote katika Afrika Mashariki. Kilikuwa na
1252 maandishi mengi yaliyokuwa yakiongezeka kwa wingi, na hiyo ndiyo
1253 sababu Kamati ikaonelea kwamba Kiswahili pekee ndicho kinachofaa
1254 kwa elimu ya watu wengi.
1256 Afisi ya Kikoloni haikufuata mapendekezo ya Kamati. Kwao lilikuwa
1257 suala la kisiasa. Ilibidi Wakoloni watumie mbinu mpya kuwatawala
1258 Waafrika ambao walikuwa wamepevuka kisiasa baada ya kushiriki katika
1259 vita. Waafrika walikuwa wameutambua udhaifu wa Wazungu wakati wa
1260 vita. Ilikuwa wazi kwao kwamba iwapo wangeshirikiana wangeweza
1261 kupinga utawala wa kikoloni.
1263 Watawala wa kikoloni walikuwa na hamu ya kutumia mgawanyiko wa
1264 lugha za kwanza ili kuwatenganisha Waafrika. Kuendelea kutumiwa kwa
1265 lugha moja ya Kiswahili kungeleta matokeo yaliyo kinyume cha yale
1266 yaliyotarajiwa, kwa kuwa kungewaunganisha Waafrika. Kiingereza haki-
1267 ngekuwa na matokeo kama hayo kwa kuwa kingewaunganisha Waafrika
1268 wachache walioelimika, ambao hawangekuwa tisho kubwa kwa serikali ya
1269 kikoloni. Sera hii mpya ya kupunguza mkazo wa Kiswahili ilijitokeza na
1270 kuiudhi Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na bila shaka ndiyo
1271 Jarida linayoigusia linapotaja kwamba Kamati ilikumbwa na matatizo
1278 4.0 Kamati baada ya vita
1280 4.1 Kipindi cha Nairobi (1946-1952)
1282 Tayari tumetaja kwamba kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
1283 (I.T.L.C.) ilihamisha makao yake makuu kutoka Dar es Salaam hadi
1284 Nairobi mnamo mwaka wa 1942. Sehemu hii inahusu maisha ya kamati
1285 jijini Nairobi baada ya vita vikuu vya pili vya dunia kuanzia mwaka 1946
1286 hadi 1952. Baada ya kukaa Nairobi, makao makuu ya kamati yalihamishwa
1289 Jarida la I.L.C Bulletin halikuchapishwa mnamo mwaka wa 1946.
1290 Mkutano wa kwanza wa Kamati yote, tangu vita vianze mwaka 1939,
1291 ulikuwa mjini Nairobi tarehe 4 na 5 Machi mwaka 1946. Kama ilivyo-
1292 jadiliwa katika Sura ya Tatu hakukuwa na mikutano ya kamati yote
1293 wakati wa vita. Mikutano iliyokubaliwa ilikuwa ni ile kitengo cha kamati
1294 ambacho kilihudhuriwa na wasomaji, mwenyekiti na katibu. Kitengo
1295 kilifanya uchunguzi wa lugha na kazi zingine kama vile ukaguzi wa
1296 mashindano ya uandishi.
1298 Kama ilivyotarajiwa mabadiliko kadha yalikuwepo hasa kuhusu
1299 uanachama wa kamati baada ya vita. Kamati ilipokutana mwaka 1942
1300 Wakurugenzi wote wa Elimu kutoka Tanganyika, Uganda, Kenya na
1301 Zanzibar walikuwa wapya. Kwa hivyo walikuwa wakihudhuria kikao cha
1302 kamati kwa mara yao ya kwanza. Wasaidizi wa wahariri wa Kiafrika
1303 kutoka nchi zote nne, pia walihudhuria kikao cha Kamati kwa mara yao
1304 ya kwanza. Mbali na mabadiliko haya, pia kulikuwa na mabadiliko katika
1305 ajenda ya mkutano ambayo ilihusu zaidi masuala ya lugha zingine za
1306 Kiafrika kuliko Kiswahili. Kama itakavyojadiliwa kwa kirefu katika Sura
1307 ya Tano, Kipindi hiki cha Kamati, baada ya vita kilikuwa na mabadiliko
1308 mengi kuhusu sera ya lugha ambapo Kiingereza na lugha kadha za
1309 Kiafrika zilianza kutiliwa mkazo badala ya Kiswahili.
1311 Jarida la I.L.C. Bulletin Na. 20 lilichapishwa mwaka 1947. Kama
1312 ilivyokuwa kawaida, jarida lilikuwa na maoni mengi kuhusu lugha kutoka
1313 kwa wasomaji. Mwandishi mmoja ambaye makala yake yametokea katika
1314 majarida ni A. N. Tucker kutoka School of Oriental and African Studies,
1315 Chuo Kikuu cha London. Katika maandishi yake yanayohusu mtindo wa
1316 kuandika lugha, anasema kwamba lugha zingine za Kibantu zatakikana
1317 zitumie mtindo wa kuandika Kiswahili kama kielekezo. Hata hivyo
1321 anatahadharisha kuhusu miundo tofauti ya baadhi ya lugha za Kibantu
1322 kama vile kuwepo na irabu saba badala ya tano za Kiswahili na hali ya
1323 kuwa na irabu mbili zilizofuata katika neno moja (ambapo irabu hizo
1324 zinasababisha neno liwe na maana tofauti). Tucker anatahadharisha
1325 kwamba tofauti kama hizo zitiliwe maanani wakati wa kuunda mtindo wa
1326 kuziandika lugha za Kibantu.
1328 Katika mwaka wa 1946 uliotangulia, jumla ya miswada ishirini na mbili
1329 ilikabidhiwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ili iishughulikie.
1330 Vitabu kumi na moja vya Kiswahili vilichapishwa na vitabu vingine vitano
1331 vikatafsiriwa na wafanyakazi wa afisi ya katibu mtendaji. Mashindano ya
1332 uandishi wa Kiswahili yaliendelea kuwavutia washiriki wengi kutoka
1333 shule za Kiafrika hata ingawa hakukuwa na walioshiriki kutoka shule za
1336 Jarida la I.L.C. Bulletin halikuchapishwa katika miaka ya 1948, 1949 na
1337 1950 ambapo mabadiliko kadha yalikuwa yakitendeka. Licha ya hivyo,
1338 jumla ya vitabu vipya ishirini na sita vya Kiswahili vilichapishwa wakati
1339 huo. Pia wahariri wa Kamati pamoja na katibu walikabidhiwa miswada
1340 156 (mia moja hamsini na sita) kuishughulikia.
1342 Mnamo mwezi wa Disemba mwaka wa 1949 Rev. B. J. Ratcliffe katibu
1343 wa Kamati alistaafu. Rev. Ratcliffe alifika Afrika ya Mashariki kwa mara
1344 ya kwanza mwaka 1899 alipoanza kazi za kidini katika wilaya ya Tana
1345 River nchini Kenya. Uhusiano wake na Kamati ya Kiswahili ya Afrika
1346 Mashariki ulianza hapo mwaka 1930 alipochaguliwa kuwa mhariri
1347 kuwakilisha Kenya. Alishikilia wadhifa huo hadi mwaka 1937 alipo-
1348 ajiriwa kuwa katibu baada ya kifo cha Frederick Johnson aliyekuwa
1349 katibu wa kwanza wa Kamati.
1351 Shughuli kubwa aliyoifanya Ratcliffe kama katibu ilikuwa ni kuha-
1352 kikisha kwamba kamusi mbili Standard Swahili-English na English-
1353 Swahili zimechapishwa. Kamusi hizo zilikuwa zimehaririwa na Frederick
1354 Johnson kutegemea msingi uliowekwa katika kamusi za Madan. Ratcliffe
1355 aliweza kutetea vilivyo, matumizi ya msamiati wa lahaja tofauti za
1356 Kiswahili. Kufuatia juhudi zake, msamiati wa lahaja za Kenya, hasa
1357 Kimvita uliweza kuingizwa kwenye kamusi - jambo ambalo halinge-
1358 dhaniwa kwamba lawezekana mwaka 1928.
1360 Baada ya Ratcliffe kustaafu, mkurugenzi wa East African Literature
1361 Bureau, Bwana C. G. Richards alishikilia wadhifa wa katibu kwa muda.
1362 Baada ya Richards, Bwana H. E. Lambert alichaguliwa kuwa kaimu wa
1363 katibu hadi mwezi wa Agosti 1952 wakati W. H. Whiteley alipouchukua
1366 Wakati jarida la I.L.C. Bulletin la mwaka wa 1951 lilipochapishwa,
1367 tayari Kamati ilikuwa imeundwa upya. Kamati ilibadilisha jina kutoka
1371 lnter-Territorial Languages (Swahili) committee (I.L.C.), likawa East
1372 African Inter-Territorial Language (Swahili) Committee (E.A.I.L.C.).
1373 Tangu Kamati hii ya Kiswahili ya Afrika Mashariki iundwe mwaka 1930,
1374 ilikuwa chini ya (mamlaka ya ) halmashauri ya Magavana wa Afrika ya
1375 Mashariki. Kwanzia Januari moja mwaka 1948 Kamati ilianza kuwa chini
1376 ya tume ya East African High Commission.
1378 Katika mwaka wa 1950 kulikuwa na mkutano uliohudhuriwa na
1379 maafisa wakuu wa Kamati kutoka nchi zote za Afrika ya Mashariki
1380 pamoja na Bwana C. G. Richards aliyewakilisha halmashauri ya uchapi-
1381 shaji wa vitabu - East African Literature Bureau. Mwenyekiti wa
1382 mkutano huo alikuwa ni afisa tawala wa East African High Commission.
1383 Mkutano huo uliitishwa kujadili kazi za Kamati tangu kuanzishwa kwa
1384 East African Literature Bureau. Ilikubaliwa kwamba Kamati ingeendelea
1385 kuwepo kama chombo cha lugha ambacho ni tofauti na East African
1386 Literature Bureau. Ilikubaliwa kwamba Kamati ingeendelea kujihusisha
1387 zaidi na uchunguzi wa lugha na somo la Kiswahili. Kamati pia ingebakia
1388 kuwa mamlaka ya juu kuhusu uandishi na uchapishaji wa vitabu vya
1391 Nayo halmashauri ya East African Literature Bureau ilipewa mamlaka
1392 ya utoaji na uchapishaji wa vitabu. Kazi hiyo hapo awali ilikuwa ikifanywa
1393 na Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Pia kazi ya upangaji wa
1394 mashindano ya uandishi wa Kiswahili ilikabidhiwa East African Literature
1395 Bureau hata ingawa usomaji na utoaji uamuzi wa maandishi hayo ulikuwa
1396 ukifanywa na Kamati. Kwa sababu ya ushirikiano huu wa kufanya kazi
1397 kati ya Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na halmashauri ya
1398 uchapishaji, naonelea ni bora nieleze machache kuhusu East African
1401 East African Literature Bureau iliundwa mwezi Januari, 1948 kama
1402 mojawapo ya huduma zilizotolewa na East African High Commission.
1403 Iliundwa baada ya kufanywa uchunguzi ulioagizwa na mkutano wa
1404 Magavana wa Afrika Mashariki. Uchunguzi huo ulifanywa kuanzia Julai
1405 1945 hadi 1947. Kwa maoni ya J. W. Chege (1978: 128) East African
1406 Literature Bureau ilirithi kampuni ya uchapishaji ya C.M.S. iliyojulikana
1407 kama Ndia Kuu Press (Highway Press). Meneja wa kampuni hiyo C. G.
1408 Richards, pia ndiye aliyechaguliwa kuwa mkurugenzi wa kwanza wa East
1409 African Literature Bureau. Kazi za uchapishaji za Ndia Kuu Press
1410 zilichukuliwa na East African Literature Bureau.
1412 Makao makuu ya East African Literature Bureau yalikuwa mjini
1413 Nairobi, lakini pia kulikuwa na matawi madogo huko Kampala na Dar es
1414 Salaam. Tawi la Kampala lilikuwa likihudumia Uganda nalo tawi la
1415 Dar es Salaam lilihudumia Tanganyika na Zanzibar. Pia halmashauri hii
1419 ilitoa huduma za maktaba kwa kutumia magari yaliyozitembelea shule na
1420 miji ya Afrika Mashariki. Huduma hii ya maktaba pia ilitolewa kupitia
1423 East African Literature Bureau ilianzishwa ili kutosheleza mahitaji ya
1424 vitabu yaliyokuwa yakiongezeka kwa haraka kati ya Waafrika walio-
1425 elimika. Kwa hivyo ilitarajiwa kuchapisha na kutawanya "vitabu vya
1426 fasihi kwa watu wa kawaida, vitabu vya lazima vya shule, vitabu vya kilimo
1427 na ufundi vya watu wazima, magazeti au majarida, kuwasaidia waandishi
1428 wa Kiafrika na kutoa huduma za maktaba. Mahitaji ya Waafrika
1429 yangehudumiwa kwanza, lakini pia, halmashauri hiyo ilitakikana ichapishe
1430 vitabu vya fasihi kwa Wahindi". 29*
1432 Kazi ya uandishi wa vitabu vya lazima vya shule uligawanywa katika
1435 (i) Kuandika na kuhariri miswada ya vitabu vya walimu na
1436 wanafunzi ili kutosheleza mahitaji ya ratiba za Idara za Elimu.
1437 (ii) Kufanya vivyo hivyo kwa vitabu vya ziada.
1438 (iii) Kutafsiri au kukagua tafsiri za Kiswahili, Kiluganda, Kijaluo
1439 na Kikikuyu na kufanya mpango wa tafsiri kama hizo nje ya
1440 halmashauri kwa lugha zingine zinazohitajika katika elimu.
1441 (iv) Kushughulikia miswada ya vitabu vya lazima na maswali
1442 kutoka kwa wachapishaji.
1444 Sehemu ya uchapishaji wa magazeti ya East African Literature Bureau
1445 ilichapisha gazeti la kila wiki lijulikanalo kama Tazama. Gazeti hilo
1446 lilikuwa likitolewa zaidi ya nakala 17,000. Tazama lilianza kuchapishwa
1447 na East African Standard mwaka 1956. Tafsiri ya Tazama kwa Kiluganda
1448 ilikuwa ikichapisha nakala chache sana.
1450 J. W. Chege (1978: 30) anayo maoni kwamba vitabu vya East African
1451 Literature Bureau vilinuiwa kutosheleza "mahitaji ya kikoloni ya kuko-
1452 mesha kutoridhika na ukoloni na kwamba vilichapishwa kufuatia mashauri
1453 na kibali cha Baraza la Ushauri". Ushirikiano wa East African Literature
1454 Bureau na mashirika ya uchapishaji ya Uingereza kama vile MacMillan,
1455 Longman na Thomas Nelson n.k, kwa maoni ya Chege ilikuwa ni hila ya
1456 wakoloni ya kumiliki biashara za uchapishaji. Anatoa mifano na tarakimu
1457 kuthibitisha dai lake kwamba vitabu vilivyokuwa vikinunulika kwa wingi
1458 zaidi vilipewa wachapishaji hao baada ya East African Literature Bureau
1459 kuhakikisha kwamba vingenunuliwa kwa wingi katika matoleo ya kwanza.
1460 'Mkurugenzi mkoloni' (C. G. Richards) alifaulu sana kwa hila hii hivi
1461 kwamba wakati wa kustaafu 'alipendekeza kwamba East African Literature
1464 29* East African Literature Bureau, Annual Report for 1950: 2.
1468 Bureau ivunjiliwe mbali kwa kuwa ilikuwa tayari imetimiza kazi zake na
1469 kwamba makampuni yaliyomiliki uchapishaji yalikuwa na uwezo wa
1470 uchapishaji'. (Chege 1978: 131).
1472 Kamati iliyoundwa upya ilikuwa na watu tisa, wawili kutoka kila nchi
1473 pamoja na katibu. Idadi hii ilikuwa ndogo sana ikilinganishwa na
1474 wanakamati kumi na saba - wanne kutoka kila nchi na katibu. Snoxall
1475 hufikiria kwamba kupunguzwa kwa wanakamati ilikuwa ni hatua ya
1476 maendeleo. "Ni maendeleo mazuri kwamba uwanachama wa kamati
1477 umepunguzwa kuwa kundi dogo la wataalamu wenye bidii na kwamba
1478 mashindano ya uandishi na kazi za uchapishaji wa vitabu vya shule
1479 zimechukuliwa na East African Literature Bureau" (Snoxall E.A.I.L.C.
1480 Bulletin Na. 22, 1952:3).
1482 Orodha mpya ya shughuli za Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
1483 iliyoundwa upya ilikubaliwa katika kikao cha kumi na tatu (13) cha
1484 kamati. Shughuli hizo zilizoorodheshwa hapa chini zilitilia mkazo
1485 uchunguzi katika maeneo kama vile fasihi ya Kiswahili na lahaja.
1486 Shughuli zifuatazo za Kamati zilikubaliwa:
1488 a) Kuandaa vifaa vya kutosha vya kusomesha Kiswahili.
1489 b) Kurekebisha na kuchapisha upya makamusi ya Kiswahili
1490 kutegemea matokeo ya utafiti.
1491 c) Kushirikiana na mabaraza ya lugha kuhusu mitihani.
1492 d) Kuwajulisha watu wa Afrika Mashariki mambo yanayohusu
1493 hadhi, umuhimu na maendeleo ya Kiswahili kupitia vyombo
1494 vya kutawanya habari.
1495 e) Kufanya uchunguzi juu ya historia ya Waswahili, lugha,
1496 lahaja, uhifadhi na ufafanuzi wa fasihi ya jadi ya Waswahili.
1497 f) Kuendelea kuwa na mawasiliano kati ya nchi zinazotumia
1498 Kiswahili - Tanganyika, Zanzibar, Kenya, Uganda, Rhodesia
1499 ya Kaskazini (Zambia), Nyasaland (Malawi), Somaliland
1500 (Somalia), Kongo ya Ubelgiji (Zaire) na Visiwa vya Komoro.
1501 g) Kuendelea kuwa na mawasiliano kati ya kamati na mashirika
1502 ya kielimu, vyuo, na vyuo vikuu vinavyoshughulikia Kiswahili
1503 kama vile Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Afrika ya
1504 Kusini, Leyden, Lourain na Berlin, pamoja na kuvihimiza
1505 vyuo vikuu vingine vianzishe somo la Kiswahili.
1506 h) Kuhimiza kuanzishwa kwa somo la Kiswahili katika shule za
1507 Wazungu na za Wahindi katika Afrika Mashariki ili kuwe na
1508 ushirikiano wa kijamii; na ili kuwezesha kupata wanaisimu
1509 watakaoweza kufanya uchunguzi wa somo hili katika siku za
1514 i) Kudondoa makala muhimu kuhusu somo la Kiswahili kutoka
1515 kwenye majarida ya vyuo na mashirika yanayohusika na
1517 j) Kuongoza au kukagua usomeshaji wa Kiswahili katika vituo
1518 vilivyokubaliwa ili kurekebisha mitindo isiyofaa ya kufunza
1520 k) Kufanya kazi za ukatibu wa kamati za lugha zisizo za Serikali.
1522 Orodha ya shughuli za Kamati inayo mambo mengi sana. Kama katibu
1523 Whiteley alivyokiri baadaye "Kamati ingeweza kutekeleza michache kati
1524 ya miradi iliyoorodheshwa, zaidi kwa kuwa, katibu atakuwa na kazi
1525 zingine mbali na ukatibu". (E.A.I.L.C. Bulletin Na. 23, 1953: 7).
1527 Taarifa ya mhariri ya Bulletin Na. 21 inatangaza kuajiriwa kwa
1528 Bi. D. V. Perrott wa U.M.C.A. ambaye pia ni mwandishi wa kitabu
1529 kiitwacho Teach Yourself Swahili, kuwa mhariri wa Kamati ya Kiswahili
1530 ya Afrika Mashariki huko London. Kazi hii mpya ingemwezesha muajiriwa
1531 kuiwakilisha Kamati huko London, hasa katika kuisoma miswada
1532 inayochapishwa huko Uingereza. Hapo awali miswada hiyo ilikuwa
1533 ikitumwa katika ofisi ya katibu kusomwa. Kuwa na mhariri huko London
1534 kulinuiwa kupunguza gharama za kutuma miswada kati ya London na
1537 Toleo la E.A.I.L.C. Bulletin Na. 22 la 1952 lilikuwa na makala muhimu
1538 ya somo la Kiswahili. Makala hayo ni pamoja na jinsi ya kusomesha
1539 Kiswahili kama lugha ya kigeni iliyoandikwa na Ali Ahmed Jahadhmy,
1540 viambishi KA na U iliyoandikwa na J. Williamson pamoja na makala ya
1541 H. E. Lambert kuhusu vile tafsiri inavyoathiri Kiswahili.
1543 Katika mkutano wa kumi na nne (14) wa kila mwaka uliokuwepo
1544 Nairobi Oktoba 17, 1951, Kamati ilijadili mambo kadha kuhusu lugha na
1545 katiba pia. Pamoja na hayo kamati ilijadiliana kuhusu uwezekano wa
1546 kuyapeleka makao makuu yake huko Kampala katika Chuo cha Makerere.
1547 Pendekezo la kuishirikisha Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na
1548 Makerere liliwasilishwa kwa mkuu wa Chuo cha Makerere na afisa tawala
1549 wa East African High Commission mwezi Januari 1952. Baraza la Chuo
1550 lilijadili pendekezo hilo na kulipitisha mwezi Aprili mwaka huo huo.
1551 Mapatano hayakuchukua muda mrefu kufikiwa kwa sababu Taasisi ya
1552 Ucunguzi wa Shughuli za Jamii ya Afrika Mashariki ya huko Chuoni
1553 tayari ilikuwa imeanzisha uchunguzi wa lugha.
1555 Katibu mpya Bwana Wilfred Howard Whiteley alikuwa tayari ameajiri-
1556 wa kama mchunguzi mwandamizi wa isimu na lugha za Kibantu na
1557 Taasisi ya Uchunguzi wa Shughuli za Jamii. Whiteley alijifunza Kiswahili
1558 katika School of Oriental and African Studies, Chuo Kikuu cha London
1562 kwa miaka miwili. Pia alikuwa amefanya kazi kwa muda wa karibu miaka
1563 mitatu kama afisa wa shughuli za jamii huko Tanganyika. Akiwa huko
1564 Makerere, Whiteley angeendelea na uchunguzi wake kwa lugha kadha za
1565 Kibantu huko Tanganyika mbali na kazi zake za kutoa mihadhara.
1567 Mwezi Septemba 1952 katibu mpya, W. H. Whiteley, alishika usukani
1568 kutoka kwa katibu wa muda, H. E. Lambert mjini Nairobi. Whiteley
1569 aliyahamisha makao makuu ya Kamati hadi Chuo cha Makerere Kampala
1570 ambapo kamati iliambatanishwa na chuo hicho mwaka huo huo wa 1952.
1571 Whiteley aliposhika usukani kazi nyingi za Kamati zilihusu kutoa idhini
1572 ya kuchapishwa kwa miswada baada ya kuisoma na kuirekebisha vilivyo.
1573 Mradi mwingine uliokuwa shughuli kubwa ya Kamati, hasa katibu, ni ule
1574 wa kuchapisha jarida la E.A.I.L.C. Bulletin ambalo lilikuwa jukwaa la
1575 kujadili masuala muhimu yanayohusu Kiswahili.
1577 Akiwa Makerere, Whiteley alijikuta na shida ya kufanya kazi zote za
1578 ukatibu kwa kuwa, kama tulivyotaja, alikuwa na kazi za uchunguzi na
1579 kusomesha pia. Ilikuwa vigumu kwake kufanya kazi hizi zote pamoja na
1580 kusoma miswada ipatayo minne kila mwezi ambayo ilipelekewa kamati
1581 kuishughulikia. Kwa hivyo Whiteley aliwaajiri wahariri watatu wa muda,
1582 kumsaidia. Mmoja alitoka Makerere na wawili walitoka Dar es Salaam.
1583 Afisa tawala wa muda pia aliajiriwa ili kuvipanga vizuri vitabu vya
1584 maktaba ya Kamati na kufanya mambo mengine kama vile kupanga vizuri
1587 Shughuli za uchapishaji wa vitabu hazikuwa tena mikononi mwa
1588 Kamati, kama tulivyoeleza. Kwa hivyo, kufikia mwaka 1953 waandishi
1589 wengi walikuwa wakiipeleka miswada yao moja kwa moja kwa East
1590 African Literature Bureau bila ya kupata ithibati ya Kamati. Isipokuwa
1591 miswada hiyo iwe ni ya vitabu vya shule, East African Literature Bureau
1592 haikutakikana isisitize kuwepo kwa kibali cha Kamati kabla ya kuvichapi-
1593 sha vitabu. Kwa hivyo Kamati ililifikiria jambo hili na kuamua kutoa
1594 idhini kwa vitabu vichache vilivyochaguliwa kama vile, vitabu vya sarufi
1595 na vitabu vya lazima vya kutumiwa shuleni. Kusomwa na Kamati kwa
1596 miswada mingine kulikomeshwa. Uamuzi huu uliipatia afisi ya katibu
1597 nafasi ya kupumua kwa kuwa uliiondolea kazi ya kuchosha ya kuisoma
1598 miswada mingi ambayo baadhi yake haikuambatana na shughuli za
1599 kamati mbali na kuwa imeandikwa kwa Kiswahili.
1601 Mwaka uliofuata, 30* Whiteley, alijaribu kutoa sababu za msimamo wake
1602 mpya kuhusu ithibati kwa kusema kwamba, kusisitiza Kiswahili kiwe na
1603 umbo maalum kulisababisha lugha ionekane kama iliyobuniwa kwa
1604 kukosa uhalisi wake.
1607 30* Tazama E.A.I.L.C. Bulletin Na. 23 ya 1953.
1611 4.2 Kipindi cha Makerere (1952-1960)
1613 Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ilikuwa na makao yake
1614 makuu Makerere, Kampala kuanzia mwaka 1952 hadi mwaka 1962.
1615 Katika sehemu hii nitajadili shughuli za kamati kufikia mwaka 1960 kwa
1616 kuwa shughuli za kati ya mwaka 1960 na 1962 zinahusu zaidi sura ya sita
1617 inayojadili kubadilika kwa kamati kuwa Taasisi ya Uchunguzi wa
1620 Jarida la E.A.I.L.C. Bulletin Na. 23 la 1953 linayo makala ya kurasa
1621 ishirini iliyoandikwa na H. E. Lambert kuhusu lahaja ya Kivumba cha
1622 kisiwa cha Wasini na jimbo karibu na Vanga katika kusini mwa pwani ya
1623 Kenya. Lambert pia anajadili utenzi wa kutekwa kwa mji wa Tumbe na
1624 Waswahili (Wavumba) kutoka Vanga pamoja na shairi la kumsifu Mwana
1625 Mnga. Maandishi haya yalikuwa ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na
1626 Lambert huko Vanga ambacho ni kijiji cha Waswahili cha kusini zaidi
1627 nchini Kenya. Shairi hilo la mwisho lasemekana kwamba lilitungwa na
1628 mshairi mashuhuri Muyaka, lakini kama Lambert anavyoeleza, hakuna
1629 ushahidi wa kutosha kuthibitisha au kukanusha dai hili.
1631 Kufikia wakati huu, Kamati ilikuwa tayari imeanza kuchunguza zaidi
1632 lahaja za Kiswahili. Makala ya Lambert yalikuwa ni mfano tu wa matokeo
1633 ya uchunguzi huo. Baadhi ya matokeo ya uchunguzi huo wa lahaja
1634 yalichapishwa katika Jarida la E.A.I.L.C. Bulletin lakini mengine yali-
1635 chapishwa kama vitabu kama tutakavyoendelea kujadili.
1637 Mnamo mwaka wa 1954 jarida lilibadilishwa jina kutoka Bulletin hadi
1638 Journal. Pia jina la Kamati lilibadilishwa kutoka jina refu la East African
1639 Inter-Territorial Language (Swahili) Committee, hadi East African Swahili
1640 Committee. Katika makala ya mhariri jarida la EASC Journal Na. 24 la
1641 1954, Whiteley anaeleza kwamba hapo awali jarida lilikuwa likichapisha
1642 taarifa rasmi fupi za habari kwa raia ambayo ni maana halisi ya neno
1643 Bulletin. Anasema kwamba neno Journal linafaa zaidi kwa jarida jipya
1644 litakalokuwa kubwa kuliko Bulletin na litakalochapisha makala ndefu
1645 zaidi zenye kuamsha msisimko wa wasomi ili kuwafanya watoe mchango
1646 wao kwa kuandika makala. Kuanzia na toleo la 1954 Whiteley alitarajia
1647 matoleo yote ya jarida yawe kielelezo katika makala yote yanayochapishwa.
1649 Toleo la 1954 ni mfano bora wa aina ya jarida alilolitaka Whiteley.
1650 Lilikuwa na makala ndefu kuhusu vimiliki katika Kiswahili sanifu
1651 iliyoandikwa na O. B. Kopoka. Baada ya kupata makala ya Kopoka,
1652 katibu ambaye pia ni mhariri wa jarida, alimwuliza H. E. Lambert aandike
1653 kuhusu vimiliki katika lahaja huku akitoa mifano kutoka lahaja kadha za
1654 Kiswahili. Mwishowe anaongeza makala inayojadili vimiliki katika
1655 Kidigo kutokana na maandishi ya Z.M.S. Zani ili kulinganisha na
1659 Kiswahili na kukamilisha mjadala huu wa vimiliki. Mbali na vimiliki,
1660 jarida hili linayo makala kadha ya uchambuzi wa vitabu.
1662 Katika jarida hili la 1954 pia tunafahamishwa kwamba tayari Kamati
1663 imeanzisha uchunguzi wa lahaja za Kiswahili pamoja na uchambuzi wa
1664 matumizi ya Kiswahili katika magazeti.
1666 Katika mkutano wa kumi na saba (17) wa Kamati ya Kiswahili ya
1667 Afrika Mashariki uliokuwepo kati ya Februari 10 na 12 1954 ilikubaliwa
1668 kwamba nakala zote za Jarida la EASC Journal zitakuwa zikiuzwa
1669 kuanzia wakati huo. Kabla ya hapo nakala za E.A.I.L.C. Bulletin zilikuwa
1672 Jarida la EASC Journal Na. 25 la 1955 limechapisha makala nyingi
1673 kuhusu Kiswahili. Makala hizo ni pamoja na ya W. H. Whiteley kuhusu
1674 lahaja ya Kimvita, makala ya O. B. Kopoka inayohusu maneno yanayoishia
1675 kwa irabu yenye kuonyesha nia inayotazamia na vile yanavyotumiwa
1676 katika mashairi ya zamani ya Kiswahili. E. B. Haddon pia anaijadili hiyo
1677 nia ya kutazamia katika makala yake. Kurasa zilizobaki za jarida zinazo
1678 makala za uhakiki au uchambuzi wa vitabu pamoja na barua za wasomaji.
1680 Kujadiliwa kwa undani kwa nia inayotazamia kunatokana na utaratibu
1681 mpya wa jarida ulioanzishwa na Whiteley wa kuandika makala ya
1682 kitaaluma ya Kiswahili. Matoleo mengine ya jarida yaliyochapishwa
1683 wakati Whiteley akiwa katibu wa Kamati yalifanana na hayo yaliyojadiliwa
1684 hapo juu. Yaelekea hakukuwa na kiwango kilichowekwa cha urefu wa
1685 makala zilizochapishwa. Kati ya zile ndefu sana ni Habari za Wakilindi
1686 makala (kitabu) yenye karibu kurasa 50 iliyoandikwa na Abdallah bin
1687 Hamed bin Ali Liajjemi na kuchapishwa na EASC Journal Na. 27 1957.
1688 Orodha za istilahi au msamiati wa kitaaluma zimechapishwa katika
1689 matoleo kadha ya jarida. Kwa mfano, istilahi za uchaguzi zimechapishwa
1690 katika EASC Journal Na. 27 la 1957 na istilahi za ujenzi zimechapishwa
1691 katika EASC Journal Na. 28/1 la 1958.
1693 Katika mwaka wa 1956, mbali na kuchapisha jarida kamati ilianza
1694 kutayarisha vitabu vya ziada ambavyo vingechapishwa kama nyongeza
1695 kwa jarida. Karibu vitabu hivyo vyote vilikuwa tenzi. Utenzi wa Vita vya
1696 Wadachi kilichohaririwa na J. W. T. Allen kilikuwa tayari kimechapishwa
1697 katika mwaka 1955 kama kitabu cha ziada ya EASC Journal Na. 25.
1698 Miaka miwili baadaye Utenzi wa Vita vya Majimaji kilichoandikwa na
1699 Abdul Karim bin Jamaliddini kilichohaririwa na W. H. Whiteley kili-
1700 chapishwa kama kitabu cha ziada ya EASC Journal Na. 27 la 1957. Vitabu
1701 vingine vya ziada vilichapishwa mwaka wa 1958. Vitabu hivyo ni Maisha
1702 ya Siti Binti Saad cha Shaaban Robert EASC Journal Na. 28/1 na
1703 Maisha ya Hemed bin Mohammed, Yaani Tippu Tip Kwa Maneno Yake
1704 Mwenyewe kilichoandikwa utangulizi wa kihistoria na kufasiriwa na Bi
1708 Alison Smith. Kitabu hiki kilikuwa cha ziada ya Jarida la EASC Journal
1711 Nyongeza ya kamusi ambayo ilitarajiwa kuchapishwa kama kijitabu
1712 ilichapishwa katika jarida la EASC Na. 26 la 1956. Wazo la kuchapisha
1713 nyongeza ya kamusi lilijadiliwa katika mikutano kadha ambayo ni pamoja
1714 na mkutano wa kumi na tisa (19) wa kila mwaka wa Kamati wa Desemba
1715 1955. Maneno yaliyokusudiwa kuchapishwa katika nyongeza hiyo ya
1716 kamusi yalichapishwa katika matoleo kadha ya jarida.
1718 Wazo la kuchapisha nyongeza ya kamusi ya Kiswahili-Kiingereza na
1719 Kiingereza-Kiswahili yaonekana lilikuwa limetupiliwa mbali kufikia
1720 mwaka 1959 ambapo katibu aliulizwa atafute njia za kupata pesa za
1721 kuchapisha kamusi timilifu ya Kiswahili-Kiingereza. Wazo la kamusi
1722 mpya lilizuka baada ya kulinganisha kamusi sanifu ya Kiswahili-Kiingereza
1723 na kamusi kubwa zaidi za lugha "ndogo" kuliko Kiswahili. Kamati
1724 ilionelea kwamba ikiwa ushirikiano wa watawala wa Kibelgiji huko
1725 Kongo ungepatikana, kamusi za Kiswahili-Kiingereza na Kiswahili-
1726 Kifaransa zingechapishwa wakati mmoja. Kwa kufanya hivyo gharama
1727 ingepunguzwa na pengo kati ya Kiswahili sanifu na lahaja ya Kingwana
1730 Makala kubwa za jarida la EASC Journal la 1956 zilikuwa ni pamoja na
1731 mchangio wa Wajerumani katika somo la Kiswahili katika miongo ya hivi
1732 karibuni iliyoandikwa na Prof. E. Dammann na utafiti wa istilahi za ukoo
1733 wa Waswahili iliyoandikwa na A. H. J. Prinns. Pia jarida hilo lilichapisha
1734 makala fupi iliyoitwa "Halmashauri ya Kiswahili ya Afrika Mashariki"
1735 iliyoandikwa na Shaaban Robert wa Tanganyika. Mwandishi anasema
1736 kwamba Kiswahili kiliondolewa katika vyuo vya Uganda. Pia anatoa hoja
1737 kwamba Wakenya walikuwa wakisomesha Kilatini badala ya Kiswahili
1738 katika vyuo vyao. Ni wazi, hata ingawa Shaaban Robert hakuthibitisha
1739 hoja yake, kwamba watawala wa kikoloni walikuwa tayari wameanza
1740 kupunguza matumizi ya Kiswahili katika vituo vya elimu.
1742 Kwa mara ya kwanza, tunafahamishwa kwamba kamati ilikuwa
1743 ikikadiria mitihani ya Kiswahili ya watahini wa Chuo Kikuu cha
1744 Cambridge. Kamati ilikuwa ikiwashauri kuhusu muundo na kupendekeza
1747 Katika Jarida, EASC Journal Na. 27 la 1957, katibu, W. H. Whiteley,
1748 anaalika maoni na mchangio kwa nyongeza ya kamusi ya Kiswahili sanifu.
1749 Yaonekana hamu ya wanakamati kuendelea na shughuli zao ilikuwa
1750 imeanza kufifia kwa kuwa tawala za kikoloni za Afrika Mashariki
1753 31* Mabadiliko ya sera ya lugha yaliyojadiliwa katika sura ya nne hayakuiwezesha Kamati
1754 kutimiza lengo hili.
1758 hazikuonyesha shukrani bali ziliipuuza Kamati. Alipokuwa akiwapa
1759 moyo na kuwahimiza waandike kamusi, Whiteley aliongeza kusema
1762 "Hata ingawa kazi ya kutayarisha kamusi ya Kiswahili-Kiingereza
1763 imekaribia kwisha idadi ya maoni tuliyoyapata ni ndogo kuliko
1764 ilivyotumainiwa. Je, yawezekana wazungumzaji wa Kiswahili wakose
1765 mapenzi kwa lugha yao kiasi cha kwamba kazi muhimu kama hii
1766 inapita bila wao kujali? Ama ni wanakamati - ambao Kamati yote
1767 hutegemea - ambao wamekosa hamu ambayo wanatarajiwa kuo-
1770 Yeyote mwenye ulegevu huu wa kutojali asijiliwaze kwa kuamini
1771 kwamba hii ni kazi ya kitaaluma tu ambayo haina umuhimu wa
1772 kufaa. Mahitaji ya kuwasiliana vya kutosha tayari yamedhihirishwa
1773 kwa ukatili nchini Kenya kwa muda wa miaka minne iliyopita, na ni
1774 ujinga kudhania kwamba Kiswahili hakina matatizo kama hayo." 32*
1775 (EASC Journal Na. 27, 1957: 6).
1777 Tabia ya kutojali Kiswahili ya serikali za kikoloni za Afrika Mashariki
1778 na ulegevu wa wanakamati ulianza kudhuru moyo wa kufanya kazi wa
1779 maafisa wa Kamati. Pia katika jarida hilo hilo la 1957, mchunguzi msaidizi
1780 Bwana O. B. Kopoka anaripotiwa kuwa amehuzunishwa sana kwa kuwa
1781 wanakamati hawaonyeshi kupendezwa na kazi yake kuhusu sarufi ya
1782 Kiswahili. Kutokana na uchunguzi wa Bwana Kopoka tayari vitabu viwili
1783 vya sarufi - Miao na Matendo vilikuwa vimechapishwa. Baadaye,
1784 mwaka 1959 Bwana Kopoka alijiuzulu kazi ya mchunguzi msaidizi na
1785 akaanza kufanya kazi na Kampuni ya Shell. Baada ya kujiuzulu huko,
1786 Kamati ilisimamisha kazi za uchunguzi wa sarufi. Pia, katika jarida la
1787 Kamati Na. 30 la 1959, tunajulishwa kwamba kamati imesikitishwa kwa
1788 kufahamishwa kwamba serikali ya Tanganyika haihitaji tena sarufi na
1789 kwamba haitaki kazi aliyoifanya Bwana Kopoka (uk. 19).
1791 Katika mwaka 1958, kamati ilieleza kusikitishwa kwake na idadi ndogo
1792 ya Waafrika waliokuwa wakinunua jarida. Huku kukiwa na wanunuzi
1793 kutoka sehemu kadha za Ulaya, hakukuwa hata na mtu mmoja aliye-
1794 linunua kutoka Zanzibar. Ingawa hivyo, kwa jumla, idadi ya wanunuzi
1795 ilikuwa ikiongezeka kutoka 350 mwaka 1952, kufikia 600 mwaka 1958.
1796 Kuanzia mwaka 1958 ilikatwa shauri kuchapisha jarida mara mbili kwa
1797 mwaka kwa sababu ya kuongezeka kwa makala za kuchapishwa.
1799 Suala la ununuzi wa majarida lilizuka tena mwaka mmoja baadaye.
1802 32* Ni dhahiri kwamba sentensi ya mwisho inazungumzia juu ya hali ya hatari nchini Kenya.
1803 Serikali ya kikoloni ya Kenya iliona wazi kwamba haikuwa na ujuzi wa lugha wa kutosha
1804 kupenya njama za Mau Mau kwa kutumia Kikikuyu, Kimeru au Kiembu.
1808 Katika maoni ya mwandishi wa Jarida la Kamati - EASC Journal
1809 Na. 29/1 la 1959, Whiteley alitaja kwamba hakukuwa na Mhindi au
1810 Mwafrika yeyote aliyekuwa akilinunua hata ingawa makala kadha katika
1811 kila toleo pamoja na vitabu vyote vya ziada vilikuwa vikitarajiwa
1812 kusomwa na Waafrika. Whiteley analaumu ukosefu wa njia bora za
1813 usambazaji majarida. Ni wazi pia kwamba, tatizo hili pia lilisababishwa na
1814 kutotangazwa vyema kwa shughuli za Kamati na Kamati yenyewe haiwezi
1815 kujiepusha na lawama hii. Katika kurasa zingine za jarida hilo imetajwa
1816 kwamba, wakiwa katika shughuli za kufanya uchunguzi wa Kihadimu,
1817 Kitumbatu na Kipemba huko Zanzibar na Pemba, Kamati ilisikitika
1818 kuona kwamba watu wa Zanzibar na Pemba hawakujua kuwepo kwa
1821 Katika mkutano wa kila mwaka wa 1957, Kamati ilionyesha wasiwasi na
1822 masikitiko yake kuhusu kiwango cha chini cha Kiswahili kilichokuwa
1823 kikitumika katika vipindi vya idhaa mpya ya Kiswahili ya B.B.C.
1825 Jarida la 1958 - EASC Journal Na. 28 limechapisha makala ya
1826 mfululizo wa mihadhara mitano ya kila mwezi iliyotolewa Tanga kwa
1827 kudhaminiwa na "Jumuia ya Taaluma ya Kiswahili" ya Tanga. Sehemu ya
1828 pili ya makala ya Prinns kuhusu istilahi za ukoo wa Waswahili pamoja na
1829 majina ya Kiswahili ya samaki wa baharini pia yamechapishwa katika
1832 Kwenye mkutano wa kila mwaka wa Septemba 1958, wazo la kuanzishwa
1833 kwa kamati ya ukusanyaji, uhariri na uchapishaji wa makala za kihistoria
1834 ulijadiliwa. Iliripotiwa katika mkutano huo kwamba Liwali wa Pwani,
1835 Kenya, Sheikh Mbarak Ali El Hinawy angekuwa radhi kuwa mwenyekiti wa
1836 kamati hiyo. Hata hivyo Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ilikuwa
1837 na wasiwasi. Whiteley anatahadharisha kwamba "bila shaka familia
1838 nyingi zinashuku kwamba Wazungu wataitumia miswada yao kwa njia
1841 Hofu za Waswahili zilikuwa na msingi kwa sababu hata ingawa
1842 Wazungu walihifadhi miswada hiyo, wengine, kama vile Jan Knappert,
1843 wameichapisha baadhi ya miswada hiyo kuwa vitabu ghali sana huko
1844 Ulaya. Vitabu hivyo havipatikani Afrika Mashariki na hata vikipatikana
1845 ni ghali sana hivi kwamba wenye miswada hawawezi kupata pesa za
1846 kuvinunua licha ya kuwa baadhi yao walilipwa pesa kidogo na wengine
1847 hawakulipwa chochote kwa miswada yao. 33*
1850 33* Mifano ya vitabu vya Jan Knappert ambavyo Mswahili wa kawaida hawezi kuvigharamia
1851 ni pamoja na vitabu vya mashairi ya kiislamu Swahili Islamic Poetry vilivyochapishwa na E.
1852 J. Brill, huko Leiden, Netherlands mwaka 1971, na kitabu chenye tenzi za karne nne: Four
1853 Centuries of Swahili Verse: A Literary History and Anthology chenye kurasa 323 kilicho-
1854 chapishwa London na Heinemann mwaka 1979.
1858 Mpango ungefanywa ili miswada kama hiyo ichapishwe na Kamati ya
1859 Kiswahili ya Afrika Mashariki. Pesa ambazo zingepatikana kutokana na
1860 kuuzwa kwa vitabu vilivyochapisha zingewekwa kwenye wakfu ambao
1861 ungetumiwa kuwanufaisha Waswahili kwa njia kama vile kugharamia
1862 masomo ya juu ya watoto wao, kugharamia uchunguzi zaidi, au kwa
1863 huduma za jamii. Kamati ilijua wazi kwamba Waswahili hawakuwa tayari
1864 kupeana miswada yao, na hiyo ndiyo sababu walihitaji msaada wa watu
1865 mashuhuri wa pwani kama vile Liwali Sheikh Mbarak Ali el Hinawy.
1867 Kamati ya kihistoria iliundwa. Ilikutana kwa mara ya kwanza tarehe 27
1868 Juni 1959. Wafuatao walihudhuria:
1869 1) Sheikh Mbarak Ali El Hinawy.
1870 2) Bwana J. S. Kirkman wa Mombasa.
1871 3) Bwana J. W. T. Allen - Katibu mtendaji wa Kamati ya
1872 Kiswahili ya Afrika Mashariki.
1873 4) Bwana Shihabuddin Chiraghdin - wa Mombasa.
1874 5) Sheikh Hyder Mohammed El Kindy - wa Mombasa ambaye
1875 alikuwa katibu wa hii kamati ndogo.
1877 Wanachama wafuatao wa hiyo kamati waliomba radhi kwa kutoweza
1879 1) Sir John Grey wa Zanzibar.
1880 2) Sir Said bin Ali Mugheiry wa Pemba.
1881 3) Dkt. G. S. P. Freeman-Grenville wa Mafia.
1882 4) Sheikh Muhammad Kassim Mazrui wa Malindi.
1883 5) Sheikh Mohammed bin Ali bin Hamed Buhry wa Tanga.
1885 Kamati hiyo ilipewa jukumu la kukusanya miswada mingi ya kihistoria
1886 iwezekanavyo. Ilikubaliwa kwamba makala na miswada yote itakayo-
1887 kusanywa atapelekewa katibu katika chuo cha Makerere. Katibu ali-
1888 takikana kuiorodhesha na kuipa nambari miswada hiyo na ikiwezekana
1889 angeinakili na kuipeleka nakala moja kwa mwenyekiti na nyingine kwa
1890 mwenye mswada kama shukrani kwa ushirikiano wake - (Tazama:
1891 EASC Journal Na. 30, 1959: 13). Yaonekana kwamba suala la mwenye
1892 haki za kunakili na kuchapisha miswada na makala hayo halikushughu-
1895 Zaidi ya hayo, Kamati iliamua kuchunguza uwezekano wa kupiga picha
1896 ndogo (microfilm) maandishi ya kale yaliyokuwa katika hifadhi za
1897 Makerere na Mombasa. Katibu aliombwa kutafuta msaada wa pesa
1898 kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada ili kuwezesha ukusanyaji wa
1899 miswada. Kiasi fulani cha pesa kilitumiwa kununua miswada kutoka kwa
1900 watu ambao hawakuwa tayari kuitoa bure.
1902 Ripoti ya mkutano wa 21 wa kila mwaka uliokuwepo kati ya tarehe 10
1903 na 13 Septemba 1958 huko Tanga, Tanganyika, imechapishwa katika
1907 jarida Na. 28/1 la 1958. Kamati ilijadili hali ya baadaye ya Kamati kwa vile
1908 kushirikishwa kwake kwenye Taasisi ya Uchunguzi wa Shughuli za Jamii
1909 ya Afrika Mashariki katika Chuo cha Makerere kwa kipindi cha miaka
1910 mitano kungemalizika mwisho wa mwaka wa masomo wa 1959/60.
1911 Wakati huo Taasisi ilikuwa ikigharamia nusu ya mshahara wa katibu na
1912 hakukuwa na uhakika ikiwa pesa zingepatikana na kuigharamia kamati
1913 baada ya hapo. Wanachama wa Kamati walikubaliana kuonyesha
1914 umuhimu wa Kamati kwa serikali zao ili kuiwezesha Kamati kupata pesa
1915 baada ya kwisha kwa muda wa kuwa kwenye Taasisi. Makisio mapya ya
1916 kuigharamia kamati yalipelekewa serikali (zote) ili kufikiriwa.
1918 Kufikia wakati wa mkutano uliofuata wa kila mwaka kati ya tarehe 9 na
1919 11 Septemba huko Mombasa, serikali za Afrika Mashariki zilikuwa bado
1920 hazijajibu ombi la Kamati. Kwa hivyo Kamati haikuwa na uhakika iwapo
1921 wangepata pesa ambazo walikuwa wameomba. Ilionekana kwamba
1922 Kamati zaidi ilikuwa chombo cha uchunguzi ambacho kingegharamiwa
1923 na serikali mpaka kitakapojiunga vizuri na Chuo Kikuu.
1925 Katika ripoti ya kila mwaka ya 1958 - 1959 iliyochapishwa kwenye
1926 EASC Journal Na. 30 la 1959, katibu mpya J. W. T. Allen anaeleza
1927 kwamba Kamati ilipata shida kubwa za kiidara kwa sababu ya kuondoka
1928 kwa katibu W. H. Whiteley, msaidizi wake Bi. Fawler na Bwana O. B.
1929 Kopoka. Pia anaripoti kwamba hakukuwa na matumaini ya kupata pesa
1930 zingine kutoka kwa serikali. Ilibidi Kamati ipunguze gharama zake kwa
1931 kuajiri makarani wa muda inapowezekana na kwa kuhamisha ofisi za
1932 Kamati hadi University Hall ambapo Allen alikuwa akifanya kazi ya
1933 mlinzi. Ilibidi maktaba ya Kamati iwekwe amana katika maktaba ya Chuo
1934 Kikuu cha Makerere kwa sababu ya kukosa chumba kulikosababishwa na
1937 Uamuzi wa kupunguza matumizi zaidi. ulifikiwa katika mkutano wa kila
1938 mwaka uliokuwepo kati va tarehe 4 na 5 Septemba 1959. Katika mkutano
1939 huo, Kamati ilikata shauri kutochapisha vitabu vya ziada tena kwa sababu
1940 ya gharama kubwa ya uchapishaji. Kwa bahati nzuri Kamati ilikuwa na
1941 ushirikiano bora na East African Literature Bureau na mkurugenzi wake,
1942 C. G. Richards, alikuwa amehudhuria mkutano huo. Badala ya vitabu
1943 hivyo vya ziada ya majarida, East African Literature Bureau ilikubali
1944 kuanza kuchapisha mfululizo wa vitabu wenye kujulikana kama Johari za
1945 Kiswahili. Wangeanza kuchapisha vitabu viwili viwili kila mwaka.
1946 Ilikubaliwa pia kwamba vitabu vya kwanza vya Johari za Kiswahili
1947 ambavyo vingechapishwa na Kamati kama vitabu vya ziada ya majarida
1949 1) Utenzi wa Vita vya Wadachi.
1950 2) Utenzi wa Abdirrahmani na Sufiyani.
1955 4) Utenzi wa Seyyida Hussein bin Ali. 34*
1957 Mkurugenzi wa East African Literature Bureau pia alikubali kuchapisha
1958 toleo jipya la kitabu kilichosahihishwa cha Tippu Tip.
1960 Kufikia mwaka 1959 vitabu vifuatavyo vya uchunguzi wa lahaja za
1961 Kiswahili vilikuwa tayari vimechapishwa na Kamati ya Kiswahili ya
1963 1) Ki-Mtang'ata - A Dialect of Mrima Coast na W. H. Whiteley,
1965 2) Ki- Vumba - A Dialect of the Southern Kenya Coast na H. E.
1967 3) Chi-Jomvu and Ki-Ngare - Sub dialects of the Mombasa
1968 Area na H. E. Lambert, 1958.
1969 4) The Dialects and Verse of Pemba - An Introduction na W. H.
1971 5) Chi-Chifundi - A Dialect of The Southern Kenya Coast na
1974 Kwa sababu ya matatizo ya kipesa ya Kamati, Allen aliandika maoni ya
1975 mhariri ya EASC Journal Na. 30 la 1959 na kutishia kwamba Kamati ya
1976 Kiswahili ya Afrika Mashariki haingeweza kuendelea kufanya kazi yake
1977 kikatiba. "Ni lazima ipanuke, iwe kitu kikubwa au ikomeshe jitihada za
1978 kuendelea", akaandika. Anailaumu nia mbaya ya kikoloni ya kupuuza na
1979 kutojali Kiswahili kwa kusababisha mashaka hayo ya Kamati. 35*
1981 Allen anaeleza kwamba Kamati ni kama mji uliozingirwa. Ikikoma
1982 kujitahidi itapoteza kile kilichochukua miaka mingi ya kazi ngumu
1983 kukipata. Lingine la kufanya ni kwa kamati kuvumilia kuendelea na
1984 kutumaini kwamba watapata mwokozi. Kamati ilikuwa katika hali ya
1985 kukata tamaa, na Allen alijitahidi juu chini kutafuta msaada wa pesa
1986 kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada.
1988 Kwenye mkutano wa Kamati wa kila mwaka uliokuwepo mwezi
1989 Septemba 1959 Kamati ilijulishwa kwamba Chuo Kikuu cha Makerere
1990 kilikuwa kimependekeza kuundwa kwa kamati ya chuo ya kushughulikia
1991 somo la Kiswahili. Kamati hiyo ingetoa mapendekezo yake kwa Kamati
1992 ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.
1994 Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Kamati ilikubali pendekezo la
1995 kamati ya chuo kikuu la kuanzishwa kwa Taasisi ya Uchunguzi wa
1996 Kiswahili. Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ilikubali pendekezo
1997 hilo hata ingawa ilielewa wazi kwamba kuendelea kwa "Kamati kungeishia
2000 34* Majina kamili, pamoja na watunzi au waandishi na wahariri yapatikana katika bibliografia.
2001 35* Tazama sehemu ya kubadili sera dhidi ya Kiswahili katika sura ya Tano ambapo Allen
2002 amenukuliwa kwa kireru.
2006 kwenye mwanzo wa kipindi kipya cha miaka mitano (au mapema zaidi)".
2007 Kamati vilevile ilipendekeza kwamba, kamati ya chuo ihakikishe kwamba
2008 washauri wenye ujuzi wa isimu, elimu jamii na historia wanashirikishwa
2009 katika kuanzishwa kwa taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Kamati vile
2010 vile ilitaraji kwamba, serikali za Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar
2011 zitaendelea kuisaidia Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili kifedha ikiwa
2012 Makerere au ikihamia katika chuo kikuu kingine.
2014 Makala kuu zilizochapishwa mwakawa 1960 (EASC Journal Na. 31) ni
2015 pamoja na sehemu ya pili ya makala ya Sir John Gray kuhusu historia ya
2016 Zanzibar, sehemu ya pili ya makala ya W. H. Whiteley kuhusu lahaja ya
2017 Zanzibar mashambani na makala ya Mwidani bin Mwidadi iliyohaririwa
2018 na Lyndon Harries kuhusu kuanzishwa kwa mji wa Rabai. (Sehemu za
2019 kwanza za makala ya Sir John Gray na W. H. Whiteley zilichapishwa
2020 katika EASC Journal Na. 30 la 1959.) Mjadala wa matumizi ya Kiswahili
2021 nchini Zaire, Rwanda na Burundi ulioandikwa na Hamis Kitumboy na
2022 makala ya B. Lecoste kuhusu sarufi ya Kiswahili cha Kongo ya Ubelgiji
2023 (Zaire) yalichapishwa pia katika jarida hilo la 1960.
2025 Mnamo tarehe 23 Mei 1961 ilitangazwa huko Makerere kwamba Wakfu
2026 wa Calouste Gulbenkian ya Lisbon umetoa msaada wa pauni elfu tisa
2027 (?9000) na kwamba kiasi kama hicho kitatolewa na Hazina ya Maendeleo
2028 ya Makoloni. Pesa hizo zilitolewa kugharamia mchunguzi mmoja na
2029 wasaidizi wake kwa miaka mitatu pamoja na usafiri na gharama zingine ili
2030 kukiwezesha Chuo Kikuu cha Makerere kianzishe Taasisi ya Uchunguzi
2033 Ripoti hiyo iliyotolewa kwa magazeti pia inaeleza kwamba Afrika
2034 Mashariki pamoja na Kongo (Zaire), wana lugha moja kuu ya mawasiliano
2035 ambayo hueleweka kwa urahisi na Waafrika wa eneo hilo, kwa sababu
2036 imefanana sana na lugha zao. Inapendekezwa kwamba chuo au taasisi ya
2037 uchunguzi wa Kiswahili ianzishwe kwa kupanua kazi za Kamati ya
2038 Kiswahili ya Afrika Mashariki ili kukuza uchunguzi katika lugha ya
2039 Kiswahili. Pia inaelezwa kwamba serikali za Afrika Mashariki zingeendelea
2040 kugharamia shughuli za kiidara ili pesa zilizotolewa zitumike zaidi katika
2041 shughuli za uchunguzi.
2047 5.0 Kiswahili na sera ya lugha
2049 5.1 Kiswahili na sera ya lugha nchini Uganda
2051 Historia ya maendeleo na usanifishaji wa Kiswahili pamoja na shughuli
2052 za Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki hugusia zaidi vile hali
2053 ilivyokuwa Tanzania na Kenya kuliko Uganda. Labda sababu yake ni
2054 kwamba Kiswahili hakikupewa nafasi ya kuenea huko kama kilivyoenea
2055 Kenya na Tanzania. Wabaganda walipinga kusomeshwa kwa Kiswahili
2056 katika shule zao wakati ambapo serikali ya kikoloni ilikuwa tayari kukuza
2057 Kiswahili. Wakati sera ya lugha ilipobadilika dhidi ya Kiswahili kote
2058 katika Afrika Mashariki kuanzia muongo wa 1950 Kiswahili kiliondolewa
2059 shuleni kwa kuwa hakikuwa tena lugha iliyotambulika kusomeshwa
2060 nchini Uganda. Kabla sijayajadili mabadiliko ya sera ya lugha dhidi ya
2061 Kiswahili, kwanza nitaijadili sera ya lugha nchini Uganda, na vile
2062 ilivyokuwa ikibadilikabadilika, kufikia wakati Kiswahili kilipoondolewa
2065 Kuanzia mwaka wa 1925 suala la ni lugha zipi za Kiafrika zitakazo-
2066 tumika kusomesha katika madarasa ya mwanzo ya shule za msingi kote
2067 nchini Uganda, lilijadiliwa na serikali ya kikoloni. Kwanza uamuzi
2068 ulitolewa kwamba Kiluganda itumike katika eneo lote lililokuwa likitumia
2069 lugha za Kibantu. Kisha kamati ikaundwa kuchagua lugha muafaka ya
2070 kutumia katika eneo la Kinailoti la Mikoa ya Kaskazini na Mashariki.
2071 Kamati hiyo pia ilitakikana kutayarisha tafsiri ya vitabu vya shule katika
2072 lugha zilizochaguliwa. Kiingereza kingetumika kuanzia madarasa ya juu
2073 ya shule za msingi na kuendelea.
2075 Mwaka 1926 Idara ya Elimu iliamua kutumia lugha tatu za Kiafrika
2076 katika shule za msingi.
2079 1) Kiluganda - iliyotumiwa Buganda na sehemu ya kaskazini ya
2081 2) Kiacholi - iliyotumiwa katika Mkoa wa Kaskazini.
2082 3) Kiateso - lugha iliyotumiwa katika shule za eneo la kati la
2085 Lugha zingine zote za Kiafrika zilitambuliwa kuwa "lahaja ndogo"
2086 ambazo hazingetumiwa ila katika shule za malezi. Kiwango hicho cha
2090 elimu kilisemekana kwamba hakikuhitaji vitabu na kwamba wanafunzi
2091 wengi hawakuendelea na masomo huko kwa kuwa walijiunga na shule za
2092 msingi ambako wangetumia moja kati ya lugha tatu zilizochaguliwa. 36*
2094 Kufikia 1927 vitabu kadha vilikuwa vimeandikwa kwa Kiluganda
2095 lakini kulikuwa na matatizo katika zile lugha zingine mbili. Gavana
2096 aliandika kumbukumbu kuhusu jambo hili, nalo baraza la kutoa mashauri
2097 kuhusu elimu ya Waafrika likaijadili kwa kirefu. Matokeo yake ni
2098 kwamba ilionekana muafaka Kiacholi na Kiateso zitumiwe kama lugha za
2099 kusomesha katika shule za msingi zilizokuwa katika maeneo hayo tu (ya
2100 Acholi na Teso). Ilikubaliwa kwamba Kiswahili kisomeshwe kama somo
2101 katika shule za msingi na kwamba vitabu vya masomo kama vile afya,
2102 jiografia na kilimo viandikwe kwa Kiswahili. 37*
2104 Uamuzi wa kusomesha Kiswahili ulifikiwa kwa sababu ya matatizo
2105 ambayo hayakuweza kutatuliwa wakati huo ya kutafsiri vitabu kwa lugha
2106 za Kiateso na Kiacholi. Sababu nyingine kubwa pia ni ile athari
2107 iliyotokana na kutumiwa kwa Kiswahili katika nchi jirani za Kenya,
2108 Tanganyika na Zanzibar. Ripoti ya Idara ya Elimu ya Mwaka wa 1927
2109 inaongeza kwamba "Aidha lugha hizi mbili si lugha za kwanza za watu
2110 wengi walioko katika maeneo hayo, na kwao Kiswahili hakitakuwa shida
2111 kukielewa kuliko Kiateso na Kiacholi" (uk. 10).
2113 Kwa hivyo sera ya lugha iliruhusu kutumiwa kwa lugha za kwanza
2114 kusomesha wanafunzi wote katika miaka miwili ya kwanza ya masomo
2115 kiwango ambacho vitabu havikuhitajika sana. Baada ya kiwango hicho,
2116 wanafunzi walianza kujifunza Kiswahili, lugha ambayo iliwawezesha
2117 kusoma idadi kubwa ya vitabu ambavyo vilikuwa vikiongezeka kwa
2118 wingi. Kiswahili kilitambuliwa kuwa lugha ya pekee ambayo ingerahisisha
2119 mawasiliano katika nchi za Afrika Mashariki. Kilitambuliwa kuwa lugha
2120 ya watu wengi ambayo ingetumiwa katika kuvichapisha vitabu vingi vya
2121 shule na vya fasihi. Gavana Gowers aliyekuwa Gavana wa Uganda wakati
2122 huo alikiunga mkono Kiswahili. Katika mwaka 1928 alipendekeza
2123 Kiswahili kitumiwe badala ya Kiluganda kama lugha ya elimu na utawala
2124 nchini Uganda (Ladefoged et. al. 1971: 88).
2126 Sera hii ya kufunza lugha za kwanza zikifuatiwa na Kiswahili ilifuatwa
2127 katika mikoa yote ya Uganda isipokuwa mkoa wa Buganda. Hapo
2128 mwanzoni Kiswahili kilipingwa katika Mkoa wa Mashariki, lakini
2129 baadaye kilikubalika kuliko Kiluganda ambayo ingetumiwa ikiwa
2130 Kiswahili hakingetumika. Katika Mikoa ya Kaskazini na Magharibi
2131 mabadiliko ya kuanza kutumia Kiswahili yalitajwa kuwa "yalipendwa
2134 36* Education Department, Annual Report ya 1926 uk. 11.
2135 37* Education Department, Annual Report ya 1927 uk. 10.
2139 sana na watu wote". 38* Kwa sababu ya sera hii mpya ya lugha, vitabu vya
2140 shule vilivyokuwa vikitumiwa Tanganyika vilianza kutumika katika shule
2141 za Uganda kuanzia mwaka 1928. Pia Mkurugenzi wa Elimu nchini Uganda
2142 alipendekeza kuanzishwa kwa shirika la kutafsiri vitabu vya Kiswahili ili
2143 kuhudumia nchi za Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar.
2145 Mwaka 1928 Ronald Snoxall alihamishwa kutoka Tanganyika kwenda
2146 Uganda kama Msimamizi wa Elimu ya Msingi. Snoxall alikuwa na ujuzi
2147 wa nchi ambayo ilikuwa ikitumia Kiswahili kama lugha ya kufunza katika
2148 shule za msingi. Idara ya Elimu ya Uganda ilihitaji msaada wake katika
2149 jaribio la kufuata sera ya lugha ya Tanganyika. 39* Vituo vya elimu
2150 vilivyokuwa vikihudumia nchi nzima yaonekana viliunga mkono kwa
2151 dhati sera mpya kuhusu Kiswahili. Shule ya Ufundi ya Kampala, kwa
2152 mfano, iliamua kutofundisha Kiingereza. Badala ya Kiingereza, Kiswahili
2153 kilifundishwa kwa kuwa ndicho lugha ya mawasiliano kote Afrika
2154 Mashariki. Kama alivyosema mkuu wa shule hiyo, Bwana Savile, shule
2155 hiyo ilikuwa ikihudumia nchi nzima pamoja na watu wenye kuzungumza
2156 lugha zisizo za Kibantu ambao hawangeielewa Kiluganda.
2158 Mwezi Januari 1928 chuo cha serikali cha kufunza walimu wa shule za
2159 msingi kilianzishwa. Katika chuo hiki, Kiswahili kilitumiwa kama lugha
2162 Katika ripoti yake ya 1928 mkuu wa chuo hicho, Kampala Normal
2163 School, A. J. Lush, alisema kwamba mitihani ya Kiswahili ilionyesha
2164 maendeleo ya kuridhisha katika mazungumzo na maandishi. Mwalimu wa
2165 Kiswahili, Sheikh Abdul Rahman Mahomet, aliajiriwa kutoka Zanzibar
2166 mwaka huo wa 1928. Mwezi Februari 1929 mkuu wa chuo pamoja na
2167 wanafunzi wake sita walitembelea Mombasa ambako walijifunza Kiswahili
2168 kwa muda wa miezi mitatu.
2170 Matumizi ya Kiswahili yalikuwa yakienea vizuri kote nchini Uganda
2171 mwaka 1929 isipokuwa Buganda. Wanafunzi wa Uganda kutoka shule za
2172 serikali na za misheni walipelekwa Mombasa, Kabaa na Zanzibar ili
2173 kupewa mafunzo ya Kiswahili. Vilevile Kiswahili kilifunzwa kwa mafanikio
2174 katika chuo cha walimu cha misheni ya C.M.S. Mukono na chuo cha
2175 walimu cha misheni ya White Fathers, Bikira. Katika vyuo kadha
2176 Kiswahili kilifunzwa badala ya Kiingereza.
2178 Urahisi wa Mwafrika kujifunza lugha nyingine ya Kiafrika badala ya
2179 Kiingereza ulitambuliwa. Kiswahili kilionekana kwamba kinafaa kuliko
2180 lugha zingine za Kiafrika kwa sababu kulikuwa na vitabu vingi vilivyo-
2181 andikwa kwa Kiswahili. Haingewezekana kuchapisha vitabu vyote
2184 38* Education Department, Annual Report 1928 uk. 9.
2185 39* Education Department, Annual Report ya 1928 uk. 6.
2189 vinavyohitajika shuleni katika lugha nyingi za Kiafrika kwa sababu ya
2190 gharama ya kuchapisha nakala chache kwa kila lugha. Vitabu vya
2191 Kiswahili viliuzwa kwa wingi nchini Uganda. Kuanzishwa kwa kamati ya
2192 Kiswahili ya Afrika Mashariki kulikuwa kunangojewa kwa hamu nchini
2193 Uganda kwa kuwa kungesaidia kuchapishwa kwa vitabu vingi vya
2196 Ripoti ya maendeleo ya misheni ya C.M.S. ya Elgon inaonyesha
2197 kwamba walianza kufunza Kiswahili kwa mara ya kwanza mwaka 1929.
2198 Baadhi ya walimu na wanafunzi wa chuo cha walimu cha misheni hiyo
2199 walipelekwa Mombasa kufunzwa Kiswahili ili wasaidie katika kuanzishwa
2200 kwa somo la Kiswahili. 40* Wakati huo huo, Katibu wa Elimu wa shule za
2201 misheni Katoliki ya Mataliani, W. Gotta alitoa ripoti kwamba hata
2202 ingawa Kiswahili kilikuwa somo jipya, kilipokelewa vizuri katika madarasa
2203 ya shule za msingi na vyuo vya walimu katika eneo la Gulu. Baadhi ya
2204 shule za msingi za Gulu, Kitgum, Moyo, Ama na Ngal zilikuwa na
2205 matatizo ya kusomesha Kiswahili. Lakini iliripotiwa kwamba masista
2206 wote waliokuwa wakiongoza shule hizo walikuwa tayari wamekwenda
2207 Dar es Salaam ili kujifunza Kiswahili.
2209 Ripoti ya Koloni ya Uganda ya mwaka 1929 inasema yafuatayo kuhusu
2210 maendeleo ya Kiswahili:
2212 "Ufunzaji wa Kiswahili tayari umeanzishwa katika Mkoa wa Masha-
2213 riki na maendeleo mazuri yamepatikana. Lugha hii itasomeshwa
2214 kote katika vyuo vya kufunza walimu wa shule za vijijini isipokuwa
2215 Buganda. Vitabu vilivyoko, ambavyo vimekusudiwa kutumiwa na
2216 makabila ya Afrika Mashariki yanayojua Kiswahili havifai kwa
2217 makabila ya bara ambao wanaanza kujifunza lugha hiyo; utayarishaji
2218 wa vitabu vinavyofaa zaidi yafaa iwe kazi ya kwanza ya Kamati
2219 mpya ya Kiswahili ya Afrika Mashariki." 41*
2221 Juhudi za kueneza ufunzaji wa Kiswahili nchini Uganda zilivuma
2222 mwaka 1930 wakati mradi mahsusi wa kufunza walimu wa vijijini kwa
2223 miaka miwili ulipoanzisha vituo 29 kote katika Mikoa ya Mashariki,
2224 Kaskazini na Magharibi. Masomo yaliyokuwa yakifunzwa ni dini, kilimo,
2225 mbinu za kufunza, afya na Kiswahili. Ufunzaji wa Kiswahili ulinuiwa
2226 kuhakikisha kwamba walimu wa gredi C watakaofaulu watakuwa wame-
2227 jiandaa vya kutosha kusitawisha ufunzaji wa Kiswahili katika shule zao.
2228 Wawakilishi wawili wa serikali na wengine wawili wa misheni waliwakilisha
2229 Uganda kwenye mkutano wa kwanza wa kamati ya Kiswahili ya Afrika
2230 Mashariki uliokuwepo Nairobi mwezi Aprili 1930.
2233 40* Education Department, Annual Report ya 1929 uk. 31.
2234 41* Uganda Annual Colonial Reports: Annual Report 1929, uk. 31, London, 1930.
2238 Sera hii ya kueneza Kiswahili iliendelezwa na misheni mwaka wa 1930.
2239 Misheni ya C.M.S. iliripoti kuenea kwa matumizi ya Kiswahili bora.
2240 Misheni ya White Fathers iliwafunza Kiswahili walimu wa zamani kumi
2241 na watatu ili wahitimu kuwa walimu wa kudumu. Katibu wa Elimu wa
2242 misheni ya White Fathers, C. Robbiard alisema kwamba ni rahisi sana
2243 kwa Mwafrika kujifunza lugha nyingine ya Kiafrika hivi kwamba baadhi
2244 ya walimu wao walijifunza wenyewe. 42*
2246 Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ilikutana Makerere Uganda
2247 mwezi Aprili 1931 kwa mara ya kwanza. Katika mkutano huo kazi
2248 muhimu ilikamilishwa kuhusu usanifishaji wa uandikaji wa maneno ya
2249 Kiswahili yaliyoazimwa kutoka lugha za kigeni.
2251 Mwezi Juni 1931 Baraza la Kutoa Mashauri Kuhusu Elimu ya Waafrika
2252 lilikutana na kutoa maoni kwamba Kiluganda iendelee kuwa lugha ya
2253 kusomesha masomo mengine katika Mkoa wa Buganda na kwamba
2254 Wabaganda wakipenda wanaweza kuanzisha somo la Kiswahili. Pia
2255 shauri ilikatwa kwamba walimu wa vyuo vya walimu vya serikali
2256 wafunzwe ili kusomesha Kiswahili katika shule ya King's African Rifles
2257 (KAR), shule za polisi, na shule zingine za msingi zilizoko kwenye maeneo
2258 yenye lugha tofauti. Baraza hilo la kutoa mashauri pia lilisema kwamba:
2260 "Vyuo vya walimu vya misheni vinavyopata ruzuku vya Nabumali,
2261 Ngora, Arua, na Gulu lazima vifunze Kiswahili kwa wanafunzi
2262 wanaosomea huko. Kwamba katika maeneo yenye mchanganyiko
2263 wa lugha, Kiswahili kisomeshwe kama somo la shule za msingi mara
2264 tu walimu wanapopatikana kutoka vyuo hivyo, lakini lugha za
2265 kwanza za maeneo hayo ziendelee kuwa lugha za kufundishia.
2266 Kwamba, Kiswahili kisomeshwe katika chuo cha ufundi cha serikali
2267 ambacho kitasomesha vijana kutoka kote nchini." 43*
2269 Pingamizi ya kwanza kubwa dhidi ya Kiswahili ilianza mwezi Septemba
2270 1931 wakati maaskofu wa misheni nne za Church Missionary Societies,
2271 pamoja na Kabaka wa wakati huo, Sir Daudi Chwa, walipomkabidhi
2272 Waziri wa Nchi anayesimamia Makoloni (ya Uingereza) kumbukumbu
2273 kulalamika dhidi ya kutumiwa kwa Kiswahili kama lugha ya pekee ya
2274 kusomesha masomo mengine katika shule za msingi. Nilipomhoji Ronald
2275 Snoxall alikiri kwamba karibu wahubiri wote wa Church Missionary
2276 Society (C.M.S.) walikuwa Wabaganda waliotaka kueneza lugha yao ya
2277 Kiluganda. Walitoa madai ya uwongo kwamba watu wote nchini Uganda
2278 walifahamu Kiluganda. Katika kumbukumbu yao, maaskofu pamoja na
2279 Kabaka walidai kwamba watu walikuwa wakilazimishwa kujifunza
2282 42* Uganda Annual Colonial Reports. Annual Report ya 1929 uk. 31, London, 1930.
2283 43* Education Department, Annual Report ya 1931, uk. 6.
2287 Kiswahili kinyume cha kupenda kwao. Dai hili halikuwa la kweli. Sera ya
2288 lugha ya Gavana Sir William Gowers ilihimiza Kiswahili katika maeneo
2289 yenye mchanganyiko wa lugha yaliyokuwa nje ya Buganda. Kwa sababu
2290 ya pingamizi hii dhidi ya Kiswahili wamisheni wengi walikosa hamu ya
2291 kujifunza lugha hii.
2293 Jibu la Idara ya Elimu lilisema kwamba kumbukumbu hiyo ilitokana na
2294 kutoielewa sera ya serikali ya kutumiwa kwa lugha za kwanza katika
2295 madarasa mawili ya kwanza ya shule za msingi na kutumiwa kwa lugha
2296 hizo za kwanza pamoja na Kiswahili kama lugha za kusomesha masomo
2297 mengine katika madarasa mawili yafuatiayo. Kumbukumbu haikutaka
2298 Uganda itumie Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kama nchi zingine za
2299 Afrika Mashariki kwa kuwa walitaka lugha ya Uganda (bila shaka -
2300 Kiluganda), iwe lugha ya mawasiliano nchini Uganda. Waganda, na zaidi
2301 Wabaganda, waliogopa na kwa hivyo hawakutaka kuanzishwa kwa
2302 shirikisho la Afrika Mashariki (Tazama Ladefoged et al 1971: 89).
2304 Mwaka 1932 suala la lugha ya kusomesha masomo mengine lilitatuliwa
2305 na serikali iipoamua kwamba masomo yote isipokuwa hesabu (hisabati)
2306 yasomeshwe kwa kutumia lugha za kwanza za maeneo mbalimbali. Somo
2307 la hesabu lilisomeshwa kwa Kiswahili, lugha ambayo wakati huo ilikuwa
2308 ikisomeshwa kama somo katika shule zote za msingi nje ya eneo la ufalme
2309 wa Buganda na Wilaya ya Busoga. Ripoti ya mwaka ya Koloni, ya 1931,
2310 ilionyesha kwamba Kiswahili kilikuwa kikianzishwa kwa utaratibu kama
2311 lugha ya kusomesha masomo mengine katika madarasa mawili ya mwisho
2312 ya shule za msingi katika wilaya zinazotumia lugha za Kinailoti. Katika
2313 Wilaya za Kibantu, Kiswahili kilikuwa kikisomeshwa kama somo isipo-
2314 kuwa katika Mkoa wa Buganda na Wilayani Busoga ambapo Kiluganda
2315 ilikuwa ikitumiwa katika madarasa yote ya shule za msingi. Ripoti za
2316 koloni za kila mwaka zilirudia habari hizi kati ya 1931 na 1936. Katika
2317 mwaka 1937 Ripoti ya Mwaka ya Koloni ilitaja kwamba Kiswahili
2318 kilisomeshwa kama somo katika madarasa mawili ya mwisho ya shule za
2319 msingi. Haya yalikuwa mabadiliko, lakini mradi Kiswahili kiliendelea
2320 kuwa katika ratiba ya masomo ni hakikisho kwamba kilikuwa kikienea
2321 kama lugha ya mawasiliano nchini Uganda.
2323 Ubora wa Kiswahili kikilinganishwa na Kiingereza ulitiliwa mkazo tena
2324 na Bwana E. G. Morris, Mkurugenzi wa Elimu, katika Ripoti ya Mwaka
2325 1932. Morris aliandika yafuatayo:
2327 "Huku inapomchukua kijana hodari Mwafrika muda wa miezi sita tu
2328 kujifunza lugha ili aweze kukisoma kitabu cha Kiswahili na kukielewa
2329 barabara, ingemchukua angalau miaka sita ya kujifunza Kiingereza
2330 kwa makini ili aweze kukielewa kitabu cha Kiingereza cha kiwango
2331 sawa. Ni vigumu kuelewa vile watetezi wa Kiingereza wanavyotaraji
2335 kusitawisha elimu ya Waafrika kwa kutumia lugha ya Ulaya kama
2336 lugha ya kusomesha masomo mengine." 44*
2338 (Inasikitisha kwamba baada ya zaidi ya nusu ya karne moja tangu
2339 maneno hayo yaandikwe vile hali ilivyo siyo tu kwamba lugha hiyo ya
2340 Ulaya ndiyo inasomesha bali Kiswahili kilichokuwa kikitetewa hata
2341 hakisomeshwi kama somo katika shule za msingi nchini Uganda).
2343 Katika "shule za kati" (shule ambazo zilitoa mafunzo ya kazi) lugha ya
2344 kusomesha ilikuwa ama Kiluganda katika eneo la kifalme la Buganda na
2345 Wilaya ya Busoga au Kiswahili katika sehemu zingine za Uganda.
2347 Lugha ya kusomesha katika vyuo vya walimu vya serikali ilikuwa ni
2348 Kiswahili. Ili kuonyesha vile ilivyokuwa rahisi kwa Waafrika kujifunza
2349 Kiswahili E. G. Morris anatoa mfano wa Mwalimu Omwami Y. Kakoza
2350 aliyeanza kujifunza mwezi Januari 1932 na ilipofika Septemba mwaka
2351 huo alifaulu mtihani wa Lower Government Standard Examination kwa
2352 kupata alama za juu zaidi - asilimia 89 1/2.
2354 Mwaka 1934 Kamati Kuu ya Church Missionary Society ya Diocese ya
2355 Elgon iliamua kwamba kuanzia wakati huo, masomo yote katika Chuo
2356 cha Kidini na cha Walimu cha Bawalasi yatasomeshwa kwa Kiswahili. Pia
2357 Kamati Kuu iliamua kutumia Kiswahili katika shule za msingi za misheni
2358 zilizokuwa katika maeneo ya mchanganyiko wa lugha.
2360 Mwaka 1935 mabadiliko yalifanywa kuhusu majina ya viwango tofauti
2361 vya elimu. Badala ya shule za malezi, shule za msingi, shule za kati ya chini,
2362 kati ya juu na sekondari ya chini, zote zilijulikana kama shule za msingi au
2363 shule za sekondari. Kila kiwango kilikuwa cha miaka sita. Mkaguzi
2364 wa shule za msingi katika mwaka huo wa 1935 alilalamika kwamba
2365 kulikuwa na uhaba wa vitabu vya shule vilivyoandikwa kwa lugha za
2366 kwanza zilizokuwa zikitumiwa kusomesha. Wakati huo huo kulikuwa na
2367 ongezeko la vitabu vya Kiswahili, lugha ya mawasiliano nje ya Mkoa wa
2368 Baganda na Wilaya ya Busoga. Serikali ilionyesha wasiwasi kuhusu
2369 kushuka kwa kiwango cha Kiingereza mashuleni kwa sababu walimu
2370 waliotarajiwa kukifundisha walikosa mazoezi baada ya kupelekwa kufanya
2373 Mkutano wa kila mwaka wa Wakurugenzi wa Elimu wa Kenya,
2374 Uganda, Tanganyika na Zanzibar ulikuwa Makerere katika Februari na
2375 Machi 1936. Kati ya mambo waliyoafikiana ni kwamba kulikuwa na
2376 umuhimu wa kuongeza vitabu vya Kiswahili. Hali ya Kiswahili nchini
2377 Uganda ilitiliwa nguvu na mkutano wa kila mwaka wa Kamati ya
2378 Kiswahili ya Afrika Mashariki uliokuwepo Makerere mwezi Februari
2381 44* Education Department, Annual Report ya 1932 uk. 5.
2382 45* Education Department, Annual Report ya 1935 uk. 43.
2386 1936. Lugha ya kusomesha katika "shule za kati" zilizokuwa zikifunza
2387 taaluma mbalimbali, zilizokuwa zikipewa ruzuku ya serikali, ilikuwa
2388 Kiswahili, isipokuwa Buganda na Busoga. Katika kiwango hicho cha
2389 shule, walimu Waganda wapatao 50 walikuwa wakifundisha zaidi ya
2390 wanafunzi Waganda 700, kwa kutumia Kiswahili mwaka huo wa 1936.
2392 Kulikuwa na washiriki 14 wa mashindano ya uandishi wa Kiswahili
2393 kutoka Uganda. Saba kati yao walipata zawadi. Wanne kati ya wale
2394 waliopewa zawadi walikuwa Wabaganda. 46*
2396 Ripoti ya Koloni ya mwaka 1938 yaonyesha kwamba Kiswahili
2397 kiliendelea kusomeshwa katika miaka miwili ya mwisho wa shule za
2398 msingi katika Wilaya za Kinailoti. Pia Kiswahili kiliendelea kuwa somo
2399 katika shule za Wilaya ya Kibantu isipokuwa katika Mkoa wa Buganda na
2402 Katika miaka ya vita, 1939-1945 shule zilitumiwa kutawanya taarifa za
2403 vita zilizoandikwa katika lugha nne, ambazo ni Kiingereza, Kiswahili,
2404 Kiluganda na Kigujerati. Habari hizo zilikusudiwa kubatilisha uvumi na
2405 propaganda. Mwaka 1942 Halmashauri ya Elimu ya Wanajeshi ya Afrika
2406 Mashariki (East African Army Education Corps) ilianzishwa. Moja kati
2407 ya madhumuni yake ilikuwa ni kupunguza matatizo ya mawasiliano kwa
2408 kufunza wanajeshi Waafrika Kiingereza na kuwafunza wanajeshi Wazungu
2409 ama Kiswahili, Chinyanja au Kisomali.
2411 Mkutano uliitishwa Makerere mwezi Oktoba 1944 kujadili kumbu-
2412 kumbu ya lugha katika shule za kuelimisha Waafrika iliyotolewa na
2413 Kamati ya Kutoa Mashauri ya Elimu Katika Makoloni. Maoni ya
2414 mkutano huo yalikuwa kwamba "Kiingereza pekee ndicho kilistahili
2415 kutambuliwa kuwa lugha ya baadaye ya mawasiliano". 47* Hata hivyo
2416 mkutano huo haukutetea kutumiwa kwa Kiingereza katika shule za
2417 Buganda. Ulipendekeza kwamba muda wa kusomesha Kiingereza uonge-
2418 zwe na kwamba lugha za kwanza zilistahili kusomeshwa kwa makini zaidi
2419 kote katika vyuo na vituo mbalimbali. Lugha zilizochaguliwa kusomeshwa
2420 hivyo, zilikuwa Kiluganda, Kirunyoro-Rutooro, Kiacholi (Kijaluo cha
2421 Kaskazini), Kiateso na Kilugbara. Haya yalikuwa mabadiliko makubwa
2422 ya sera. Kufikia mwaka 1944 sera ya lugha ilikuwa ikihimiza Kiswahili na
2423 lugha za kwanza. Sera mpya ilihimiza Kiingereza na lugha za kwanza.
2424 Haikutoa nafasi ya kusomeshwa kwa Kiswahili katika elimu ya Uganda. 48*
2427 46* Education Department, Annual Report ya 1937 uk. 6.
2428 47* Education Department, Annual Report ya 1944, uk. 7.
2429 48* Uganda iliendelea kuwakilishwa katika Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki katika
2430 miaka yake yote 1930-1964. Kati ya 1945 na 1946 Wakurugenzi wa Elimu wa Afrika
2431 Mashariki walikuwa na mikutano ya kujadili suala la kuanzishwa kwa kampuni ya uchapishaji
2432 wa vitabu katika chuo kikuu cha Halmashauri ya Fasihi na Lugha ya Afrika Mashariki
2433 ambayo baadaye ilikuwa East African Literature Bureau.
2437 Kutiliwa mkazo kwa lugha za kwanza katika shule za msingi haku-
2438 kufurahiwa hasa huko Buganda. Afisa wa Elimu wa Mkoa alisema
2441 "Labda jambo lililozusha ubishi mwingi sana kati ya walimu na shule
2442 za msingi lilikuwa ni kuondolewa kwa Kiingereza kuwa lugha ya
2443 kusomesha masomo mengine katika shule za msingi na kutahiniwa
2444 kwa mitihani yote ya mwisho wa mwaka kwa lugha za kwanza.
2445 Mabadiliko haya hayajatekelezwa vizuri." 49*
2447 Mwaka 1946 Kiswahili kiliendelea kusomeshwa katika shule za msingi
2448 za maeneo ambayo yalitaka kisomeshwe. 50* Ripoti ya mwaka 1948
2449 inaonyesha kwamba lugha sita za Kiafrika zilikuwa zimekubaliwa kuwa
2450 lugha za kusomesha katika shule za msingi. Lugha hizo sita ni Kiluganda,
2451 Kirunyoro-Rutooro, Kijaluo cha Kaskazini, Kiateso, Kilugbara na
2452 Kiswahili (Ladefoged et. al. 1971: 91).
2454 Mwaka 1949 Kiswahili kilikuwa kikitumiwa kama lugha ya kusomesha
2455 masomo mengine katika shule mbili tu (za pekee) za serikali, za watoto wa
2456 askari polisi na askari wa magereza. Hii ni kwa sababu Kiswahili
2457 kiliendelea kuwa lugha ya mawasiliano ya majeshi. Katika shule zingine
2458 zote, watoto walisomeshwa kwa lugha zao za kwanza kufikia darasa la
2459 nne. Lugha zingine tano za Kiafrika zilizotambuliwa zilibaki Kiluganda,
2460 Kirunyoro-Rutooro, Kiacholi au Kijaluo cha Kaskazini, Kiateso na
2461 Kilugbara. Lugha zingine za kwanza zingetumika katika madarasa mawili
2462 ya kwanza ya shule za msingi.
2464 Kiingereza hakikutumiwa kama lugha ya kusomesha masomo mengine
2465 katika shule za msingi isipokuwa katika sehemu chache baada ya kibali
2466 maalum. Hata hivyo kilikuwa kikisomeshwa kama somo katika madarasa
2467 ya tano na sita na kingesomeshwa mapema zaidi mradi tu kisitatize
2468 kusomeshwa kwa masomo mengine. Shule za watu binafsi zilisomesha
2469 Kiingereza katika madarasa ya chini na kwa hivyo ziliwavutia wanafunzi
2472 Vyuo vya kuwafunza walimu wa lugha za kwanza ambavyo viliwafunza
2473 walimu wa kusomesha madarasa ya kwanza hadi ya nne vilinuiwa
2474 kusomesha kwa lugha za kwanza tu pamoja na kusomesha somo la
2477 Katika shule za Magoa lugha ya kusomesha ilikuwa ni Kiingereza
2478 kuanzia mapema katika muongo wa 1950. Katika shule zingine za
2479 Wahindi, Kihindi na Kigujerati zilitumiwa kusomesha masomo mengine.
2482 49* Education Department, Annual Report ya 1945 na 1946 uk. 9.
2483 50* Uganda Annual Colonial Report ya 1946 uk. 51.
2484 51* Education Department, Annual Report ya 1949 uk. 8.
2488 Katika shule chache za msingi za Kiafrika ambapo somo la Kiingereza
2489 lilianzishwa mapema, ilionekana kwamba hakikuathiri masomo mengine.
2490 Kufuatia pendekezo la kundi la Binns na Kamati ya de Bunsen ya 1952,
2491 ilikatwa shauri somo la Kiingereza lianzishwe katika madarasa ya chini ya
2492 shule za msingi. Kabla ya hapo, somo la Kiingereza halikupendekezwa
2493 katika madarasa manne ya kwanza katika shule za msingi. Ingechukua
2494 muda kabla walimu wa kutosha hawajafundishwa ili matokeo ya taratibu
2497 Pigo kubwa zaidi la Kiswahili nchini Uganda lilikuwa tangazo la 1952
2498 kwamba Kiswahili hakitambuliwi tena kama somo katika shule za
2499 Uganda. 52* Shule ambazo hazikuhusika ni za polisi na watoto wao. Lugha
2500 tano za Kiafrika ambazo tumezitaja ziliendelea kuwa lugha za pekee za
2501 Kiafrika zilizotambuliwa katika elimu. Lugha zingine za Kiafrika zinge-
2502 tumika tu katika madarasa mawili ya kwanza kama tulivyotaja. Lugha za
2503 kusomesha masomo yote katika miaka yote sita ya shule za msingi zilibaki
2504 hizo lugha tano za Kiafrika, nacho Kiingereza hakikusomeshwa sana
2505 kabla ya darasa la tano. Lakini shule zilihimizwa zianze kukisomesha
2506 katika madarasa ya chini.
2508 Ripoti ya Idara ya Elimu ya mwaka 1953 inatambua kwamba hata
2509 ingawa msimamo wa elimu ni kwamba mtoto hujifunza vizuri anapotumia
2510 lugha ya mama yake, lugha za Kiafrika zinazotumiwa katika shule za
2511 Uganda si lugha za mama za watoto wengi nchini Uganda. Hii ni kwa
2512 sababu ni lugha tano tu zinazotumiwa kielimu katika nchi yenye lugha
2513 nyingi. Serikali haikuwa tayari kutumia lugha zote za Uganda mashuleni
2514 kwa sababu ya gharama kubwa. Kulikuwa na maoni kwamba ikiwa
2515 Kiingereza kingesomeshwa vizuri katika madarasa ya mwanzo ya shule za
2516 msingi, watoto wangeanza kukitumia kama lugha ya kusomesha masomo
2517 mengine badala ya kubadilisha kutoka lugha ya mama hadi lugha nyingine
2518 ya Kiafrika iliyotambulikana (moja kati ya zile lugha tano).
2520 Ili kuwafunza walimu wa kusomesha Kiingereza katika madarasa ya
2521 mwanzo ya shule za msingi, masomo maalum ya kuwafunza Kiingereza
2522 yalitayarishwa mwaka 1954. Mwaka huo huo mafunzo ya kuwafunza
2523 walimu wa kusomesha kwa kutumia lugha za kwanza yalikwisha. Baadhi
2524 ya vyuo vilivyokuwa vikifunza walimu hao vilifungwa, na vingine
2525 vilipanuliwa na kufanywa kuwa vyuo vikubwa. Kuanzia 1958 serikali
2526 ilihakikisha kwamba Kiingereza kilisomeshwa kama somo muhimu
2527 kuanzia darasa la tatu. Kiingereza kilitiliwa mkazo zaidi mwaka 1960
2530 52* Education Department, Annual Report ya 1952 uk. 8. Tangazo lasema hivi: "Kiswahili si
2531 lugha inayotambulika tena katika shule za Uganda, kwa sasa, kinatumika tu katika shule za
2532 polisi na watoto wao kwa kuwa kingali lugha rasmi ya jeshi la polisi".
2536 baada ya kuunganishwa kwa shule ambazo hapo awali zilikuwa zimega-
2537 wanywa katika shule za Waafrika, Magoa, na Wazungu.
2539 Kama tulivyojadili katika sehemu hii, kutumiwa kwa Kiswahili katika
2540 elimu nchini Uganda kulianza vizuri kukiwa na msaada kamili wa serikali.
2541 Kiswahili hakikuungwa mkono na baadhi ya Waganda - hasa Waba-
2542 ganda. Kufuata mabadiliko ya siasa katika Afrika Mashariki, Kiswahili
2543 kiliondolewa katika shule za Uganda mwaka 1952. Hata baada ya uamuzi
2544 huo mkali Uganda iliendelea kuwa mwanachama na kutoa pesa za
2545 kuigrarimia Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki hadi 1964.
2547 Upinzani dhidi ya Kiswahili uliofanywa na Wabaganda wakati wa
2548 ukoloni labda ulitarajiwa kwa vile walivyokuwa na nafasi maalum katika
2549 nchi ya Uganda. Hali haiko hivyo tena katika Uganda huru. Uganda, sawa
2550 na majirani zake wa Afrika Mashariki na kati, inahitaji Kiswahili katika
2551 kujenga umoja wa taifa na kwa mawasiliano ya kimataifa. Kwa muda wa
2552 karibu karne moja Kiingereza kimeshindwa kuyatatua matatizo ya lugha
2553 ya Uganda. Si lugha ya mwananchi wa kawaida na kingechukua zaidi ya
2554 karne nyingine kuwa hivyo. Kiswahili chastahili kupewa nafasi ya kuwa-
2555 unganisha wananchi wa Uganda. Hatua ya kwanza ni kuanza kukisomesha
2556 katika shule nchini Uganda.
2560 Mzee alipotolewa nje alikuwa kama mtu mwenye wazimu.
2561 Alikuwa akitetemeka kwa woga. Alitembea kwa haraka
2562 kutoka nje. Moyo wangu ulivurugika kwa mchanganyiko
2563 wa hasira na huzuni nilipoona mzee akikimbia Serikali
2564 yake. Mzee alipokuwa akitoka nje sikuona kitu kingine
2565 isipokuwa kwamba wazee walikuwa wakitukimbia. Uhusiano
2566 kati yao nasi ulikuwa ukikatika. Niliona wazazi wakiwakimbia
2567 watoto wao ambao sasa walikuwa kama simba. Kwa kuwa
2568 mzee huyu alikuwa amevaa shati ambalo lilikuwa limepasuka
2569 mgongoni niliweza kuona mgongo wake vizuri sana. Kweli
2570 niliona wazee wakitupa migongo. Mgongo wa mzee huyu sasa
2571 ulikuwa kama ukurasa ambao haukuandikwa maneno; ulikuwa
2572 kama ubao mweusi uliofutwa upande mmoja.
2574 Maneno yaliyokuwa yameandikwa upande mwingine
2575 sikuweza kuyasoma. Mawazo haya yalikuwa bado yakinizu-
2576 nguka ndani ya bongo na damu yangu mata tu niliposikia
2577 Mkuu wa Wilaya akipiga kelele: "Mwingine aingie!"
2579 Yule msichana aliingia. Alipoingia tu Mkuu wa Wilaya
2580 alisikika akisema: "Aa! Pili karibu!" Mlango ulifungwa.
2582 Mwanzoni walikuwa wakizungumza kwa sauti ya chini,
2583 lakini baadaye walijisahau. Walianza kuzungumza kwa
2587 sauti ya juu. Hata sisi tuliokuwa nje tuliweza kusikia
2588 maneno yaliyokuwa yakisemwa.
2590 "Pili, mpango huu unauonaje?"
2591 "Hata mimi nimechoka na sinema. Kila Jumapili
2592 sinema. Afadhali Jumapili hii twende Serengeti tukawaone
2595 "Basi kama ni Serengeti inafaa twende Jumamosi ili
2596 tulale huko siku mbili maana ni mbali kidogo."
2598 "Haya, vizuri. Lakini mimi leo nimechoka sana; utakuja
2599 kunichukua jioni twende sinema?"
2601 "Tutakuja kama saa mbili hivi. Utamwambia shemeji
2604 Waliendelea kuzungumza kwa muda mrefu. Mambo
2605 waliyosema yalikuwa mengi. Mara kucheka, mara "Mimi
2606 sitaki", na mara "Huniamini". Nilisikia mlio wa kiti
2607 kikibururwa chini. Nafikiri Mkuu wa Wilaya alikuwa akiinuka.
2609 "Lete kitambaa changu! Hakika mimi siwezi kutoka nje
2610 bila kitambaa kichwani!".
2612 Kwa muda mfupi uliofuata walizungumza tena kwa sauti
2613 ya chini. Ilikuwa baada ya muda huu msichana alipotoka
2614 nje. Nilipokuwa nikiingia ndani nilisikia watu nje wakimgunia.
2616 Kweli nilipoingia ndani sikuweza kuamini kwamba
2617 aliyekuwa mbele yangu ndiye alikuwa Mkuu wa Wilaya.
2618 Alikuwa kijana mwenye umri wa miaka thelathini hivi. Mara
2619 tu nilipoingia na kutazamana uso kwa uso kila mmoja aliweka
2620 matuta usoni, kwani tulifahamiana tangu zamani.
2622 "Habari ya asubuhi," nilimsabahi.
2624 "Asante, keti kitini."
2626 "Mimi nilikuwa na shida kidogo."
2628 "Ndiyo kusema sasa huna."
2630 "Nina shida," nilijisahihisha ili kumpendeza. "Natafuta
2634 kazi ya muda. Miezi mitatu hivi."
2638 Nilikasirika kidogo, lakini hasira yangu niliimeza kwa
2639 kuuma meno. "Mimi Kazimoto, mwanafunzi wa Chuo
2640 Kikuu - Dar es Salaam."
2642 "Huko ndiko mnakofunzwa jinsi ya kuwasabahi wakubwa
2645 "Mimi ninatafuta kazi."
2647 "Hata mimi nilipokuwa Makerere nilikuwa nikiwaheshimu
2648 watu. Au labda kwa kuwa umesoma Chuo Kikuu unafikiri
2651 "Kusoma Chuo Kikuu siyo dhambi," nilimjibu. "Lakini
2652 mimi hayo hayakunileta hapa. Mimi ninatafuta kazi."
2654 "Huna adabu! Kaa nje kwanza, unanichelewesha kazi
2655 bure. Utaingia humu mtu wa mwisho."
2657 Nilisimama. Kwa muda nilimtazama machoni.
2659 "Unasikia! T-o-k-a nn-nje!"
2663 Msichana aliyekuwa akinifuata aliingia ndani. Kwa kuwa
2664 nilikuwa nimekwisha sikia kwamba kulikuwa na kazi nilikaa
2665 pale kwa muda; zaidi ya hayo watu walikuwa wamebaki
2668 Yule msichana hakukawia sana mle ndani. Alipotoka nje
2669 nilimwona anatembea kuelekea kwangu. Nilifikiri kwamba
2670 labda alikuwa ametumwa na Mkuu wa Wilaya kuja
2671 kuniambia jambo fulani.
2673 "Mwalimu, siku hizi uko wapi?"
2675 "Bado ninaendelea na masomo."
2677 Ingawa nilimjibu, nilikuwa sikumbuki mahali nilipopata
2678 kumfundisha. Nilikuwa nimekwisha fundisha shule nyingi
2679 kwa muda. Shule zingine sikumaliza hata miezi miwili.
2680 Niliona haya kidogo kuona kwamba kwa muda wote ule
2684 nilikuwa nikijitahidi kugusa kiuno cha mwanafunzi wangu.
2686 "Kwa muda wote huu ulikuwa bado hujanitambua. Mimi
2687 nilipokuona tu nilikukumbuka mara moja."
2689 "Samahani, nimesahau jina lako."
2693 "Siku hizi uko wapi? Habari za Jangwani?"
2695 "Jangwani nilimaliza mwaka jana. Siku hizi ninafanya
2700 "Ninafundisha, lakini ninatarajia kuacha kazi hivi hivi
2705 "Kazi ngumu, pesa kidogo. Haya kwa heri."
2709 Alipokuwa amekwenda nilikumbuka wazi kwamba Salima
2710 alikuwa mmoja kati ya wasichana waliokuwa wakisoma shule
2711 ya wasichana ya Jangwani huko Dar es Salaam. Ingawa
2712 wakati huo alionyesha mapenzi kwangu, mimi sikutaka, kwa
2713 kuogopa kwamba wanafunzi wengine wangetambua wange-
2714 fanya fujo na ingekuwa vigumu kuendesha darasa. Zaidi ya
2715 hayo ufundishaji wakati huo ulikuwa ni mtihani na mkaguzi
2716 alikuwa akikaa darasani. Salima alinifanya sasa nikumbuke
2717 tena wale wasichana waliokuwa wakikaa mbele. Wasichana
2718 hao, kwa vile walivyokuwa wamezoea kukaa walinifanya
2719 nifundishe nikitazama juu ya vichwa vya wanafunzi.
2720 Hili ndilo kosa ambalo mkaguzi alinikumbusha karibu kila
2723 Wakati nilipokuwa nikifikiria mambo haya niliona mtu
2724 wa mwisho anaingia ofisini. Sura ya Mkuu wa Wilaya
2725 ilinijia tena kichwani. Nilijongea karibu ili nipate kuingia
2726 tena. Ilikuwa wakati huu nilipovumbua kwamba nilikuwa
2727 nimesahau kufunga kifungo kimoja cha suruali yangu.
2731 Jambo hili lilinuidhi sana. Nilianza kufikiri mabarabara
2732 yote ya mjini niliyokuwa nimepita nikiwa katika hali hiyo;
2733 pia watu wote niliowaona. Lakini mara mlango ulifungu-
2734 liwa. Yule mtu alitoka. Niliingia.
2736 "Naam, Bwana mkubwa sana, nafikiri sasa kiburi
2739 "Mimi sina kiburi. Shida yangu kazi."
2743 Nilikaa mbele yake, tukawa tunatazamana. Nilipotupa
2744 macho juu ya meza niliona visusu viwili. Kimoja
2745 kimeandikwa In kingine Out. Ilikuwa ndani ya kile
2746 kijikapu cha In nilimoona picha za wasichana watatu
2747 ambao sasa niliweza kuwafahamu - Vumilia, Pili na Salima.
2748 Ndani ya kijikapu cha Out niliona bahasha za kiserikali.
2749 Juu ya meza niliona barua ambayo ilikuwa bado kwisha
2750 kuandikwa. Niliweza kuona maneno machache: "Salima
2751 natumaini kwamba hutakasirika sana; wale wasichana sina
2754 Haya yote niliyaona kwa haraka Mkuu wa Wilaya
2755 alipokuwa anafunga kabati, kwani nilipoketi tu juu ya kiti
2756 yeye aliinuka. Alipomaliza kufunga kabati nilimwona
2757 anachukua funguo zingine mfukoni mwake. Nafikiri zilikuwa
2758 funguo za gari lake.
2760 "Samahani, ninataka kufunga ofisi. Saa nane na nusu sasa.
2763 Nilimtazama machoni kwa mshangao.
2765 "Kazimoto, fika kesho asubuhi." Mimi niliendelea kumkazia
2768 "Bwana Manase," nilimwita.
2770 "Ndiyo, unanifahamu; lakini sasa nimo kazini."
2778 "Manase," nilimwita tena.
2780 "Kazimoto," aliniita.
2782 Nilisimama pale nikamtazama dakika chache, kisha nikatoka
2783 nje kwenda kutafuta chakula; njaa ilikuwa inaniuma.
2786 Naam, Mkuu wa Wilaya, Bwana Manase, tulikuwa tukiishi
2787 kijiji kimoja. Ukweli ni kwamba tulikuwa majirani. Tangu
2788 utoto tulikuwa tumezoeana. Manase alipokuwa bado mtoto
2789 mdogo tulikuwa tukimwita "Popo" kwa vile masikio yake
2790 yalivyokuwa makubwa. Kati ya wanafunzi tuliokuwa tukisoma
2791 darasa la kwanza Manase ndiye alikuwa akifikiriwa kuwa
2792 mjinga wa mwisho. Ninakumbuka kwamba siku moja Manase
2793 alilia sana darasani bila kupigwa. Sababu yenyewe ilikuwa
2794 kwamba mwalimu alimwekea zero kubwa yenye macho
2795 mawili na meno yakimcheka. Kwa kuwa alikuwa jirani yangu,
2796 mara nyingi alikuwa akishinda nyumbani kwetu na nikimsaidia
2799 Uadui kati yangu na yeye ulianza tulipokuwa darasa la
2800 nne. Siku moja, pale shuleni nilichimba shimo dogo na fupi.
2801 Ndani ya shimo hili niliweka maji. Niliwaita wanafunzi kama
2802 kumi hivi. Walipojongea niliwaambia, "Shimo hili ni refu
2803 sana huwezi ukagusa mwisho wake."
2805 "Labda kuna nyoka?" wengine waliuliza.
2809 Manase alijitokeza. "Mimi ninaweza kugusa mwisho
2812 "Haya jaribu," nilimwambia.
2814 Manase alitumbukiza mkono. "Mbona fupi," alisema.
2816 "Umegusa chini?" nilimwuliza.
2820 "Ebu tuzolee mchanga wa chini," nilimwambia.
2822 Manase alipotoa mkono, alikuwa amejaza mbolea ya
2823 ng'ombe mkononi mwake. Wanafunzi walimzomea, akalia.
2827 Tangu siku hiyo Manase alinichukia na nyumbani kwetu
2828 hakufika tena kuja kuongea.
2831 Kama ilivyo kawaida ya watoto wadogo uadui huu
2832 haukuendelea, kwani wakati wa mavuno ulipowadia tulijikuta
2833 tunatega ndege pamoja. Baada ya mavuno tulizoea pia kupita
2834 mashambani tukitafuta yale mawele yaliyosahauliwa
2835 kuvunwa. Yale tuliyopata tulizoea kwenda kuuza kwa padri
2836 mmoja wa Kizungu wa misioni yetu. Nakumbuka siku moja
2837 baada ya kuuza mawele yetu tulipita kaburini ili kula mapera.
2838 Tulipokuwa tumepanda tulisikia viatu vya padri akizunguka
2839 kaburini akisoma kitabu kama ilivyo kawaida yao. Tulifikiri
2840 kwamba alikuwa hawezi kutuona. Tulikaa kimya mtini.
2841 Alipofika karibu na mti tuliokuwa tumeranda alisimama
2842 akawa anasoma kitabu chake hapo. Alisimama kwa muda
2843 mrefu; halafu tuliona kidevu chake kinainuliwa juu.
2846 Tulishuka hali tukitetemeka. Alituongoza hadi chumbani
2847 mwake. Tulipofika chumbani tuliambiwa kwenda kuzoa
2848 mchanga nje. Tulifanya vile. Tulipoingia chumbani tuliambiwa
2849 kuumwaga juu ya sakafu, na juu ya mchanga huu tuliamrishwa
2850 kupiga magoti. Baada ya muda mfupi tulilia kwa maumivu.
2851 Hapo ndipo alipotwambia kulala chini. Tulipigwa fimbo tano
2854 "Haya kaeni!" Tulikaa.
2856 "Baba zenu nani?" Tulimwambia.
2858 "Ninyi watoto wa Wakristo ndio mwaiba mali ya kanisa!
2859 Hamfahamu kwamba kuiba ni dhambi? Tajeni amri za
2862 "Rudieni amri ya saba mara nne!" Tulifanya hivyo.
2866 "Ndiyo," tulijibu pamoja.
2871 Padri alitupa vijitabu viwili vya Katekesimu. "Haya nendeni
2872 nyumbani! " Tulitoka kwa haraka kwa mchanganyiko wa
2875 Tulikuwa darasa la nane uadui uliporudi tena, lakini
2876 mara hii kwa bahati mbaya. Wakati wa mavuno
2877 ulikuwa umekaribia, mimi nilikuwa nimesimama juu ya
2878 ulingongo katikati ya shamba la mawele la baba yangu;
2879 Manase alikuwa katika shamba la baba yake. Tulikuwa
2880 tukiwinga ndege. Tulianza mchezo wa kutupiana mawe kwa
2881 teo. Kwa bahati mbaya Manase alinipiga kichwani damu
2882 ikanitoka. Nilikimbilia nyumbani hali nikilia. Kwa muda
2883 hatukuonana tena na Manase.
2885 Tulikuwa marafiki tena tuliposhinda wote kuingia darasa
2886 la tisa kwani tulishinda kwenda shule moja. Urafiki ulirudi
2887 hasa siku niliyomwokoa kutoka mtoni. Tulikuwa tukioga
2888 mtoni Manase alipoanguka mahali ambapo maji yalikuwa
2889 marefu. Kwa kuwa alikuwa hajui kuogelea alianza kuzama.
2890 Wenzangu walikimbia. Mimi niliogelea mara kwenda
2891 kumchukua. Karibu nife naye, lakini kwa bahati nzuri
2892 niliweza kumvuta mpaka maji mafu. Macho yake yalikuwa
2893 mekundu. Jioni hiyo, baba yake aliposikia aliniletea kuku
2897 Wakati tukiwa darasa la kumi, kwa mshangao wa kila mtu,
2898 akili za Manase ziliongezeka sana, akawa akiongoza darasa.
2899 Mwaka huu mimi sikuumaliza. Nilipatwa na ugonjwa wa
2900 kifua kikuu. Nilikaa hospitalini kwa muda wa mwaka mmoja
2901 mzima. Nilipotoka hospitalini nilikuwa na nia ya kusoma
2902 kufa kupona, lakini mwaka huo baba akashindwa kulipa ada
2903 ya shule; shule nikaacha, nikatafuta kazi. Manase akawa sasa
2904 miaka miwili mbele yangu. Kazi nilifanya kwa muda wa
2905 mwaka mmoja ili kuhakikisha kwamba nilipata pesa za
2909 kutosha kuweza kunifikisha darasa la kumi na mbili. Wakati
2910 huu wote Manase alikuwa rafiki na jirani mwema mpaka
2911 alipomaliza Makerere na kujinyakulia shahada ya B.A.
2912 Wakati huu uhuru ulikuwa umekwisha ingia. Jina la Nyerere
2913 likawa likiimbwa hata na watoto wadogo. Mwafrika akawa
2914 Mwafrika; Mzungu akawa Mzungu; Mhindi akawa Mhindi na
2915 Mwarabu akawa Mwarabu. Kwa ufupi kila mtu akaanza
2916 kuona ukweli wa hali yake. Aliyejiona tofauti alirudi
2917 kwao. Kina Manase wakawa watu waliohitajika sana ili
2918 kushika uongozi wa nchi. Manase akawa ofisa mkuu wa
2919 elimu, huko Tanga. Alifanya kazi vizuri sana. Akahamishwa
2920 hadi Dar es Salaam. Akawa ametolewa kwenye matawi na
2921 kuletwa kwenye shina.
2923 Ilikuwa wakati huu Manase aliponifanyia ujeuri mkubwa.
2924 Alifanya kosa ambalo nilikuwa siwezi kumsamehe. Kisasi
2925 kilianza kuukera moyo wangu. Kosa hili ndilo lililotufanya
2926 tuzungumze namna ile ofisini. Nilipoingia, kusema haki,
2927 nilikuwa sitegemei kumkuta yeye, kwani baada ya kosa hili
2928 nilikuwa sifahamu mahali alikokwenda.
2930 Baada ya kukumbuka maisha yetu haya ya zamani, na
2931 baada ya kulikumbuka kosa hili, nilijikuta nikisema moyoni:
2932 "Lazima nijilipize kisasi; nimezaliwa kama yeye; mimi
2933 mwanamume kama yeye. Haiwezekani. Lazima nijilipize
2934 kisasi." Mara nilistukia nagongana na mwanamke fulani
2937 "Kaka, mbona hivi!" alisema. "Siku hizi hamwoni watu?"
2939 "Samahani, dada yangu, mawazo yangu yalikuwa mbali,"
2942 "Mawazo gani, unataka kuua mtu?"
2944 Sikutaka kuzungumza naye zaidi. Niliendelea na njia
2945 yangu. "Sasa ninakwenda wapi?" nilijiuliza moyoni. "Ndiyo,
2946 njaa inaniuma, kwa hiyo nilikuwa na nia ya kutafuta hoteli."
2950 Nilikumbuka kwamba hoteli niliyokuwa nikitafuta nilikuwa
2951 nimeiacha nyuma. Nilirudi. Nyuma kidogo niliona kibao
2952 kimeandikwa "Hoteli ya Wananchi". Niliingia ndani kuagiza
2953 wali na nyama ya kuku.
2955 Wakati nikila watu ambao walikuwa wameenea vumbi
2956 waliingia hotelini. Ilionekana kwamba wafanya kazi wa humo
2957 hotelini waliwatambua mara moja. Walikuwa wasafiri kutoka
2958 Dar es Salaam, kama nilivyokuja kuelewa baadaye. Chakula
2959 walicholetewa kilikuwa tofauti na kile walichoniletea mimi.
2960 Ingawa nilikuwa mbali kidogo niliweza kuona kwamba wali
2961 walioletewa ulikuwa mbaya. Lakini kwa kuwa walikuwa na
2962 njaa kubwa hawakuweza kutambua kwamba walipewa uporo.
2963 Sikushangaa sana. Mambo haya nilikuwa nimekwisha yaona
2964 yakitendeka katika sehemu nyingi za nchi yetu wakati nikiwa
2967 "Mwishowe tumefika, saa ishirini na saba," mmoja kati yao
2970 "Mimi mgongo unaniuma sana, sijui kwa nini?"
2972 "Sababu ya mabarabara mabaya."
2974 "Sijui serikali inafanya nini?"
2976 "Watajali nini wakati wao wanapita hewani?"
2978 Mazungumzo yao sikuyafuata zaidi, kwani karibu na meza
2979 niliyokuwa nimekaa walikuwa wamekaa wazee wawili
2980 wakisimuliana hadithi zao za miaka miwili mitatu iliyopita,
2981 na masikio yangu yalivutiwa upande huo.
2983 "Bwana we! Niulize mimi nikwambie!" mzee mwenye
2984 sharubu alimwambia mwenziwe huku akigonga meza kwa
2985 mfupa kusisitiza wazo lake. "Kwa muda wa miaka miwili
2986 nilikuwa dereva wa mkuu mmoja wa mkoa. Wewe fikiri mzee
2987 kama mimi, mkuu wa mkoa ananiambia 'kanitongozee
2988 msichana'. Ni jambo ambalo mara nyingi liliniudhi. Heshima
2992 yangu yote kwenda kuipoteza mbele ya msichana mdogo!
2993 Na mvi zangu kichwani! Halafu nikishamleta nyumbani
2994 kwake au hoteli, anasemaje? 'Utakuja kumchukua saa kumi
2995 na moja asubuhi umrudishe.'Mimi usingizi napoteza, yeye
2998 "Wewe unajua upande mmoja tu," mwenziwe alidakia.
2999 "Mimi nilikuwa nikishika faili zao za mishahara. Maofisa
3000 wote hawa usiwaone nje matumbo kuning'inia! Wengi kati
3001 yao wanapokea shilingi mia mbili kwa mwezi!"
3005 "Madeni, ndugu yangu, madeni. Utakuta wengi wana
3006 mikopo ajabu! Magari yote mikopo; maredio makubwa, yote
3007 mikopo; majiko ya kupikia, yote mikopo; karibu kila kitu
3008 cha maana kiko chini ya mkopo!"
3010 Walipoona kwamba kila mtu alikuwa akiwatazama
3011 walimaliza chakula chao wakatoka.
3013 Kwa muda kulikuwa na hali ya unyamavu pale hoteli, hali
3014 hii ilinifanya nimkumbuke Manase. Niliinuka kwa hasira
3015 huku nikiuma meno. Bilauri ya maji iliyokuwa juu ya meza
3016 yangu ilianguka na kupasuka. Nilikuwa karibu nitoke nje
3021 "Samahani," nilisema. Nililipa.
3023 Kwa mara ya kwanza wazo la kumkata Manase vipande
3024 vipande lilinijia kichwani mwangu wakati nikirudi katika
3025 nyumba ya wageni nilimokua nimekodi chumba cha kulala.
3028 Jioni hiyo kulikuwa na mchezo wa kuigiza katika jumba la
3029 maendeleo. Mchezo huo ulikuwa ukichezwa na wanafunzi
3030 wa shule ya wavulana ya Nsumba. Nilikata shauri kwenda
3031 kuutazama ili kutuliza kichwa changu kidogo chenye kiburi.
3035 Wanafunzi hawa walicheza michezo miwili. Mchezo wa
3036 kwanza ambao ulichekesha sana watu ulikuwa juu ya baba
3037 mmoja aliyekataa kupeleka mtoto wake mgonjwa hospitali.
3038 Mchezo wa pili ulikuwa mchezo wa mapenzi. Yule mchezaji
3039 aliyefungua mchezo huu alisimama katikati, na kwa sauti,
3040 hali akisambaza mikono yake alitamka maneno haya:
3042 "Ndugu zangu, katika mchezo huu mtaona kwamba chuki
3043 haina nguvu kama wale uwachukiao wanakupenda. Utawezaje
3044 kuwachukia wale wakupendao? Kweli, mwanadamu hawezi
3045 kumchukia mwanadamu mwenziwe isipokuwa matendo yake.
3046 Ndugu zangu, mtaona kwamba kujilipiza kisasi kwa watu
3047 wakupendao ndio mwanzo wa mapenzi. Ndugu zangu,
3048 mtaona kwamba mwisho wa mwanadamu ulianza alipoweza
3049 kutembelea miguu miwili. Pia mtaona ugonjwa utakaowama-
3050 liza akina mama wenye mabinti."
3052 Aliinama. Watazamaji walipiga makofi.
3054 Mchezo ulikwisha saa nne. Nilipotoka nje nilikuwa na nia
3055 ya kwenda kulala mara moja, lakini kwa kuwa katika nyumba
3056 ya wageni nilimokuwa nimekodi chumba kulikuwa na bar
3057 nilikata shauri kunywa kidogo.
3059 Mbele yangu alikuwa amekaa mwanamke mmoja aliyekuwa
3060 akinitazama mara mbili mbili. Mimi sikuonyesha alama yo
3061 yote ya kumhitaji; nilikunywa pombe yangu kimya. Mbwa
3062 abwekaye haumi, aumaye ni yule kimya. Hii ndiyo ilikuwa
3063 njia yangu kupata wanawake. Nilipoagiza chupa ya pili
3064 mwanamke huyu alikuwa amehamia karibu nami.
3068 "Tusker," alijibu kwa haraka.
3070 Niliagiza chupa mbili za Tusker. Tulikunywa pamoja mpaka
3071 saa sita. Walipofunga bar nilinunua chupa moja ya Grenado.
3072 Chupa hii tuliinywa pamoja chumbani mwangu.
3074 "Unatoka wapi?" aliuliza. Nilimwambia.
3078 "Jina lako nani?" Nilitafuta moja.
3080 "Kumbe unatoka sehemu moja na Manase." Nilikubali.
3082 "Mhuni huyo! Amemwachisha kazi mwalimu mmoja, sasa
3083 anaishi pamoja naye."
3085 "Salima?" niliuliza kwa mshangao.
3087 "Huyo huyo! Lakini siye huyo peke yake, ana msichana
3088 mwingine katika mtaa wa Uhuru."
3090 "Ndiyo kusema anataka kumwoa Salima?"
3092 "Inaonekana vile, lakini tena tunasikia baba yake
3093 amekwisha kumtafutia mchumba mwingine huko nyumbani
3094 kwao. Wanasema kwamba Bwana Manase amemkataa kwa
3095 sababu ni mshamba mno; wengine wanasema anataka kuwaoa
3098 Nilihisi kwamba huyo msichana wa shamba alikuwa Vumilia.
3100 Mawazo juu ya Manase yalianza tena kuvuruga akili zangu.
3101 Nilianza kunywa pombe nyingi ili nilewe upesi nisahau
3102 mambo. Chupa ilikuwa bado kwisha mawazo haya yalipopotea:
3103 mwanamke huyu aliweka kichwa chake juu ya miguu yangu.
3105 "Bwanangu, mimi usingizi umenipata, tukalale!"
3107 Hakuweza hata kusimama. Nilimbeba hadi kitandani. Hata
3108 nguo nilipaswa kumvua. Nilishangaa kukuta hirizi kiunoni
3109 mwake. Hirizi hii niliitoa na kuiweka juu ya meza. Baada ya
3110 kumvua nguo zote nilifunga mlango, nikazima taa.
3112 "Utakwenda lini nyumbani?" yule mwanamke aliniuliza asubuhi.
3116 "Utalala humu tena?"
3120 "Leo usiku usinipe pombe nyingi."
3124 "Ninataka kukuonyesha mchezo halisi wa kwetu."
3130 Wakati huo alikuwa akijaribu kuinuka kutoka kitandani.
3132 "Usinitazame!" aliniambia. Nilitazama pembeni.
3134 "Aa! Iko wapi?" alipiga kelele.
3142 "Kwa nini uliitoa?" aliuliza kwa wasi wasi.
3144 "Kwa nini nisiitoe?"
3146 "Mimi siwezi kutunza mtoto wako." Alivaa nguo kwenda
3147 kuoga. Baada ya kuoga tulipeana kwa heri ya kuonana.
3149 Alipokuwa amekwenda nilikumbuka kwamba nilipaswa
3150 kumwona Manase asubuhi hiyo. "Jambo zuri ni kwamba
3151 nilipata usingizi," nilisema moyoni. Wazo la kufika tu ofisini
3152 nimchome Manase visu vya tumboni lilinijia tena kichwani.
3153 "Huenda nami nikanyongwa," nilisema moyoni. "Sitapata
3154 faida yo yote isipokuwa kuwaacha wazazi wangu taabuni.
3155 Jambo la maana ni kujaribu kumpa Manase maisha magumu
3156 hapa duniani. Nisipoweza basi nitajilipiza kisasi kwa njia
3157 ingine." Nilikata shauri kwenda kumwona Manase ofisini
3160 Siku ya kwanza nilipoingia ofisini kwa Manase nilikuwa na
3161 nia ya kuomba kazi ya muda. Yeye alifikiri kwamba nilikuwa
3162 nakuja kumwuliza juu ya kosa alilofanya. Kwa hiyo alijaribu
3163 kutumia lugha kali kama kwamba nilikuwa nakuja kwa
3164 ugomvi. Kwa kuwa siku hiyo sikusema neno lo lote kuhusu
3165 jambo hilo Manase aliona kwamba sikuwa na kinyongo. Sasa
3166 nilipoingia hakuwa mkali kama siku ya kwanza.
3168 "Karibu ukae, Kazimoto," alisema mara tu nilipoingia.
3172 "Kuhusu habari ya kazi nafikiri utapata. Tunahitaji vijana
3173 kama nyinyi katika kufanya kazi hii ya kuhesabu ng'ombe.
3177 Wewe utapata shilingi mia sita kila mwezi ufanyao kazi."
3178 Alifungua kabati kutoa karatasi za maswali na mambo
3179 mengine yaliyohitajika kujazwa. Alinipa mkononi.
3180 "Nafikiri sasa umefurahi, sivyo? Unaweza kwenda."
3182 Nilikuwa karibu kutoka nje nilipofikiri kwamba ilikuwa
3183 lazima nimwulize juu ya jambo hilo alilotenda - tendo la
3186 "Manase," nilimwita. Alinitazama. "Jambo gani ulifanya?"
3187 nilimwuliza hali nikimtazama usoni. Mara moja sura
3188 ilimgeuka. Nilimwona anafungua mdomo pole pole.
3190 "Kazimoto, huelewi vizuri hadithi yenyewe."
3192 "Hadithi nimekwisha isikia, Manase."
3194 "Halikuwa kosa langu."
3198 "Hakika Rukia mchokozi sana. Yeye ndiye alinianza."
3202 "Unaona. Siku moja usiku nilipokuwa nimekwisha lala
3203 usingizi nilisikia mtu anagonga mlango wangu, 'Nani huyo!'
3204 nilisema kwa sauti. 'Ni mimi Rukia, fungua mlango.' Kuna
3205 nini?' nilimwuliza. 'Wewe fungua mlango tu'. Nilipofungua
3206 mlango aliingia chumbani mwangu; alilala juu ya kitanda
3207 changu. Sasa wewe fikiri Kazimoto, mwanamume kama
3208 wewe ungefanya nini?"
3210 "Mambo yote ninayafahamu. Unafikiri sifahamu maisha
3213 "Hata mimi ninayafahamu maisha yako. Ninafahamu
3214 kwamba usiku ulikuwa na Pili. Huwezi kunidanganya
3215 kwamba wewe bikira katika mambo haya (nilishangaa kwa
3216 nini sikuweza kumtambua Pili: mwanamke akiwa mawindoni
3217 hugeuka sura). Pia ninayafahamu maisha ya Rukia. Bila shaka
3218 utakubaliana nami nikisema kwamba Rukia alikuwa malaya
3219 tangu alipoota maziwa."
3223 "Unamwita malaya!" nilisema kwa hasira.
3229 "Rukia ni malaya. Kama umekasirishwa na jambo
3230 lililotokea kwa bahati mbaya unaweza kufanya jambo lo lote
3231 upendalo! Sijali sasa! " alisema kwa hasira. "Sasa hata kazi
3232 hupati!" Karatasi nilinyang'anywa.
3234 "Tutaona! " nilimwambia kwa hasira kubwa.
3236 Nilipokuwa njiani kelekea chumbani kwangu niliweza
3237 kuyakumbuka yale maneno barabara. Nilijaribu kuyarudia
3240 "Ndugu zangu, katika mchezo huu mtaona kwamba chuki
3241 haina nguvu kama wale uwachukiao wanakupenda. Utawezaje
3242 kuwachukia wale wakupendao? Kweli..."
3248 Rukia hakuwa mwingine isipokuwa ndugu yangu aliyenifua-
3249 ta mimi. Ndugu mwanamke pekee, mwema, ndugu mfanya-
3250 kazi. Uzuri wake, kama nilivyosikia watu wakisema, ulikuwa
3251 uzuri wa aina ya pekee. Uzuri ambao hata kipofu aliweza
3252 kuuona. Kwa hiyo sisi nyumbani tukawa tunaona mwanga
3253 mbele ya maisha yake. Tabia yake, kama tulivyoiona
3254 nyumbani, ilikuwa nzuri ingawa ni vigumu kufahamu mambo
3255 ya wasichana. Kwa kuwa alikuwa mzuri Baba na Mama
3256 walitaka kumwachisha shule ili aolewe, kwani alipokuwa
3257 bado darasa la sita alikuwa amekwisha chumbiwa na vijana
3258 watatu. Mawazo ya wazazi wangu niliyapinga, nikayashinda.
3260 Rukia alishindwa kuingia darasa la tisa, lakini mimi
3261 nilikuwa na nia ya kumwelimisha. Nilimtafutia shule, na
3262 baada ya kupita kichinichini kama ilivyokuwa kawaida,
3263 nilipata shule moja huko Dar es Salaam. Taabu sasa ikawa
3267 mahali pa kupanga: shule yenyewe haikuwa na malazi kwa
3270 Manase wakati huu alikuwa akiishi Oysterbay, na kwa
3271 kuwa alikuwa na nyumba kubwa nilifikiri ataweza kuishi na
3272 ndugu yangu. Licha ya nyumba kuwa kubwa wakati huu
3273 ulikuwa wakati ambao uhusiano kati yangu na yeye ulikuwa
3274 mzuri. Nilipomwambia Manase taabu yangu alikubali kukaa
3275 na ndugu yangu. Wakati huo mimi nilikuwa nimekwisha ingia
3278 Mwaka wa kwanza nafikiri ulipita salama. Mambo yalianza
3279 mwaka wa pili alipoingia darasa la kumi. Nilipozungumza
3280 naye mwaka huo alinieleza kwamba alikuwa na shida kidogo
3281 tu. Kwa kuwa hakueleza vizuri shida yake nilifikiri kwamba
3282 ilikuwa njia ya kuzungukia akitaka kuomba pesa. Nilimpelekea
3283 shilingi sitini, nikitumaini kwamba msichana aweza tu
3284 kujitunza akiwa na pesa za matumizi.
3286 Nilipokutana naye siku ingine alinishukuru kwa pesa
3287 nilizompa, lakini katika mazungumzo aliniuliza swali ambalo
3288 lilinitia wasiwasi. Alisema: "Sijui Manase ni mtu wa namna
3289 gani." Hapo ndipo nilipoanza kuhisi kiini cha shida yake.
3290 Niliona wazi kwamba Manase alikuwa akijaribu kufanya
3291 mambo yasiyotakikana.
3293 Siku chache baadaye nilipata barua kutoka kwa ndugu
3294 yangu. Ilikuwa imeandikwa kwa hasira. Msitari wa kwanza
3295 ulisema: "Kaka usiponitafutia mahali pengine pa kukaa mimi
3296 nitarudi nyumbani. Heri kuacha shule!" Niliona kweli
3297 kwamba alikuwa amekwisha sumbuliwa sana. Siku hiyo
3298 nilipanda basi hadi Oysterbay. Nilipofika nyumbani kwa
3299 Manase sikukuta mtu ye yote nyumbani, isipokuwa mbwa
3300 aliyekuwa amefungwa karibu na mlango kulinda wezi.
3301 Nilirudi mjini. Nilijitahidi kutafuta nafasi, lakini rafiki zangu
3302 wengine waliokuwa wakiishi mtaa wa Magomeni Mapipa
3306 walikuwa na vyumba viwili tu. Chumba cha maongezi na
3307 chumba cha kulala, basi. Niliona hatari zaidi katika uchache
3308 wa vyumba kuliko katika tabia ya mtu mwenyewe. Kwa
3309 hiyo nilimwandikia barua ndugu yangu nikimweleza shida
3310 ya kupata mahali pengine. Nilimwomba avumilie, mwaka
3313 Kwa muda wa mwezi mmoja sikuonana naye na sikupata
3314 barua kutoka kwake. Nilifikiri kwamba Manase alikuwa
3315 ameacha mchezo wake na kwamba ndugu yangu alikuwa
3316 akiishi bila kusumbuliwa. Ilikuwa baada mwezi mmoja
3317 uliofuata nilipopata tena barua kutoka kwake, nayo
3318 nilipoifungua ilikuwa imeandikwa, juu kabisa, neno "SIRI".
3322 Moyo wangu siku hizi hauna raha. Lakini leo
3323 nimechukua kalamu ili nikueleze mambo yote.
3324 Nimeona kwamba siwezi kuwa nakuficha wewe
3325 mambo, hali mambo yenyewe sasa hayawezi
3326 kufichika. Wewe ukiwa kaka yangu na ndiye
3327 uliyenitafutia nafasi hii ya shule ninakupa heshima.
3328 Fahamu kwamba mambo haya sijapata kumweleza
3329 mtu mwingine isipokuwa wewe peke yako.
3331 Kaka, uliponileta hapa nilikaa kwa raha kwa muda
3332 wa juma moja tu. Baada ya juma hiyo niliona Manase
3333 anaanza kunitazama kwa njia ya ajabu. Baada ya
3334 majuma mawili mambo yalizidi kuwa mabaya, kwani
3335 nilipokuwa naoga siku moja niliona jicho lake
3336 kwenye tundu la ufunguo.
3338 Mwishowe aliniambia wazi alichokuwa anataka.
3339 Nilimwambia: 'Manase! Kaka yangu akifahamu
3340 litakuwa jambo la aibu sana!' Lakini yeye alijibu
3344 kwamba wewe ni mwanamume kama yeye. Alifikia
3345 hata hatua ya kutumia nguvu! Na kweli alitumia
3346 nguvu bila utashi wangu.
3348 Kaka, sitaki kukupotezea muda wako wa kujifunza
3349 kwa kusoma barua ndefu. Mimi maisha yangu
3350 yameharibika. Shule nimekwisha acha. Jambo ambalo
3351 limenisikitisha sana ni hili lifuatalo: Jana usiku, Manase
3352 alirejea nyumbani mlevi. Alikuwa na tikiti ya basi.
3353 Baada ya kunitukana kwa maneno ambayo siwezi
3354 kukuandikia alianza kupanga vitu vyangu sandukuni.
3355 Leo atanisindikiza hadi kituo cha basi. Kaka, machozi
3356 yanilengalenga, sijui nitasema nini kwa Baba na Mama.
3357 Usifike kuja kuniaga kwenye kituo cha basi nisije
3362 Nduguyo, Rukia Mafuru.
3364 Hasira iliyonipata baada ya kusoma barua hii haina kifani.
3365 Nilijikuta nasema moyoni "Kulikokuwa na mwanga sasa giza!
3366 Manase ana kiburi namna gani! Mimi mwanamume kama
3369 Kwa muda wa siku moja sikuweza kuhudhuria masomo
3370 kwa vile kichwa changu kilivyokuwa kimevurugika. Wakati
3371 huu sikuweza kwenda kumwona Manase. Hasira yangu
3372 ilikuwa kubwa vile kwamba kama ningekwenda bila shaka
3373 ugomvi na vita vingalitokea. Licha ya hasira wakati wa
3374 mitihani ulikuwa umekaribia, nami nikiwa mwaka
3375 wa pili nilipaswa kufanya vizuri ili kuingia mwaka wa tatu.
3377 Miezi miwili ilipita. Na baada ya mitihani nilikata shauri
3378 kwenda nyumbani nikiwa na wazo la kutafuta kazi ya muda
3382 kama ikiwezekana. Wakati huu sikuwa na habari kwamba
3383 Manase alikuwa amekwisha hamishwa.
3385 Nikiwa ndani ya stima kuelekea nyumbani kisiwani,
3386 hadithi hii yote ilinijia kichwani tena. Nilitoa ile barua
3387 niliyoandikiwa na ndugu yangu. Niliisoma tena kwa makini
3388 kuona kama kulikuwa na uwongo ndani yake. Niliona wazi
3389 kwamba Manase alikuwa akisema uwongo. "Manase anamwa
3390 ndugu yangu malaya!" nilisema moyoni. Niliikunja ile barua
3391 nikairudisha mfukoni. Nilianza tena kufikiri jinsi ya kujilipia
3392 kisasi. Nilikumbuka kwamba nilikuwa nimekata shauri
3393 kufanya maisha yake yawe magumu hapa duniani.
3395 Watu walipoanza kuinuka waliniondoa katika ndoto.
3396 Nilipotazama nje niliona kwamba mji wa Nansio ulikuwa
3397 umekaribia. Niligundua kwamba hata stima ilikuwa
3398 imekwisha punguza mwendo. Baada ya dakika tano tulifika.
3399 Nilipotoka nje nilikwenda nilikwenda mara moja kwenye kituo cha
3400 basi. Kwa nauli ya shilingi moja nilipanda basi lililokuwa
3401 likipita katika kijiji cha kwetu-Mahande. Kutoka barabarani
3402 pale basi liliponishusha, ulikuwa mwendo wa kilometa moja
3403 kufika nyumbani. Njiani nilikutana na watu wengi; ajabu
3404 ilikuwa kwamba kila mtu niliyekuwa nikikutana naye njiani
3405 alinitazama kwa mshangao hata wale walionifahamu. Mtu
3406 wa kwanza kuzungumza naye alikuwa kijana mmoja
3407 tuliyekuwa tukisoma pamoja zamani. Yeye sasa alikuwa
3408 ameoa na alikuwa na watoto watatu.
3410 "Wewe kwa nini umekuja nyumbani?" aliniuliza kwa
3411 mshangao bila hata kunisalimu kwanza.
3413 "Kwa nini? Mbona huwa nakuja nyumbani karibu kila
3416 "Heri ungebaki huko. Huku umejileta hatarini."
3420 "Hatari gani? Hujui?
3426 "Ndugu yangu, utasimuliwa nyumbani."
3428 Aliponiambia maneno haya ya mwisho alikwenda zake.
3429 Sikupata nafasi ya kuweza kumwuliza zaidi. Lakini nilianza
3430 kufikiri moyoni ni mambo gani aliyokuwa akizungumzia.
3433 Mtu wa pili kukutana naye alikuwa mzee. Mzee huyu
3434 alikuwa akipeleka ng'ombe wake mtoni kunywa maji.
3435 Alikuwa ameenea vumbi nyweleni.
3437 "Kazimoto! Umekuja kujionea mwenyewe!" alisema.
3445 "Mambo fulani yametokea pale nyumbani kwenu ambayo
3446 yameshangaza kijiji kizima cha Mahande."
3448 Nilianza kufikiri kwamba mimba ya ndugu yangu
3449 ndiyo ilikuwa ikikanganya kijiji kizima. Lakini kwa wakati
3450 huu hili halikuwa tena jambo la ajabu kama zamani. Lilikuwa
3451 limekwisha tokea kwa wasichana wengi kijijini, wasomao na
3452 wasiosoma. Zaidi ya hayo kwa njia gani mimba ya ndugu
3453 iliweza kuniweka hatarini?
3455 Nilikuwa nimekaribia kisima walichokuwa wakikoga na
3456 kuteka maji wanawake wa kijijini. Njia hii ilikuwa ikipita
3457 karibu sana na kisima hiki. Nilipokaribia karibu kabisa,
3458 nilisikia sauti za wasichana. Kama ilivyo desturi, nilipiga
3465 "Vaeni wanaume tupite!"
3467 "Ngoja kidogo!" walijibu. Baada ya muda nilisikia, "Tayari!"
3469 Nilipojitokeza walikuwa bado hawajavaa. Nilipita na
3470 sanduku langu, sasa begani, hali nikitazama pembeni.
3474 Niliwasikia wakicheka. Lakini mimi sikuwatazama. Nilisikia
3475 wakimwambia msichana mmoja: "Furahi basi! Bwana yako
3478 "Sasa mnataka nini?" msichana yule aliwajibu.
3480 "Mbona sanduku lataka kumwangusha na wewe huendi
3483 Nilifahamu huyo msichana alikuwa nani. Hata nilipokuwa
3484 nimefika mbali kidogo niliweza bado kusikia sauti zao.
3485 Walikuwa wakicheka. Niliona kwamba sasa wakati wa
3486 kusahau vitabu ulikuwa umeingia na kwamba nilikuwa
3487 nimeyafikia maisha yanayoitwa "maisha".
3489 Njia ya kwenda nyumbani kwetu ilipita nyumbani kabisa
3490 kwa Mzee Kabenga - baba'ke Manase. Nilimkuta Kabenga
3491 amekaa juu ya kichuguu kilichokuwa karibu na mji wake,
3492 fimbo mkononi, akitazama ng'ombe wake wawili wakila
3495 "Kazimoto," alisema kwa unyenyekevu, "sisi tu wazima,
3496 lakini mambo yanayotokea nyumbani kwenu hapo
3501 "Wewe nenda tu nyumbani. Baba yako hutamkuta, lakini
3502 nafikiri mama yako ataweza kukueleza."
3506 "Hayo pia mama yako atakueleza."
3508 Nilipokuwa nazungumza na Mzee Kabenga sauti yangu
3509 ilikuwa imesikika nyumbani. Niliwaona wadogo zangu
3510 wanakuja mbio kama kwamba atakayekuwa wa kwanza
3511 kunifikia atapata zawadi. Mara moja sanduku langu
3512 lilichukuliwa juu juu. Wengine hawakupata mzigo.
3514 "Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kumwona."
3516 "Mimi nilimsikia zamani!"
3520 "Baba amekula kuku wako wote; alikuwa anasema
3521 kwamba ukifika tukwambie kwamba wameliwa na bweha!"
3523 "Machungwa yameiva; mwaka huu mengi sana!"
3525 Mwishowe nilikata shauri kuzungumza nn mmoja tu kati
3526 yao yaani Kalia, mtoto ambaye nilikuwa nampenda sana
3527 kati ya wadogo zangu.
3529 "Baba yupo nyumbani?" nilimwuliza Kalia.
3531 "Baba! Nyumbani hayupo!"
3535 "Sisi hatukuambiwa."
3537 "Nyumbani kuna mambo gani?"
3539 "Siku hizi hatulali!"
3543 "Utaona leo usiku. Siku hizi wanafika karibu kila siku."
3547 "Watu gani? Nani anawafahamu? Hakuna ambaye amekwisha waona."
3549 "Wewe, Kalia, endelea tu kusemasema mambo hayo. Wewe
3550 ndiye utapigwa leo," wenziwe walimwonya.
3552 "Nani atawapiga?" niliwauliza. Wote walinyamaza.
3554 Tulikuwa tumefika nyumbani. Kuingia tu niliona kwamba
3555 kulikuwa na mambo fulani ambayo yalikuwa hayaendi sawa.
3556 Kila mtu alikuwa na huzuni. Kila mtu alikuwa akitembea pole
3557 pole kama mgonjwa, wala hapakuwa na mtu aliyefurahia
3558 sana kufika kwangu nyumbani kama ilivyokuwa kawaida
3559 nyakati zingine. Hata Mama hakufurahi.
3561 Nilipomwona dada yangu Rukia na tumbo kubwa, fikara
3562 kwamba Manase alikuwa amemharibia maisha yake ya mbele
3563 zilinijia kichwani. Alinisalimu kwa mbali hali ameinamisha
3564 kichwa. Hakujaribu kunitazama usoni. Mimi niliona kwamba
3565 tatizo la Rukia ndilo lilikuwa bila shaka tatizo lililokuwa
3566 likiwasumbua. Lakini baada ya kusalimiana na Mama
3570 aliyekuwa amekaa juu ya ngozi ya mbuzi kwa huzuni,
3571 nilishangaa kuona kwamba hakuzungumza juu ya tatizo hili
3572 la Rukia. Badala yake alianza kuniuliza kwa nini nilikuja
3575 "Hufahamu kwamba sisi wote hapa maisha yetu yamo
3576 hatarini? Kwa kuwa wewe umesoma nafikiri we ndiwe
3577 utakuwa wa kwanza kuuawa."
3581 "Ungekuwa mtu mwenye kusikia maneno ya watu
3582 ningekwambia urudi huko ulikotoka."
3586 "Hayo si mambo ya kuuliza."
3588 "Na Baba amekwenda wapi?"
3590 "Nitakueleza kesho pumzika kwanza."
3592 Wakati huo huo niliona moshi unaanza kutoka jikoni na
3593 Rukia alikuwa humo amekaa karibu na mafiga.
3595 Nilipomaliza kula nilianza kufungua sanduku langu ili
3596 kutoa matandiko na kutayarisha kitanda. Nilikuwa nikipanga
3597 vitabu vyangu mezani niliposikia mtu akibisha hodi.
3598 Nilifungua. Kabenga akaingia.
3601 "Karibu, Kabenga, karibu," nilisema.
3603 "Asante, mwanangu," alijibu.
3605 "Karibu kiti, usiogope."
3607 "Vitabu hivi vyote umekwisha vimalizia kichwani?"
3608 aliuliza huku akikaa.
3610 "Mbona nimekuja na vichache tu, vingine nimeviacha
3615 "Kazi tunayofanya ni kubwa mno; ngumu kama ya
3618 "Ah, mtoto wangu, usiseme kazi ya jembe. Kazi ya jembe
3619 inamnyofoa mtu hata anakuwa mzee siku si zake."
3623 "Sisi jembe letu ni kalamu."
3625 "Kweli, lakini kalamu haimfanyi mtu akatoka jasho."
3626 Alinyamaza kwa muda mfupi. "Kazimoto," alianza tena,
3627 nimekuja kuuliza kama una habari yo yote kuhusu mtoto
3632 "Huyu mwenda wazimu," alijibu.
3638 "Kwa nini unamwita mwenda wazimu?"
3640 "Kazimoto, hata wewe unafahamu. Mambo aliyoyafanya
3641 hayakutupendeza, mimi pamoja na wazazi wako. Wewe fikiri,
3642 watu tumesikilizana namna hii kwa muda mrefu, halafu Manase
3643 anatenda jambo kama hili!"
3645 "Hata mimi niliposikia nilishangaa," nilisema.
3647 "Ni mwenda wazimu. Ninakwambia ukweli ni mwenda
3648 wazimu. Tena kabla ya kuendelea ningependa utusamehe
3649 kwa mambo aliyoyatenda. Ni mwenda wazimu! Wewe tazama -
3650 ndugu yako alipokuja nyumbani na kutueleza yote
3651 yaliyotokea, mimi pamoja na mke wangu Tuza na wazazi
3652 wako tulikata shauri amwoe. Tulimwandikia barua, na wote
3653 tuliweka sahihi zetu. Mimi nilianza kazi ya kuposa. Barua ya
3654 kwanza tuliyopata kutoka kwake ilisema kwamba atafikiri.
3655 Hii hapa, unaweza kuisoma." Niliisoma.
3661 "Sasa, baada ya muda tulimwandikia tena barua tukimwuliza
3662 kama alikuwa amekwisha kata shauri. Kusema kweli
3663 tulimwambia wazi kwamba hapakuwa na haja ya kukata
3664 shauri: alikata shauri siku ya kwanza alipoanza mambo hayo.
3665 Lakini barua aliyotuandikia tena ilikuwa ya kijinga. Isome
3666 mwenyewe, mimi siwezi kukwambia maneno ya kijinga kama
3670 hayo kwa mdomo wangu." Niliichukua na kuisoma.
3673 Ninawaarifuni kwamba kwa sababu fulani kubwa
3674 siwezi kumwoa Rukia. Nimekwisha pata mchumba
3675 mwingine, na mzuri kuliko Rukia. Kama nia yenu ni
3676 kutaka mimi nioe, semeni tu, nami nitawaambia
3677 mahali anapoishi ili muanze kazi ya kuposa. Lakini
3680 "Umeona sasa kijana mwenzio!"
3684 "Sasa sisi hatufahamu jambo la kufanya. Lakini siwezi
3685 kuamini kwamba mtoto wangu Manase anaweza kuharibu
3686 uhusiano wetu mzuri kati yangu na baba'ko. Vijana vya siku
3687 hizi! Eti mpaka mjichagulie wenyewe! Msichana mzuri
3688 huonekana na watu wengi. Hivi ulipokuwa safarini kuja
3689 huku hukupata kuonana naye?"
3695 "Hata mimi mwenyewe niligombana naye. Anamwita ndugu yangu malaya."
3697 "Unaona sasa! Watu mmesoma pamoja."
3699 "Manase anaonekana kuwa mtu mwenyewe kiburi sana
3702 "Hicho ni kiburi hakika, na kiburi hakifai." Kabenga
3703 alitikisa kichwa chake kwa huzuni. "Hata kama amekataa
3704 kumwoa msichana huyu, maadam amekubali kwamba mimba
3705 ni yake angekuwa anamtumia pesa za matumizi mbeba mwana.
3706 Lakini mtoto wetu amekataa. Kama angetuma pesa sisi
3707 tungeendelea kumnunulia samaki mpaka atakapojifungua,
3708 maana mtoto ni wetu."
3712 Tulinyamaza kwa muda.
3714 "Labda una habari zo zote juu ya binti yangu Sabina,"
3717 "Sabina sina habari zake maana huwa hatuandikiani barua."
3719 "Labda naye amekwisha pata mimba, nasikia siku hizi
3720 anafundisha huko Tabora."
3722 "Sabina ni msichana atunzae usafi."
3724 "Dansi ya kushikana wawili-wawili ilipoingia nchini
3725 usafi ukaisha, mwanangu."
3727 "Atakuja lini livu," niliuliza.
3729 "Ametuandikia barua kwamba atakuja mwezi ujao. Mama
3730 yako amekwisha kueleza mambo yanayotokea hapa?"
3734 "Labda atakueleza baadaye."
3736 "Ni mambo gani hayo?"
3738 "Mambo haya yalianza kuonekana na baba yako.
3739 Alipojaribu kufahamu watu wanaofanya hivyo alipigwa.
3740 Baadaye alikuja kuniambia mimi. Tukiwa wawili tulijaribu
3741 kuwatafuta kwa mikuki lakini kila mara nilipokuwapo
3742 hawakuonekana. Ni wajanja sana."
3744 "Mimi nitajaribu kuwapiga," nilisema.
3746 "Wewe bado mtoto mdogo, afadhali usijaribu, watu hao
3749 "Wana nguvu sana!" nilistaajabu.
3751 "Ndiyo. Mambo yenyewe si ya kuambiwa, Kazimoto,
3752 utayaona mwenyewe karibuni. Kijiji kizima kinafahamu."
3754 "Kuna habari fulani ambazo zimenishangaza sana," nilisema.
3756 "Habari gani?" Kabenga aliuliza.
3758 "Nimesikia kwamba Manase atamwoa Vumilia karibuni.
3759 Kabenga alishangaa. Hakuwa na neno la kusema kwa muda.
3761 "Hayo pia nilikuwa nataka kukwambia. Mimi huwa sifichi
3762 jambo lo lote," alisema.
3766 "Nieleze, nilimwambia.
3768 "Kwanza nikuulize swali moja," alisema.
3770 "Uliwahi kusikia kwamba Manase ana kimada?"
3772 "Nimesikia kwamba siku hizi ni kama ameoa."
3774 "Jina la msichana huyo nimelisahau kidogo lakini ni jina
3779 "Ndiyo, Salima. Sasa tuliposikia kwamba mtoto wetu
3780 amepotoka na kwamba anataka kuoa mwanamke kutoka
3781 mbali tulikata shauri kumtafutia mchumba mwingine. Mke
3782 wangu Tuza akatoa wazo kwamba tumchumbie Vumilia kwa
3783 sababu tuliona alikuwa hawezi kushaurika kumwoa Rukia.
3788 "Hata Manase naye tumemwandikia barua amekubali
3789 kumwoa Vumilia. Kama mambo yakienda vizuri nafikiri
3790 atamwoa baada ya miezi miwili."
3792 Kabenga aliyasema maneno haya hali akiinuka
3793 kwenda nyumbani kwake. Giza lilikwa limekwisha ingia. Aliniacha
3794 mimi na mawazo mengi.
3797 Ilikuwa usiku tunakula na wadogo zangu karibu na moto.
3798 Wanawake walikuwa wakila jikoni, niliposikia mbwa wanaanza
3799 kubweka hali wakitazama upande kulikokuwa mwembe.
3800 Niliona watoto wanaanza kutetemeka kwa hofu. Wanawake
3801 jikoni walikaa kimya.
3803 "Kuna nini?" niliuliza. Watoto walinyamaza.
3804 "Sh! Kamata!" niliwahimiza mbwa wawili. Hapo hapo
3805 nilisikia sauti ya Mama kutoka jikoni.
3807 "Kazimoto! Unataka kufanya nini? Wewe nyamaza tu!
3808 Sikutaka kusikiliza maneno ya Mama. Niliinuka. Nilikwenda
3812 chumbani kwa Baba kuchukua mkuki.
3816 Mbwa waliponiona nakuja na mkuki mara moja walikimbia
3817 kuelekea kwenye mwembe, mimi nikawa nawafuata nyuma.
3818 Kwa kuwa nilikuwa nimekaa kwenye moto kwa muda mrefu,
3819 sikuweza kuona vizuri. Nilikuwa sijafika mbali niliposikia
3820 mbwa mmoja aliyekuwa ametangulia anabweka. Nilimwona
3821 anarudi akichechemea, mguu mmoja juu, huku akilialia kwa
3822 maumivu. Mbwa wa pili alikimbilia miguuni mwangu. Wadogo
3823 zangu walikuwa wamekwisha kimbilia jikoni. Hofu kubwa
3824 ilinipata kama kwamba simba wa Tsavo walikuwa mbele
3825 yangu. Hofu yangu ilikuwa kubwa zaidi kwa sababu sikuwa
3826 na bunduki, na wala sikufahamu hatari iliyokuwa mbele
3827 yangu ilikuwa kubwa kiasi gani.
3829 "Umeona?" Mama alisema. "Unafikiri wewe mwanamume
3832 Nilirudisha mkuki mahali nilipoutoa. Nilikwenda ndani ya
3833 nyumba yangu kulala. Nilipofika kitandani nilianza kufikiri:
3834 "Haya ndiyo mambo niliyokuwa nikiambiwa. Hao ndio watu
3835 wanaosemekana kuwa na nguvu. Lakini kwa nini wawe
3836 wanakuja nyumbani kwetu tu? Sijui nifanye jambo gani ili
3837 niweze kuwakomesha! Siamini kwamba kuna wachawi
3838 duniani. Lazima tu wawe watu wa kawaida. Na ni watu
3839 ambao wanaishi kijijini humu humu."
3841 Niliona kwamba watu wote wa nyumbani kwetu walikuwa
3842 wamekwisha nyang'anywa utu wao, hapakuwa na mtu tena
3843 pale nyumbani. Sikutaka kugeuzwa na hofu kama wao; wao
3844 walikwisha kuwa watu ambao hawawezi hata kuguna.
3845 Niliona kwamba kazi kubwa iliyokuwa ikinikabili sasa ilikuwa
3846 siyo ya Rukia lakini kufikiria njia ya kuweza kuwakomesha
3847 watu hawa waliokuwa wakiuchezea mji wa kwetu.
3851 Usingizi ulikuwa bado kunipata wadogo zangu walipokuja
3852 kulala chumbani ndani ya nyumba yangu. Rukia alikwenda
3853 kulala na Mama ndani ya nyumba ya Baba. Usiku wa manane
3854 nilisikia vishindo nti! nti! kuzunguka nyumba yangu.
3856 Hofu ilinishika lakini nilipiga moyo konde. Niliamka
3857 kwenda kuchungulia dirishani. Mara vishindo vilikoma, lakini
3858 sikuweza kuona mtu ye yote. Vishindo vilipoacha kusikika
3859 nilikwenda tena kulala kitandani. Nilikuwa bado sijajifunika
3860 niliposikia ndani ya nyumba ya Baba, Rukia na Mama
3861 wakipiga mayowe: "Tumekufa ! Tumekufa! "
3863 Mara moja nilitoka nje na shuka yangu pamoja na panga
3864 maana mimi ndiye mwanamume peke yangu niliyekuwa
3865 nikitegemewa. "Kuna nini?" niliuliza. Nilipofika karibu na
3866 nyumba nilisikia watu kama wawili wakikimbia. "Fungueni
3867 mlango!" Walifungua, nikaingia: Niliona mchanga mwingi
3868 sana juu ya vitanda.
3870 "Basi - " Mama alisema, "mchanga huu ulikuwa ukimwagika
3871 kama mvua kupitia dirishani.
3873 "Ondoeni mchanga mlale," niliwaambia. Walifanya hivyo.
3875 Niliondoka kwenda nyumbani mwangu. Nilikuwa bado
3876 sijafika niliposikia wadogo zangu wanalia. Nilipoingia tu,
3877 mchanga haukumwagwa tena.
3879 Nilikata shauri kulala na kuwaacha wafanye mambo yao.
3880 Sikusikia vishindo tena nilipolala kitandani. Kwa muda
3881 nilifikiri juu ya maajabu haya, lakini mwishowe usingizi
3882 ulinichukua mpaka asubuhi nilipoamshwa na Kalia.
3884 Wakati nikipiga mswaki asubuhi nilitembeatembea
3885 kuzunguka mji nikitazama chini. Niliweza kuona nyayo za
3886 watu, lakini sikuweza kuzitambua. Nilipofika chini ya
3887 mwembe niliona nyayo nyingi. Ilionekana kwamba hapo
3888 ndipo walipokuwa wamesimama.
3890 Siku nzima sikuwa na raha. Nilikuwa nikifikiria jambo la
3894 kufanya. Hata chakula cha mchana sikula vizuri. Baada ya
3895 kula nilijaribu kusoma hadithi lakini niliona kwamba
3896 nilikuwa siifuati. Nilitupa kitabu juu ya meza, nikachukua
3897 sabuni kwenda kuoga mtoni. Niliporudi nilianza kuchana
3898 nywele zangu, mara nikamwona Kalia anaingia chumbani
3899 mwangu hali akitabasamu.
3901 "Umefurahia nini?" nilimwuliza.
3907 "Yuko pale! Husikii!"
3913 Mara moja nilifahamu, maana Kalia ndiye tulikuwa
3914 tukimtumia kama posta yetu.
3916 "Anafanya nini?" nilimwuliza.
3922 "Ndiyo, ameniambia kwamba ametangulia."
3926 "Amesema pale mahali penu pa kawaida."
3928 "Asante, Kalia, nitakwenda sasa hivi."
3930 "Amesema usikawie sana."
3934 Kalia aliondoka chumbani anakimbia kuwaona wenzake
3935 ambao walikuwa wakimpigia miunzi waende mtoni kuoga.
3936 Nilipomaliza kuchana nywele nilifungua sanduku na kutoa
3937 kitambaa cha gauni. Nilikikunjia ndani ya karatasi na
3938 kuondoka kabla ya Mama kuniuliza mahali nilikokuwa
3939 nakwenda. Maswali ya Mama kuhusu kokote nilikokwenda
3940 yalikuwa yamekwisha niudhi.
3942 Mahali petu pa kawaida hapakuwa mbali sana. Lilikuwa ni
3943 shamba la mihogo mbali kidogo na nyumbani kwetu. Mwenye
3947 shamba hili alikuwa mvivu kupalilia; kama angekuwa na
3948 nguvu za kupalilia mahali petu pangekuwa wazi. Lakini kwa
3949 mshangao nilikuta mihogo yenyewe imekwisha chimbwa na
3950 mahali petu palikuwa wazi kama uwanja wa mpira. Nilikuwa
3951 bado nikishangaa nilipoona, mbele kidogo karibu na shamba
3952 jingine la mihogo, msichana amesimama amenipa mgongo,
3953 kanga ilikuwa imeshuka kutoka kichwani kufunika mabega.
3954 Moyo wangu ulianza kudunda; naye aliposikia viatu vyangu
3955 alianza kung'oa vijani na kukata vijiti vilivyokuwa karibu.
3956 Nilipomkaribia nilimshika begani na kujaribu kumgeuza
3959 "Niache," alisema huku akicheka.
3963 "Unaponishika unaniumiza."
3965 "Mimi nakutazama tu."
3967 "Kwani hujaniona, au labda umenisahau "
3969 "Vumilia, habari ya siku nyingi?"
3971 "Hali yangu nzuri kama mti usioliwa na mchwa."
3973 "Mti usioliwa na mchwa una nini?"
3975 "Unafanya nyumba isianguke mapema," alisema. Halafu
3976 aligeuka kunitazama. "Kazimoto, mimi mzima kama shilingi
3977 ya masikini iliyosahaulika mfukoni."
3981 "Hata barua hamna!" Nilikosa la kujibu.
3983 "Mama yako amefika? Tulikuwa naye kisimani."
3987 "Ndiye ameniambia kwamba alikuacha nyumbani wakati
3988 alipoondoka; na jana je, ulifika salama? Tulikuona na sanduku
3991 "Kwa nini hukuja kunisaidia?"
3993 "Acha," alisema pole pole, "watu wanakuja."
3999 "Ninasema acha; mimi hayakunileta hayo."
4001 "Acha mchezo," nilimwambia kwa ukali kidogo.
4003 "Mwenye baridi ndiye ajongeaye moto. Wewe ulipaswa
4006 "Nilikuwa nataka kumtuma Kalia. Uliniwahi kidogo tu."
4009 "Vumilia, kweli tuondoke hapa, tumesimama njiani."
4011 "Tangulia," aliniambia.
4013 Nilitazama kila upande wa njia, halafu niliingia mihogoni
4014 hali nimeinama. Wakati huo nilikuwa nimesahau uanachuo.
4015 Nilipofika katikati ya shamba nilikaa. Nilianza kung'oa
4016 majani ili kutayarisha kitanda. Kwa muda wa dakika tano
4017 sikusikia kama Vumilia alikuwa anakuja. Baada ya muda
4020 "Kwa nini umekawia namna hii?" nilimwuliza.
4022 "Ulipotoka tu baba yako akapita. Anasema anatoka safari."
4028 "Mbona unakaa mbali namna hii? Huoni?" Nilimwonyesha
4031 "Mm!" aliguna na kupandisha mabega juu kama alama ya
4034 "Umesema mwenyewe - mwenye baridi ndiye ajongeaye
4035 moto," nilisema. Niliinuka kwenda karibu naye. Nilianza
4036 kumpapasa kiunoni. Nilianza kumvua nguo.
4038 "Acha nivue mwenyewe!" alisema.
4040 "Upesi kabla majani yetu hayajakauka."
4042 Muda ulikuwa mfupi. Ilikuwa baada ya muda huu
4043 nilipotambua kwamba majani tulikuwa tumekwisha yaacha
4044 pembeni, na kwamba mti mmoja wa mhogo niliokuwa
4045 nimekanyaga ulikuwa umeng'oka. Nilianza kumkumuta
4050 "Kazimoto, unafahamu livu hii tunaagana!"
4052 "Bado sijafahamu sawa sawa."
4054 "Mpango wangu wa ndoa umekaribia kutekelezwa.
4055 Nafikiri baada ya miezi miwili!"
4057 "Bahati mbaya sana."
4059 "Kwa hiyo utakapokuwa unakuja kunichukua usiku fika
4060 kwa uangalifu, kwa sababu siku hizi Mama ananichunga sana.
4062 "Nitakuja kukuchukua Jumamosi," nilimwambia.
4068 "Sina nafasi siku hiyo; fika Jumapili."
4070 "Haya nitakuja. Nilikuwa na zawadi kidogo ya kukupa."
4071 Nilimpa kile kitambaa. Aliifungua upesi ile karatasi.
4072 Alikiona. Alitabasamu.
4074 "Asante sana," alisema. "Nafikiri kimekugharimu shilingi nyingi.
4076 "Thelathini na tano tu."
4078 "Thelathini ni pesa nyingi sana." Alikitia ndani ya kanga.
4079 "Nakwenda. Kwa heri," alisema.
4081 "Unapita wapi?" nilimwuliza.
4087 Kila mtu alishika njia yake na kutopa upande mwingine
4088 wa shamba. Nilipofika nyumbani nilikuta kweli Baba amekaa
4089 "Tutayazungumza kesho," alisema. Baada ya kumsalimu
4090 nilikwenda nyumbani mwangu. Nilikuta Kalia amekwisha
4091 toka mtoni. Alikuwa akitumia shanuo langu. Nipoingia aliguna.
4093 "Kwa nini unaguna?" nilimwuliza.
4095 "Hata mimi naona tu," alisema.
4099 "... kwamba yule msichana ulimwona."
4105 "Tumekutana naye njiani anatoka huko huko ulikokuwa.
4106 Alikuwa amefurahi sana. Mara kwa mara huwa anatuuliza
4107 utakuja lini." Alinyamaza kwa muda.
4109 "Ngoja niweke wei halafu nikupe mambo yako," alisema.
4110 Alijaribu kuweka wei aliyokuwa anasema. Alipomaliza niliona
4111 kwamba wei aliyoweka ilikuwa imejipinda kama alama ya
4112 vema. Alichukua kitabu changu kimoja kilichokuwa mezani,
4113 na humo alitoa barua.
4115 "Hii barua yako. Nilikuwa nayo hata kabla hujaenda
4116 kumwona. Lakini alikuwa ameniambia nikupe baada ya
4119 Niliifungua kwa haraka. Bila kutegemea, poda nyingi
4120 ilimwagika juu ya kitanda changu na kipande kidogo cha
4121 karatasi kilitoka. Kalia alitoka nje huku anacheka. Nilimsikia
4122 akiwaeleza wenziwe nje.
4124 "Kalia, nitakupiga!" nilimwambia. Lakini Kalia alicheka
4125 tu na kukimbilia nyumbani kwa Kabenga kula machungwa.
4126 Nilisikia Kabenga akimwambia Kalia angoje mpaka kesho,
4127 kwani ilikuwa haifai kula machungwa jioni.
4129 Kalia alikuwa kijana ambaye mara nyingi aliweza
4130 kuzungumza nami kama mwenzangu ingawa alikuwa na umri
4131 wa miaka kumi na mitano tu. Tulikuwa tumezoeana, naye
4132 alikuwa haniogopi tena. Mimi mwenyewe nilipenda kutembea
4133 naye; wasichana wangu wote aliwafahamu na matendo yangu
4134 nao aliyaona. Yeye pia alipenda sana kunifuata. Mara fulani
4135 nilikuwa namrudisha nyumbani hasa nilipokuwa na safari
4136 ya kwenda mbali. Alizoea kusikitika, kwa hiyo nikawa
4137 namtoroka. Kalia alimaliza darasa la saba tu. Aliposhindwa
4138 alianza kujishughulisha nyumbani na takataka; mwishowe
4139 akawa fundi wa kushona viatu na kunyoa.
4141 Kalia alipokimbia nilifungua kile kijikaratasi ili kusoma
4145 ujumbe uliokuwamo. Niliona msitari mmoja tu: "Ninaomba
4148 Giza lilikuwa limekwisha ingia na niliona Baba akikoka moto.
4149 Furaha yangu ilipungua nilipokumbuka yale mambo
4150 yalioyokuwa yakitokea nyumbani kwetu usiku. Niliona
4151 kwamba hata mimi hofu ilikuwa imekwisha anza kunitawala.
4152 Siku hiyo tulikula bila kusikia vishindo vyo vyote,
4153 hata mbwa hawakubweka.
4155 "Umekwisha zungumza na ndugu yako?" Baba aliuliza
4160 "Jibu lako nililifahamu. Kazimoto, mambo ya wasichana
4161 yamekuingilia vile kwamba watu wa nyumbani umewasahau."
4163 "Mambo ya wasichana sihusiani nayo."
4165 "Unasema nini? Mtoto gani wewe? Unataka kunidanganya
4166 mimi? Kazimoto, uwongo huu wote uliupata wapi? Unafikiri
4167 mimi sikukuona unanyatia mihogoni?"
4169 "Basi, basi Baba, nisamehe," nilisema upesi.
4171 "Ndiyo, Kazimoto, ukitaka kuwa rafiki yangu sema ukweli
4174 "Ndiyo uliniona," nilisema.
4176 "Kwa kuwa hufahamu habari za hapa nyumbani, basi mimi
4177 nitakuambia. Kazimoto, tangu ufike hapa ndugu yako
4180 Alipomaliza kusema maneno hayo aliinuka kwa hasira
4181 kwenda kulala na kuniacha mimi nikishangaa. Nami niliinuka
4182 kwenda jikoni alikokuwa amekaa Mama na Rukia. Nilipoingia
4183 jikoni nilimkuta Mama anakula; lakini niliona kwamba
4184 hakula chakula kingi maana ugali ulikuwa umenyofolewa
4185 mara tatu tu. Nilimwona Rukia amelala chini juu ya kanga,
4186 kichwa chake amekiweka juu ya miguu ya Mama. Mama
4187 alikuwa akimpangusa kwa kanga machozi yaliyokuwa
4191 yakitiririka kila wakati.
4193 "Rukia," nilimwita pole pole. "Rukia," niliita tena.
4194 Hakuniitikia. Nilijaribu tena. "Rukia, jaribu kula chakula
4195 kidogo." Hakuniitikia. Badala yake alianza kulia kwa kelele.
4197 "Kazimoto," Mama alisema. "Kazimoto, tuache tupumzike,
4198 tuache tulie. Huu ni ugonjwa umeletwa na vijana na utatuma-
4199 liza sisi kina mama wenye mabinti. Ninajiona kwamba
4200 nitakwenda pamoja na binti yangu."
4202 Machozi yalimlengalenga. Niliona hapa hapa kuwa mahali
4203 pangu. Niliondoka pole pole nikawaacha wanalia wote pamoja
4204 huku wamekumbatiana.
4207 Kesho yake asubuhi Kalia ndiye aliyeniamsha. Nilipokuwa
4208 nikipiga mswaki niliwaona Kabenga na mkewe wakiongozana
4209 kuja nyumbani kwetu. Kwa kuwa kulikuwa na baridi bado
4210 wote walikuwa na shuka mabegani. Walipofika ndani ya
4211 nyumba ya Baba, niliwasikia wakiuliza habari ya Rukia.
4212 Mama aliwajibu kwamba mgonjwa aliomba uji asubuhi.
4213 Walifurahi na kusema kwamba maadam ameanza kunywa uji
4214 karibu atakula chakula cha kawaida. "Tunamwombea apone,"
4215 walisema. Nilipomaliza kuvaa nilistukia kumwona Kalia
4216 anakuja chumbani mwangu.
4218 "Kazimoto, unaitwa na Baba."
4222 "Ndani ya nyumba yake. Amesema harakisha."
4224 Nilikwenda. Nilipofika chumba cha mazungumzo nilikuta
4225 kiti kimoja kimebaki kwa ajili yangu. Kabenga na Baba
4226 walikuwa pia wamekalia viti. Tuza na mama yangu walikuwa
4229 "Kazimoto," Baba alianza kuzungumza, "tumekuita ili
4230 tujadiliane juu ya mambo ambayo hata wewe mwenyewe
4231 umekwisha yaona. Yalipotokea, mimi pamoja na Kabenga
4235 tuliona hawa hawakuwa watu wengine isipokuwa wachawi.
4236 Nilifunga safari kwenda nchi za mbali kuwaona waganga.
4237 Huko waganga wameniambia wazi kwamba ni kina Masesa
4238 na watoto wake. Hawa ndio watu ambao huwa wanakuja
4239 hapa usiku. Na sababu yenyewe nimeambiwa kwamba ni
4240 mashamba. Unafahamu kwamba sisi tuliletwa hapa na
4241 serikali, ingawa kweli tumekaa kwa muda mrefu. Sasa Bwana
4242 Masesa anataka tuhame ili achukue tena mashamba yake."
4244 "Masesa anaishi wapi?" niliuliza.
4246 "Ni kaka yangu," Kabenga alijibu, "isipokuwa yeye anaishi
4247 katika kijiji kifuatacho cha Kigara."
4249 "Kwa hiyo mashamba haya ni yenu?" nilimwuliza Kabenga.
4251 "Ni yetu ndiyo, lakini mimi sina matata."
4253 "Sasa tufanyeje?" Baba aliuliza.
4255 "Hata mimi nimo hatarini," Kabenga alisema, "kwa hiyo
4256 mimi naona afadhali tupeleke mambo haya barazani."
4258 "Barazani kama kwamba tumekwisha waona!" Mama
4261 "Wachawi hatuwezi kuwaona," Tuza naye alijitokeza.
4263 "Mimi nitawashika," nilisema.
4265 "Wewe!" Baba alishangaa.
4267 "Ndiyo," nilijibu haraka.
4269 "Wachawi wajanja," Kabenga alisema. "Hata sasa
4270 inawezekana wapo hapa wanatusikiliza."
4272 Hapo ndipo nilipowaambia maneno niliyoambiwa na
4275 "Kuwashika wachawi ni jambo rahisi sana," nilianza.
4276 "Jambo moja kuhusu wachawi ni kwamba wana pua kali sana
4277 kama wanyama. Wanafahamu sana harufu ya mwanadamu,
4278 kwa sababu mtu ambaye huota moto ana harufu ya pekee.
4279 Wachawi wakitaka kwenda kutembea usiku hawasogelei
4280 moto muda wa siku tatu nne; halafu wakitoka nje usiku
4284 huvaa nguo ambazo huwa zimetunzwa nje majanini ili
4285 kupoteza harufu kwa umande. Wengine huenda uchi. Kwa
4286 hiyo watembeapo ni vigumu kuwaona. Ukitaka kuwaona
4289 "Labda kuna ukweli ndani yake," Kabenga alisema.
4291 "Jaribu," Baba alisema.
4293 "Leo," Mama alisema.
4295 "Mimi sidhani kwamba atafanikiwa," Tuza alisema.
4297 "Leo haiwezekani," nilijibu, "kwa sababu nguo zangu
4298 lazima zikae nje kwa muda wa siku kadhaa."
4300 Mkutano ulipokwisha, wote walikubali kwamba nijaribu.
4301 Kwa muda wa siku tatu sikukaa karibu na moto na mara
4302 nyingi mchana nikawa nakaa kivulini ili kupoteza harufu
4303 yote ya kibinadamu. Nguo za kaniki zilipelekwa majini.
4304 Mwishowe siku ambayo nilikuwa nimeahidi kuwavizia ilifika.
4305 Nilitengeneza kiti cha kamba juu ya mwembe ambao, chini
4306 yake, nilizoea kuona nyayo zao. Ilikuwa siri kubwa, hata
4307 wadogo zangu nyumbani hawakufahamu isipokuwa sisi
4308 watano. Siku hiyo Kabenga alikuja kulala kwetu ili kuona
4309 yatakayotokea. Siku hiyo nilikula chakula cha jioni kama
4310 saa kumi na mbili. Baada ya kula nilipanda mtini pamoja
4311 na upinde, mishale minne na mkuki. Usiku huo hawakuja.
4312 Nilifanya hivi kwa muda wa siku tatu, lakini sikufanikiwa.
4313 Kiini cha mambo haya kiliendelea kuwa fumbo kubwa.
4319 Jumanne, niliondoka nyumbani asubuhi. Nilikuwa na nia
4320 ya kumtoroka Kalia. Rukia alikuwa bado hajaanza kula
4321 vizuri, lakini niliona lazima kwenda kumsalimu rafiki yangu
4322 na kumpa pole kwa maafa yaliyompata. Rafiki yangu,
4323 Kamata, alikuwa akiishi katika kijiji cha Saku. Kamata
4324 alikuwa mmoja kati ya rafiki zangu ambao nilizoea kuwate-
4325 mbelea mara nne au zaidi wakati wa likizo. Yeye alikuwa
4326 ameoa na alikuwa na watoto wawili. Alikuwa na mji wake
4327 peke yake, wenye nyumba mbili, ya kulala na jiko.
4328 Nilipokuwa nikisoma naye katika shule ya msingi, Kamata
4329 alikuwa amenitangulia mwaka mmoja, lakini alishindwa
4330 kuingia darasa la tisa. Aliposhindwa, hakufanya uhuni
4331 wafanyao watoto wengi washindwao darasa la saba siku hizi.
4332 Alitambua mara moja kwamba kazi ya ofisi haikuwa yake
4333 tena. Alikaa miaka miwili halafu akaoa. Mama yake alipofariki,
4337 siku chache baada ya harusi, Kamata alishika mji na
4338 kuuchukua. Baba yake alikufa zamani, na Kamata hakupata
4339 kuona sura yake; alikuwa bado mtoto mchanga wakati huo.
4341 Kamata alikuwa mkulima stadi. Alikuwa na shamba kubwa
4342 la migomba; shamba la mpunga karibu na ziwa; kishamba
4343 kidogo cha kabichi na shamba kubwa la viazi. Alikuwa pia
4344 na mitego mitano ya samaki. Alikuwa kijana nadhifu sana.
4345 Wakati alipokuwa hafanyi kazi nguo zake zilikuwa safi daima.
4346 Baiskeli yake ilikuwa ikisafishwa karibu kila siku. Visu vyote
4347 nyumbani vilikuwa na makali daima. Ubaya wake ambao
4348 ulifanya vijana majirani wamchukie kidogo ni kwamba
4349 alikuwa haazimi kitu chake. Hata juu ya baiskeli yake alikuwa
4350 ameandika: "Utaazima Kesho".
4352 Huyu ndiye Kamata, rafiki yangu, ambaye nilikuwa
4353 nikienda kumtembelea. Asubuhi kabisa nilichukua baiskeli
4354 yangu juu juu ili isipige kelele na kumwamsha Kalia ambaye
4355 alikuwa bado usingizini. Nilipoitoa nje nilifunga mlango pole
4356 pole. Baba, Mama, Rukia, sikuwasabahi. Niliondoka bila
4357 kumwambia mtu ye yote mahali nilikokuwa nakwenda.
4358 Ulikuwa karibu umbali wa kilometa tano hivi kutoka
4359 Mahande kwenda Saku. Njiani nilikutana na watu wengi:
4360 wenye majembe; wenye watoto mgongoni na wengine
4361 waliokuwa na safari kama mimi. Niliendesha baiskeli yangu
4362 nikipanda vilima na kushuka. Ule utoto wa kupanda kila
4363 kilima ulikuwa umekwisha ondoka.
4365 Nilifika nyumbani kwa Kamata saa nne. Nilimkuta Matilda,
4366 mke wa Kamata, akichanja kuni kwa shoka. Mtoto mmoja
4367 alikuwa mgongoni, wa pili alikuwa amekaa chini ya kivuli
4368 cha mti, kiazi mkononi. Mji wote ulikuwa umefagiliwa vizuri.
4370 Matilda alitupa shoka chini aliponiona.
4372 "Karibu! Karibu!" alipiga kelele.
4374 "Starehe, Kamata hayupo?"
4378 "Hayupo. Amekwenda kuondoa mitego yake majini."
4382 "Lazima atakuwa hapa kabla ya saa sita."
4384 "Ninakwenda ziwani kumngojea."
4388 "Ninakwenda kupunga hewa ziwani kidogo."
4390 "Kazimoto, hata wewe unafahamu Kamata alivyo.
4391 Asipokukuta nyumbani atakuja kunikaripia kwamba
4392 sikukukaribisha vizuri."
4394 Baada ya kuzungumza naye kwa muda aliniruhusu kwenda
4395 ziwani. Nilimwacha akiingiza baiskeli yangu ndani.
4397 Nilipofika ziwani nilikuta wavuvi watano wakishona
4398 matundu ya mitego yao. Walikuwa wakifanya kazi hii kwa
4399 haraka sana. Mikono yao ilikuwa myepesi sana. Walikuwa
4400 wakifanya kazi hii hali wakisimuliana hadithi na kucheka
4403 "Kamata anaweza kuwa wapi?" niliuliza.
4405 "Kamata?" mmoja aliniuliza tena.
4409 "Kuna uzima au msiba?"
4429 "Hapo Mahande unatoka sehemu gani?"
4433 "Kamata atarudi karibuni. Ameondoka zamani na
4437 mtumbwi wake, Wewe mgeni wake, sivyo?"
4441 "Unaweza kukaa hapo mchangani umngoje."
4443 Nilikaa, nikawa nawatazama wanafanya kazi yao. Kijana
4444 mmoja ambaye nilifikiria mjinga kati yao ndiye alikuwa
4445 akisimulia hadithi. Alikuwa kijana mfupi mwenye ndevu.
4446 Meno yake yalikuwa nje daima utafikiri anacheka.
4448 Baada ya kijana huyu kusimulia hadithi yake ambayo
4449 ilichekesha sana watu, kila mmoja alianza kutoa hadithi yake;
4450 zote zilihusu wanawake. Walisema kwa lugha ya matusi vile
4451 kwamba nilianza kufikiri moyoni kama walikuwa wamekwisha
4452 sikia kitu fulani kiitwacho dhambi. Mmoja kati yao alijidai
4453 kwamba kwa wanawake tu alikuwa amebakiza makabila
4454 machache ya nchi hii. Alianza kutaja kila kabila akitoa
4455 kasoro zao. Hapo ndipo nilipoanza kufikiri moyoni kwa
4456 nini nilisoma mpaka Chuo Kikuu. Nilianza kujiuliza kwa nini
4457 nilisoma kile kitabu cha zamani - Biblia. Niliwaonea wivu
4458 wenzangu ambao tuliachana darasa la nne. Wao sasa walikuwa
4459 wakicheza zeze na kupiga vishindo kwa furaha. Niliona
4460 kwamba elimu ilikuwa sumu ya furaha yangu. Kila siku
4461 kusoma vitabu na magazeti nisiwe nyuma ya wakati. Sasa
4462 niliona tofauti kati ya maisha yangu na yao. Kwa wakati huu
4463 wazo la kuacha shule ili niishi kama wao lilinijia kichwani.
4465 Sikuona sababu ya kusumbuliwa na mawazo, kuwa na
4466 wajibu mkubwa zaidi, halafu kufa kama wao na labda
4467 kwenda motoni, wao mbinguni - faida gani?
4469 "Huyo Kamata anakuja," walisema wakitazama ziwani.
4470 Jinsi walivyoweza kuona mtumbwi sijui, maana mimi
4473 "Inaonekana kwamba leo hakupata samaki wengi," mmoja
4476 Alipofika karibu niliona mtumbwi wake ukipanda na
4480 kushuka juu ya mawimbi. Alipofika karibu sana niliona
4481 kwamba hakuwa na shati kifuani. Mwishowe mtumbwi wake
4482 uligusa mchanga. Kamata alitoka na kusukuma mtumbwi
4483 wake. Alikuwa amekwisha niona.
4485 "Kazimoto! Nisamehe, sikujua! La sivyo nisingekawia
4488 "Umefanikiwa?" wavuvi walimwuliza.
4490 "Siku hizi samaki wamekataa kufa," aliwajibu.
4491 Na kweli hakufanikiwa. Wale samaki wachache aliokuwa nao
4492 aliwafunga kwenye ncha mbili za mti. Yeye alisimama
4493 katikati na kuwabeba. Wengi walikuwa bado wazima na
4494 mikia yao ilikuwa ikipigapiga.
4496 "Twende nyumbani, Kazimoto," aliniambia. "Jamani
4497 mtanisamehe nimepata mgeni."
4499 "Lakini utakuja?" wavuvi walimwuliza.
4503 "Kule. Umlete mgeni." Walipeana alama fulani ambazo
4506 "Ndiyo nitakuja," aliwajibu.
4508 Tuliondoka kuelekea nyumbani. Tulipokuwa njiani Kamata
4509 aliniita "Kazimoto."
4513 "Bila shaka ulikuwa umekwisha sikia mambo yaliyonipata."
4515 "Ndiyo, nilisikia bado nikiwa Dar es salaam. Kusema haki
4516 nimekuja leo kukupa pole kwa yote yaliyokupata. Nilifika
4517 Jumamosi; ingawa Rukia hana hali nzuri nimeona vizuri kuja
4520 "Nitakusimulia tukifika nyumbani," alisema.
4522 Tulipofika nyumbani, Matilda alituandalia chakula - ndizi
4523 mbichi ambazo zilikuwa zimepikwa vizuri sana, samaki
4524 wengi sana na viazi vichache. Matilda alikula peke yake
4525 jikoni pamoja na watoto. Baada ya kula Kamata alianza
4531 "Kazimoto, furahi kuniona sasa. Nilikuwa maiti, na
4532 ninafikiri kwamba sasa ungekuwa unalia karibu na kaburi
4533 langu. Nilikuwa mfu. Hadithi yenyewe ni hivi: Siku moja
4534 vijana wawili walinipitia hapa kwenda kunywa pombe. Vijana
4535 hao ni majirani. Tulipofika huko kwenye pombe tulikunywa
4536 sana. Kumbe wenzangu walikuwa na hila mbaya.
4537 Giza lilipoingia walianza kuwa wanajitilia pombe kidogo,
4538 mimi nikitiliwa pombe nyingi. Mwishowe nilijiona naanza
4539 kulewa. Niliwaomba ruhusa kuondoka, lakini wao walikataa.
4540 Waliahidi kunisindikiza mpaka nyumbani. Niliendelea
4541 kunywa. Karibu kama saa sita za usiku waliniambia kwamba
4542 walikuwa tayari kunisindikiza. Nilijaribu kusimama, nilijiona
4543 bado na nguvu za kuweza kutembea bila kushikiliwa.
4544 Tulipofika mbali kutoka mahali pa kunywea pombe, mmoja
4545 wao alisema: 'Kamata'."
4547 "Nilisimama. Mara niliona kila mmoja kati yao ameshika
4548 rungu. Hofu kubwa ilinishika na pombe yote iliruka. Niliona
4549 mwisho wa maisha yangu hapa duniani.
4551 "'Jamani! Kweli mniue! Mniue kabisa', nilijitetea."
4553 "'Ua kabla hajasema maneno mengi!' mmoja alisema.
4554 Hapo hapo nilipigwa rungu la mgongo. Nilianguka chini."
4556 "'Jamani kweli sasa mmeniua!'"
4558 "Mara moja nilisikia rungu linalia juu ya kichwa changu.
4559 Nilizimia. Kesho yake asubuhi nilipozindukana nilijiona
4560 nimelala ndani ya maji. Majani yalikuwa marefu hata sikuweza
4561 kuona mahali po pote. Akili ziliponirudia sawa sawa nilikaa
4562 kwa muda nikifikiri. Nilikumbuka hadithi kidogo. Niliona
4563 nguo zangu zimeenea damu. Nilipojishika kichwani nilishangaa
4564 kutupa vidole ndani ya shimo. Nilianza tena kuogopa.
4565 Nilijiona maiti tena. Nilijaribu kusimama. Maumivu yalikuwa
4566 mengi mno. Niliposimama niliona kwamba nilikuwa nimelala
4570 karibu na ziwa. Nilisikia sauti za watu. Nilijivuta pole pole.
4571 Wale watu waliponiona walistuka, kama kwamba waliona
4572 mzuka fulani. Ndio wale vijana ambao ulikuwa nao ziwani.
4573 Nilipowakaribia walinitambua: "'Kamata! Umekuwaje?'"
4576 "Nipelekeni nyumbani nikamwone mke wangu," niliwaambia.
4578 "'Waliponifikisha nyumbani, mke wangu alianza kulia
4579 badala ya kunitafutia maji na kunisafisha.' Wale vijana waliosha
4580 vidonda vyangu. Maumivu yalikuwa makali. Niliomba
4581 nipelekwe hospitali mara moja. Baada ya kuwaeleza kwa
4582 ufupi walinipeleka hospitali ya Bukonyo. Siku hiyo daktari
4583 alikuwa amelala. Nilishugulikiwa na mayaya. Baadaye
4584 tuliambiwa kwamba daktari alikuwa amelewa pombe ya
4585 moshi na alikuwa hawezi kuwaona wagonjwa. Kesho yake
4586 asubuhi daktari aliniona. Nilimweleza kisa chote. Polisi
4587 walipelekwa kuwashika wale vijana ili wawekwe rumande
4588 mpaka nitakapopona. Inasemekana kwamba mtu fulani
4589 aliwaona huko Uzinza Geita wakijiita majina mengine.
4590 Mimi nilikaa hospitali kwa muda wa mwezi mmoja. Tazama
4591 kichwa hiki!" Alinionyesha ngeo yake.
4593 "Kule mtoni ulifikaje?" nilimwuliza.
4595 "Mimi sikuwa na fahamu wakati huo. Lakini inaonekana
4596 kwamba waliponipiga sana na kudhani kwamba nimekufa
4597 waliniburura na kunitupa ziwani. Mungu bariki walinitupa maji
4598 mafu, na badala ya kuanguka kifudifudi nilianguka chali pua
4599 na mdomo juu ya maji. Umande wa usiku pamoja na maji
4600 chini ya mgongo yalinisaidia na kunifanya nizindukane asubuhi.
4602 "Unafahamu kwa nini walitaka kukuua?" nilimwuliza tena.
4603 Kamata alitazama upande wa jikoni. Matilda alikuwa naye
4606 "Sababu yenyewe mpaka leo hii sijapata kuielewa vizuri,"
4611 "Lakini mimi ninafahamu wazi kwamba sijawatendea jambo
4612 lo lote baya," alimaliza. Tulinyamaza kwa muda.
4614 "Kazimoto, utaweza kukaa hapa nasi majuma mangapi?"
4617 "Ikiwezekana nitarudi leo saa kumi; hiyo ndiyo saa
4618 niliyokuwa nimepanga."
4620 "Labda unataka kunichekesha. Huwezi kuja kuzungumza nasi
4621 kwa muda mfupi namna hii. Lala mpaka kesho. Huu ni
4622 mji wako, Kazimoto."
4624 "Ndiyo - lakini kama nilivyokwambia hapo awali nilimwa-
4625 cha Rukia mgonjwa sana."
4627 "Bado hajajifungua?" Matilda aliuliza kwa sauti.
4631 "Labda atazaa mapacha. Nilimwona majuma mawili
4632 yaliyopita. Tumbo lilikuwa kubwa."
4634 "Sijui wasichana wanafikiri nini,"Kamata alisema. "Ulikuwa
4635 umekazana kumsomesha lakini shukrani yake ni kutojiheshimu.
4636 Nafikiri amekusikitisha sana."
4640 Kamata alitazama jua. Aliinuka. Alijinyosha halafu alipiga -
4643 "Matilda sisi tunakwenda matembezi. Tutarudi usiku.
4644 Fahamu kwamba tuna mengi."
4646 "Kamata, huo ndio ubaya wako. Sasa unakwenda
4647 kumnywesha mgeni. Yeye atarudi amelewa wewe mzima.
4648 Usimpe mgeni mapombe mengi."
4650 "Kwani mimi nitakuwa namnywesha? Lete kibuyu.
4651 Nitakuletea hata wewe." Matilda alitafuta kibuyu upesi
4652 upesi. Alikileta baada ya kukiosha ndani.
4654 "Twende, Kazimoto." Tuliondoka. Tulipokuwa tumefika
4655 mbali na mji, Kamata aliniita, "Kazimoto."
4661 "Sikutaka kukueleza pale nyumbani kisa kilichofanya
4666 "Sababu yenyewe ni kwamba wale vijana walijaribu
4667 kumtongoza mke wangu. Alipowakataa waliona kwamba
4668 alikuwa akiwakataa kwa sababu mimi nilikuwa hai. Kwa
4669 hiyo walikata shauri kuniua. Lakini siku za mwanadamu
4670 kweli zimehesabika. Makumi yangu yaliyokuwa yamewekwa
4671 pembeni na Mungu kwa ajili yangu yalikuwa hayajatimia."
4673 Kamata aliponiambia hivyo niliamini, kwa sababu Matilda
4674 alikuwa mwanamke mzuri sana. Ingawa alikomea darasa la
4675 saba watu wengi wa maana - yaani wenye vyeo vya juu -
4676 walipeleka posa. Uzuri wake ulivuma Ukerewe nzima.
4677 Alipokata shauri kuolewa na Kamata kila mtu alishangaa.
4678 Wazazi wake walijaribu kupinga uchumba huu, lakini Matilda
4679 hakupenda kuolewa na mtu mwingine isipokuwa Kamata.
4680 Mwishowe wazazi wake walikubali, lakini moyoni kitu fulani
4681 kilikuwa bado kikiwachoma. Kwa kutaka kumkatisha tamaa
4682 Kamata walidai mahari makubwa sana. Kamata alikuwa
4683 tayari kulipa, kwani baba yake alipofariki alimwachia pesa
4684 nyingi kutokana na kazi ya uvuvi. Kamata alimwoa Matilda.
4685 Watu wengi walisema kwamba Matilda alivutwa na ule usafi
4686 wa Kamata. Kwa kuwa Kamata mwenyewe alipenda usafi
4687 alimtunza mkewe vizuri sana akawa anaonekana bado
4688 msichana hata baada ya kuzaa watoto wawili.
4690 "Hata mimi zamani nilikuwa na nia ya kuoa msichana
4691 mzuri sana, sasa ninaona kwamba ni hasara," nilisema.
4693 "Unasema uzuri wa sura?" aliniuliza.
4697 "Kwa nini usioe msichana mzuri?"
4699 "Wanaomtamani wanakuwa wengi mno. Kutoka maskini
4704 "Labda usemayo ni kweli, Kazimoto; mke wangu
4705 amekwisha nipoanza mara nyingi mno. Na mara hizo zote
4706 nikiponea chupu chupu. Utaoa lini?" aliniuliza.
4708 "Sijapata bado msichana anayenipenda. Ye yote
4709 nimwendeaye ananirusha. Mwishowe nimekata tamaa."
4711 "Usikate tamaa," aliniambia. "Katika kutafuta mchumba
4712 usiogope kushindana. Hata kama alikurusha usikate tamaa.
4713 Mimi mwenyewe wakati nikitafuta mwanamke wa kuoa
4714 nilirushwa mara nyingi sana. Mwishowe nilianza kufikiri
4715 kwamba labda duniani hapa nilikuwa wa mwisho katika
4716 ubaya. Lakini hiyo yote ilikuwa kumbe haraka ya bure.
4717 Wangu alikuwa bado hajaja. Kwa hiyo, Kazimoto, wako yupo
4718 atakuja. Lakini hawezi kujileta kama wewe hujaribu."
4720 "Lakini mimi ninataka kuoa mapema iwezekanavyo;
4721 mwaka kesho kama ikiwezekana."
4723 "Haraka ya nini? Kijana kama wewe na elimu yako hiyo
4724 wanawake utawaona wengi baada ya masomo. Kwa sasa wewe
4725 soma tu. Sisi wakulima na wavuvi tunaoa mapema kwa
4726 sababu ndilo jambo la maana tu tunalofahamu katika maisha
4727 yetu na watu wengine. Lakini wewe elimu bado iko mbele yako. "
4729 "Hakuna huku msichana ye yote asomaye?" niliuliza.
4731 "Huku wanaosoma ni wachache. Wengi wanakomea darasa
4732 la saba. Kama unataka hao ni wengi."
4734 "Nikioa msichana wa darasa la saba lazima awe mzuri
4739 "Bila shaka umekwisha sikia kichekesho cha mwanamke
4740 aliyekwenda kwao kwa sababu bwana'ke alisema 'some
4743 "Kazimoto, mke ni mke tu. Kwani wale waliosoma
4744 wameongeza nini katika hali yao ya uke? Utalipiga litalia
4750 "Ingawa litalia kama kibuyu, lakini linafikiri na ninaweza
4751 kujadili nalo mambo ya juu yaliyoandikwa na wataalamu."
4753 "Kazimoto, acha mchezo. Mambo ya maana ya kuzungu-
4754 mza na mke wako ni yale yahusuyo aila. Na hayo
4755 hayakuandikwa." Nilisikia mlio wa ngoma na kelele za watu.
4757 "Kuna harusi?" niliuliza.
4759 "Hapana. Hizo ni ngoma ziitwazo Mbugutu; zinachezwa
4760 kwenye pombe, hasa pombe ya ndizi."
4762 "Ndiko tunakokwenda?"
4767 Tulipofika wale wavuvi walikuwa wametungoja kwa hamu
4768 sana. Mara tu walipotuona walitukaribisha. Huo ndio
4769 ulikuwa mji wao. Ulikuwa mji mkubwa sana wenye nyumba
4770 kumi. Kama tukihesabu na majiko zilikuwa nyumba kumi na
4771 tano. Mji wote ulikuwa umezungukwa na shamba kubwa la
4772 migomba, na ulikuwa mji wenye mawe mengi katikati. Mawe
4773 haya ndiyo wanywaji walikuwa wamekalia. Wapiga ngoma
4774 walikuwa na mtungi wao mkubwa sana. Mimi na Kamata
4775 tulipelekwa katika kikundi cha wazee. Nafikiri kwamba
4776 hawa wazee walikuwa pia wamekaribishwa kama sisi. Kundi
4777 la vijana na wanunuzi lilikuwa mbali kidogo na wazee. Wengi
4778 kati ya vijana walikuwa wakicheza ngoma. Kulikuwa na
4779 vikundi vingine vidogo vidogo vimetapakaa huko na huko
4780 kati ya migomba. Wanawake fulani fulani walikuwa
4781 wamechanganyikana na wanaume. Wanawake watatu
4782 walikuwa wakicheza ngoma.
4784 Tulipokaa nilimwona yule kijana aliyekuwa akisimulia
4785 hadithi kule ziwani asubuhi, amebeba mtungi mkubwa kati
4786 ya mikono na miguu yake. Aliuweka katikati. Tulimshukuru.
4787 Baada ya kuuwekea mchanga pembeni ili usianguke aliuacha.
4791 "Wazee," alisema, "na mgeni wetu ambaye ametujia leo.
4792 Karibuni. Wakerewe walisema kwamba asiye na kiuno naye
4793 huvua. Hiki ndicho nilichoweza kupata."
4795 Wote tulishukuru pamoja. Tulianza kunywa tukifuata
4796 duara. Pombe ilikuwa nzuri, nami niliinywa kwa pupa.
4798 Mazungumzo ya wazee yalianza. Kila mtu alikuwa kimya
4799 na walikuwa wakizungumza mmoja mmoja. Walizungumza
4800 juu ya watemi wa zamani; mwanzo wa makabila na matawi
4801 mbali mbali ya watu wa Ukerewe. Walizungumza juu ya vita
4802 vya zamani; juu ya watu mashuhuri; watu ambao waliweza
4803 kupanda mti hali mkono mmoja wameshika fahali; watu
4804 ambao waliwanyoa wenzao kwa chupa watake wasitake.
4805 Walizungumza juu ya mwanamke aliyesemekana
4806 kaanguka kutoka mbinguni na mkia akazaa watoto na
4807 baadaye akatoweka. Walizungumza juu ya mashindano
4808 ya ngoma kati ya Wakerewe na Wasukuma. Kwa vyo vyote,
4809 mambo mengi yalikuwa mazuri kusikiliza lakini mimi
4810 nilijiona niko nje ya mazungumzo hayo. Niliwauliza
4811 maswali kadhaa, lakini hayakujibiwa vizuri. Baada ya kuchoka
4812 na hadithi zao walinielemea mimi. Walianza kuniuliza
4815 "Unasoma wapi?" mzee mmoja aliniuliza.
4819 "Rafiki yako alikuwa akisema unasoma Makerere."
4821 "Ndiyo," Kamata alidakia, "nilikuwa nikiwaeleza kwamba
4822 unasoma katika shule kama ile ya Makerere."
4824 "Kumbe wewe umesoma sana," yule mzee aliniambia.
4825 "Sijui kama utaweza kunieleza jambo hili: Uhuru tumekwisha
4826 upata. Zamani mkoloni alikuwa akitengeneza pesa kidogo
4827 kwa sababu alikuwa hataki tuendelee na alikuwa akituonea
4828 katika mambo mengi. Hii haikuwa nchi yao. Yote haya
4829 tumeambiwa na wanasiasa. Sasa uhuru tumepata. Kwa nini
4833 Serikali haiwezi kutengeneza pesa nyingi sana kila mtu awe
4836 Lilikuwa swali gumu la uchumi kueleza hasa kati ya wazee
4837 kama hawa. Uchumi nilikuwa sijui lakini ili kutunza heshima
4838 yangu ya elimu nilijitahidi kuwaeleza lakini hata hivyo
4839 walikuwa bado wakinitazama tu wakitegemea kuelezwa zaidi.
4840 Niliona kwamba walikuwa hawaelewi. Mzee yule aliendelea
4841 kuniuliza, "Lakini wewe huoni dhahiri kwamba wakuu wa
4842 Serikali ndio wanaozitengeneza. Wao wanazo sisi hatuna; na
4843 hawafanyi kazi kutuzidi."
4845 Nilijaribu kueleza. Hata hivyo hawakutosheka na jibu langu.
4847 Mzee mwingine aliuliza, "Swali la pesa tuliweke pembeni.
4848 Mimi nitafurahi sana kama utaweza kunieleza kwa nini
4849 mwezi unapoonekana ni mdogo na unapotua unakuwa
4850 mkubwa na mwekundu."
4852 Hapo nilipashwa kukiri kwamba nilikuwa sijui. Niliwaambia
4853 kwamba nilikuwa sijifunzi somo hilo na kwamba somo hilo
4854 liliitwa Jiografia. Niliposema hivyo tu wazee hawakuwa na
4855 shauku tena ya kuniuliza maswali. Hawakuona tofauti kubwa
4856 kati yangu na wao. Mambo yaliharibika nilipoanza kuwaambia
4857 kwamba huenda hakuna Mungu. Wazee wote walikataa kabisa.
4858 Mzee mmoja aliinuka kwenda nyumbani.
4860 "Mnazungumza na mwehu!" alisema kwa kelele. "A!
4861 Anasema kwamba hakuna Mungu! Yeye nani! Labda yeye
4862 ndiye anataka awe Mungu. Hakuna Mungu! Mtoto wa nani?
4863 Mababu na mababu wamekwenda; wamechukuliwa na nani?
4864 Nafikiri mnafunzwa kusoma kumbe mnafunzwa kuvuta
4865 bangi!" Alipomaliza kusema maneno haya alikwenda
4866 nyumbani akitupa mikono juu kwa kutokubaliana na usemi
4867 wangu: "Hakuna Mungu! Mwehu! Mwehu!"
4869 Nilisikia yule kijana aliyeleta pombe akimnong'oneza
4870 Kamata: "Mgeni wako ameanza kupatwa na pombe. Lakini
4874 mwambie azungumze juu ya mambo mengine au aache kabisa
4875 la sivyo ataharibu kikao."
4877 "Tunaweza kuhama," Kamata alimwambia.
4879 "Ndiyo. Mnaweza kwenda nyuma ya nyumba yangu.
4880 Nitawaletea pombe yenu huko."
4882 Kamata aliponiambia kuhama sikupinga, nilikuwa nimesikia
4883 maneno yote. Tulipofika nyuma ya nyumba hiyo, kijana
4884 alituletea mtungi mdogo wa pombe. Kamata alikaribisha
4885 vijana wawili zaidi waje wanywe pamoja nasi, lakini yule
4886 kijana alikataa na kuwafukuza.
4888 "Kama pombe ikiwashinda chimbeni shimo mumwage
4889 humo," alisema. Tulianza kunywa peke yetu. Kwa kuwa kila
4890 mmoja kati yetu aliogopa kulewa sana tulikunywa pole pole.
4892 "Unamwona yule mwanamke aliyevaa kitambaa kichwani,"
4893 Kamata aliniambia. Kabla sijajibu aliinuka na kwenda
4896 "Kila kitu tayari," Kamata alisema aliporudi, "isipokuwa
4897 angependa kuzungumza nawe kwa muda mfupi."
4899 "Yaani niende pale alipo kama wewe?"
4901 "Hapana atakuja hapa mwenyewe." Baada ya muda mfupi
4902 yule mwanamke kweli alikuja.
4904 "Kaka, habari?" alisema.
4906 "Nzuri," nilimjibu. "Unakaribishwa."
4910 "Kazimoto," Kamata alisema, "ninakwenda kucheza
4911 ngoma kidogo, nikute mambo yenu yamekwisha malizika."
4913 Aliondoka. Nilianza kufikiri namna ya kumwanza huyu
4914 mwanamke ambaye nilikuwa sijapata kukutana naye.
4920 Nilimtilia pombe nyingi. Alikunywa kidogo halafu
4921 akanirudishia. "Nafikiri rafiki yangu amekwisha kueleza kila
4925 kitu, sivyo?" Aliinamisha kichwa chini.
4929 "Unataka nirudie tena maneno yale yale."
4933 "Ninakuhitaji wewe."
4943 "Unanihitaji mimi vipi?" aliuliza.
4945 "Mwanamke anahitajika kwa kitu gani?"
4947 "Kwa ndoa; wengine kwa siku moja."
4949 "Tuseme kwa siku mbili."
4957 "Sasa tukatishe mambo. Leo usiku au vipi?" Alinyamaza
4958 kwa muda. Alinitazama.
4962 "Nitakwambia tukionana."
4964 "Unasoma au unafanya kazi?"
4968 "Kumbe mtoto mdogo. Unasoma wapi?"
4970 "Dar es salaam. Bado hujajibu swali langu."
4972 Aliinama. Halafu sauti ndogo ilitoka. "Haya."
4974 "Sikusikia," nilisema kwa sauti.
4976 "Haya," alirudia tena kwa sauti hali ameinama.
4978 "Kunywa pombe." Alikunywa kidogo. Halafu aliinuka
4983 "Ninakwenda kucheza. Nitamwambia Kamata zaidi."
4989 Nilimwona akizungumza na Kamata. Baada ya mazungumzo
4990 yao alikuja kunywa pombe. Yule mwanamke aliendelea
4991 kucheza. Tulikunywa mpaka tulipoona kwamba tulikuwa
4992 tumekwisha lewa. Kwa vyo vyote tulikuwa hatuwezi
4993 kuumaliza ule mtungi. Tuliwaita wale vijana waliotukaribisha.
4994 Tuliwashukuru na kuwaomba ruhusa ya kuondoka. Walitwa-
4995 mbia twende na pombe yetu. Pombe iliyotushinda tuliiweka
4996 ndani ya kibuyu. Wale vijana walitusindikiza kidogo halafu
4997 walirudi. Tulipokuwa njiani peke yetu Kamata aliniambia,
4998 "Yule mwanamke amesema atakuja nyumbani peke yake.
4999 Yeye akisema huwa hadanganyi. Huo ndio uzuri wake."
5001 "Labda wazazi wake wakali. "
5003 "Wapi! Ni wajinga. Binti yao huwa anawatukana
5008 "Kwa sababu yeye ndiye huwa anawalisha na kuwavika
5009 kwa pesa apatazo kutoka kwa mabwana mbali mbali."
5011 "Kwa nini hawawezi kumwoza?"
5013 "Hajapata wachumba. Nani ataoa makapi. Huyo sasa
5014 amekuwa mpira, wa kudunda na kuacha hapo, wengine pia
5017 Tulipofika nyumbani Matilda aliamka mara moja kuja
5018 kutupokea. Alituletea chakula. Ajabu kwangu ilikuwa kuona
5019 wingi wa samaki unapita ugali. Wakati wa kula, Kamata
5020 alinihimiza kumeza samaki tu niache kula ugali.
5022 Baada ya kula tulianza kunywa pamoja na Matilda. Pombe
5023 hiyo ndiyo ilinifanya nilewe kuzidi kiasi changu. Tulipokuwa
5024 tunakunywa tulisikia hodi mlangoni.
5026 "Karibu," Kamata alisema.
5028 Yule mwanamke aliingia. Alikuwa amevaa nguo zingine,
5029 na alikuwa akinukia marashi. Alikaa. Tulikunywa pamoja
5034 "Jina lako nani?" nilimwuliza.
5036 "Nyabuso," alijibu. "Na wewe jina lako nani?"
5038 "Mimi Kazimoto bin Machozi ya Simba." Alicheka kidogo.
5040 Tuliendelea kwa muda. Kamata alipotambua kwamba
5041 usingizi ulikuwa umenipata aliniomba nifuatane naye ili
5042 anionyeshe kitanda changu. Tulikwenda kulala.
5044 Kesho yake asubuhi Matilda ndiye aliyeniamsha.
5046 "Kazimoto, saa nne sasa, amka!"
5048 "Saa nne!" nilishangaa. Nilipotazama saa yangu niliona
5049 kwamba ilikuwa saa nne na nusu. Nilitafuta suruali yangu ili
5050 nivae, lakini sikuiona. "Suruali yangu niliacha wapi?"
5053 Nilipouliza hivyo tu Matilda alicheka sana. Nilimsikia
5054 Kamata pia akicheka. Nilihisi kwamba jambo la ajabu lazima
5055 liwe limetokea. Kama si la ajabu basi lilikuwa jambo la
5058 "Lakini suruali yangu niliacha wapi? Sidhani kwamba
5059 nililewa vile kwamba nilianza kutembea uchi!"
5061 "Kazimoto," Kamata alisema, "nitakueleza baadaye. Kwa
5062 sasa nitakuazima suruali yangu moja."
5064 "Maji ya kuoga nimekuwekea tayari uani," Matilda
5065 aliniambia. Nilikwenda kuoga. Baada ya kuoga nilijiona
5066 afadhali kidogo. Nilivaa suruali ya Kamata. Suruali ya
5067 mwingine ni ya mwingine. Niliona kwamba upepo ulikuwa
5068 ukiingia mwingi sana. Kamata alikuja chumbani kunieleza.
5070 "Kazimoto," alisema hali akicheka, "suruali yako
5071 imechukuliwa na Nyabuso."
5073 "Kwa nini?" niliuliza.
5075 "Anasema wewe si mwanamume."
5079 "Ndiyo, wewe. Hukuweza kufanya jambo lo lote."
5085 "Amechukua suruali yako kama adhabu."
5089 "Ndiyo. Ulimpotezea muda wake na ulimsumbua bure."
5093 "Ndiyo. Bila shaka unafahamu ninataka kusema nini."
5095 "Sasa nitafanya nini?"
5097 "Utafanya nini? Sahau tu suruali yako."
5099 "Suruali yangu ninaweza kuisahau. Lakini..."
5103 "Sifa yangu imeharibika. Yule mwanamke atatangaza."
5105 "Unataka kurudisha jina lako?"
5107 "Kama ikiwezekana." Aliinuka. Alinipiga begani.
5109 "Kazimoto, jina la bure lakini moto hauwaki. Nitamleta
5110 tena leo. Usiniaibishe tena."
5112 "Leo sitakunywa pombe. Unafahamu usiku nilipofika
5113 kitandani nilikufa."
5115 "Haya tutaona leo. Usife tena kwa usingizi."
5117 Baada ya chakula cha mchana Kamata aliondoka nyumbani.
5118 Aliniambia nimngoje nyumbani kwa muda mfupi."
5120 "Unakwenda wapi?" nilimwuliza.
5122 "Hapa karibu. Nitarudi sasa hivi."
5124 Alipoondoka nilikwenda kupiga usingizi kidogo. Kwa kuwa
5125 nilikuwa bado nimechoka usingizi ulinipata mara tu nilipoweka
5126 mbavu zangu juu ya godoro. Matilda aliniamsha saa kumi na
5127 moja. Aliniambia kwamba nilikuwa naitwa katika chumba
5128 cha maongezi. Niliinuka. Nilipofika chumba cha maongezi
5129 nilimwona Kamata na vijana wawili kati ya wale watano
5130 wamekaa kimya wakiningoja. Mtungi mkubwa wa pombe
5131 ulikuwa mbele yao. Nilikaa. Baada ya kusalimiana na wale
5132 vijana Kamata alisema, "Kazimoto, jana tulikuwa
5133 tumekaribishwa na hawa vijana. Mimi nilikuwa bado
5134 sijakufanyia jambo lo lote. Kwa hiyo leo nami nimejaribu
5138 kupata kitu kidogo kama hiki ambacho tutakifurahia pamoja
5141 Wote tulishukuru. Tulianza kunywa. Lakini mimi nilikuwa
5142 mjanja. Mara nyingi niliweka mdomo tu. Muda mrefu
5143 haukupita mara Kamata akatambua. Alinishurutisha kumaliza
5144 kiasi alichonitilia. Wakati huu mazungumzo kuhusu vijana wa
5145 siku hizi yalianzishwa na wale vijana. Mwanzoni mazungumzo
5146 yalikuwa kati yao wawili tu.
5148 "Nasikia binti Kasembe ana mimba ya miezi saba," mmoja
5151 "Mama yake anasema mitano."
5153 "Mimi nimesikia saba na ametiwa mimba hiyo na kijana
5154 fulani mchafu mchafu. Sijui wasichana hawana macho?"
5156 "Msichana alikuwa darasa la kumi na mbili na ametiwa
5157 mimba na kilevi kama sisi."
5159 "Wazazi wa msichana huyu wamekataa kumkubalia kijana
5160 huyo kumwoa binti yao."
5162 "Kwa nini?" niliwauliza.
5164 "Wanasema hastahili," mmoja kati yao alisema.
5166 "Mnafikiri nini kisa cha uovu huu wote?" niliwauliza.
5168 "Uovu gani?" Kamata aliniuliza.
5170 "Huu uovu wa watoto kuanza mchezo mbaya wangali
5173 "Kazimoto," Kamata alisema, "mimi nafikiri maovu haya
5174 yote yameletwa na watu wa nje. Kwanza Waarabu. Hao ndio
5175 wameharibu nchi za pwani. Halafu Wazungu hawa, Waingereza.
5176 Mjerumani nasikia hakukaa muda mrefu sana. Lakini
5177 Mwingereza ameleta sinema, magazeti na mambo mengine
5178 mengi ambayo hukimbiliwa na vijana wa siku hizi."
5180 "Hayo yote ni bure," kijana mmoja alisema, "sababu hasa
5181 ni kwamba ulimwengu umegeuka. Zamani mvulana alipata
5182 umri wa miaka kumi na tisa au ishirini kabla ya kujiona mtu
5186 mzima. Siku hizi mvulana mwenye umri wa miaka kumi na
5187 minne amekwisha anza kununua wembe dukani. Wasichana
5188 hao ndio wamezidi. Miaka kumi tu, utafikiri maziwa ya
5189 mwanamke mzima. Ulimwengu huu umegeuka."
5191 "Haya yote ni sawa," Matilda alisema, "lakini nionavyo
5192 mimi sababu yenyewe hasa ni kwamba malezi ya watoto
5193 siku hizi yamelegea sana. Wakati mimi nilipokuwa kama wao
5194 ilikuwa mwiko kukutwa na kaka nimesimama na mvulana ye
5195 yote; siku hizi kaka anaweza kumletea ndugu yake barua
5196 kutoka kwa mvulana mwenziwe. Maana yake nini? Wengine
5197 wanaweza kushikana viunoni dansini - kaka na dada!"
5199 Kijana mwingine alitoa wazo lake pia. Yeye alisema
5200 kwamba sababu kubwa ilikuwa kwamba vijana wa siku hizi
5201 wanadharau wazazi wao. Dharau hii imeletwa na elimu.
5202 Wanafikiri kwamba mawazo yote ya wazee ni ya kijadi.
5204 Mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu, kila mtu
5205 ameshikilia wazo lake. Mimi mwenyewe ingawa niliuliza
5206 swali hili, nilikuwa sijapata kulifikiria kwa makini. Nilikaa
5209 Tuliendelea kunywa mpaka saa mbili usiku Matilda
5210 alipoivisha chakula. Baada ya kula tuliuzunguka ule mtungi.
5211 Saa tatu Matilda alikwenda kulala. Alituacha sisi tunaendelea.
5212 Saa tatu na nusu Kamata alikwenda kufungua mlango wa
5213 nyuma. Alikawia sana kurudi. Tulifikiri kwamba alikuwa
5214 amekwenda kujisaidia. Aliporudi alininong'oneza sikioni:
5216 "Yumo tayari chumbani mwako."
5218 "Tunafahamu sana," kijana mmoja alisema.
5220 "Kwa nini msimwambie aje kunywa tu pombe pamoja
5221 nasi," kijana mwingine aliongezea.
5223 Sisi hatukutaka kusema zaidi juu ya jambo hilo. Kwa kuwa
5224 wote tulikuwa tumekwisha patwa na pombe tulianza kuimba.
5225 Kamata ndiye alianzisha:
5229 Kula tunakula lakini wafuasi wangu,
5230 Tunakwenda tunalia kama bibi arusi,
5231 Kule gizani kwenye mlango usiofunguka,
5232 Kwa yule amezaye bila kutafuna,
5233 Kuzimuni wote tutakwenda.
5235 Wote tuliitikia kwa kurudia maneno hayo hayo. Wimbo
5236 huu hata mimi niliufahamu kichwani kwa sababu ulikuwa
5237 wimbo wa mshairi mashuhuri kisiwani ambaye nyimbo zake
5238 zilikuwa zikiimbwa hata na watoto wadogo.
5240 Pombe ilikwisha saa tano usiku. Tulipeana kwa heri ya
5241 kuonana kesho yake asubuhi.
5243 "Wazee wetu walisema kwamba usiku wageni
5244 hawasindikizwi," Kamata aliwaambia wale vijana. Waliondoka
5245 kwenda kwao wakiyumbayumba.
5247 "Kila mtu amekwisha ingia ndani ya nyumba?" Kamata
5248 aliuliza baada ya muda mfupi
5252 Alifunga mlango wa nyumba. Nilipoingia chumbani mwangu
5253 taa ilikuwa bado ikiwaka. Yule mwanamke alikuwa amekwisha
5254 lala. Pembeni niliona suruali yangu imewekwa juu ya kiti
5255 kama kikombe cha mashindano. Ilikuwa imefuliwa na
5256 kunyooshwa vizuri sana. Nilikaa kitandani. Yule mwanamke
5257 aliamka. Aliponiona alipiga mwayo mrefu.
5259 "Usingizi ulikuwa umenipata," alisema.
5261 "Umechoka sana leo nini?" nilimwuliza.
5263 "Shauri ya pombe," alijibu. Alianza kunipapasa mgongoni.
5264 "Nilisikia watu wakiimba," alisema.
5268 "Nilikuwa nawasikia kwa mbali."
5270 "Kwa nini hukuja kunywa pombe?"
5272 "Sikutaka wale vijana wanione, ni waongo sana."
5278 "Basi kesho utasikia maneno. Leo pia umelewa sana?"
5281 "Leo ni mzima kabisa."
5283 "Jana ulifanya nini? Ulinisumbua bure. Sikuweza kupata
5286 "Utanisamehe. Tuone leo mambo yatakwendaje."
5288 Baada ya kuvua nguo zangu nilijitupa kitandani tukawa
5289 tunatazamana uso kwa uso. Tulicheka.
5291 "Wewe kijana mpole sana. Kijana mpole namna hii kwa
5292 nini hutafuti mwanamke mzuri ukaoa kuliko kusumbuka na
5293 mikweche kama sisi?"
5295 "Kwani wewe mkweche?" nilimwuliza.
5299 "Nakuona bado u msichana.
5301 "Nina watoto wanaolingana na wewe."
5303 "Ninafahamu kwamba una watoto wawili wadogo."
5305 "Kamata ndiye amekwambia?"
5307 "Watu wengine. Ninataka nami unizalie watoto wangu."
5311 "Wewe na mimi," nilisema. Tulitazamana machoni.
5312 Tulinyamaza na kuzima taa.
5314 Kesho yake asubuhi yule mwanamke aliniamsha saa kumi
5315 na moja. Tulizungumza kwa muda wa robo saa. Aliniomba
5316 anwani. Niliwasha taa na kumwandikia. Yeye pia alinipa
5317 yake. Saa kumi na moja na nusu aliniomba nimsindikize ili
5318 afike nyumbani kwao kabla ya wazazi wake kuamka. Tukiwa
5319 njiani kwenda kwao aliniomba nisimsahau kwa barua.
5320 Aliniomba nirudi tena kumtembelea Kamata kabla ya kwenda
5321 shule. Mimi nilimwahidi kwamba sitamsahau kamwe.
5322 Nilimwambia kwamba nikipata nafasi nitarudi tena. Nilimsindikiza
5326 mpaka nyumbani. Alipoingia ndani ya nyumba nilirudi
5327 peke yangu. Nilifika nyumbani kwa Kamata saa moja na nusu
5328 baada ya kutangatanga. Sababu yenyewe ilikuwa kwamba
5329 nilipotea njia. Nilipofika nyumbani nilikuta maji ya kuoga
5330 yenye moto tayari uani. Baada ya kuoga nilimwambia
5331 Kamata na Matilda kwamba nilitarajia kuondoka siku hiyo
5332 saa kumi. Wote walisikitika sana. Waliniomba nikae nao juma
5333 moja. Niliwaeleza hali ya nyumbani. Mwishowe waliniruhusu
5334 niondoke lakini kwa huzuni.
5336 Mazungumzo yetu siku hiyo yalikuwa juu ya yule
5337 mwanamke - Nyabuso. Waliniambia kwamba huyo Nyabuso
5338 aliweza kunifuata hata Dar es salaam kama akipata nauli.
5339 Walinieleza kwamba alikuwa mwanamke ambaye alikuwa
5340 akichukiwa sana na wanawake kijijini. Yeye aliweza kumfuata
5341 mume nyumbani na kumwita "bwana'ngu" mbele ya mke
5342 wake halali. Aliweza kumzomea mwanamke ye yote ambaye
5343 alikuwa akifahamiana na bwana'ke. Walinieleza kwamba
5344 walimu wa shule moja ya msingi ndio walikuwa mawindo
5345 yake. Walinieleza pia kwamba Mkuu wa Wilaya alikuwa naye
5346 amejijenga hapo. Mazungumzo yaliendelea mpaka saa sita.
5347 Ingawa yalikuwa mazuri, hayakuwa ya kusisimua sana.
5348 Kamata na Matilda walikuwa bado na huzuni kwa sababu ya
5349 kuondoka kwangu siku hiyo.
5351 Baada ya chakula cha mchana, Kamata alichukua mundu
5352 wake. Aliniomba nimngoje kwa muda mfupi. Aliingia ndani
5353 ya shamba lake la migomba. Baada ya muda mfupi alirudi
5354 na mikungu miwili ya ndizi. Alikwenda tena. Alirudi na
5355 mikungu mingine miwili. Saa zangu za kuondoka zilipokaribia
5356 alifunga mikungu hii juu ya baiskeli yangu. Aliifunga kwenye
5357 ncha za mti mikungu miwili upande mmoja, miwili upande
5358 mwingine. Saa kumi kamili niliondoka. Niliwaambia kwamba
5359 muda ulikuwa hauniruhusu kukaa zaidi. Niliwaambia wawape
5363 salamu zangu wale vijana na wawaambie kwamba sikuweza
5364 kufika kwao kuwaaga kwa sababu ya haraka. Kamata alifunga
5365 nyumba. Alichukua baiskeli yangu kunisindikiza. Mbwa wake
5366 alikuwa mbele kabisa akiongoza njia. Naye alikuwa akikojoa
5367 katika kila njia panda. Kamata na baiskeli alifuata. Mimi
5368 nilikuwa nyuma yake nikifuatwa nyuma na Matilda na
5369 watoto. Walinisindikiza mpaka barabarani, kilometa moja
5370 hivi kutoka nyumbani.
5372 "Nafikiri sasa utaweza kupanda mpaka nyumbani bila
5373 kushuka," Kamata alisema. "Hakuna mipando mingi.
5374 Tutakuacha ujiharakishe mwenyewe."
5376 "Asante kwa kunisindikiza," niliwambia.
5378 "Utarudi lini kututembelea?" Matilda alisema.
5380 "Sidhani kama nitapata nafasi tena. Nina kazi nyingi sana
5383 "Fika tena siku ingine," Matilda alisema kwa sauti yenye
5386 "Haya, nitajaribu, lakini siwezi kusema kwa uhakika."
5388 Kamata alinipa baiskeli yangu. Tuliagana tena. Nilipanda
5389 na kukanyaga baiskeli yangu. Niliondoka. Nilipotazama
5390 nyuma niliwaona bado wamesimama wakinitazama. Baadaye
5391 nilipotazama nyuma tena sikuweza kuwaona. Nilikuwa
5392 nimekwisha kata kona ya barabara. Mimi mwenyewe nilianza
5393 sasa kusikitika. Niliwakumbuka kina Kamata, Matilda, wale
5394 vijana na yule mwanamke. Nilijaribu kukumbuka jina lake.
5395 "Nyabuso," nilisema moyoni.
5398 Nikiwa juu ya baiskeli nilijiona katika hali ya upweke.
5399 Mawazo mengi yalinijia kichwani. Mara niliona baiskeli
5400 yangu inaongeza mwendo: nilikuwa nimefikia mteremko
5401 mkali. Nilijaribu kufunga breki baada ya kuona kundi la
5402 ng'ombe mbele yangu barabarani kabisa. Nilifunga breki
5406 kwa nguvu. Nilisikia kitu fulani kama mlio wa chuma.
5407 Badala ya kupunguza mwendo, baiskeli ilianza kwenda
5408 kasi sana. Nilitambua mara moja kwamba sikuwa tena
5409 na breki za nyuma. Niliogopa kutumia za mbele.
5410 Kutahamaki niliona ng'ombe mmoja hatua kumi hivi
5411 mbele yangu. Nilimgonga ubavuni. Nilisikia ng'ombe
5412 analia. Baiskeli ilianguka mbali na mimi nilipita juu ya
5413 mgongo wa ng'ombe na kuanguka upande mwingine.
5414 Kidogo ng'ombe yule anikanyage tumboni aliporuka
5415 kuwakimbilia wenzake. Nilisikia watoto waliokuwa
5416 wakichunga wale ng'ombe wakinicheka na kunizomea:
5418 "Hilo! Lina bahati! Kama lingeanguka juu ya pembe, leo
5419 lingeona cha mtema kuni!"
5421 "Tazama mandizi yake!" walisema.
5423 Niliinuka. Niliona damu kidogo juu ya goti. Nilipotembea
5424 sikusikia maumivu yo yote. Baiskeli yangu haikuharibika.
5425 Usukani tu ndio ulikuwa ukitazama pembeni. Niliunyosha
5426 tena. Ndizi zangu kweli ziliharibika sana, lakini kati yake
5427 mikungu miwili ilikuwa mizuri bado. Ile iliyoharibika
5428 niliifunga vizuri juu ya karia, miwili mingine niliiacha
5429 ikining'inia pembeni. Nilipotazama baiskeli vizuri niliona
5430 kwamba mnyororo ulikuwa umetoka. Niliuweka tena. Nilipanda.
5431 Niliona inakwenda sawasawa. Kwa kuwa haikuwa na breki
5432 nilishuka katika kila mteremko. Kwa sababu hii nilifika
5433 nyumbani usiku kabisa kila mtu amekwisha lala. Mbwa wa
5434 nyumbani kwetu waliponiona walibweka, lakini waliponita-
5435 mbua walikuja kunilaki na kupigapiga mikia yao juu ya miguu
5442 Ile mibweko ya mbwa mwanzoni ilimwamsha Mama.
5443 Nilipofika chumbani mwangu nilikaa kwanza kwa muda juu
5444 ya kitanda nikifikiria mambo niliyoyaona kwa siku mbili
5445 zilizopita. Lakini mara nilisikia mlango unagongwa.
5447 "Ingia!" nilisema kwa sauti. Mama aliingia mikono nyuma
5448 kama mtu aendaye kilioni.
5450 "Ulikuwa wapi?" aliuliza kwa upole.
5452 Mimi nilinyamaza kwa sababu mara nyingi nilikuwa
5453 nimemwambia asiniulize swali kama hilo.
5455 "Kazimoto, ulikuwa wapi kwa muda wa siku mbili
5456 zilizopita? Uliondoka bila kutuarifu na kurudi kwenyewe
5457 unarudi usiku wa manane. Umezaliwa, Kazimoto, na kuna
5460 "Unataka nini?" nilimwambia.
5462 "Kazimoto, fahamu kwamba mimi ninakupenda sana,
5466 huwezi kuondoka bila kunipasha habari. Ungeuawa je -
5469 "Mapenzi ya kitoto namna hiyo mimi siyapendi. Kila siku
5470 niondokapo nyumbani unaniuliza 'Unakwenda wapi?'. Mimi
5471 nimekwisha kuwa mtu mzima sasa, na sitaki wewe uwe
5472 unafahamu njia zangu zote. Hata kama nikiwa nakwenda kwa
5473 wanawake unataka nikueleze?"
5475 "Kazimoto, mtoto wangu, ulimwengu wa sasa hauna rafiki.
5476 Mambo yanayotokea hapa yaonyesha kwamba lazima
5477 ujiangalie. Jana usiku mambo haya yametokea tena. Kwa
5480 "Mimi siioni hatari yo yote."
5482 Alinitazama. Mara moja aliona vumbi kidogo juu ya nguo
5487 "Ndiyo, lakini sikuumia."
5489 "Huwezi kutambua sasa, maumivu utayasikia kesho.
5490 Lakini bila shaka umeumia. Nikuchemshie maji?"
5492 "Hapana, sikuumia. "
5494 Aliondoka. Nilifunga mlango. Mara baada ya muda mfupi
5495 mlango uligongwa tena. Nilifungua tena.
5497 "Kazimoto, usifunge mlango, ninakutayarishia chakula."
5499 "Usihangaike namna hiyo. Nitakula kesho."
5501 "Hapana, huwezi kulala na njaa."
5503 Alikwenda jikoni. Baada ya muda mfupi chakula kililetwa.
5504 Nilishangaa kumwona mama analia machozi. "Kazimoto,
5505 ninasikitika mboga haitoshi."
5507 "Inatosha sana," nilimwambia.
5509 Baada ya kuweka chakula mbele yangu, nilianza kula.
5510 Yeye alisimama pembeni kidogo. Aliponiona nakula
5513 "Utakapomaliza kula weka vitu pembeni. Nitavichukua
5517 kesho asubuhi." Alitoka nje. Ingawa alitoka amefurahi kidogo
5518 nilianza kumhurumia. Nilianza kujilaumu kwamba nilikuwa
5519 mkali kwake bila sababu. Lakini baadaye niliona kwamba
5520 nilifanya vizuri kumwambia, kwani nilikuwa sitaki mapenzi
5521 ya namna hiyo yaendelee.
5523 Kesho yake asubuhi, yaani Ijumaa, Mama ndiye alikuwa wa
5524 kwanza kuja chumbani mwangu kuchukua vyombo. Kwa
5525 kuwa sasa nilikuwa nasikia maumivu kwenye goti na bega
5526 nilimwambia Mama atafute njia ya kuweza kunikanda. Kwa
5527 haraka alitafuta yale majani yatumikayo katika kazi hii.
5528 Baada ya muda mfupi niliitwa jikoni. Majani yalikuwa
5529 yamelazwa juu ya makaa ya moto. Alianza kunikanda mguu,
5530 halafu bega. Wakati akinikanda nilimwuliza habari kuhusu
5531 Rukia. Aliniambia hali yake haikuwa mbaya sana. Alikuwa
5532 amekwisha anza kula kidogo.
5534 "Lakini kwa nini Rukia amesikitishwa sana na mimba?
5535 Wasichana wengine wanapata mimba, lakini wanacheka na
5536 kufurahi kama kawaida."
5538 "Aibu, Kazimoto, aibu ndiyo inamsumbua. Rukia ni
5539 msichana mwenye haya sana. Hataki kuonana na watu. Na
5540 anaona aibu hasa mbele yako."
5542 "Lakini kweli hakuna sababu ingine?"
5544 "Ninakumbuka siku moja nilipokuwa namtuliza
5545 aliniambia, 'Mama hufahamu masikitiko yangu. Nilitegemea
5546 sana kukusaidia lakini sasa siwezi: maisha yangu yameharibika.'"
5548 Baada ya kunikanda nilimwambia achukue zile ndizi
5549 chumbani mwangu, ili akampikie Rukia badala ya ugali.
5550 Mama alifurahi sana.
5552 Saa tatu, Baba na Kabenga waliingia chumbani mwangu.
5553 Hawakukaa. Baba alichungulia tu, aliponiona aliniambia
5554 niende nyumbani kwake. Nilipokwenda niliwakuta Kabenga
5555 na Baba wananingoja. Nilipokaa Baba alianza: "Kazimoto,
5559 tuna maneno machache ya kukwambia. Kabenga, ebu
5560 mweleze mtoto huyu."
5562 "Ndiyo, Kazimoto," Kabenga alianza, "unafahamu sasa
5563 umekuwa mtu mzima. Huwezi kurudi kutoka safari ukafika
5564 kukaa ndani ya nyumba yako kimya mpaka baba yako aje
5565 akuone. Mtu akitoka safari anasalimiana na watu wote wa
5566 nyumbani. Hata kama hukutoka safari ni kawaida kuamkia;
5567 lazima ufahamu uzima wa nyumba ingine ingawa mnaishi mji
5568 mmoja. Ukitembea huko nje watu watakuuliza 'nyumbani
5569 hawajambo?' Utajibuje kama hukuwasabahi asubuhi? Kuna
5570 hadithi ya kijana mmoja ambaye alikuwa hamjulii hali mama
5571 yake wakati wa asubuhi. Mama yake alikufa usiku. Yeye bila
5572 kujua alikwenda kilabuni kunywa pombe. Watu walikuja
5573 kumpasha habari huko huko kilabuni. Kazimoto, wewe ni
5576 "Jambo la pili," Baba alisema, "ni kwamba uliondoka hapa
5577 bila kutuarifu. Mama yako alikuwa halali. Siku moja alitembea
5578 kijiji kizima akiuliza kama maiti yako ilikuwa imeonekana
5579 mahali fulani. Mambo ya kina mama usiyachukulie kama ya
5580 kipuuzi. Ninasikia ulimjibu kwa ukali sana usiku. Ninataka
5581 kusikia ukinijibu hivyo hata mimi."
5583 Sikutaka ubishi nao. Kwa hiyo nilikiri makosa yangu.
5584 Baada ya kunipa maonyo zaidi walinipa ruhusa kuondoka.
5586 Kwa muda wa siku mbili kichwa changu kilikuwa
5587 kimepumzika huko nyumbani kwa Kamata. Sasa matata
5588 yalianza tena. Nami nilikuwa nimekuja nyumbani likizoni
5589 kupumzisha kichwa changu ambacho kilikuwa kimekwisha
5590 anza kuwanga kwa sababu ya kusoma.
5596 Ikiwa siku ya Jumapili, siku ambayo Vumilia alikuwa
5597 ameniambia niende kumchukua, na ndugu yangu akiwa
5598 amekwisha anza kula kidogo ingawa si sana, sikuona
5599 kipingamizi cho chote cha kuweza kunizuia kwenda
5600 matembezi usiku. Ni kweli kwamba Baba alikuwa amenionya,
5601 lakini sikuona kwa nini alipaswa kuhusika sana na mambo
5602 yangu. Kwa hiyo siku nzima nikawa namfikiria Vumilia,
5603 jinsi ya kumleta na kumrudisha bila mama yake kutambua.
5604 Katika kumfikiria, hadithi yake ilinijia tena kichwani.
5605 Vumilia alikuwa mmoja kati ya wale wasichana ambao
5606 hutunza ahadi. "Mungu mmoja, sikuongopei!" alizoea kusema
5607 wakati akitoa ahadi. Lakini Vumilia hakuonekana kuwa
5608 msichana mwenye furaha: alikuwa hajapata kumwona baba
5609 yake. Jambo hili lilimfanya apoteze wachumba kwani wengi
5610 walimwita mtoto wa vichakani.
5614 Hili halikuwa kosa lake. Lawama yote ilimwendea Tegemea
5615 - mama yake. Tegemea alipokuwa bado mwanamwari
5616 alifanya kazi ya umalaya. Alikuwa ametembelea miji mingi
5617 ya mwambao, Mombasa hadi Mtwara. Katika kurandaranda
5618 kwake alizaa watoto kadhaa, lakini wote hao walichukuliwa
5619 na baba zao. Tegemea alipoona kwamba vijana walikuwa
5620 hawamchukui, na kwamba kwa siku nzima alilala na shilingi
5621 tatu tu za mlevi fulani, alijiona siku zake zinakwisha, akakata
5622 shauri kuacha umalaya. Mimba aliyokuwa nayo aliitunza
5623 vizuri, akamzaa Vumilia, na mara moja akarudi kisiwani
5624 Ukerewe kabla ya yule bwana aliyehusika kuja kudai mtoto wake.
5626 Mahali alipokuja kuishi hapakuwa mbali sana na kwetu.
5627 Tegemea akajulikana sana kijijini kwa Kiswahili chake cha
5628 upesi na mawimbi; akaitwa Mswahili. Buibui alilokuja nalo
5629 kutoka pwani likawa kitisho kijijinii, akaacha kulivaa. Pole
5630 pole Uislamu akauvua, akaanza kula nyamafu na Ramadhani
5631 akawa anaisikia tu redioni. Mwishowe akaanza kuwa anapika
5632 pombe ya moshi. Pesa alizopata humo ndizo zilizomwezesha
5633 kuishi, kwani aliporudi kutoka pwani mikono yake, kama ya
5634 kiwete, ilikuwa haiwezi kushika jembe kutwa nzima.
5636 Maisha ya Tegemea mimi nilikuwa siyajali. Mimi nilimfa-
5637 hamu sasa Vumilia ambaye nilikuwa na uhusiano naye. Ya
5638 zamani hayanuki. Usiku ulipoingia, baada ya kula, tulikwenda
5639 kulala. Tulipoona kwamba wazee walikuwa wamekwisha
5640 lala, mimi na Kalia tulichukua fimbo zetu, tukashika njia
5641 kuelekea nyumbani kwao Vumilia. Kwa kuwa tulikuwa
5642 wawili na mwezi ulikuwa ukiwaka hatukuogopa cho chote.
5643 Nilishangaa nilipomwona Kalia aliyekuwa nyuma yangu,
5646 "Kuna nini?" nilimwuliza.
5652 Kutazama nyuma tuliona mbwa wa nyumbani kwetu.
5653 Tuliwarudisha kwa kuwatupia mawe. Tuliendelea. Yeye
5656 Mwishowe tuliukaribia mji wa Tegemea. Mji wenyewe
5657 ulikuwa na nyumba moja yenye vyumba vinne. Yeye alilala
5658 chumba chake, Vumilia chumba kingine karibu na mlango wa
5659 nyuma. Chumba kingine kilikuwa cha maongezi, na kilicho-
5660 baki kilikuwa kikitumika kama jiko. Tulipofika nyumbani
5661 kwa Tegemea tulianza kutembea pole pole kwa uangalifu,
5662 lakini hata hivyo, ng'ombe aliyekuwa amefungwa kwenye
5663 mti alitoa pumzi ndefu tulipopita karibu naye. Kalia sasa
5664 alirudi nyuma yangu, tukawa tunanyatia kuelekea upenuni.
5665 Ndani ya chumba cha Vumilia taa ilikuwa imekwisha zimwa.
5666 Chumba cha Tegemea kilikuwa bado na mwanga.
5668 "Tumewahi sana," Kalia alisema pole pole.
5670 "Nyamaza," nilimwambia.
5672 Tulikwenda kwa vidole mpaka mlango wa nyuma,
5673 tukajibanza ukutani.
5675 "Ha! ha! ha! ha!" tulisikia sauti ya jambazi fulani likicheka
5676 chumbani kwa Tegemea. "Kama ningeoa mwanamke kama
5677 wewe, nafikiri ningepata furaha hapa duniani. Mke wangu,
5678 ingawa nimezaa naye watoto wamekua, nilimwoa kwa
5679 kufanyaje tu. Leo nikitoka hapa nafikiri nitampa mgongo
5682 "Uwongo wako!" Tegemea alisema.
5684 "Babu atafufuka kama nikisema uwongo. Unafikiri nina
5687 "Uwongo wako! Mbona hata hujafikiria kunioa?"
5689 "Mimi ningeweza kukuoa isipokuwa jambo moja kuhusu
5690 wewe linanichukiza."
5694 "Usikasirike lakini."
5698 "Sema, ni jambo gani?"
5700 "Una tamaa sana ya pesa, yaani huwezi kumpenda mtu
5701 bila pesa. Huku shamba mwanamke hanunuliwi. Lakini mimi
5702 umenimalizia karibu pesa zote anazoniletea mtoto wangu.
5703 Hata hivyo bado hutosheki. Sasa unadai gauni. Unafikiri
5704 mimi pesa nitazitoa wapi?"
5706 "Kama jambo la gauni limekuudhi vaa suruali yako uende
5707 zako! Gauniii! Gauni! Gauni limekuwa gauni. Vaa suruali
5708 uende zako! Leo hufanyi jambo lo lote nami. Yaani
5709 unanifikiria mimi masikini omba-omba. Gauni! Mwenzio
5710 napoteza heshima yangu yote mbele ya binti yangu kwa ajili
5711 yako; unafikiri kuwa hatusikii! Mapenzi gani kuliko hayo?
5712 Gauni! Haya chukua suruali yako!"
5714 "Hasira yote hii ya nini?"
5716 "Nimesema v-a-a s-u-r-u-a-l-i u-ende zako!"
5718 "Unataka kunitoa nje kama kwamba sikuzaa! Haya
5721 "He! he! he! " Tegemea alicheka. "Sasa hizi pesa umezitoa
5722 wapi? Bwana'ngu kila siku matata. Ngoja kidogo niweke mto
5723 wa pili." Tulisikia mlango wa chumba unafunguliwa.
5724 "Ninakwenda kujisaidia, nitarudi sasa hivi. Nikute umelala."
5726 Tuliposikia hivyo tuliondoka karibu na ukuta. Tuliinama
5727 ndani ya majani yaliyokuwa karibu na nyumba. Tegemea
5728 alitoka nje na kanga moja, akakojoa karibu sana nasi.
5729 Hakukawia akarudi ndani.
5731 Tulirudi tena ukutani. Kalia alikuwa akicheka kwa ndani
5734 "Anayezungumza humo ndani umemtambua?" aliniuliza.
5736 "Nafikiri nimemtambua."
5740 "Kumbe mzee huyu hatari! Uhusiano ulianza lini?"
5742 "Tangu zamani," Kalia alisema, "isipokuwa mlikuwa bado
5746 hamjagongana kama leo. Nasikia uhusiano huu ndio umeleta
5747 ule mpango wa kumwoza Vumilia kwa Manase. Tuza anapinga
5748 sana uchumba huu, na Manase mwenyewe hapendi. Juzi juzi
5749 walimtuma Vumilia kwenda kuzungumza kidogo na Manase.
5750 Lakini nasikia Vumilia alimkuta Manase anaishi na kimada.
5751 "Gonga dirisha umechukue mke wako twende, naona baridi."
5753 Alipomaliza kusema hivi mlango wa nyuma ulifunguliwa
5756 "Mbona mnazungumza kwa sauti ya juu namna hii?"
5759 "Tayari twende?" nilimwuliza.
5761 "Ngoja nivae,"alijibu. Alirudi ndani. Hakukawia.
5762 "Twendeni; tangulieni mbele kidogo."
5764 Tulitangulia. Tulimwacha nyuma akifunga mlango.
5765 Baada ya muda alikuwa pamoja nasi.
5767 "Wanaume wawili bado mnatembea na fimbo; woga
5770 "Hatuogopi kitu cho chote," nilijibu.
5772 "Mtanirudisha saa ngapi?" aliuliza.
5774 "Saa kumi na mbili."
5776 "Saa kumi na mbili kutakuwa karibu mchana. Mimi nataka
5779 Wakati huu nilisimama kujisaidia. Kalia na Vumilia
5780 waliendelea mbele. Hawakufika mbali nao wakasimama
5781 kuningoja. Nilimwona Kalia anamshika Vumilia kiunoni.
5783 "Acha! Humwogopi kaka yako?" Vumilia alisema.
5785 "Wewe shemeji yangu, kwa hiyo usijali sana."
5787 Nilipowakaribia Kalia aliondoa mkono wake. Tuliendelea
5788 kimya mpaka nyumbani. Tulipofika nyumbani, tulipita
5789 mlango wa nyuma. Ndani ya nyumba Kalia alianza kutoa
5790 manung'uniko yake ambayo nilifikiria kuwa ya kitoto.
5793 miaka mia moja iliyopita, Afrika Mashariki
5794 imekumbwa na mabadiliko mengi ya kiuchumi na kisiasa.
5795 Mifumo ya jamii imebadilika. Katikati ya karne iliyopita
5796 baadhi ya jamii zetu zilikuwa katika hatua mbalimbali za
5797 mfumo wa ujima; baadhi zilikuwa katika hatua mbalimbali
5798 za mfumo wa ukabaila. Bali katika kipindi hiki dharuba ya
5799 ubeberu katika umbo la ukoloni na baadaye ukoloni mam-
5800 boleo imezisukumizia jamii zote hizi katika mfumo wa
5801 ubepari. Ukoloni umerutubisha mbegu za upinzani na utaifa,
5802 na umejikuta ukikabiliwa na madai ya wananchi ya uhuru na
5803 demokrasi na usawa wa kiuchumi. Baada ya uhuru madai
5804 haya yamepenya pia - na ilibidi yapenye - katika utamaduni,
5805 katika fasihi, na hasa katika ushairi. Mikatale ya kisiasa na
5806 kiuchumi ya ukabaila na ukoloni imekataliwa. Mikatale ya
5807 kisanaa (km. katika ushairi) vile vile imekataliwa. Mipaka ya
5808 kisanaa iliyowekwa na jamii hizo kwa matumizi na manufaa
5809 ya mabwana wa jamii hizo imekiukwa.
5811 Mgogoro huu wa ushairi ni sehemu na ni tokeo la
5812 mivutano hiyo ya kijamii. Mazingira mapya ya mwamko wa
5813 kitaifa baada ya uhuru, mwamko wa kujitafuta asili na
5814 kujitafutia mustakbala wenye matumaini mapya kwa umma
5815 umewachochea watu waanze kusaili mapokeo yote, mazuri na
5816 mabaya, na waanze kutafuta miundo mipya ya kijamii na
5817 miundo mipya ya kisanaa yenye kusadifu vizuri zaidi hali na
5818 migogoro ya leo. Bali miundo hii mipya ya kisanaa haitafutwi
5822 ile iwe badala ya ile ya zamani; inatafutwa ili iwe ni nyongeza
5823 kwa ile iliyopo, na iwe ni mchango wa kizazi hiki katika utajiri
5824 wa sanaa tulioachiwa na vizazi vilivyotangulia. Na si miundo
5825 yote ya sanaa inayopendekezwa kutumika sasa ni mipya;
5826 baadhi ni ya kale iliyokuwa imesahauliwa na ambayo sasa
5827 inafufuliwa kwa sababu inaweza kubeba maudhui ya leo.
5828 Baadhi ni miundo ya kawaida ya kifasihi simulizi ambayo
5829 inaingizwa katika fasihi andishi ya Kiswahili.
5831 Mgogoro huu, basi, ni wa kihistoria na umekusanya nguvu
5832 zake toka nyakati za nyuma. Tangu mwanzo wa ukoloni
5833 pamekuwa na ukinzano "usiotamkwa" baina ya wale
5834 waliotunga kwa kufuata kanuni za mapokeo na wale
5835 waliotunga mashairi guni. Mvutano huu uliendelea hadi
5836 ukafikia wakati ambapo ilibidi hata kina Amri Abedi
5837 waukubali ushairi huu ni mtindo katika ushairi wa Kiswahili,
5838 hasa baada ya tafsiri ya Shakespeare: Juliasi Kaisari,
5839 iliyofanywa na Rais J.K. Nyerere. Kadhalika mgogoro huu
5840 umekusanya nguvu kutoka katika uwili wa fasihi yetu: fasihi
5841 simulizi na fasihi andishi, na mwamko wa kifasihi wa
5842 kuiangalia fasihi simulizi kwa jicho jipya, kwa madhumuni ya
5843 kuitumia kuirutubisha fasihi andishi (katika ushairi wa fasihi
5844 simulizi ambayo haijaathiriwa hata kidogo na maandishi ni
5845 nadra sana kukuta vina na urari wa mizani). Kwa hiyo, basi,
5846 chimbuko la mgogoro huu limechangamana sana. Maelezo ya
5847 wanajadi hayatuambii lolote juu ya jambo hili.
5849 Licha ya mazingira ya kiuchumi na kisiasa, hata
5850 mazingira ya kiisimu ni mazuri, na yanaurutubisha mgogoro
5851 huu. Hivi leo Kiswahili si lugha ya Pwani tena kama
5852 ilivyokuwa karne mbili zilizopita, ila inazidi kuwa chombo cha
5853 utamaduni wa Afrika Mashariki nzima. Leo hii maana ya
5854 dhana "fasihi ya Kiswahili", "ushairi wa Kiswahili" si ushairi
5855 au fasihi ya watu wa Pwani, bali ni ushairi na fasihi ya watu
5856 wa Afrika Mashariki inayoeleza hali halisi ya hapa kwa lugha
5857 ya Kiswahili. Kwa ufupi, leo Kiswahili katika matumizi yake
5858 mbali mbali (ya kawaida, ya kifasihi, n.k. ) hakikubali
5859 ufafanuzi wowote uliojikita katika misingi finyu ambayo
5860 haizingatii hali mpya iliyopo.
5862 Maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa
5863 tuliyoeleza yamekuwa na tokeo moja kubwa na muhimu sana
5864 la kitamaduni: kukua na kupanuka kwa elimu. Baada ya
5865 Uhuru, elimu ya msingi, sekondari, vyuo na chuo kikuu
5869 imepanuliwa. Somo la Kiswahili (lugha na fasihi) limewekewa
5870 mkazo mkubwa katika mashule na vyuo. Wanafunzi na
5871 walimu wa Kiswahili wamepata nafasi ya kudadisi kitaaluma
5872 masuala mengi ya kifasihi, likiwemo suala la "ushairi ni nini".
5873 Wamepata pia nafasi ya kusoma fasihi za mataifa mengine, na
5874 hivyo kupanua mawazo yao kuhusu fasihi. Wameona namna
5875 watu wa mataifa mengine wanavyotunga au walivyokuwa
5876 wakitunga ushairi wao. Wameulinganisha ushairi huo na
5877 ushairi wa Kiswahili na wa makabila mbali mbali ya Afrika
5878 Mashariki na wamegundua kuwa, mbali na lugha, yapo
5879 mambo mengi yanayofanana baina ya ushairi wa mataifa
5880 mbali mbali - ule ulioandikwa na ule unaosimuliwa kwa
5881 mdomo tu. Imedhihirika pia kuwa msisitizo juu ya vina na
5882 mizani ulikuwa umeukwamisha ushairi wa Kiswahili katika
5883 umbo lisilobadilika. Hali hii ilipingana kimsingi na kanuni ya
5884 sanaa ya uumbaji. Washairi wengi wa Kiswahili wakawa
5885 hawaumbi; wakawa wanayapanga tu mawazo yao katika
5886 umbo la vina na mizani na mhariri wa Uhuru na Mzalendo
5889 Zaidi ya hayo, imedhihirika pia kuwa fikra kuwa vina na
5890 urari wa mizani ni "roho" na "uti wa mgongo" wa ushairi
5891 imepotoka kimsingi; ni nadharia ya ushairi ambayo haiwezi
5892 kuthibitika katika uchambuzi thabiti wa kitaaluma. Kwa hiyo,
5893 basi, upotofu wa fikira yenyewe ni kichocheo kingine cha
5896 Katika makala haya nia yetu ni kuyachunguza madai na
5897 hoja za wanajadi ambazo wamekwisha kuzitoa katika
5898 mjadala huu. Tutachunguza dai lao kuwa ushairi wa mtiririko
5899 ni wa kigeni (Kizungu); tutachunguza fikira zao kuhusu
5900 ushairi guni wa Kiswahili; tutachunguza fafanuzi zao juu ya
5901 hulka ya ushairi; tutayahakiki maelezo yao juu ya maana ya
5902 ushairi; na kisha tutatoa maelezo yetu kuhusu ushairi ni nini.
5903 Kwa hakika mawazo mengi ambayo tutayasema hapa tulik-
5904 wisha kuyasema katika makala ambazo tumeandika juu ya
5905 suala hili, katika makongamano, mihadhara, malumbano ya
5906 kishairi, n.k. Hata hivyo, kwa faida ya wale ambao
5907 hawajasoma makala zetu, na kwa manufaa ya wale wadhanio
5908 kuwa nia yetu ni kuua ushairi wa Kiswahili, na mwisho, kwa
5909 faida ya wale wadaio kwamba eti sisi tunadai kuwa "ushairi
5910 wa Kiswahili wenye kanuni za kawaida haufai tena",
5911 tunaziweka hoja na maelezo yetu hapa ili yaeleweke
5915 kinaganaga, kama watakuwa tayari kuyasoma kwa nia ya
5918 Upekee wa ushairi wa Kiswahili uko katika kanuni za
5919 vina na urari wa mizani?
5921 Vina na urari wa mizani ni mambo ambayo kwa karne
5922 nyingi yalifikiriwa kuwa muhimu sana katika ushairi wa Asia
5923 na Ulaya. Mpaka hii leo, ushairi wa Kiarabu, kama ushairi wa
5924 Kiswahili, bado unayasisitiza mapambo haya. Lyndon Harries
5927 Kwa mujibu wa arudhi ya Kiarabu, ilishikiliwa
5928 kuwa, bila ya kujali urefu wa shairi, vina vya
5929 mwisho katika kila ubeti lazima vipatane tangu
5930 mwanzo hadi mwisho wa shairi. Kwa hiyo hata
5931 katika tungo zenye vina vya kati, mtunzi akisha
5932 amua tu kutumia kina fulani katika kipande eha
5933 kwanza, ilibidi akitumie kina hicho hicho hadi
5934 mwisho. Watunzi wengi walipendelea zaidi kutunga
5935 mashairi ambayo vina vyake vya kati ni tofauti na
5936 vile vya mwisho... Utaratibu wa namna hii bado
5937 unafuatwa katika mashairi mengi ya Kiswahili.
5939 Maneno haya karibu yanakubaliana na maneno ya Mnyam-
5940 pala, ambaye amesema:
5942 Shairi liwe na vina vinavyopatana, hususa mwishoni
5943 mwa kila ubeti, kwa shairi lote zima, ingawa vina
5944 vya katikati vikosekane kwa utenzi wote.
5946 Kauli ya Amri Abedi pia inakubaliana na maneno hayo:
5947 Kwa desturi vina vya silabi ya 16 (vya mwisho) huwa
5948 vya namna moja katika beti zote za shairi zima.
5949 Sheikh Amri Abedi mwenyewe, kwa kusoma mashairi ya
5950 Kiingereza, Kihindi, na Kiarabu, alikiri kuwa ushairi wa
5951 Kiswahili hauna upekee wowote na wala siyo tofauti sana na
5952 ushairi wa mataifa hayo:
5954 Mpaka makamo haya nimesoma mashairi ya lugha
5955 ya Kiingereza, ya Kiurdu, ya Kiarabu, na kadhalika
5956 ya Kiajemi aliyonifundisha mmoja katika masheikh
5957 zangu, Maulana Jalal-ud-Din Qamar H.A. Kwa njia
5958 hii nimeweza kujua angalao chembe namna watu wa
5959 mataifa mengine wanavyokusanya fikira na
5960 Kuzipanga, namna ambayo si mbali na ile
5961 iliyotumiwa na watungaji mashuhuri wa Kiswahili
5967 Katika utangulizi wake kwa diwani ya Mnyampala, Waadhi
5968 wa Ushairi,Amri Abedi alitoa kauli ambayo inabidi ijadiliwe
5969 kwa kuwa imezua upotofu usio wa lazima. Alisema:
5970 Wasemao kuwa mashairi ya Kiswahili asili yake ni
5971 Kiarabu wanazua. Lau wangekuwa wanajua
5972 Kiarabu wasingesema hivyo. Taratibu za mashairi
5973 ya Kiarabu na ya Kiswahili ni tofauti kabisa. Ukweli
5974 ni kwamba Waislamu waliandika habari na
5975 masimulizi ya dini na nyimbo au ushairi wa Kiarabu
5976 kwa herufi za Kiarabu. Lakini kanuni za mashairi ya
5977 Kiarabu ni tofauti kabisa na za mashairi ya
5980 Kauli hii ya Sheikh Amri Abedi ni potofu kabisa. Ushairi wa
5981 Kiswahili na Ushairi wa Kiarabu si tofauti kabisa. Sheikh
5982 Saadani Kandoro, kwa kutaka kuonyesha ushairi wa
5983 Kiswahili ulivyo tofauti kabisa na ushairi wa Kiarabu,
5984 anaziorodhesha tofauti hizo:
5986 1. Ubeti wa shairi la Kiswahili huwa na mistari 3,
5987 4, 5, au zaidi. Na hivyo ndivyo yalivyo mashairi
5988 mengi ya Kiswahili katika vitabu na magazeti.
5989 Lakini ubeti wa shairi la Kiarabu huwa na
5992 2. Mstari huo wa shairi la Kiarabu hugawanyika
5993 sehemu mbili na kila sehemu inaitwa misraa.
5995 3. Mashairi ya Kiarabu hayana shuruti za vina.
5996 Shairi lenye kuendeleza vina vya kati mpaka vya
5997 mwisho huonekana si shairi la Kiarabu.
5999 4. Mashairi ya Kiswahili si lazima vina vya mwisho
6000 vifanane tangu mwanzo hadi mwisho, ingawa
6001 huwa vizuri zaidi hali hiyo ikiwepo katika shairi
6002 la Kiswahili. Kitu cha lazima ni kufanana kwa
6003 vina vya kila ubeti."
6004 Hebu tuzidadisi kauli hizi za Kandoro.
6006 Anasema ubeti wa shairi la Kiswahili huwa na mistari 3,
6007 4, 5 au zaidi. Kauli hii inabidi kurekebishwa na kuwa: ubeti
6008 wa shairi la Kiswahili huwa na mistari 2, 3, 4, 5 au zaidi.
6010 Anasema kuwa ubeti wa shairi la Kiarabau huwa na
6011 mstari mmoja tu. Jambo hili lazima litazamwe kwa uangalifu
6012 zaidi, na haifai kulipitia juu jau tu. "Ubeti" (wingi: beti) ni
6013 neno lenye asili ya Kiarabu. Kufuatana na utaratibu wa kijadi
6017 wa shairi (kasida) la Kiarabu, kila ubeti unazo misraa mbili.
6018 Lakini neno hili, katika ushairi wa Kiswahili, inavyoelekea
6019 limepanuka: shairi la Kiswahili siku hizi laweza kuwa na
6020 ubeti wenye vipande au "misraa" nyingi. Hili si jambo la
6021 kustaajabia. Isitoshe kabla ya kuingizwa kwa hati ya Kirumi,
6022 mashairi na tenzi nyingi za Kiswahili zilizoandikwa kwa hati
6023 ya Kiarabu zilikuwa na mstari mmoja tu kila ubeti. Mstari
6024 huo (au ubeti huo) ulitakiwa ujitosheleze kwa maana.
6026 Sifa hii ya kujitosheleza imo pia katika ushairi wa
6027 Kiswahili, ingawa Saadani Kandoro hakuitaja. Washairi wa
6028 Kiswahili wanakubaliana kuwa ubeti wa shairi la "jadi" ni
6029 lazima ujitosheleze kwa maana, yaani maana yake isiwe nusu
6030 nusu. Kadhalika, mstari wa shairi la Kiswahili unapaswa
6031 kujitosheleza, yaani utoe dhana kamili, usiwe nusu sentensi.
6032 Kanuni hii ya kujitosheleza imo pia katika ushairi wa Kiarabu.
6033 Mtaalamu mmoja wa ushairi wa Kiarabu, A. J. Arberry,
6034 anaeleza hivi "Katika ushairi wa Kiarabu, ilifikirika kuwa ni
6035 dosari kuruhusu muundo wa sentensi kuvuka ubeti (au
6036 mshororo mmoja wenye misraa mbili) na kuendelezwa katika
6037 mshororo unaofuata, kila mshororo ulifikiriwa kuwa ni kauli
6040 Anasema kuwa "shairi la Kiarabu halina shuruti za vina".
6041 Kauli hii lazima irekebishwe na kuwa: Shairi la Kiarabu
6042 halina shuruti za vina vya kati. Na kwa nini "shairi lenye
6043 kuendeleza vina vya kati mpaka vya mwisho" lionekane siyo
6044 la Kiarabu? Kwa kweli hata shairi la Kiswahili halina shuruti
6045 ya vina vya kati na yapo mashairi mengi ambayo hayana vina
6046 vya kati na bado yanakubalika kuwa ni ushairi wa Kiswahili.
6047 Utenzi wa Hamziya, mathalan, una kina cha bahari tu, hauna
6050 Mashairi mengi ya zamani (kabla ya mwaka 1700) hayana
6051 vina vya kati (vya misraa), yamezingatia kabisa kawaida za
6052 ushairi wa Kiarabu kama anavyozieleza Kandoro (ingawa
6053 anasahau au hajui kuwa baadhi ya mashairi ya Kiarabu yana
6054 vina vya kati). Aidha, kauli hii ya Kandoro haikubaliani sana
6055 na kauli ya Amri Abedi isemayo:
6057 Kwa desturi vina vya silabi ya 16 huwa vya namna
6058 moja katika beti zote za shairi zima, na vina vya
6059 silabi ya 8, kwa desturi inayotumika sana, huwa
6060 tofauti ubeti hata ubeti.
6062 Sheikh Amri Abedi alitaka kutueleza kuwa ushairi wa
6066 Kiswahili ni tofauti kabisa na wa Kiarabu, jambo ambalo
6067 hakuthibitisha. Kandoro alitaka kututhibitishia kuwa ushairi
6068 wa Kiarabu ni tofauti na wa Kiswahili. Je, ni kweli kuwa
6069 ushairi wa Kiswahili ni tofauti kabisa na ushairi wa Kiarabu?
6071 Kwa hakika ingewafalia sana wanajadi iwapo wangejion-
6072 doa katika "uzalendo" finyu, katika gamba la "Uswahili", na
6073 kuuona ukweli kuwa arudhi ya Kiswahili imeathiriwa sana na
6074 arudhi ya Kiarabu, ingawa ushairi wa Kiswahili asili yake siyo
6075 Uarabuni. Kanuni iliyotajwa hapo juu, ya "vina vya silabi ya
6076 mwisho kuwa vya namna moja katika beti zote za shairi zima,
6077 na vina vya kati kuwa tofauti tofauti" iko katika ushairi wa
6078 Kiarabu na wa Kiswahili. Vile vile urari wa mizani katika beti
6079 zote za shairi ni kanuni katika ushairi wa Kiarabu na wa
6080 Kiswahili. Mifano aliyoitoa Kandoro katika kitabu chake
6081 haitupatii picha sahihi ya muundo wa shairi la Kiarabu kwa
6082 kuwa amedondoa mshororo mmoja mmoja tu. Hebu tutoe
6083 mfano wa shairi zima hapa chini:
6084 (Katika hati ya Kiarabu)
6086 (Katika hati ya Kirumi)
6090 Hamil - ul - hawa ta'ibu yastakhifuhu - utarabu
6091 Inn baka'a yahikku lahu laysa maa bihi la'abu
6095 Kulama inaqadha sababu minki 'ada li sababu
6096 Tadhakina lahiyatan wal - muhibu yantahibu
6097 Ta'a jabiyna min sagamy sihaty hiya al - ajabu 14
6101 Mtu mwenyewe hawa yu mchovu, jaziba humpepesua.
6102 Akilia yuna haki, jukumule si mzaha.
6103 Sababu moja ya dhiki yangu ikiisha nyingine hurejea
6105 Wewe wacheka kwa furaha wakati muhibu wako aom-
6107 Waajabia dhiki yangu - kwamba ningali na siha ndiyo
6110 Hapa tunaona kuwa kina cha kati katika mstari wa kwanza
6111 kinapatana na kina cha mwisho, lakini vina vya mwisho ni
6112 vile vile toka mstari wa kwanza hadi wa mwisho. Na hii ndiyo
6113 desturi ambayo imekuwa ikifuatwa katika ushairi wa
6114 Kiarabu, na hata leo hii inafuatwa.
6116 Suala la athari za ushairi wa Kiarabu kwenye ushairi wa
6117 Kiswahili si jambo ambalo lahitaji mjadala mrefu kwa vile ni
6118 dhahiri sana. Waandishi wa kwanza wa mashairi ya Kiswahili
6119 wali kuwa masheikh na walimu wa dini, waliotaalamika
6120 katika lugha ya Kiarabu na Kurani (wengi wao wakiwa
6121 Waarabu au wale waliochanganya nasaba). Na kwa kuwa kila
6122 kitu eha asili ya Kiarabu kilikuwa ndicho kipimo eha
6123 ustaarabu, hata walipoanza kuandika mashairi au kutafsiri
6124 kasida au tenzi za Kiarabu kwa Kiswahili walilichukua kuwa
6125 ni jambo linalokubalika kuwa shairi lazima liwe na urari wa
6126 vina na mizani. Dhana nyingi za ushairi wa Kiarabu zikaanza
6127 kutumika katika ushairi - andishi wa Kiswahili. Msamiati
6128 wenyewe unaotumika, shairi, ubeti, mizani, hamziya, tasmit,
6129 takhimis, tathlitha, tarbia, n.k., ni wa Kiarabu. Ni kweli
6130 ingawa mitindo mingi ilianzishwa, lakini mitindo hiyo yote
6131 ilikuwa kwenye urari wa mizani na vina. Hali inayosemwa
6132 hapa inafanana na ile iliyousibu ushairi wa Ulaya baada ya
6133 enzi za ustawi wa himaya ya Wayunani, ambapo washairi
6134 wengi walifuata kanuni zilizokuwa na asili ya kanuni za
6135 ushairi wa Kiyunani.
6137 Kumbe utungaji wa mashairi katika vina na urari wa
6138 mizani si aambo liwezalo kuupambanua ushairi wa Kiswahili:
6142 kwa asili si jambo la Kiswahili, bali ni athari ya kigeni
6143 (Kiarabu). Kuyaita mambo haya "roho" ya ushairi wa
6144 Kiswahili ni sawa na kusema kuwa hapakuwa na ushairi wa
6145 Kiswahili kabla ya kufika kwa Waarabu. Maneno ya wanajadi
6146 yangeweza kusemwa pia na Mwarabu au Mwajemi kuhusu
6147 ushairi wa kwao. Kwa kweli yalikwisha kusemwa na
6148 mtaalamu mmoja wa ushairi wa Kiarabu, R.A. Nicholson, am-
6149 baye anatuambia hivi:
6151 Ushairi usio na vina ni jambo geni kwa Waarabu,
6152 ambao kwao vina si pambo la kuvutia au "kifungo
6153 chenye udhia", bali ndiyo roho ya ushairi.
6155 Kwa upande mwingine, ushairi wa asili wa Kiswahili (na wa
6156 Kibantu kwa jumla) hausisitizi vina wala urari wa mizani.
6157 Kwa hiyo basi malenga wa Kiswahili wanaotetea vina na
6158 mizani hawatetei mambo ya msingi katika ushairi wa
6159 Kiswahili, bali wanatetea athari za Kiarabu, ijapokuwa
6160 kinafsi sio kusudi lao. Kwa kweli wengi wanaamini kuwa
6161 wanachokitetea ndio "Uafrika". Vina na mizani haviupam-
6162 banui ushairi wa Kiswahili, bali vinaunasibisha na ushairi wa
6163 kigeni, hasa wa Kiarabu na Kiajemi.
6165 Lipo dai moja la kuchekesha kuwa ushairi wa mtiririko ni
6166 barua, insha au mkusanyo wa maneno tu bila utaratibu
6167 wowote. Dai hili ni la kuchekesha kwa sababu hakuna andiko
6168 lolote lenye mantiki na maana ambalo halina utaratibu
6169 wowote. Pili barua si lazima iwe nathari. Katika ushairi wa
6170 Kiswahili ipo desturi ya kuandikiana barua kishairi. Barua
6171 hizo huitwa risala, na kwa kawaida huanza kama hivi: "Risala
6172 ninakutuma..." au "Tumwa ukifika (mahala)..." n.k. Kwa hiyo
6173 inawezekana shairi fulani la mtiririko likawa ni barua na ni
6174 ushairi wakati huo huo.
6176 Kuhusu ushairi wa mtiririko kuwa "insha" jibu litatolewa
6177 baadaye tutakapojadili maana ya ushairi na mbinu za
6178 ushairi. Jambo la kudokeza hapa ni kwamba mashairi ya
6179 mtiririko si "huru" hata kidogo, yanazo mbinu, kunga na
6180 kanuni yake, na si rahisi kuyatunga. Ila katika kanuni zake
6181 hizo kuna uhuru mkubwa wa kubuni na kutunga. Kanuni
6182 yake kuu, ambayo kila mtungaji wa shairi yabidi aitimize,
6183 kanuni ambayo ndiyo roho ya mashairi haya, na roho ya fasihi
6184 kwa jumla, ni kwamba muundo wa shairi lazima uamuliwe na
6185 kufungamana na mawazo, mtiririko wa hisia, na makusudio ya
6186 mtunzi. Msimamo wetu hapa ni kwamba hakuna muundo au
6190 miundo maalum ambayo lazima ivaliwe na kila shairi, au
6191 sheria maalum zisizotanguka ambazo lazima zikaririwe na
6192 kila mshairi kama "sala ya bwana".
6194 Sasa na tuyapitie kwa ufupi madai mawili yanayotumiwa
6195 na wanajadi kuuhujumu ushairi wa mtiririko. Dai la "ugeni"
6198 "Ugeni" katika Ushairi wa Kiswahili
6200 Wanajadi kama vile hayati Chiraghdin, Mayoka, Kandoro,
6201 Al - Amin Mazrui na Ibrahim Sharif wanakubaliana kuwa
6202 vina na urari wa mizani ndivyo vitambulisho vya ushairi wa
6203 Kiswahili. Ndiyo maana wakauita ushairi wa mtiririko wa
6204 kina Kezilahabi, E. Hussein, Jared Angira, Crispin Hauli. F.
6205 Senkoro, na wengine kuwa ni mtindo wa Kizungu kwa lugha
6206 ya Kiswahili. Wanajadi wengine, kama Tigiti Sengo,
6207 wanaukubali kuwa ni ushairi, lakini si ushairi wa Kiswahili.
6208 Msimamo huu wa wanajadi unatokana na fikira potofu juu ya
6209 "ugeni", au "upya"; pili unatokana na kutoijua hulka na
6210 historia ya ushairi wa Kiswahili.
6212 Kwani ugeni wanaouhofu ni nini? Ugeni si jambo la ajabu
6213 sana. Ugeni wa kitu katika uwanja fulani wa maisha unaweza
6214 kujitokeza kwa namna tatu: ama kitu chenyewe ni kipya
6215 kabisa, na kimetoka nje; au kitu cha asili kilichokuwepo
6216 kimeathiriwa na kitu kigeni ama kitu hicho ni kipya na
6217 kimegunduliwa mahali hapo hapo. Ndipo watu baadaye
6218 huweza kusema kuwa "kitu hiki kina asili ya huko" au "kile
6219 kimeathiriwa na hicho", au "hiki kilibuniwa na fulani". Kwa
6220 mujibu wa maelezo haya, Uislamu una asili ya Kiarabu,
6221 Ukristu una asili ya Kiyahudi, mifumo ya elimu na serikali
6222 tuliyo nayo ina asili ya Kizungu, riwaya na tamthiliya ya
6223 Kiswahili vina asili ya Kizungu, taarabu ina asili ya Kiarabu,
6224 .nk. Sasa je, ushairi wa mtiririko una asili ya Kizungu?
6226 Kwa hakika, dai hili la wanajadi lingekuwa sahihi iwapo
6227 mtindo wa namna hii usingekuwapo katika fasihi simulizi ya
6228 Kibantu, ambayo ni pamoja na ile ya Kiswahili; na iwapo
6229 ingekuwa ni kanuni mojawapo ya sanaa ya ushairi kutovyaza
6230 mitindo mingine ghairi ya ile iliyopo. Mtindo usiofuata vina na
6231 urari wa mizani ni wa kijadi katika fasihi ya Kiswahili na
6232 Kibantu. Na ujadi wa mtindo huu ni ujadi wa utangu; mtindo
6233 wa vina na urari wa mizani umekuja baadaye kabisa.
6235 Kwa mtu yeyote ambaye amekwisha kushughulika na
6239 fasihi simulizi lau kidogo jambo hili si gumu kueleweka. Ipo
6240 mifano mingi ya ushairi wa namna hii. Hapa chini tutatoa
6241 mifano michache kwa manufaa ya wale ambao hawajui
6244 Mfano wetu wa kwanza ni wimbo (ushairi) wa kubem-
6250 makiwa ya baba na mama
6251 baba na mama watende
6254 kazi kumega matonge.
6256 Huu ni wimbo ambao umekuwa ukiimbwa na kina mama wa
6257 Kiswahili kubembelezea wana wao, ingawa unagusa pia hali
6258 halisi ya kukandamizwa kwa wanawake: kulazimishwa na
6259 wazazi kuolewa na mwanamume mzee. Athari ya mguso wa
6260 wimbo huu hasa unatokana na lugha ya mkato, na takriri,
6261 yaani marudiorudio ya maneno au silabi fulani fulani
6262 yanayovuta hisi za msikilizaji, mwimbaji, au msomaji (silie...
6263 silie... wani... wani... makiwa...makiwa... baba na mama... baba
6264 na mama... wa... wa... hali... hale... ). Katika wimbo huu
6265 tunaona kuwa kipande cha kwanza, cha pili, cha tatu, cha
6266 tano, cha sita, cha saba, cha nane vina urari wa mizani nane;
6267 kipande cha nne kina mizani tisa. Vina katika maana ya
6268 wanajadi havipo ila katika misitari minne ya mwisho tunaona
6269 utaratibu namna hii:
6271 baba na mama watende
6276 Katika mstari wa kwanza fungu-konsonanti -nd- linalingana
6277 na fungu-konsonanti la mwisho katika mstari wa tatu; na
6278 silabi ya mwisho mstari wa pili -ngwe- inatofautiana kidogo na
6279 -nge- ya mstari wa nne. Lakini, ukweli ni kuwa urari wa
6280 mizani unatokana na mahadhi ya wimbo huo, na haupo kwa
6281 sababu ni "roho" ya ushairi!
6283 Sasa tutazame mfano wa ushairi wa majigambo kutoka
6284 kwenye fasihi simulizi ya Kihaya. Jigambo hili ni la kiwindaji;
6285 mwindaji alilitamba mbele ya mtemi baada ya kutoka kwenye
6289 uwindaji wa mafanikio:
6291 Natonya nko'rulabyo, ninye Nilyegira eya Ngaiza
6293 Ruyango eya Karashani
6294 Karashani eya Keitirimbila
6295 Keitirimbila eya Kagomborora
6296 Kambaile ndy'omwange mpulila engoma zajuga zona
6297 Ngambila mukazi wange Kabigumila
6298 Nty'ompe eichumu Iyange Kanywa-bwamba
6299 amoi no omuhoro gwange. Rutema bitega
6301 Omukazi ai mushaija wange
6302 kankuchumbile akatoke
6303 Nti mukazi wange tokichumba
6304 byakuhya mara kandi tokokya
6305 byakujumbula, nti shana okwate
6306 akashweko kake ondabye omumaino
6309 Nilwo nayebembeize embwa yange
6311 Ekajumala kuluga Omwihangiro
6312 Lyamkumbya na Kairu, ekashoora
6313 Omurushanga Iwa Karebe
6314 nkahulila yambilikira, nti tora!
6315 Waitu elyo nachumisile nilyo
6316 Rugaba kandekelele ao,
6317 ebigambo bingi bikatanga enkoko
6319 Waitu batole ebikwato byange ebi.
6322 Naingia kama radi, ni mimi Niyegira mtoto wa
6324 Ngaiza mtoto wa Ruyango
6325 Ruyango mtoto wa Karashani
6326 Karashani wa Keitirimbila
6327 Keitirimbila wa Kagombolola
6328 Nilipokuwa kwangu nilisikia ngoma (za wito)
6333 Nikamwambia mke wangu Kabigumila
6334 Nipe mkuki wangu "Mnywa-Damu"
6335 pamoja na mundu wangu "Mkata-Miguu"
6336 nitoke kuitika wito.
6337 Mke wangu akanisihi:
6338 Mume wangu hebu nikupikie ndizi kwanza
6340 Mke wangu huwezi kupika zikaiva
6341 Wala huwezi kuchoma upesi upesi
6342 labda chukua jani la mgomba (lililotumika
6344 Unipitishie katika meno
6347 Ndipo nilipotangulia na mbwa wangu Usiyem-
6349 Aliteremka kutoka mbuga ya Lyamkumbya
6350 na Kairu hadi kwenye msitu wa Karebe
6351 Nikasikia ananiita (kwa kubweka )
6353 Mheshimiwa, mkuki mmoja niliotupa mnyama
6355 Ee, Mpaji (Rugaba) nikomee hapo
6356 Maneno mengi yalimzuia kuku kutawaza
6357 (baada ya kwenda haja)
6358 Mpaji, pokea mawindo haya.
6360 Hatuna haja ya kujadili mbinu zilizotumika katika kijigambo
6361 hiki. Jambo muhimu hapa ni kuona kuwa hakuna urari wa
6362 mizani na vina katika ushairi huu. Na ushairi wote katika
6363 fasihi simulizi za Kibantu uko hivi - labda tu uwe umeingiliwa
6364 na maandishi pamoja na kanuni za vina na urari wa mizani.
6366 Kwa nini jigambo hili tunaliita "ushairi"? Jibu la swali
6367 hili tutalipata hapo baadaye tutakapojadili maana na kunga
6368 za ushairi. Kutokana na mifano hii, tunaweza kuhitimisha
6369 kuwa dai la wanajadi kuwa ushairi wa mtiririko una asili ya
6370 Kizungu halina msingi wowote. Wahenga wetu wamekuwa
6371 wakiimba au kusema ushairi wa namna hii kwa miaka nenda
6372 miaka rudi. Hapa lazima tuongeze jambo moja: tusidhani
6373 kuwa ipo tofauti ya ajabu baina ya "free verse" ya Kiingereza
6374 na ushairi huu. Pengine tofauti kubwa tunayoweza kuitaja ni
6375 kuwa "free verse" ni ushairi wa vitabuni, na ushairi huu ni
6379 ushairi uishio pamoja na shughuli za kimaisha, kama kubem-
6380 beleza mtoto, kujigamba, n.k.
6382 Je, mtiririko ni mashairi gani?
6384 Suala la ushairi guni lilijitokeza katika mgogoro huu hasa
6385 kwa sababu ilitokea rai kuwa mashairi "mapya" ya mtiririko
6386 ni mashairi guni. Ushairi guni, Chiraghdin anasema, ni "tungo
6387 ambayo haikutosheleza sharuti za lugha, mizani, na vina".
6388 Kwa Sheikh Amri Abedi, ushairi guni ni ushairi "usio na
6389 vina". Kandoro na Mayoka wanakubaliana kuwa ushairi guni
6390 ni "ushairi wenye dosari". Kwa jumla, wanajadi
6391 wanakubaliana kuwa ushairi guni haufuati kanuni za vina au
6392 za urari wa mizani, au yote mawili. Kwa nini basi mashairi sa
6393 mtiririko yasiitwe mashairi guni, hasa kwa kuwa hayafuati
6396 Swali hili limepatiwa majibu tofauti toka kwa wataalamu
6397 na washairi mbalimbali. Farouk Topan anasema mashairi
6398 haya hayawezi kuitwa guni kwa kuwa "uguni" ni tokeo la
6399 kushindwa kufuata kanuni za vina, urari wa mizani na
6400 kutosheleza na watunzi wa mashairi haya hawajashindwa
6401 lolote. Chiraghdin naye, kwa kuwa anaamini kuwa mtindo
6402 huu ni wa Kizungu (blank verse au free verse), hawezi kuyaita
6403 mashairi guni. Hatuelezwi tofauti iliyopo baina ya mashairi
6404 guni na blank verse au free verse, bali tunaelezwa tu kuwa
6405 "tungo hizi zikikubaliwa .. basi ushairi wa Kiswahili utakuwa
6406 umeanguka kitakotako" (Iwapo ushairi guni umekuwepo
6407 tangu zamani na haujauangusha ushairi wa Kiswahili, kuna
6408 haki gani ya kudai kuwa ushauri wa mtiririko utauangusha
6409 ushairi wa Kiswahili?) Hata hivyo, msimamo wa Chiraghdin
6410 unaelekea kuwa na mkinzano ndani yake. Katika utangulizi
6411 wake kwa Malenga wa Mrima, anasema: "Shairi la Kiswahili
6412 hukosa umbo lake likikosa vina na mizani; na hapo huwa
6413 haliitwi tena shairi." Kisha anaongeza: "Umbo lake likilemaa
6414 huwa bado ni shairi, lakini huwa ni guni." Iwapo umbo la
6415 shairi ni vina na mizani, tungo itaendeleaje kuitwa shairi
6416 Iwapo haina vina na mizani? Upotofu wake unazidi
6417 anaposema kuwa umbo la ushairi la vina na mizani limekuwepo
6418 tangu ukale wa ushairi, na kwamba kilichobadilika ni kuv-
6419 yazwa kwa bahari mbalimbali za ushairi: "Kumetokea na
6420 kukua kwa bahari mbalimbali za ushairi katika hilo umbo
6421 lake." Tumeshaonyesha kuwa vina na urari wa mizani ni
6425 athari za kigeni; hatuna haja ya kujirudia hapa.
6427 Mayoka na Kandoro wanakubali kuwa shairi guni ni
6428 shairi lenye dosari, lakini wanakanusha kuwepo kwa ushairi
6429 huu katika ushairi wa Kiswahili. Mayoka anasema: "Kwa
6430 kweli ushairi guni hauko katika ushairi wa Kiswahili." Kan-
6431 doro naye anasema: "Kwa ufupi wa maneno, hakuna aina ya
6432 shairi 'guni'. Mtunzi mwenye kujua hawezi kujigamba kwa
6433 kutunga tungo zenye kasoro na kuziita mashairi. Hathubutu
6434 hata kidogo kwani jambo hilo litamvunjia hishima yake."
6435 Ama kweli hii ni "ufupi wa maneno.. kwani "urefu" wake
6436 unaonyesha kuwa ushairi guni upo, hata kama wautungao
6437 hujivunjia "hishima".
6439 Kitu ambacho Amri Abedi mwenyewe (ambaye wanadhani
6440 wanatetea sheria alizoandika) alikikiri na kukiheshimu,
6441 Mayoka na Kandoro wanakikanusha. Yaelekea walifanya
6442 hivyo kwa kudhani kuwa wakikubali kuwepo ushairi guni
6443 katika ushairi wa Kiswahili basi tungedakia na kuuita
6444 mtiririko ushairi guni.
6446 Kwa kuwa yaelekea wapo watu wengine wenye fikira
6447 kama za kina Mayoka, basi inafaa tuchunguze, lau kidogo,
6448 iwapo kweli guni ni umbo mojawapo katika ushairi wa
6451 Historia ya ushairi-andishi wa Kiswahili inatuonyesha
6452 kuwa ushairi guni umekuwepo tangu zamani. Pili, historia hii
6453 inatuonyesha kuwa kwa kadiri ushairi guni ulivyozidi kuishi
6454 pamoja na ushairi uliofuata kikamilifu kanuni za vina na
6455 urari wa mizani, ndivyo ulivyozidi kukubalika kuwa ni fani
6456 mojawapo ya ushairi wa Kiswahili, hasa baada ya malenga
6457 mashuhuri kuukubali, na hata baadhi yao kuutunga.
6459 Tuchunguzapo kurasa za matoleo mbalimbali ya gazeti la
6460 Mamboleo tunakuta mashairi ambayo hayakufuata kanuni
6461 hizo. Katika toleo la 10, Oktoba 1923, tunakuta shairi
6462 "Shangilieni Mgeni Mambo Leo Kaingia", lililotungwa na
6463 Said Bin Kikulacho, ambalo, kwa kadiri ya kanuni za
6464 wanajadi lina dosari. Hapa tunadondoa beti chache:
6466 Mamboleo ana sifa zilizotupendeza
6467 Na mtakapo sifa zake kidogo nitawaambia
6468 Habari nyingi za pwani na bara hutuambia
6469 Shangilieni mgeni Mamboleo kaingia...
6473 Na zikiwa habari ambazo hazipendezi
6474 Wenyi kuleta habari za fitina na kutukanana
6475 Fahamu atakujibu pasipo jina kutaja
6476 Shangilieni mgeni Mamboleo kaingia...
6478 Atupa habari za wezi waliopo tuwajue
6479 Twajua kuvunja nyamba kuna na wa Relwe
6480 Kuna Kampuni Sinzia mikononi hukuibia
6481 Shangilieni mgeni Mamboleo kaingia..."
6483 Kwa kweli, baadhi wa washairi wa siku hizo walikuwa
6484 hawajali vina vya kati kamwe (k.m. Mdanzi Hanassa), na
6485 wengine hawakujali sana urari wa mizani (Limo, Mdanzi)
6486 Lakini shairi ambalo halikutumia vina kabisa ni lile lililotoka
6487 kwenye Mambo Leo ya Desemba 1928, juu ya mnazi,
6488 lililotungwa na A. Pacha. Kwa vile sanaa ya shairi hili ni ya
6489 hali ya juu inafaa tulidondoe lote.
6491 Mnazi (Jibu la Shairi la Mti Gani wa Faida Ushindao Miti
6495 1. Hili ni jawabu, la maswali yako
6496 Nililojaribu: na kwa Mamboleo
6497 Nasihi niseme: uniwie radhi,
6498 Ewe! Bwana Khamis: idadi ya miti
6499 Uliyohasibu: imepungukiwa
6500 Kwani mimi MNAZI umenirukia.
6502 2. Sitafidhulika: wala kudharau,
6503 Utani wa miti: iliyo wenzangu,
6504 Kila mmojawapo humfaa bin Adam,
6505 Kwa leo, kwa kesho: humleta usalam.
6506 Hapana kibovu: kwa mwenyi busara,
6507 Na Mwenyezi Mungu yote amelinga.
6509 3. Niruhusu bwana: nitoe sauti,
6510 Nionye mafaa: yashindayo miti,
6511 Hapa Tanganyika: Unguja na Pemba.
6512 Ni tangu asili: watu hunipenda.
6513 Linafahamisha: MNAZI jina langu
6514 Upunga, kitale, kidaka na dafu.
6518 4. Koroma na nazi: mbata na majoya
6519 Ni majina nane: tunda langu moja:
6520 Kila mtu huchuma: kwa maonji yake.
6521 Chakula, cha kunywa: apendavyo yeye.
6522 Faida ingine: sijasema bado,
6523 Nisaburi tena usivunje moyo.
6525 5. Ijapo kungine: naliwa na mwezi
6526 Pia kwa nasibu, kuwa zimwi nazi,
6527 Makumbi usumba: hufaa kwa mengi;
6528 Hata na kifuu: cha kuteka maji
6529 Kizio cha nazi: kombe la kunywea.
6530 Sisangae, Bwana, bado sijakoma.
6532 6. Na tui la nazi, bin Adam hufyonza
6533 Akiisha kunguta: huweka machicha
6534 Kisha pata mbata: huwapa vinyama
6535 Vifae kunona: huleta faida.
6536 Uwongo sisemi, sicheki dhihaka
6537 Sifa yangu mnazi nani atasema?
6539 7. Na matawi yangu, hutumiwa pia.
6540 Bora fuadi uwe, ujue kusuka
6541 Ukuti ununu: na kifumuwale,
6542 Kuti la ukumba: kuti la upande,
6543 Kuti la kiungo: toka upongoo,
6544 Ufikiri sasa ukaone mambo.
6546 8. Shambani tembea, kaone majengo
6547 Yao walimaji, vinyumba vidogo,
6548 Pasi mti na nyasi: mimi peke MNAZI,
6549 Nakifu kukinga: mvua jua kali,
6550 Sokoni enenda: pakacha taona,
6551 Ni chombo kizuri pakia matunda.
6553 9. Hayo ni mafaa: na wangu uzuri,
6554 Ukiri, naomba: tazama matawi,
6555 Kwa pepo mwanana: vizuri hunepa
6556 Kama binti Fundi: mikono hupunga.
6557 Shingo langu refu: mikono ya mbinu,
6558 Umbo langu lote mapambo matupu.
6562 10. Hilo ni jawabu: la maswali yako
6563 Nililojaribu: na kwa Mambo Leo
6564 Nasihi niseme: uniwie radhi.
6565 Ewe! Bwana Khamisi: idadi ya miti
6566 Uliyohasibu: imepungukiwa
6567 Mimi peke Mnazi naweza kushinda.
6569 Shairi hili (isipokuwa kwa mistari 6 hivi yenye mizani 13)
6570 linao urari wa mizani 12, iliyogawanyika nusu kwa nusu,
6571 mizani 6 kila kipande. Ingawa tunakuta hapa na pale upo
6572 upatanifu wa vina vya mwisho katika mistari miwili, lakini
6573 upatanifu huo umetokea kwa nasibu tu. Katika shairi hili
6574 mtunzi, badala ya kuongea yeye mwenyewe na Bwana
6575 Khamisi, ameupa mnazi nafsi ya utu; na mnazi umeongea ana
6576 kwa ana na Bwana Khamisi kueleza sifa zake. Mbinu hii
6577 imelifanya jibu la mtunzi liwe na mvuto wa pekee - mvuto am-
6578 bao pengine usingepatikana iwapo Bwana Pacha engeongea
6579 ana kwa ana na Bwana Khamis juu ya sifa za mnazi.
6581 Bwana Pacha si mtunzi pekee wa kiwango cha juu aliyediriki
6582 kutunga ushairi guni. Shaaban Robert, yule "Simba wa
6583 Uswahilini, alitunga ushairi huu pia. Ubeti wa kwanza wa
6584 shairi lake "Muombwa" umekaa hivi
6586 Muombwa ni wewe Mungu
6589 Na heri katika nchi,
6593 Na katika shairi lake "Nimeambiwa" ubeti wa kwanza una
6596 Habari nimeambiwa Tanganyika yastawi,
6597 Habari hii ni njema nikikumbuka matendo,
6598 Na kazi walizofanya watu wenu wa zamani,
6599 Kwa bidii kubwa sana mpaka hili likawa.
6600 Matendo ya watu wetu, wanawake na waume,
6601 Katika kila taifa yanawanyanyua watu,
6602 Na nchi ikawa nzuri au kuwatupa chini.
6606 Mfano mwingine wa shairi guni lililotungwa na Shaaban
6607 Robert ni "Mtu Mwema", na ubeti wake wa kwanza uko hivi:
6609 Mtu ambaye ni mwema japokuwa hana dini,
6610 Awe kafiri mkubwa wa sala na wa ibada,
6611 Lakini huonekana hadhuru mtu mwingine,
6612 Na mwanawe hamdhuru au mwana wa mwenziwe,
6613 Mwana ambaye si wake kinuni hatamponda,
6614 Kisha akaoe mke kusudi azae mwana!
6615 Wema ni kama johari tena ni nuru ya mtu.
6617 Katika mifano hii ya beti za mashairi ya Shaaban Robert,
6618 tunaona kuwa ijapo yanafuata urari wa mizani lakini
6619 hayakufuata utaratibu wa vina. Na mifano hii inaelekea
6620 kutangua, au kurekebisha, ufafanuzi wa Shaaban Robert juu
6621 ya ushairi. Katika hotuba yake ya mwaka 1958, anasema:
6623 Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama
6624 nyimbo, mashairi, na tenzi... Kina ni mlingano wa
6627 Mifano hiyo hapo juu inatuonyesha kuwa mashairi haya si
6628 sanaa ya vina hata kidogo. Tukifuata ufafanuzi wa Amri Abedi,
6629 ni mashairi guni. Tukifuata ufafanuzi wa Kandoro, labda si
6630 guni kwa sababu watunzi wameyatunga hivyo kwa
6631 kukusudia, si kwa kushindwa.
6633 Amri Abedi, alipokuwa akiandika kitabu chake Sheria za
6634 Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri, alitambua kuwa mashairi
6635 guni yapo ila hakuyashughulikia kwa kuwa "hayatiliwi nguvu
6636 na sio maarufu". Ndiyo maana Juliasi Kaizari kilipochapishwa
6637 na Lyndon Harries akarukia na kusema kuwa mtindo wa taf-
6638 siri umefuata ushairi guniwa Kizungu, Amri Abedi
6639 alikanusha dai hilo kwa kusema:
6641 Ajabu ni kwamba hivi karibuni tu Rev. Lyndon
6642 Harries alitamani sana ionekane kuwa baadhi ya
6643 mashairi ya Kiswahili yana asili ya mashairi ya
6644 Kiingereza. Mheshimiwa Baba wa Taifa alipotoa
6645 tafsiri ya Julius Caesar kwa ushairi wa guni au usio
6646 na vina Lyndon Harries alirukia kusema kuwa
6647 washairi wa Kiswahili hawana desturi ya kuandika
6651 mashairi yasiyo na vina, na kwa kuwa Waingereza
6652 ndiyo wenye desturi hiyo basi kazi ya Baba wa Taifa
6653 asili yake ni ya Kiingereza! Ilimradi hawaoni raha
6654 kuona cho chote kina asili ya Kiafrika! Kikifanana
6655 na Kiarabu basi Kiarabu ndiyo asili, kikifanana na
6656 Kiingereza basi Kiingereza ndiyo asili! Je, Kiswahili
6657 chenyewe hakiwezi kuwa na fani ambazo asili yao ni
6660 Kweli, bila kusahau kuwa tamthiliya inayozungumziwa ina
6661 asili ya Kiingereza, Kiswahili kinazo fani ambazo asili yake ni
6662 Kiswahili chenyewe, na miongoni mwa hizo ni ushairi guni na
6663 ushairi wa mtiririko. Maneno hayo ya Sheikh yangefaa kuam-
6664 biwa wanajadi wanaoshikilia kuwa mtindo huu ni wa
6667 Kutokana na hayo tuliyokwisha sema, tunaona kuwa
6668 ushairi guni ni mtindo katika ushairi-andishi wa Kiswahili
6669 ambao umekwisha kukubalika. Ingawa mwanzoni ulihusishwa
6670 na 'dosari', lakini katika miaka ya 1960 ulikuwa unatam-
6671 buliwa kuwa ni mtindo wenye hadhi kamili katika ushairi wa
6672 Kiswahili. Ndiyo maana Shaaban Robert hakuhofu "kujivun-
6673 jia hishima" kwa kuandika ushairi guni, kama ambavyo
6674 Bwana Pacha, katika mwaka 1928, hakuingiwa hata na fikira
6675 ya kujivunjia hishima" mbele ya malenga wenzake. Sasa basi
6676 ushairi huu "mpya" tunaweza kuuita "ushairi guni"?
6678 Jibu la swali hili litategemea mtazamo wa mtu kuhusu
6679 ushairi guni. Iwapo tutashikilia rai ya Farouk Topan, kwamba
6680 "uguni" ni tokeo la kushindwa kufuata kanuni za vina na
6681 urari wa mizani, tutasema kuwa mtindo huu siyo guni. Iwapo
6682 tutashikilia dhana ya Amri Abedi kuwa mashairi guni ni yale
6683 yasiyo na vina tu, bali yana mizani (kama mifano ya shairi la
6684 Pacha na mashairi ya Shaaban Robert inavyoonyesha), vile
6685 vile tutahitimisha kuwa mashairi haya siyo guni kwa kuwa
6686 siyo lazima yawe na urari wa mizani. Lakini iwapo tuna
6687 dhana ya "uguni" ambayo ni pana zaidi, ishikiliayo kuwa guni
6688 ni shairi lisilofuata kanuni za urari wa vina na mizani, basi
6689 mashairi haya tutayaita mashairi guni. Kwa mujibu wa
6690 mtazamo huu ushairi wa kitamthiliya tuukutao kwenye kitabu
6691 cha F. Nkwera Johari Ndogo na J.K. Nyerere (Mfasiri) Juliasi
6692 Kaizari ni ushairi guni; na pia ushairi wa kimasimulizi wa E.
6693 Hussein katika kitabu chake, Jogoo Kijijini, tutauita ushairi
6697 guni uliochangamana na ushairi wenye kufuata kanuni za
6698 vina na urari wa mizani.
6700 Yamkini sasa tumefika mahali ambapo inabidi tuliingilie
6701 suala lenyewe la msingi: Ushairi ni nini?
6705 Hadi hapa tumekwishakuona kuwa ushairi wa Kiswahili si
6706 sanaa ya vina kama Shaaban Robert alivyotuambia; na wala
6707 vina na urari wa mizani siyo roho au uti wa mgongo wa
6708 ushairi wa Kiswahili kama Abdilatif, Mayoka na wanajadi
6709 wengine wanavyohubiri. Kwa hakika, mojawapo ya sababu ya
6710 wanajadi kuamini kuwa shairi lazima liwe na umbo maalum,
6711 na kuwa umbo hilo lazima litawaliwe na vina na urari wa
6712 mizani, ni kuwa dhana yao ya ushairi imetawaliwa na utaratibu
6713 wa kimaandishi. Hebu tulidadisi jambo hili zaidi.
6715 Ni rahisi kuthibitisha kuwa umbo la shairi la vina na
6716 mizani ni la kimaandishi, kwani karibu watu wote hapa kwetu
6717 hulitambua shairi kama linavyoonekana kwenye ukurasa wa
6718 karatasi (uwe ukurasa wa Uhuru, au wa Mzalendo au wa
6719 diwani yoyote ya mashairi). Kwa mujibu wa mtazamo huu, in-
6720 sha ni insha kwa vile huonekana imeandikwa kwa njia ya
6721 mjazo; na shairi ni shairi kwa vile laonekana lina vina na
6722 urari wa mizani. Hebu tuangalie andiko hili hapa chini:
6724 Pasipo na mwanamke dunia ingekuwaje?
6725 Mwanamme peke yake sijui angeishije! Maisha yetu
6726 ya kwanza yangekosa msaada; ya kati yakawa giza
6727 kwa furaha kuwa shida; na ya mwisho yangekuwa ni
6728 ghali kwa pesa moja: ingekuwa si dunia kwa
6731 Andiko hili lililoandikwa kwa njia ya mjazo, bila shaka
6732 laonekana kuwa nathari. Lakini andiko hilo hilo tukigeuza
6733 umbo lake, "dhana" ya watu wengi juu ya hulka yake itageuka
6736 Pasipo na mwanamke dunia ingekuwaje?
6737 Mwanamme peke yake sijui angeishije!
6738 Maisha yetu ya kwanza yangekosa msaada;
6739 Ya kati yakawa giza kwa furaha kuwa shida;
6743 Na ya mwisho yangekuwa ni ghali kwa pesa moja:
6744 Ingekuwa si dunia kwa uchache wa faraja.
6746 Umbo hilo haliwakanganyi watu wengi: waliangaliapo mara
6747 moja hurukia kusema kuwa ni shairi, na wakiulizwa kwa
6748 nini hujibu kuwa andiko lina vina, urari wa mizani, n.k.
6749 Tuchukue andiko jingine lifuatalo:
6751 Wakadha namshukuru Mungu
6752 Kwa ajili ya sahibu yangu
6753 Mtunzi na kungwi wa mizungu
6755 Mfadhili na mwenye jamala
6756 Mashuhuri kwa mashairi ya muwala
6757 Na uandishi wa makala
6758 Ambaye ameniomba niandike hii dibaji
6759 Asaa iwafariji wasomaji
6760 Ambao sanaa hii wanaitaraji
6761 Niwabainishie yaliyo muhimu
6762 Kuhusu Kiswahili na utungaji
6763 Na kubatilisha riwaya za mafukala.
6765 Katika andiko hili tunaona upatanifu wa aina fulani wa vina
6766 vya 'ngu', 'la', na 'ji', ni 'mu' tu ambayo haina kina chenziye. Na si
6767 ajabu wapo watu ambao wanaweza kuliita andiko hili ubeti
6768 wa shairi lenye dosari au guni, kwa sababu wameona
6769 upatanifu fulani katika umbo lake. Kumbe andiko lenyewe
6770 katika uasili wake lilikuwa katika umbo la mjazo kama
6773 Wakadha namshukuru Mungu kwa ajili ya sahibu
6774 yangu, mtunzi na kungwi wa mizungu, Mathias
6775 Mnyampala, mfadhili na mwenye jamala,
6776 mashuhuri kwa mashairi ya muwala na uandishi wa
6777 makala, ambaye aliniomba niandike hii dibaji asaa
6778 iwafariji wasomaji ambao sanaa hii wanaitaraji,
6779 niwabainishie yaliyo muhimu kuhusu Kiswahili na
6780 utungaji, na kubatilisha riwaya za mafukala.
6782 Kutokana na hayo yaliyokwishasemwa, tunaona kuwa
6783 "ana ya ushairi" ya wanajadi imefinywa kwenye "umbo
6784 maalum lenye utaratibu wa vina na urari wa mizani", ambayo
6788 kwa kweli ni dhana ya kimaandishi. Na nathari kwao ni an-
6789 diko lolote ambalo halina utaratibu huo. Wanayaangalia
6790 matumizi ya lugha katika tabaka mbili zisizoingiliana:
6791 matumizi ya kishairi na yale ya kinathari. Mtazamo huu
6792 kuhusu lugha umepotoka sana, na hapo baadaye tutaonyesha
6793 upotofu wake. Kwa sasa inafaa tulikabili suala la ushairi ni
6796 Iwapo "umbo" lionekanalo kwenye karatasi haliwezi
6797 kutiwa maanami katika ufafanuzi wowote thabiti wa
6798 ushairi, basi ushairi ni nini? J.A. Ramadhani, katika makala
6799 yake juu ya ushairi, ameeleza kwa urefu na kwa undani
6800 maana na sifa za ushairi. Mambo mengi muhimu ameyataja.
6803 (1) Ushairi huanza na hisi au mchomo unaosababishwa na
6806 (2) Hisi hizo huwasilishwa kwa msomaji kwa njia ya lugha
6807 teule ya kitamathali;
6809 (3) Hisi hizo lazima ziambatane na mawazo na mtazamo
6812 (4) Hali ya kishairi inahusiana kidogo na hali ya kindoto
6813 au tabia ya kuona yasiyoonekana na kuwania
6816 (5) Ushairi umefungamana na ubuni, na kwa hiyo hauwezi
6817 kuwekewa sheria zisizobadilika, na kwamba kuogopa
6818 kubuni kunadumaza maendeleo ya ushairi wa
6821 (6) Uwezo wa kubuni wa mshairi umetoka kwa Mungu am-
6822 baye ndiye mfalme wa sanaa zote.
6824 (7) Shairi ni muungano wa fani na yaliyomo (maudhui).
6826 Kimsingi, ufafanuzi huo wa ushairi hautofautiani sana na
6827 ufafanuzi alioutoa Kezilahabi. Anatuambia kwamba:
6829 Ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa
6830 kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno
6831 fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonyesha ukweli
6834 Fafanuzi hizi mbili zinarekebisha ile fikira ya wanajadi
6835 kwamba ushairi lazima uwe na urari wa mizani na vina. Hata
6836 hivyo, fafanuzi hizi zina upungufu wake.
6838 Upungufu wa maelezo ya Ramadhan umo hasa katika
6839 imani yake kuwa uwezo wa kishairi unatoka kwa Mungu.
6840 Hapa sipo mahali pa kujadili imani ya kidini ya Ramadhan
6844 juu ya uwezo wa kishairi; suala hili ni kubwa na pengine
6845 linahitaji makala ya pekee. Inatosha tu tukisema kuwa ni
6846 kawaida ya falsafa za kidhanifu kumuweka Mungu kuwa
6847 chimbuko la mema aliyo nayo mtu; na kumuweka shetani
6848 kuwa chimbuko la mabaya yote. Upungufu wa kauli ya
6849 Kezilahabi hasa umo katika fungu la maneno "ukweli fulani
6850 wa maisha". Je, ni kweli kuwa ushairi lazima ueleze ukweli
6851 fulani wa maisha, na siyo uongo? Hali halisi inatueleza kuwa
6852 wapo washairi wasemao ukweli fulani kuhusu maisha, na
6853 wapo wengine wasemao uwongo, na pia mshairi mmoja
6854 anaweza kusema ukweli katika shairi moja na uwongo katika
6855 shairi jingine. Fikra hii ni potofa kama ile isemayo kuwa
6856 mshairi ni chemchemu ya hekima.
6858 Jambo ambalo halikutiwa maanani katika fafanuzi hizo
6859 linahusu dhima ya fasihi na ushairi kama vyombo vya
6860 kuburudisha na kustarehesha watu. Ushairi hauelezi mawazo
6861 tu kama kemia au fizikia. Ushairi lazima uguse hisi, lazima
6862 umsisimue yule anayeusema, kuusoma au kuuimba na yule
6863 ausikilizae. Shairi lisilogusa hisi ni kavu na butu, na hata
6864 kama limesarifiwa katika vina na urari wa mizani, shairi hilo
6865 litaishia katika kuhibiri tu. Na fasihi ikisha hubiri mahubiri
6866 makavumakavu kama kasisi mimbarini, bila mvuto wowote
6867 wa kifasihi, itakuwa imeshindwa kugusa pale ambapo
6868 inapaswa kugusa - hisi za watu. Kwa hiyo basi ufafanuzi
6869 thabiti wa ushairi lazima uzingatie uwezo wake wa kugusa hisi
6872 Kutokana na hayo tuliyokwisha sema, tunaweza kutoa
6873 ufafanuzi wa ushairi ambao unazingatia yale yaliyokwisha
6874 semwa na hao hapo jua, pamoja na dhima ya ushairi ya
6875 kugusa moso au hisi. Nao ni huu: Ushairi ni sanaa inayopam-
6876 banuliwa kwa mpangilio maalum wa maneno fasaha na yenye
6877 muwala, kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara, katika
6878 usemi, maandishi, au mahadhi ya wimbo, ili kueleza wazo au
6879 mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani, kuhusu maisha au
6880 mazingira ya binadamu, kwa njia inayogusa moyo. Hapa lazima
6881 tuseme kuwa, ingawa ushairi wa aina yoyote unaweza
6882 kuimbwa, lakini siyo kila kiimbwacho kitaitwa ushairi.
6883 Ushairi ni sanaa ya lugha, na usanaa wake uko katika
6884 "mpangilio maalum wa maneno fasaha yenye muwala, kwa
6885 lugha ya mkato... kwa njia ya kugusa moyo", siyo katika uim-
6886 baji, unaweza kuuongezea (au hata kuupunguzia!) mguso.
6890 Kwa mujibu wa maelezo haya, uimbaji wa hesabu au aya
6891 kutoka kwenye kitabu cha siasa si ushairi.
6893 Ufafanuzi huo wa ushairi unazingatia halka ya ushairi
6894 usiofuata urari wa vina na mizani na ule unaofuata urari huo;
6895 ule ulio katika fasihi simulizi na ule ulio katika fasihi andishi.
6896 Jambo moja linalojitokeza ni kuwa ushairi ni lugha katika
6897 hali ya matumizi maalum; na matumizi maalum haya ni
6898 matumizi ya kisanaa ya vipengele vya lugha. Hapa chini
6899 tutajadili kwa ufupi baadhi ya vipengele muhimu
6900 vinavyoupambanua ushairi.
6902 VIPENGELE VYA USHAIRI
6904 Washairi wa jadi wanadai kuwa "vina na mizani ndio uti wa
6905 mgongo wa ushairi." Dai hili ni batili kifasihi, kwani linageuza
6906 kipengele kimoja kidogo cha kisanaa kuwa ndicho msingi wa
6909 John Ramadhani amezieleza sifa za ushairi kwa urefu na
6910 vizuri zaidi. Yeye ametaja mambo yafuatayo yaliyo mahimu:
6912 1) Katika ushairi vitu hupewa nafsi na utu;
6914 2) Picha ni sifa muhimu ya ushairi;
6916 3) Ushairi huweza kuwa na mpangilio wa maneno usio wa
6919 4) Ushairi una ridhimu, mlingano wa sauti na mapigo;
6921 5) Shairi ni lazima lionyeshe sifa ya kiumbaji, lisiwe ni
6922 nakala ya shairi jingine.
6924 Yote haya ni sawa, ila sisi tutajaribu kuyafafanua zaidi
6925 na kuongezea sifa zingine ambazo hazikutajwa. Suala hili
6926 tutalijadili kwa kufuata vichwa hivi:
6928 1) Mpangilio wa maneno
6932 3) Tamathali za usemi
6934 4) Takriri na ridhimu
6936 5) Hisia za kishairi
6942 Watu wengi wameichukulia kuwa kweli isiyopingika kuwa
6943 mpangilio wa maneno (mfuatano wa vipashio vya sentensi)
6944 katika ushairi ni tofauti na ule ulio katika nathari. Mpangilio
6945 wa maneno hufuata kanuni za miundo inayowezekana katika
6949 lugha fulani. Tukichukua Kiswahili, kwa mfano, sentensi
6950 iliyozoewa sana ni ile yenye muundo huu:
6952 Kiima - Kitenzi - changizo...
6953 Nomino - kimilikishi - kitenzi - kielezi...
6955 Katika Kiswahili tunaweza kusema:
6959 Baba yangu anajua kulima kwa plau
6961 Hii ni miundo ya kawaida ambayo imezoewa sana na
6962 wasemaji wa Kiswahili. Lakini, mzungumzaji anaweza
6963 kuipangua miundo hiyo, na kutumia miundo isiyo ya kawaida
6964 sana, kwa madhumuni ya kuleta msisitizo wa jambo fulani:
6968 Chochote mimi sijui...
6970 Jambo la kusisitiza hapa ni kuwa mtu yeyote, mradi awe ni
6971 mzungumzaji wa lugha fulani, anaweza kutunga muundo wa
6972 kawaida au usio wa kawaida sana (pengine bila yeye kujua).
6973 Mzungumza lugha anao uhuru wa kutamba katika uwanja wa
6974 lugha yake ili aweze kueleza hisia na mawazo yake. Jinsi
6975 atakavyopanga maneno katika sentensi itategemea ujuzi na
6976 ustadi na uzoefu wake katika jambo hili. Je, mshairi
6977 anautumiaje uhuru huu wa kutunga miundo iliyo ya kawaida
6978 sana, na ile isiyo ya kawaida sana?
6980 Jambo la kusisitiza hapa ni kuwa mshairi si mtu wa pekee
6981 katika ujuzi wa lugha aitumiayo kutungia mashairi yake.
6982 Jambo tuwezalo kulisema pasipo wasiwasi wowote kuhusu
6983 tofauti baina ya mshairi na mtu wa kawaida ni hili: mshairi
6984 anao uzoefu katika kutunga mashairi, lakini mtu wa kawaida
6985 hana uzoefu huo. Uzoefu huu katika sanaa hii humwezesha
6986 mshairi kuitumia miundo ya lugha hiyo kutimilizia malengo
6987 yake ya kishairi. Uhuru wa mshairi wa kuchagua muundo
6988 fulani na kuacha muundo mwingine, kupanga vipengele fulani
6989 kwa njia fulani na kuacha kuvipanga kwa njia nyingine, ni
6990 uhuru unaotawaliwa na kanuni za sanaa yake, uwezo wake wa
6991 kuvipanga vipengele hivyo ili vilete athari iliyokusudiwa
6992 hutegemea uzoefu wake, ubingwa wake, na hali aliyo nayo
6993 wakati wa kutunga shairi lake.
6995 Katika ushairi wa Kiswahili, mbinu ya upangaji wa
6996 vipengele vya sentensi kwa njia isiyo ya kawaida hutumika
7000 sana. Utakuta washairi wanasema: mzuri msichana, wangu mke,
7001 n.k. badala ya msichana mzuri, mke wangu. Miundo mingine ni
7002 kama ile tuliyoitoa mfano hapo juu (kulima baba ajua n.k.).
7003 Ipo miundo mingine isiyotumika sana katika mazungumzo ya
7004 kawaida inayotumiwa na washairi. Mpangilio huu usio wa
7005 kawaida huvuta udadisi kuliko ligha ya kawaida, na
7006 hutumika katika kusisitiza vipengele fulani vya hisi au wazo
7009 Lakini shairi siyo lazima liwe na mpangilio wa maneno
7010 usio wa kawaida ili lipendeze. Shairi linaweza kuwa na
7011 mpangilio wa kawaida tu, na athari ya mguso ikaletwa na
7012 vipengele vingine kama vile picha, takriri, n.k. Kwa hiyo,
7013 ingawa mpangilio tulioujadili unaweza kuwa alama
7014 mojawapo ya ushairi, lakini si lazima kila shairi lithibiti
7019 Picha ni matumizi ya lugha yanayopambanuliwa na utenzi
7020 mzuri wa maneno, uangalifu na udhahiri wa maelezo wenye
7021 kuhusisha na kujumuisha dhana mbali mbali tofauti ndani ya
7022 dhana moja ili kuleta taswira na athari maalum katika
7023 mawazo ya msomaji (au msikilizaji). Kezilahabi ameeleza
7024 kuwa athari hiyo aipatayo msomaji au msikilizaji wa ushairi
7025 inaweza kuwa ni ya aina ya vionjo vyenye kuhusiana na
7026 milango ya fahamu ya kusikia, kuona, kunusa na kugusa. Kwa
7027 hiyo, kwa kutumia picha, mwandishi anaweza kumfanya
7028 msomaji wake asisimke, aogope, afurahike, avutike,
7029 akirihishwe, alie, anyamae au aghadhabike kwa kuathiriwa na
7030 picha zilizoteuliwa na kusanifiwa kwa ufundi. Ugumu wa
7031 kutunga mashairi ya mtiririko uko katika utenzi na upangaji
7032 wa picha na tamathali za usemi zenye kuoana na maudhui
7033 yaliyokusudiwa zisizotengua ridhimu ya shairi na zisizofanya
7034 lugha ya shairi ipoteze uasili wake. Wakati huo huo, shairi hili
7035 liwe na uwezo wa kindanindani wa kuvutia na kudumisha
7036 hamu ya msomaji au msikilizaji hadi mwisho. Katika ushairi
7037 wa fasihi-simulizi, hamu ya hadhira hudumishwa na uteuzi wa
7038 maneno, muziki (kama ala za muziki zinatumika), mazingira
7039 au sherehe inayoambatana na tungo hiyo, ushirikishaji wa
7040 hadhira kwa kutumia kibwagizo, makofi na vipengele vingine,
7041 na umuhimu wa kijamii au kihistoria wa yale yanayoelezwa.
7045 Katika ushairi-andishi wenye vina na mizani, hamu ya
7046 msomaji zaidi hudumishwa na ulinganifu wake wa ridhimu na
7047 sauti unaotokana na vina na urari wa mizani. Mapigo ya
7048 shairi la aina hiyo hufuata mgawanyo wake katika vipande
7049 vyenye mizani sawa na shairi husomeka upesi upesi bila
7050 kuitumikisha sana akili ya msomaji. Kifani, vina na urari wa
7051 mizani katika ushairi-andishi hufanyakazi ya ala za muziki
7052 katika ushairi-simulizi.
7054 Ushairi wa mtiririko ni wa kiwango cha juu zaidi kwa
7055 sababu unakataa kupata uhai wake kutokana na mbwembwe
7056 za kijuujuu, mambo ya nje ambayo ni nyongeza muhimu juu
7057 ya ushairi, lakini si lazima yawe sehemu ya ushairi: vina na
7058 urari wa mizani. Ushairi huo unapata uhai wake na utamu
7059 wake kutokana na mfumo wake wa ndani ambao ni
7060 fungamano la matumizi mahususi ya lugha nzito, hisia nzito
7061 na maudhui ya kishairi. Mashairi haya yanamlazimisha
7062 msomaji atumie akili zaidi, ajihusishe zaidi kijaziba katika
7063 hisia za mtunzi, na atafakari zaidi, badala ya kumkokota
7064 kikuku kwa utamu wa kijuujuu wa muziki wa vina na urari wa
7065 mizani. Mtiririko ni mashairi yaliyokusudiwa yasomwe na
7066 watu wazima, mengi hayafai kusomwa na watoto wa shule za
7067 msingi kwa sababu uwezo wao wa kuichambua fasihi bado ni
7068 mdogo. Hivyo hapana shaka kuwa kwa miaka mingi ijayo
7069 mashairi yenye vina na mizani yataendelea kupendwa zaidi na
7070 watoto wadogo, mradi lugha yake isiwe ngumu sana. Kwa ajili
7071 ya adhira hiyo, mashairi ya aina hiyo ni lazima na bora yaen-
7072 delee kutungwa. Bali kwa ajili ya watu wazima waliofikia
7073 kiwango fulani cha ufahamu wa fasihi, mashairi ya aina hiyo
7074 si lazima, ingawa si mwiko kuyatunga. Kila mshairi apewe
7075 uhuru wa kutumia fani inayofungamana vizuri zaidi na
7076 maudhui yake, uwezo wake, na pia hadhira aliyokusudia.
7078 Ingawa matumizi ya lugha huweza kuzindua hisi na
7079 maono fulani katika akili ya msomaji juu ya kile
7080 kinachozungumziwa, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa
7081 uhusiano huo unaozinduliwa kati ya picha ya mawazoni na
7082 kitu halisi kinachozungumziwa (kinachochorwa) ni wa
7083 kinadharia, si wa kimaumbile au wa moja kwa moja. Hakuna
7084 uhusiano wa moja kwa moja kati ya maana au umbile la kitu
7085 na uwakilishaji wa kitu hicho katika lugha - katika neno
7086 mofimu na fonimu. Kifasihi uhusiano tuupatao tunapotumia
7087 picha ni ule unaoumbwa na akili ya msomaji mwenyewe
7091 inapozinduliwa na ustadi wa mshairi wa matumizi ya lugha
7092 na kunga nyingine za ushairi. Usanifu wa mashairi humfanya
7093 msomaji wake awe msanifu vile vile; mshairi hudokeza,
7094 msomaji hukamilisha; mshairi huumba, msomaji
7095 humalizia na kuhusisha kile kilichoumbwa na hali halisi
7096 anayoijua. Kwa hiyo msomaji wa mashairi si mpokeaji tu wa
7097 sanaa hiyo bali ni mpokeaji msanii vile vile.
7099 Hebu tuutazame mfano ufuatao unaotoka katika shairi la
7100 Shaaban Robert, "Mtu na Malaika".
7104 Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
7105 Wa huku hafiki huko, wala halina malisho.
7106 Halishibishi huchosha, njiaye ina uchovu,
7107 Na tabu isiyokwisha, wala hupati utuvu.
7108 Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka,
7109 Na milima akapanda, apendako akafika.
7110 Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
7111 Na mitoni akavuka, hata alikonuia.
7112 Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dirani,
7113 Hupati kupanda bara, na hushuki baharini.
7114 Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia.
7116 Katika dondoo hii tunapewa picha tatu mahsusi. Picha ya
7117 kwanza ni neno linalozunguka... Mshairi anatuambia kuwa neno
7118 ambalo halifuati njia iliyonyooka 'neno lenye mzunguko"
7119 halifikii mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa "halina
7120 malisho". Hapa neno limefanywa kuwa kitu chenye uwezo wa
7121 kutembea, kuzunguka. Athari ya neno hilo kwa anayehusika ni
7122 kwamba halileti shibe wala utulivu, linachosha: "Halishibishi
7123 huchosha". Hapa tunapewa picha ya shibe, neno linapewa
7124 uwezo wa chakula - kitu yakini kinachoshikika na
7125 kinacholiwa. Bali mtu hatosheki na "chakula hicho" hatatui
7126 matatizo yake iwapo njia anayotumia ni ya mzunguko, ya
7127 kulegalega, ya ugeugeu na woga.
7129 Picha ya pili tunayopewa ni ya mtu aendaye safari ngumu
7130 kwa ujasiri na moyo na dhati, akipanda milima na kushuka
7131 mabonde, akipenya misitu na kuvuka mito, hadi kufika kule
7132 anakokwenda. Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo,
7133 anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu, alimradi anajua kuwa
7134 itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepambana na
7138 matatizo badala ya kuyakimbia. Mtu wa aina hii ndiye hupata
7139 mafanikio. "Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka".
7141 Picha ya tatu tunayopewa ni dira. Dira ni chombo
7142 kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha
7143 majira yao ili wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na
7144 mshale wake aghalabu huzungukia pale pale ulipo, katu
7145 hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo la mwandishi
7146 kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye
7147 lengo lake. Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki
7150 Picha hizi tatu kwa pamoja zinafaulu kutupa ujumbe wa
7151 mwandishi kuhusu maisha na namna ya kuyakabili:
7152 tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia. Tuamue jambo na
7153 tulifanye bila kutetereka. Tusiogope vikwazo wala matatizo.
7154 Maisha ni mapambano.
7156 Kwa kutumia picha hizi tatu, mwandishi kafaulu
7157 kufikisha kwetu ujumbe wake wa kishairi. Maudhui yake ni ya
7158 kishairi, yanapatikana kwa kuzichambua na kuzifafanua
7159 picha alizozitumia. (Shairi hili lingeweza vile vile kufasiriwa
7160 kidini kama alivyofanya J. Ramadhani katika makala yake
7161 "Ustadi wa Shaaban Robert Mshairi" Mulika No. 7, uk. 46-48)
7165 Katika dondoo tulilolichunguza picha imejitokeza kwa
7166 njia ya sitiari (kitu kimoja kuwa badala ya kitu kingine kilicho
7167 tofauti: k.m. "msitu" badala ya "matatizo", "dira" badala ya
7168 "tabia ya kukwepa matatizo" n.k.) na mpangilio wa lugha na
7169 mawazo. Dhana tatu zinazotofautiana - neno linalozunguka
7170 mtu anayesafiri kupitia msituni na baharini, n.k. na dira
7171 inayozungukia mahali pale pale ilipo zinaleta wazo moja
7172 mahsusi. Zote zimechangamana ili kujenga dhana moja.
7173 Umoja wa wazo linalozungumziwa unaimarishwa pia na
7174 mfungamano wa ubeti mzima - pana mfululizo wa fikra na hisi
7175 tangu mstari wa kwanza hadi wa mwisho, kifungu kizima ni
7176 ubeti mmoja, hakuna mgawanyo wa beti za mistari miwili
7177 miwili au minne minne. Wazo linafululiza bila kusita au
7178 kukatishwa hadi mwisho kama vile ambavyo maudhui ya
7179 shairi lenyewe yanavyotuhimiza kufululiza katika njia moja
7180 bila kutetereka hadi mwisho. Muundo wa shairi umeoana na
7185 Mpangilio wa lugha - herufi, silabi, mofimu hadi maneno
7186 na sentensi ni sharti uoane na maudhui. Washairi hutumia
7187 kunga mbali mbali za kisauti na kimpangilio ili kuleta hisia
7188 fulani. Baadhi ya kunga hizo ni onomatopea, mizani, vina,
7189 asonansi (mlingano wa sauti za irabu), konsonansi (mlingano
7190 wa sauti za konsonanti) takriri-konsonanti (marudio ya kon-
7191 sonanti) takriri-vina, n.k. Vipengele vyote hivi, isipokuwa
7192 onomatopea, ni aina ya takriri na tutavijadili chini ya mada
7197 Onomatopea ni mwigo wa sauti. Hii ni kunga inayotumiwa na
7198 washairi ili kutoa picha au dhana ya kile kinachowakilishwa
7199 au kupambanuliwa na sauti hizo. Kwa mfano tukisema:
7200 "Maji yalimwagika mwa" neno mwa ni onomatopea,
7201 linawakilisha sauti au kishindo cha maji yanayomwagika.
7202 Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu ya
7203 msamiati wa kawaida wa Kiswahili ni: pikipiki, bombom,
7204 mbwa, yowe, ngurumo, bunduki, gumia, kata, n.k.
7206 Katika shairi lake la "Cheka kwa Furaha" Shaaban
7207 Robert ametumia onomatopea ili kuleta ile dhana ya kucheka:
7209 Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
7210 Haya cheka ha! ha! ha! ndiyo ada duniani.
7211 Basi cheka kwa! kwa! kwa! kwa! usafike moyo wako
7212 Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko;
7214 Maneno yaliyoandikwa kwa italiki ni onomatopea, yanatoa
7215 picha ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni
7216 mpangilio maalum wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya
7217 dhana inayozungumziwa.
7221 Tamathali za usemi ni vifananisho au viwakilisho vya dhana
7222 fulani kwa dhana nyingine tofauti au zinazofanana. Ni usemi
7223 wenye kupanua, kupuuza au kubadilisha maana za dhahiri au
7224 za kawaida za maneno ili kuleta maana maalumu ya kishairi
7225 iliyokusudiwa na mtunzi. Tamathali nzuri hupanua,
7226 huyakinisha na huipa uhai na uhalisi zaidi dhana
7230 inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au
7231 msikilizaji wa shairi, na huacha athari ya kudumu katika hisi
7234 Tamathali zinazotumika zaidi katika ushairi ni tashbiha,
7235 meonymy, uhaishaji (personification) (Tashihisi) synecdoche,
7236 baalagha, kejeli na sitiari.
7240 Hi ni tamathali ya ufananisho au mlinganisho wa vitu viwili
7241 au zaidi. Katika tashbiha, kama ilivyo katika sitiari, huwa
7242 kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu
7243 wameviita kizungumzwa, kifananishi na kiungo. Kifananishi
7244 ndiyo usemi wenye kuzingatia maana-dhahnia, ni chombo
7245 kinachobeba mlinganisho. Kizungumzwa ndicho kitu halisi am-
7246 bacho kinazungumziwa na kifananishi kwa mafumbo. Kiungo
7247 ni zile sifa ambazo zinapatikana katika kizungumziwa na
7248 kifananishi na hivyo kuhusisha vitu hivyo viwili. Katika tash-
7249 biha, kizungumzwa na kifananishi huhusishwa bila mafumbo
7250 kwa uwazi, moja kwa moja, kwa kutumia maneno fulani ya
7251 ulinganisho, km. "kama" "fanana na", "mithali ya" n.k.
7252 Katika tashbiha hakuna maana dhahnia, bali kuna
7253 ulinganishaji wa vitu viwili vilivyo bayana. Angalia mfano
7256 Kweli ni sawa na radi inapotoa kauli...
7257 Kweli kinywani ikiwa sawa na Mto wa Nili
7258 Kweli kama msumeno hukereza sawa kweli.
7260 Katika dondoo hilo maneno yaliyochapwa kwa italiki
7261 yanaunganisha vitu viwili vinavyotofautiana na
7262 kuvifananisha. Mstari wa kwanza "kweli" inalinganishwa na
7263 radi, mstari wa pili inalinganishwa na "Mto Nili" na mstari
7264 wa tatu inalinganishwa na "msumeno".
7266 Tashihisi (uhaishaji)
7268 Washairi mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na
7269 uhai sifa za kitu chenye uhai, hasa za binadamu. Matumizi ya
7270 lugha kwa njia hiyo ndiyo huitwa uhaishaji au tashihisi.
7271 Kisanaa maelezo ya kitashihisi huwa na upekee unaomwingia
7275 msomaji akilini haraka, kwani si jambo la kawaida,
7276 mathalan, kuona mti "ukimpungia mtu mkono" au nyumba
7277 "ikimkodolea macho" mgeni. Tashihisi, basi, ni aina ya sitiari
7278 na kisanaa kazi yake ni kama ile ya sitiari, japo kwa kiwango
7279 cha kidhahnia zaidi.
7281 Mfano wa matumizi ya tashihisi:
7283 Kimya hakineni jambo, si kimya chawatazama...
7284 Kimya chaja zua mambo, pasiwe mwenye kusema...
7285 Kimya kipimeni sana, msione kutosema
7286 Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama
7287 Kimya chaja watukana kizuwe yaliyozama...
7289 Katika dondoo hili, "kimya" (ambayo ni nomino-dhahnia)
7290 kimepewa sifa za binadamu, kinaweza kunena, kutazama,
7291 kuzua mambo, kusimama nakutukana.
7293 Katika shairi lake la "Fedha", Shaaban Robert anaipa
7294 fedha sifa za binadamu:
7301 Mfano mzuri wa matumizi ya tashihisi kishairi tunauona
7302 katika shairi la Bwana Rajabu M. Kianda (Selukindo) liit-
7305 Jembe wangu nifariji, nami nikupe uzima,
7306 Jembe wewe ndiye jaji, twakuenzi zote dhima,
7307 Jembe wewe ni mpaji, wa baba na kina mama,
7308 Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
7310 Jembe wewe msifika, utuonee huruma,
7311 Jembe shamba tukifyeka, njoo ufanye kulima,
7312 Jembe njoo pasi shaka, ukija lete mtama,
7313 Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
7315 Jembe kwetu ukifika, tunapata usalama,
7316 Jembe kote umeshika, ukweli tunausema,
7317 Jembe yakija masika, nawe fika nyuma nyuma,
7318 Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
7322 Jembe jua likitoka, nawe usife mtima,
7323 Jembe usije kuchoka, au kupatwa na homa,
7324 Fanya bila kukongoka, fanya usirudi nyuma,
7325 Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
7327 Mola akupe hakika, usende kamwe mrama,
7328 Nenda upate kufika, kama tunavyokutuma,
7329 Sote huko tukifika, tutaishi kwa neema,
7330 Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
7332 Katika shairi hili "Jembe" limepewa sifa za binadamu: ni
7333 mfariji, jaji, mpaji, mtawala, mkulima; linaweza kusafiri,
7334 kubeba mtama, kufa mtima, na kupatwa na homa. Ingawa
7335 tunajua wazi kuwa jembe ni kifaa tu kinachotengenezwa na
7336 kutumiwa na binadamu, kuwa halina hata mojawapo ya sifa
7337 hizo, lakini tunaposoma shairi tunaathirika na kushawishika
7338 kuwa yasemwayo ni kweli na sana maana. Tunalikubali kwa
7339 sababu tunaelewa kuwa tukisomacho ni kiwakilishi tu, ni
7340 ishara ya dhana nyingine nzito na muhimu: Umuhimu wa
7341 kilimo katika uchumi na uhai wetu, na katika historia wa
7342 binadamu. Mtunzi katumia uwezo wake wa kisanaa kuumba
7343 picha hii ya jembe, nasi wasomaji inatubidi tutumie uwezo
7344 wetu wa kuumba na kutafsiri ishara ili tulielewe na
7345 kulifurahia shairi hili. Matumizi ya tashihisi yanaliongezea
7346 shairi hili uzito wa kimaana, na yanatushirikisha sisi
7347 wasomaji katika ufumbuzi wa "kitendawili" chake. Hivyo
7348 shairi hili linatuathiri sana kwa kuwa linatushirikisha akili
7349 zetu katika kutafakari vipengele vyake na maana yake.
7357 Nimefurahi kukutana na wewe.
7367 nimefurahi kukutana na wewe.